tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 21,859
- 18,282
Naingia kwenye mada moja kwa moja sitaki kuwachosha. Mnakumbuka vizuri madhila yaliyotupata watanzania mwaka jana wakati serikali ilipoongezeka tozo za miamala maradufu hivyo kufanya maisha ya watanzania kuwa magumu maradufu. Kana kwamba hiyo haitoshi waziri wa fedha msomi, Mwigulu Nchemba aliwakejeli watanzania kwa kusema kuwa kodi lazima zikatwe haijalishi watanzania wanaumia kiasi gani na kwamba asiyetaka kukamuliwa tozo ahamie Burundi.
Suala hili liliwauma sana watanzania lakini kwa kuwa hawana pa kukimbilia wameendelea kubakia hapa nchini na wanakamuliwa ‘kodi ya kizalendo’ kweli kweli. Kinachoudhi zaidi ni kwamba wabunge wa CCM wanaofanya haya maamuzi, hawalipi kodi, hivyo hawahusiki na kodi hizi za kizalendo kwa kuwa wao sio wazalendo bali wananchi masikini ndio wazalendo kindakindaki.
Wakati vumbi la kodi ya uzalendo halijatua, Rais Samia amerejea nchini kwa dharula kuja kusaini muswada wa bima ya afya. Baadhi ya watanzania mbumbumbu wasiojua kitu na wasiokuwa na chembe ya ufahamu wa mambo, hasa chawa wa mama, wamesikika wakishangilia kitendo hiki alichofanya Rais kama mazuzu. Wasichokifahamu ni kwamba fedha zitakazotumika kugharamia matibabu ya bima ya afya kwa wote zitatokana na ongezeko la tozo litakaloingizwa tena kwenye miamala ya kieletroniki.
Wakati muswada ulipopitishwa bungeni kwa 100% na wabunge wa CCM, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alisema moja ya vya mapato ya kugharamia matibabu haya kwa watanzania masikini ni ongezeko jipya la tozo za miamala. Sote tunafahamu kuwa miamala haibagui. Haimjui tajiri wala masikini. Inakata kotekote. Haohao masikini ambao serikali ya CCM inajidai kuwahurumia ndio hao hao watakaobebeshwa mzigo wa tozo ili kugharamia matibabu yao wenyewe. Sasa hapa unafuu upo wapi? Ikiwa wanajinasibu kuwa wanawajali masikini mbona wanawakamua tena masikini kupata fedha za kuwahudumia masikini ‘bila malipo’?
Ni mwendawzimu pekee atakayefurahia ujio wa sheria ya bima ya afya kwa wote. Tukumbuke bima ya afya ya sasa haikamui watu wasiohusika. Naomba tuelewane vizuri hapa. Mfuko wa NHIF unatunishwa kutokana na michango ya wanachama tu. Hauwagusi wasiokuwa wanachama. Lakini bima ya afya kwa wote itawagusa wote……waliomo na wasiokuwamo. Huu ni zaidi uzezeta.
Na tukumbuke kwamba sio watanzania wote wanaotegemea bima ya NHIF. Wengine wamo kwenye bima nyingine kama vile AAR, Strategies, Momentum, nk. Sasa kitakachotokea ni kwamba hata kama mtu unatibiwa kwa bima ya AAR ambako michango yako inaingia, utalazimika tena kukatwa pesa zaidi ili ziende kuhudumia wanachama wa NHIF. Maana yake ni kwamba utalazimika kujilipia bima yako ya AAR huku ukijiandaa kukamuliwa fedha zaidi ziende zikawalipie watu wengine kwenye bima nyingine ya afya isiyokuhusu ndewe wala sikio.
Watanzania tunakamuliwa mno!
Viongozi wa nchi hii wamekosa ubunifu. Wanajiendea tu kama vipepeo wasiokuwa na dira wala muelekeo. Nchi ingekuwa na watu wanaofikiri sawasawa, wasingekuja na hoja ya kutaka kuwakamua wananchi zaidi wakati wananchi hao hao wanaendelea kukamuliwa kodi ya kizalendo isiyokuwa na kichwa wala miguu. Haya ndiyo matokeo ya kutawaliwa na watu wasiokuwa na dira wala muelekeo. Wanapuyanga tu bora liende.
Nawasilisha.