Wadau poleni kwa kazi. Nikienda kwenye hoja ya msingi, Ijumaa iliyopita bungeni, Mbunge wa Gairo kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Ahmed Shabiby akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2024/2025, aliiomba serikali kuweka tozo ya Shilingi 2,000 kwa mwezi katika mitandao ya simu sambamba na mazao ili kuisaidia NHIF kuendelea kujiendesha na kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Mheshimiwa Shabiby alisema hatua hiyo itakuwa mkombozi kwa mfuko huo ili kuondoa malalamiko ya mara kwa mara.
Alisema: “Kwa hili wanaweza kulikubali au wasilikubali wengine watatukana kwenye mitandao, lakini acha watukane maana kuna watu hawapo duniani na hata mbinguni hawako. Lakini siwezi kuogopa kwa sababu mtu atatukana.
Akaendelea kusema: “Ili kuinusuru Bima ya Afya kuna umuhimu wa kuwapo chanzo ambacho kitakuwa cha uhakika katika kuchangia mfuko huo kwani wananchi wameshindwa kuchangia Shilingi 30,000 kwa ajili ya Bima ya CHF na hivi hatujajua hiyo bima kwa wote itakuwa na kiwango kipi."
Mheshimiwa Shabiby alisema ikipangwa Shilingi 300,000 na Sh.60,000 kwa matibabu ya kawaida wananchi wa vijijini kuimudu itakuwa vigumu, hivyo kushindwa kufanya kazi kwa ufanisi kama inavyohitajika, hivyo ni wakati wa wananchi kujionea huruma ili kuokoa mfuko huo.
Alisema: “Ukiangalia katika mipango ni kutaka kuwachangisha wananchi lakini namna ya kupata hii fedha itakuwa vigumu kama ilivyokuwa kwa CHF na leo hii ukiangalia wanufaika wa bima katika watanzania 100 ni watu wanane tu ambao wanalipa.
Akaongeza: “Hii inaonesha hatuna chanzo maalum cha kuchangia mfuko huu kwa kusaidia watu wasiyokuwa na uwezo wapate matibabu."
Alitaja njia za kupata chanzo hicho cha uhakika kuwa ni pamoja na kuweka tozo katika mitandao ya simu ambayo inatumiwa sana nchini.
Alisema Tanzania kuna wastani wa laini zaidi ya milioni 72. Alisema ikiwekwa tozo ya Shilingi 2,000 kwa mwezi, kwa mwaka itakuwa Sh. 24,000 sawa na Shilingi trilioni 1.728 kwa idadi ya laini hizo zote.
Mbunge huyo alishauri pia watumiaji wa mitandao hiyo wenye hadhi kama vile wabunge, wafanyabiashara, wafanyakazi kiwango kiongezwe hadi Sh.10,000 au 15,000 na kuunganishwa na kupatikana zaidi ya Shilingi trilioni mbili.
“Pamoja na kuwapo kwa kiwango hicho, wananchi wa vijijini wasiwekewe ukomo wa matibabu kutokana na kuwa na kipato kidogo ambapo wamekuwa wakikosa matibabu na dawa za muhimu,” alisema.
Shabiby alisema viwango vingine vitafutwe hata kwenye mazao ambako kila kilogramu moja itatozwa Shilingi moja au mbili kwa kuwa hata mkulima atanufaika na bima hiyo.
“Sasa kwa wale ambao hawana simu, hiyo inadhihilisha kuwa ni maskini wa kutupwa, hivyo hata hicho kiasi kidogo wasitozwe, atatibiwa kutokana na vyanzo hivyo vya mifuko,” alisisitiza.
KILICHOTOKEA BAADA YA USHAURI
Baada ya mchango huo kurushwa mitandaoni na vyombo vingine vya habari kuandika, kumekuwa na makundi.
Baadhi ya watu wamenpongeza Shabiby kuwa ushauri wake umelenga kuwasaidia Watanzania wa kipato cha chini.
Wengine walisema ushauri wake ulilenga kuwakandamiza Watanzania kwa kuzalisha tozo nyingine tena kupitia simu.
Hadi leo nilikuwa napitia mitazamo ya watu mbalimbali, kila mtu na mtazamano wake. Lakini nimeona wengi wamemuunga mkono.
JOHN HECHE ANACHOONA
Aliyekuwa Mbunge wa Tarime (Chadema), John Wegese Heche yeye aliibuka na kusema Shabiby amejiangalia yeye amimaanisha kuwa, kwa sababu ana uwezo wa kulipa hiyo 2,000 kwa mwezi.
Akatoa mfano kwamba, serikali yenyewe ina matumizi mabaya/ makubwa katika matumizi yake ambayo pengine yangepunguzwa pesa nyingine ingeelekezwa kwenye MFuko wa Afya.
MAWAZO WANGU
nimejaribu kuwaza kwa kiwango changu nikagundua kuwa, hoja ya John Heche siyo hoja ya Mbunge Shabiby.
Hoja ya Heche inajitegemea, hoja ya Shabiby inahusu ni kwa jinsi gani serikali itaweza kutafuta vyanzo vingine ili kuunusuru Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
Kama wengi tunakumbuka, bunge letu limepitisha sheria ya Bima ya Afya kwa wote. Maana yake kila mwananchi atatakiwa kukata.
Wazee wa zamani wanakumbuka ile Kodi ya Kichwa. Ilikuwa ni lazima kila kichwa iwe nayo.
Hii Bima ya Afya nayo ni lazima kila familia ikate. Kama itakuwa Shilingi 60,000 bika ndogo au Shilingi 300,000 kubwa, lakini lazima ikatwe.
Alichoongea Shabiby ni kwamba, ili kuwasaidia wananchi wa kipato cha chini, basi njia mojawapo ya kuunemesha mfuko huo ni kila mwenye laini ya simu kuchangia Shilingi 2,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na 24,000 kwa mwaka.
Ukiidadavua hiyo 2,000 kwa mwezi ni sawa na shilingi 64.5 kwa siku. Ambapo kwa mwaka ndiyo inakuja 24,000 kwa mwaka.
Tukumbuke hapa nazungumzia afya zetu jamani. Siyo kwamba hizi pesa zitaenda kujengea madaraja. Siyo kwamba zitakwenda kununulia ndege. Ni kwa ajili ya afya zetu.
Kama umekuwa ukifika hospitali mara kwa mara, utakuta watu wanaumwa. Dawa wanazoandikiwa zinatakiwa pesa nyingi. Na kundi kubwa la Watanzania hawana kipato cha uhakika.
NISIMSHIKIE AKILI MTU
Naomba niseme kuwa, sina sababu ya kushawishi kundi moja lifuate lingine. Simshikii mtu akili. Lakini kila mmoja ajaribu kufikiri kwa kina kwamba ushauri wa Ahmed Shabiby na hoja ya John Heche ipi inamsaidia mwananchi wa kipato cha chini?
IKUMBUKWE HII
Mapema mwaka huu, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha rasmi muswaada wa sheria ya Bima ya Afya kwa Wote.
Aidha, sheria hiyo imeweka bayana kuhusu upatikanaji wa bima za afya kwa watu wasiojiweza kuwa kuna baadhi ya vyanzo ambavyo vitachangia katika ulipaji wa bima hizo.
Vyanzo hivyo vilitajwa kuwa ni mapato yatokanayo na ushuru wa miamala ya kielektroniki, mapato yatokanayo na ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji vyenye kaboni (carbonated drinks), vinywaji vikali (liqour), bidhaa za vipodozi (cosmetics product), michezo ya kubahatisha na ada ya vyombo vya moto kwa kadiri itakavyopendekezwa.