Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576

Baadhi ya mahitaji ya wadau:
Naombeni kupewa orodha ya maduka ya suti za kiume (za kisasa) yaliyopo Kariakoo. Nahitaji kuyazungukia. Kwasababu ya muda siwezi ku-design kwa fundi ndo maana nataka kuitungua dukani. Shukrani.

Kariakoo au Dar ni wapi tutapata pochi, vitenge na viatu vya kike bei za jumla? Maana wenyeji wengi hawapendi kutupeleka kwenye machimbo.

Baadhi ya majibu/maelekezo ya wadau:



 
Ila kwa kuanzia nenda kwenye maduka yaliyoko nyuma ya kituo cha polisi msimbazi kwenye jengo lenye ATM ya NMB
 
Ukifika msimbazi kwenye jengo la police pale kuna road ya mkono wa kushoto na kulia. Hii ya mkono wa kulia ukinyoosha, moja kwa moja mbele huko utakutana na maduka meengi tuu yanayouza nguo na vitu vingi vinavyowahusu watoto. Ila mtaa huu bei zao kidogo huwa zimechangamka.

Nyingine ni ukiwa umesimama pale kituo cha gari za Mwananyamala au Police kwa nyuma, nyooka na hiyo njia, utakutana na T-joint ya kwanza kisha songa mbele then utakutana nayo ya pili; baada ya hiyo ya pili sasa ingia maduka ya mkono wa kulia japo huko wanauza zaidi vitenge na khanga. Ukikosa huko ingia maduka ya mkono wa kushoto huko ndo kuna nyingi zaidi za watoto.
 

Hayo.maduka hapo mbona huwa hawauzi jumla
 
Hayo maduka hapo mbona huwa hawauzi jumla
Hapo wapi sasa maana hapo me nimetaja ya sehemu mbili mkuu. Ila kimsingi kwa maduka ya kariakoo huwa ni rejareaja na jumla sasa ww unapofika mwambie muuzaji unataka kwa bei ya jumla na wengi huuza kuanzia p3.
 
hapo wapi sasa maana hapo me nimetaja ya sehemu mbili mkuu.
Ila kimsingi kwa maduka ya kariakoo huwa ni rejareaja na jumla sasa ww unapofika mwambie muuzaji unataka kwa bei ya jumla na wengi huuza kuanzia p3
Hapo maeneo ya kituo cha polisi msimbazi.

Hayo maduka yooote kuanzia kwa halima toto hadi ule.mtaa wa pili narung'ombe sijawahi pata duka la.nguo kwa jumla hasa hasa ukizunguka sana utapata tu.yenye bei nafuu
 
hapo maeneo ya kituo cha polisi msimbazi....
hayo maduka yooote kuanzia kwa halima toto hadi ule.mtaa wa pili narung'ombe sijawahi pata duka la.nguo kwa jumla hasa hasa ukizunguka sana utapata tu.yenye bei nafuu
Wauzaji wa k'koo karibia woote ujanja mwingi sasa na ww unatakiwa uwe shap. Nikija me nitakupeleka mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…