Wanne mbaroni kuhusiana na kesi ya James Temba

Wanne mbaroni kuhusiana na kesi ya James Temba

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linaendelea na uchunguzi wa tukio la mauaji ya kikatili ya mwanafunzi wa Chuo cha IFM, James Rogers Temba, ambaye mwili wake ulikutwa ukielea kwenye maji ya Mto Msimbazi, eneo la Kipawa Ilala ukiwa hauna kichwa, Aprili 30, 2026.

Polisi tayari imewakamata watuhumiwa wanne kuhusiana na tukio hilo, akiwemo Steven Rogers Chaka (31), mkazi wa Bomang’ombe mkoani Kilimanjaro na Afisa Maabara; Anna Frank Lema maarufu kama “Happines” (30), mfanyabiashara mkazi wa Tabata Chang’ombe; Twalibu Khamis maarufu “Mputo” (23) pamoja na Michael John maarufu “Tambali” (26), wote wakazi wa Kigogo Kati.
Scape goats?
 
Hapo ukiunganisha Dots si unaona kwamba Afisa Maabara Demu wake ni Happiness na James temba alikuwa anakula Happiness ,so Ofisa Maabara ikabidi akodishe hao Masela "Mputo" na "Tambali" ndiyo wakamaliza kazi ,Hayo majina yanaonyesha ni "MANDONGA WATU KAZI".


Sema Una point kichizi maana hao wahuni wawili mputo na tambali ni wa kigogo....na kigogo ni ushenzini hasa!
 
Sasa kama ni mapenzi, hawa wengine wameingiaje? Just najiuliza tu

Binafsi nadhani ni mambo ya hela, itakuwa kawapiga hela wakaungana na kuamua kummaliza!
Hao ni watuhumiwa tu mpaka sasa.
 
Wabongo ni wakatili kama binadamu wengine wowote tu wale, kitu ambacho tulikuwa hatujapata ni vichocheo au mazingira, kadri muda unavyoenda hivi vichocheo na mazingira yanakuwepo na hapo ndipo ilo evil nature iliyo katika binadamu wengi inajidhihirisha sasa.
Binadamu ni Wanyama wenye Utashi tu.
 
Yes mkuu huo ndiyo ukweli ,nilitaka niandike tangia siku ile ya tukio sema nilikuwa porini internet ilikuwa shida.

"Mimi naona mbali kwa darubini kali" - Afande Sele.
Asee mkuu hongera sana...umenifungua ubongo waah!

Hii ni deep think haina comeback 🙌
 
Erythrocyte kwa hili, huoni aibu na uzi wako

Hivi huyo kuna mtu anamsikiliza na kuweka mambo yake kichwani?

Lakn ndo viongozi wa tecdema, na hao tunajua matatizo yao!
 
Kama wale wanasema wengi wanaotekwa na kupotezwa ni sababu ya wivu ya mapenzi,dhuluma nk
Hii kauli imewapa sana watenda maovu njiaa!

Na huku chini watu wakifanyiana potezana raia
Inajuwa ni watu wa mfm ndy wametekeleza

Ova
Na mimi ndicho naamini.
Kama watu wanamteka padre na kumtupa kusikojulikana na wanakuja kusema alikuwa na stress za mapenzi na madeni hio unaonaje? unaweza kuamini mtu wa nmana hio? au ni genge la wahuni tu..

Vijana mamia kwa mamia wamepotea, wengine miili yao imeokotwa ikiwa na majeraha...

Hali inatisha sana..
 
Mkuu kwa Dunia ya sasa kila kitu kinawezekana,

Hawa wenye umri mdogo ndio rahisi zaidi kutumika coz akili zao bado zinakua hazijakomaa kisawasawa ili kupima madhara ya baadae kwa wanachokifanya.
Mkuu miaka 23 tayari anajua baya na zuri
Wachache sana wa huo umri wanaweza kufanya ukatili wa namna hii
Yani hii sio kuhusu kukomaa akili, ni ujinga na ukatili
Yani kama uthibitisho ukionekana ni asilimia 100 wanahusika, then ni kuwanyonga tu bila huruma
Miaka 23 ni dume zima linaelewa linachofanya
 
Eti serikali makini 🤣🤣..!

Kweli ni makini, tumeona majibu ya tume HURU ya Chande kuhusu 29/10
Ukifanya fujo utapigwa , yaani kama bado una ujinga basi kafanyeni tena ..
 
Usijifariji mapema na kutoa sifa

Kuna mtu yawezekana kati yao alikuwa anagongewa ila limemkuta kwakuwa walimwengu wamepima maumivu yake na tukio na wametoa ushirikiano

NB: Ni jambo jema kufatilia hili lakini kama vyombo vya usalama kwa heshima zote🙏

Mbaki jinsi mlivyo
Mimi nilishukuru kwa hatua hiyo nawe mwenye akili yakugongewa nani timamu?!
 
Mimi nilishukuru kwa hatua hiyo nawe mwenye akili yakugongewa nani timamu?!
Sawa wewe mjuaji kuliko mimi

Nipe kisa duniani kama si pesa na mapenzi kinachoweza kufanya mtu akaona raha kuchinja na kuondoka na kichwa cha mtu

Kwani jamaa ana museum.!
 
Kama una gundu la bundi, siku mbili nyuma kabla ya kukatwa kichwa umewasiliana nae, na ukamuwashia moto, but hauhusiki na kifo chake, mara police wanatrace namba wanaikuta na yako iko juu juu current call...uwiii unaenda kuminywa mbupuu!
Sio rahisi hivyo. Huwa wanafuatilia wanaacha namba ambazo wamegundua ni calls za kawaida. Kuna jamaa tulikuwa tunafanya biashara ya aina moja. Mara nyingi huwa tunashare stock ikiisha nachukua kwake na yeye vivyo hivyo. Kumbe nyuma ya pazia anauza mzigo wa Colombia. Wazee wakamfuatiliq mpaka wakamuingiza kingi. Mimi bila kujua nikawa namtafuta sana na kumtumia msg nauliziq mzigo halali simu walasg hazipokelewi baadae simu yake ikawa haipatikani kabisa. Baada ya wiki mbili nikasikia Kala miaka 30 jela kwa kuuza mzigo wa Colombia. Hata mimi nilikuwa under microscope.
 
Inawezekana pia ila kwa hii issue ya kukatwa kichwa ni Mapenzi Mabaya Mapenzi Mabaya ,Mke wa mtu ni sumu usijaribu chombeza.
Ngoja tumsikie muliro atakuja na majibu gani
Maana wengine wanasema dogo sijuwi alikiwa winger kko...kuna mambo ya sim blah blah
Wengine mapenzi nao wanasema

Ova
 
Back
Top Bottom