Wito umetoka mei 5 ya saa ngapi ?

Saa 6 usiku ? Binafsi nakumbuka mwezi uliopita MOF&P alisema wanachakata mipango ya kuondoa baadhi ya tozo ktk kila 1 ltr ya mafuta ..sasa sijui imekuwaje
Udhalimu tu. Unaweza kushangaa bei inapungua kwa tsh20/lita na kuna mazuzu ytashangilia kuupiga mwingi
 
Pm huwa ni muongo muongo sana
Yupo ikulu anachapa kazi. Katika watu waliokuwa team JPM na nimeona wametumia hekima kuliko hata walipokuwa naye, ni Bashiru Kakurwa. Huyu bwana yeye ameamua kukaa kimya kabisa bila hata kutia neno tangu mwajiri wake aage dunia. Hekima ya kiwango cha juu kabisa. Sabaya alijifanya kuhadaa umma bila kujua anawindwa ateleze kidogo tu.
 
Nchi jirani mafuta wanauza bei rahisi kuliko Tanzania na wanapitisha hapa hapa bongo halafu tukaambiwa twende Burundi kwenye vitu vya bei rahisi.
Iko siku watu watachoshwa na dhihaka za viongozi. Huyo ni waziri anawajibu watu kwa kejeli namna hiyo bila kujua kuwa maisha ni duara na inaweza kupinduliwa meza wasiamini
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu Ndg. Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

"Nawaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waiamini Serikali yao kuwa tunaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha tunapunguza gharama za maisha kwa wananchi" amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo Alhamisi Mei 5, 2022 katika kikao kilichofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Oyster bay jijini Dar es Salaam ili kufanya tathmini ya bei ya mafuta na kuangalia namna gani Serikali inaweza kufanya ili kupunguza athari ya bei ya mafuta na kuleta unafuu wa gharama za maisha kwa Watanzania.

Waziri Mkuu amesema kikao hicho kimefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameagiza viongozi wa sekta husika wahakikishe wanatafuta suluhisho la kupanda kwa bei ya mafuta hata kama bei hiyo inaendelea kupanda duniani.

"Mheshimiwa Rais ameona changamoto wanayopitia Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, hivyo kikao hiki ni matokeo ya maagizo yake ya kuhakikisha sisi kama viongozi tunatafuta suluhisho la muda mfupi na la muda mrefu ili kukabiliana na changamoto hii." amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kuwa tayari Wizara ya Nishati imeanza kutafuta njia mbadala za uagizaji wa mafuta pamoja na kupunguza makato mengineyo ili kupunguza bei ya mafuta.

"Serikali inaangalia njia mbadala za uagizaji wa mafuta, kupitia kwa wazabuni wengine kama ambavyo imeshauriwa na wabunge na tayari mchakato huo umeanza, kwa kutathmini maombi 24 ambayo yaliwasilishwa kwa Wizara na sasa wamebaki wazabuni sita ambao wameingia hatua inayofuata. Inachokifanya Serikali hivi sasa ni kujiridhisha na uwezo wao wa kusambaza mafuta kulingana na mahitaji na taratibu zilizowekwa na Serikali.” amesema.

View attachment 2212069View attachment 2212070
 
Ajabu ya mvita kuota mvinde. Gesi ya hapo kwa uwani kwetu wameshindwa kuifanyia mchakato. Leo mafuta toka bahari ya saba huko wanayafanyia mchakato.
 
SERIKALI INATAFUTA NJIA MBADALA ZA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA - MAJALIWA
*Aitisha kikao cha kutathmini bei ya mafuta

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea kutafuta njia mbadala ambazo zitapunguza gharama ya maisha kwa Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia.

"Nawaomba Watanzania waendelee kuwa watulivu na waiamini Serikali yao kuwa tunaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha tunapunguza gharama za maisha kwa wananchi," amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Alhamisi, Mei 5, 2022) katika kikao kilichofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ofisi ndogo ya Waziri Mkuu iliyoko Oysterbay, jijini Dar es Salaam ili kufanya tathmini ya bei ya mafuta na kuangalia namna gani Serikali inaweza kufanya ili kupunguza athari ya bei ya mafuta na kuleta unafuu wa gharama za maisha kwa Watanzania.

Waziri Mkuu amesema kikao hicho kimefanyika ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ameagiza viongozi wa sekta husika wahakikishe wanatafuta suluhisho la kupanda kwa bei ya mafuta hata kama bei hiyo inaendelea kupanda duniani.

"Mheshimiwa Rais ameona changamoto wanayopitia Watanzania kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta katika soko la dunia, hivyo kikao hiki ni matokeo ya maagizo yake ya kuhakikisha sisi kama viongozi tunatafuta suluhisho la muda mfupi na la muda mrefu ili kukabiliana na changamoto hii," amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kuwa tayari Wizara ya Nishati imeanza kutafuta njia mbadala za uagizaji wa mafuta pamoja na kupunguza makato mengineyo ili kupunguza bei ya mafuta.

"Serikali inaangalia njia mbadala za uagizaji wa mafuta, kupitia kwa wazabuni wengine kama ambavyo imeshauriwa na wabunge na tayari mchakato huo umeanza, kwa kutathmini maombi 24 ambayo yaliwasilishwa kwa Wizara na sasa wamebaki wazabuni sita ambao wameingia hatua inayofuata. Inachokifanya Serikali hivi sasa ni kujiridhisha na uwezo wao wa kusambaza mafuta kulingana na mahitaji na taratibu zilizowekwa na Serikali,” amesema.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Bw. George Simbachawene, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Nishati, Bw. January Makamba, Makatibu Wakuu, pamoja na watendaji wakuu wa taasisi za EWURA, TPDC na Wakala wa Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja (PBPA).
 
IMG-20220504-WA0272.jpg
 
Pm huwa ni muongo muongo sana
Huyu PM simwamini hata kidogo zile mbwembe nataka siku 14 report ya mauji ya Mtwara iko wapi? leo miezi hizi kauli ndogondogo zinakufanya ngumu kuaminika. Usiseme kitu kama unajuwa huwezi kutekeleza. Hata katika maisha ya kawaida ukiwa na mtu kila siku ahadi fake nakuja sasa hivi haji, nitakupigia simu dakika 10 tu hapigi, nitakutumia pesa yako kesho hatumi, huyu mtu utamchukuliaje? Sasa ukiwa kiongozi ndio kabisa
 
Back
Top Bottom