Rais Samia aidhinisha Muswada wa Bima ya Afya kwa Wote, sasa ni Sheria rasmi

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Najinasibu kwa kuwa consistent on issues!

Kwa muda mrefu nimeulizia na kushawishi juu ya uwepo wa sheria ya bima ya afya kwa wote ...ikiwa ni mbinu ya kistratejia kufikia uhuru wa kweli na kujitegemea katika maswala yahusuyo afya.

Mchakato huu ni mrefu sana na uligubikwa na vikwazo vingi sana.kutoka ndani na nje ya nchi.

Hatimaye umekamilika hapa sasa ndipo naweka matumaini ya kuwa na afya endelevu kwa wote.

Bima.png


---
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametia saini muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na sasa imekua sheria kamili.

Novemba 2, 2023 Bunge lilipitisha muswada huo kwa asilimia 100 na kuweka historia, baada ya mkwamo uliokuwepo kwa takribani miaka mitano tangu ulipofufuliwa upya mwaka 2018.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya jana Desemba 4, 2023 imesema muswada huo sasa umeshasainiwa na Rais na kuwa sheria kamili, baada ya kutangazwa kwenye gazeti la Serikali Desemba Mosi, 2023.

Saini ya Rais katika sheria hiyo, inaipa kazi Wizara ya Afya kuanza utungaji wa kanuni kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa sheria hiyo, ambayo itawezesha kila Mtanzania kupata huduma za afya pasipo na kikwazo cha kiuchumi.

Katika kufanikisha hayo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na masuala ya Ukimwi iliweka msisitizo wa umuhimu wa kuwa na mfuko kwa ajili ya kugharamia bima ya afya kwa watu wasio na uwezo, na Serikali iusimamie kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya.

Kupitia sheria hiyo kutakuwa na utaratibu wa utambuzi na usajili wa kundi la watu wasio na uwezo, kwa lengo la kuhakikisha wanapata huduma za afya bila kikwazo cha fedha.

Kundi hilo litajumuishwa kwenye skimu ya Bima ya Afya ya Umma kwa namna itakavyoainishwa kwenye kanuni zitakazotungwa hapo baadaye, huku akibainisha vyanzo vya mapato vitakavyotumika kugharamia skimu hiyo.

Akiusoma muswada huo bungeni kwa mara ya mwisho, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vyanzo vya mapato ya skimu hiyo ni pamoja na sehemu ya mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa.

"Kwenye vinywaji vyenye kaboni, vinywaji vikali, bidhaa za vipodozi, kodi ya michezo ya kubahatisha, ada ya bima za vyombo vya moto na mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki " alisema Waziri Ummy.

Aliuhakikishia umma juu ya huduma za matibabu kwa kundi la wananchi wasio na uwezo.
 

Attachments

  • Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.pdf
    461.1 KB · Views: 17
Sijasoma doc uliyo attach vp watoto chini ya miaka mitano wamekumbukwa bima ya afya inayojitegemea siyo kama dependant?
Maana dependants mwisho ilikuwa watu wanne what if mtu kamuweka mzazi na watoto watatu watakuwa wametimia wanne je kama alipata mtoto wa tano itakuwaje kabla hajafikisha umri wa kuanza shule atumie bima ya watoto inayopitia mashuleni?
 
Kijijini mtu maskini mkulima hiyo kilimo Cha kujikimu au mtembeza Au kondakta wa daladala au dereva au muuza Genge au mama nitilie bima ya afya anachangia shilingi ngapi?
ipo accomadated kwenye hii sheria...isome
 
Sijasoma doc uliyo attach vp watoto chini ya miaka mitano wamekumbukwa bima ya afya inayojitegemea siyo kama dependant?
Maana dependants mwisho ilikuwa watu wanne what if mtu kamuweka mzazi na watoto watatu watakuwa wametimia wanne je kama alipata mtoto wa tano itakuwaje kabla hajafikisha umri wa kuanza shule atumie bima ya watoto inayopitia mashuleni?
Isome hii sheria vizuri.bottom line ni kuwa kila mtanzania lazima awe insured kwenye afya
 
Isome hii sheria vizuri.bottom line ni kuwa kila mtanzania lazima awe insured kwenye afya
Hapa ungezungumzia mambo ya msingi yanayo msibu mtz wa kawaida ni sii wenye bima za kitibiwa us,ulaya,India na kwingineko duniani,ungeeleweka kama ungesema manufaa kwa mlala hoi ni yapi,inampunguziaje mashaka ya kufa kwa kukosa uwezo wa kupata tiba,na tofauti leo imekuwaje,je vipi wale tegemezi wa watumishi ambao wamekuwa wakinyimwa haki za msingi za tiba,au unafuu watakao upata katika utaratibu mpya.Ama ni kichaka kipya cha wanasiihasa ili wavuke salama,kipindi cha uchafuzi tuu🤣
 
Back
Top Bottom