Kupanda kwa gharama ya maisha

koryo1952

JF-Expert Member
Mar 7, 2023
380
763
Jana nilimuona Jamaa mmoja akishauri nini cha kufanya kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha.

Hoja yake ambayo mimi naiita hoja nyepesi alishauri wananchi kuwa kwa kuwa sasa nchi inapata mvua basi ni wakati muafaka watu kujikita kwenye kilimo ili kuepukana na gharama ya kupanda kwa maisha.

Kilimo pekee siyo suluhisho ya kupanda kwa gharama za maisha ila huyo jamaa alisahau kuwa

(1) Bei ya huduma pia inasababisha kupanda kwa gharama za maisha

(2) Kupanda kwa bei ya nishati ikiwemo mafuta na hivyo kuongeza bei ya bidhaa na nauli

(3) Gharama za matibabu

(4) Gharama za shule zikiwemo karo

(5) Kodi kwa ajili ya maendeleo ya nchi.

Hivyo hoja yake kuwa watu wajikite kwenye kilimo kuwa kutapunguza gharama za maisha naona kama ni hoja nyepesi.
 
kilimo na ufugaji hasa msimu huu wa masika ni miongoni mwa lainisho la kuishi bila kulalama sana ndani ya huko kunakoitwa kupanda gharama za maisha...

kubadili mtindo wa maisha, kubana matumiz na kuepuka matumizi yasio na tija wala ulazima, kufanya kazi kwa bidii pia ni njia za kujikwamua kwenye kisingizio hicho..
 
Kwa hiyo wafanyakazi waache kazi zao walizoajiriwa wakamate jembe kwenda kulima, wafanyabiashara wafunge maduka waende shamba, machinga, bodaboda wote shamba.......hii itakuwa mvurugano.​
 
Back
Top Bottom