BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote Bungeni baada ya kukwama mara mbili, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya Serikali kutakiwa kueleza chanzo cha Fedha zitakazoendesha Bima ya Afya kwa Wote, Wizara ya Fedha imeridhia kuhamisha baadhi ya Kodi na Tozo kwenda kwenye mfuko huo.

Baadi ya Kodi ni pamoja na Kodi ya Magari, Vinywaji vya Bicarbonate, Vinywaji Vikali na Tozo za Miamala itaingia moja kwa moja katika kugharamia huduma za Bima.
 
Attachments

  • MAELEZO YA MHESHIMIWA UMMY ALLY MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA AKIWASILISHA MUSWADA WA KUTUNGA S...pdf
    242.8 KB · Views: 9
Akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote Bungeni baada ya kukwama mara mbili, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya Serikali kutakiwa kueleza chanzo cha Fedha zitakazoendesha Bima ya Afya kwa Wote, Wizara ya Fedha imeridhia kuhamisha baadhi ya Kodi na Tozo kwenda kwenye mfuko huo.

Baadi ya Kodi ni pamoja na Kodi ya Magari, Vinywaji vya Bicarbonate, Vinywaji Vikali na Tozo za Miamala itaingia moja kwa moja katika kugharamia huduma za Bima.
Mpaka hapo Kodi ya miamala imegeuzwa kuwa chanzo rasmi Cha Kodi
 
Akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote Bungeni baada ya kukwama mara mbili, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya Serikali kutakiwa kueleza chanzo cha Fedha zitakazoendesha Bima ya Afya kwa Wote, Wizara ya Fedha imeridhia kuhamisha baadhi ya Kodi na Tozo kwenda kwenye mfuko huo.

Baadi ya Kodi ni pamoja na Kodi ya Magari, Vinywaji vya Bicarbonate, Vinywaji Vikali na Tozo za Miamala itaingia moja kwa moja katika kugharamia huduma za Bima.
Utapeli mwingine huo!!😂😂🤣
 
Ujinga tu( kutokujua mbinu sahihi), watu sijui lini watajifunza kubeba majukumu yao.

Ni ujamaa na kujitegemea, KUJITEGEMEA. Sio utegemezi wa kodi za wengine ndio zikatatue matatizo binafsi ya watu.

Kodi zijenge vitu vya jamii kiujumla wake. Kama mahospitali na mabarabara na mawasiliano. Sio kulipia bili binafsi za matatizo binafsi ya watu.

Mtakaobisha naomba niwakumbusje kuwa kikanuni (in principle) HAKI ndio huinua taifa, endeleeni kujidanganya kuwa HURUMA zitaliinua taifa. Hurumahuruma zikizidi zitalididimiza zaidi taifa zaidi. Tafuneni si mna akili.
 
Bima ya afya kwa watu maskini wasokua na uzazi wa mpango wasopata mlo kamili
Apo ni kuongeza tu umaskin sabu wajinga watazaa sana wakiamin matibabu ni bure
Lakin pia huwezi kuweka bima ya afya kwa watu ambao mfumo wao wa maisha bado ni duni
Malazi duni
Makazi duni
Matibabu duni
Mavazi duni
Tuboreshe kwanza maisha ya wananchi kabla ya bima ya buree lasivyo iyo bima haito dumu serikal itaingia hasara ndan ya mda mfupi iyo bima haitakua na maana yyte
 
Ukweli ni kwamba ni njia tu ya kukusanya kodi maana kila mtu itampasa kuwa nayo ila huduma zitakazotolewa utasikia watu wanalalamika. Kwa maisha ya mtanzania na umasikini huu haiwezi kusaidia
 
Ila serikali ya CCM inafanya machukizo hadharani ikijua kuwa watanzania ni wapole. Walitoa fao la kujito na kuweka fao la wenzi wa Viongozi. Sasa wanaleta bima ya Afya kwa wote ili kila mtu achangie serikali ipate mapato. Tanzania bado haijafikia huko.
 
Moja ya athari za kodi ni kushusha mauzo, hapa miamala ndo kwanza inaanza kuimarika mnaweka tozo, mpesa zianze tena kudoda, hivi mnaposema vinywaji vikali ni hannes johnwalker? Mnaongelea gokozuna na ambiance? Sikuhizi mtu anapimiwa nyaji ya jero kwenye mfuko wa nailoni tena tupachike kodi?
 
Akiwasilisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote Bungeni baada ya kukwama mara mbili, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema baada ya Serikali kutakiwa kueleza chanzo cha Fedha zitakazoendesha Bima ya Afya kwa Wote, Wizara ya Fedha imeridhia kuhamisha baadhi ya Kodi na Tozo kwenda kwenye mfuko huo.
Bima ya afya iko hoi bin taabani, wanaoifilisi ni maboss wa huo mfuko
 
Back
Top Bottom