Black Walker
Senior Member
- Oct 8, 2018
- 120
- 257
Point yako ina utapiamlo, na wewe unaonekana ni wale wa kuvimba mabega bila kitu, miji haina wenyewe ni suala la muda tu.Mshike adabu !Mmekuja mjini mnajifnya wajanja kuliko wenye miji, rudini kwenu mkalime, si mmetelekeza mashamba ya miwa, kahawa,mawese,ndizi mkayafufue acheni miji ya watu ipendeze.
Hiyo asilimia 90 umeijuaje??Kwa hiyo ni Bora kuwa na Meza ya Chakula ya Kioo halafu mnachokula Ugali wa Mtama na Matembele?
Tunaiga nini yaani kuwe na Maeneo ya NOBLES na Maeneo ya daraja DUNI au sio? Kuchafua Mji!
Kama ndani ya Wamachinga kuna watu wana Mitaji ya 5 Mil na zaidi,mbona hatujaona angalau hata pakifanyika ufuatiliaji wa nani ni yupi na anapata kiasi gani?
Kilichopo ni kufagia tu hakuna Cha mwenye Chungu au Sanduku moja ama Mzigo wa kubeba na Canter.
Tufahamu kuwa Machinga wasio na Uwezo mkubwa kihalali wapo zaidi ya 90%
Umeshawahi kwenda Rwanda mkuu..tuanzie hapoZoezi lisilo na busara hata kidogo kwa machinga
nchi za kiafrika zote zina machinga
Ni kweli mkuu , kilimo cha mboga mboga kinalipa sana, mitaa ya Kihonda Mbuyuni , mbele ya Daraja (Morogoro) vijana vijana wako bize wanapiga bustani za mbogamboga vibaya mnoo na wanamwagilia...soko nje nje na hakuna kubugudhiwa wala kudaiwa kodi wala kukimbizana na migambo wa jiji/manispaa....Ukienda Kahe kule Moshi Vijijini vijana wanapiga maboda ya mpunga, vitunguu, nyanya, hoho na mazagazaga kibao, na maisha yanaenda mtelezo kabisa....Rudini mkalime, msimdharau Samia kwakuwa ni mama, hili halikubaliki.
Hivi wa pale mnazi mmoja wameondoka kwenye ile barabara ya watembea kwa miguu?Hata wasingeunga mkono walipaswa kutekeleza agizo la serikali, sidhani kama viongozi wana nia mbaya na machinga la hasha!
Kinachofanywa ni kuweka mazingira ya miji katika utaratibu wake kwa mujibu wa miongozo ya mipango miji japo bado kasoro zipo nyingi.
Miji ilionekana kuwa michafu muda wote kila mahali, fujo tupu na kuzalisha vibaka, piga picha pale viwanja vya mnazi mmoja yaani ilifikia hatua kupishana ilikuwa shida ni mwendo wa kupigana vikumbo.
Sehemu nyingi zilianza kuwa makazi ya mateja. Mara nyingi unakutana nao wanazurura na kicheni kimoja au betri mbovu kumbe anakula timing ukikosea tu imekula kwako.
Natoa hongera kwa viongozi wetu zoezi hili litapunguza na kuondoa kero hii.
Huyu RC Makala haongei sana, yeye vitendo tuu....Nimepita Msimbazi karibu kabisa na simba sports baunsa ka wa5, na nyundo na high vision vest, wanapiga vibanda na hakuna aliyethubutu kuleta fyoko.
Manzese pamebadilika.
Serikali ipo kumbe!
Everyday is Saturday................................😎
Mkuu wa mkoa nakupongeza ...ilikuwa kila nikipanga safari ya kariakoo naishia mkuki house
Watu walidhani maksihara na walianza kumbeza kuwa hamna mmachinga atakayehama..Huyu RC Makala haongei sana, yeye vitendo tuu....
Ungewapiga tupicha tudogo mkuu...Nimepita Msimbazi karibu kabisa na simba sports baunsa ka wa5, na nyundo na high vision vest, wanapiga vibanda na hakuna aliyethubutu kuleta fyoko.
Manzese pamebadilika.
Serikali ipo kumbe!
Everyday is Saturday................................😎
Sawa,Hiyo asilimia 90 umeijuaje??
Ulifanya utafiti? Kama ulifanya utafiti basi na wao hivyo hivyo walifanya utafiti,
Btw, hapa haangaliwi nani ni nani hapa inaangaliwa uchafuzi wa mazingira, maeneo ya wazi ni mengi sana mbona Minada watu hua wanaifata? Basi ujue hata na wao wakipelekwa sehemu bado watafatwa tu,
Machinga must Go.
Tuna Ubunifu wa kiwango Cha chini sanaUonevu tu. Ajira hamna, hawatengenezi mazingira bora ya uwekezaji. Kwenye keki ya taifa wanaifuja kwa matumizi mabaya, huku nchi ni maskini balaa.
Ni maslow hieranchy of needs sio highlankWe jamaa graduate ndio kipimo cha ubinadamu ?
Kila kitu reference ni graduatuate, hatuwezi jadili jambo kuzingatia misingi ya ubinadamu?
Mbona kwenye human right, basic need, maslow highlack of need hawajajaduli kwa misingi ya graduate. Hicho kipaumbele cha graduate kinatoka wapi, mnajipa ukuu na daraja ambalo hata walionzisha elimu hawana.
Jadili katika misingi ya utu wa mwanadamu awe mtoto mkubwa,mzee, kinana,mwanamke mwanaume, mzungu,mweusu,mwarabu au mchina wite ni sawa na wanamahitaji sawa.
Vibaka wakiongezeka hiyo Nia Njema Ina manufaa ya akina nani? Au wewe unapata faida ipi?Pamoja na Nia njema kabisa iliyonayo Serikali yetu., wasiwasi wetu ni kuongezeka kwa vibaka mitaani.
Unajaribu kuandika propaganda zako za kiswahili.Wanabomoa vibanda vyenu wanaweka vibanda vyao. Mtetezi wenu ndio kashaondoka pambaneni na Hali zenu. Wajanja wameangalia wamejua mnapiga hela maeneo fulani fulani. Wametafuta njia ya kuingia hapo na ndio hio kwamba vibanda vyenu vichafu havifai kuwa hapo ILA vibanda vyao visafi ndio vinastahili! Wewe mlalahoi kibanda chako peleka kijijini kwenu huku tunataka vibanda vya akini tipisi, fishifishi na wajanja wengine wa mjini