Ripoti AfDB: Gharama kubwa za maisha zinaweza kuamsha machafuko zaidi Afrika

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
UCHUMI: Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB) imesema kuendelea kupanda kwa gharama za maisha hasa mahitaji muhimu kama Chakula, Nishati na bidhaa nyingine kunaweza kuibua hasira za Wananchi na kusababisha vurugu katika baadhi ya Mataifa ya Afrika.

AfDB imezitaja baadhi ya Nchi zinazopaswa kuchukua hatua za haraka kushughulikia masuala hayo ni Angola, Ethiopia na Kenya huku Nigeria ikiwa tayari imeanza kushuhudia kukosekana kwa utulivu kutokana na gharama kubwa za maisha.

Pia, imeelezwa kuendelea kushuka kwa thamani ya Sarafu za Fedha dhidi ya Dola ya Marekani katika Nchi nyingi za Afrika kutaongeza Bei za Vyakula kwa mwaka 2024, hali inayoweza kuchochea madai ya mabadiliko ya Kiserikali.

Taarifa hiyo imeelezwa katika Ripoti ya Makadirio ya Ukuaji wa Uchumi Afrika ambayo inaonesha Uchumi utakua kwa wastani wa 3.8% mwaka 2024 4.2.% mwaka 2025 ingawa bado AfDB imeshauri Serikali za Afrika kuhakikisha Wananchi wanamudu gharama za Maisha ili kuepusha Machafuko.

========

The African Development Bank is warning that the rising cost of energy, food and other commodities in several African countries, including Angola, Ethiopia and Kenya, could trigger social unrest. Already, people in Africa's most populous country, Nigeria, have been marching to protest the high cost of living, prompting the government to release grain from the national reserves.

The African Development Bank's notice was contained in its biannual Africa Macroeconomic Performance outlook publication released last week.

The bank said in its 2024 forecast that energy and food price increases -- along with a currency depreciation in Angola, Ethiopia, Kenya and Nigeria -- could spark internal conflict, despite Africa showing overall economic growth.

The bank also said conflicts in eastern Europe and the Middle East could trigger supply chain disruptions, exacerbate inflation across the world, and make Africa's situation more precarious.

AFDB 2023/24
 
World economic forum puppets at the wheel
" YOU WILL OWN NOTHING AND YOU WILL BE HAPPY " Kuna ujumbe mzito sana kwenye huo usemi unaotumika kwenye vikao vya world economic forum na World government summit
Hizi ni nyakati za hatari sana
Ni vile tu watu wengi ni kama kondoo
Nchi yetu yenyewe kwa sasa imeshikwa na genge la puppets wa WEF
Wakianza kuemplement hizi policies , Kwa mara ya kwanza Vichwa panzi watanzania ndio tutajua msoto maana yake ni nini
 
Back
Top Bottom