Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,129
- 35,148
Muswada wa Bima ya afya kwa wote ulifanikiwa kupitishwa bungeni mwezi uliopita, na tayari umetiwa saini na Rais wa Tanzania kuwa sheria rasmi, hivyo mchakato wa kutengeneza kanuni na taratibu za ufanyaji kazi kabla ya kuanza kutekelezwa umeanza rasmi.
Bahati mbaya sana watu wengi hawajui mifumo ya bima namna inavyofanya kazi, wengi wanadhani kupitia sheria hii watu wote watapatiwa bure Bima ya Afya (NHIF!) na kuneemeka na huduma zote za Afya popote pale hapa Tanzania bureeeee! Wakati hali ni tofauti kabisa. Kwa kifupi sana hakuna cha bure, kila mtanzania atapaswa kuchangia (direct&indirect) ili kuwezesha kila mtanzania anapewa huduma za afya.
Kwanini ninasema huenda kupitia hii sheria, afya za watanzania zikaishia kaburini, hizi ni sababu za msingi;
1. Mifuko yote ya bima za Afya iliyoanzishwa na kusimamiwa na serikali imeishia kulega lega au kufa!. Kwa mfano, serikali ilianzisha bima ya afya jamii (CHF) ikafa kabla ya kufikia hata robo ya malengo yake, ikaja na bima ya afya iliyoboreshwa (iCHF) kwa maeneo mengi imeshakufa na maeneo machache ambapo bado inafanya kazi iko mahututi. Pia serikali inasimamia Bima ya taifa (NHIF) ambayo kwa sehemu iko hoi (huduma nyingi zimeondolewa, vikwazo vya kujiunga ni vingi, uhuru wa kujitoa kwa wafanyakazi haupo, ufisadi unatisha, imekaa kibaguzi, haieleweki, hasara, hasara, hasara tupu) kiasi cha kushindwa kufikia mategemeo ya wanachama wake.
2. Ufahamu, mtizamo, mategemeo na desturi ya watanzania wengi kuhusu Bima au Bima ya afya ni duni. Kwa mfano, watanzania wengi wanawaza haya;
-Bima ya afya ipo kumtibu akiugua tu. Yaani atataka (atalipa) kuwa na Bima ya afya wakati anaumwa/kujihisi kuumwa tu, ili Bima ya afya itumike kulipa gharama ambazo angelipishwa hospitali kwa wakati huo.
-Bima ya Afya atagharamia huduma zote za matibabu yake.
-Bima ya Afya itawezesha kuwepo kwa huduma zote za matibabu kwenye kituo cha afya ambacho yeye atafika kupatiwa huduma.
-Bima ya afya itatumika kwenye hospitali zote (umma na binafsi), hivyo itampa uhuru kufika hospitali yoyote kupatiwa huduma.
3. Hakuna kiongozi yoyote wa serikali anayejua au aliyeweza kueleza kwa ufasaha na kueleweka na watoa/watumishi wa afya namna bima ya afya kwa wote atafanyakazi kiasi cha kuwa sawa, kupita au kutatua changamoto za bima za afya zilizokuwepo au zilizopo sasa. Bado ni fumbo gumu.
4. Kupitia sheria hii itapaswa mifuko iliyopo sasa ya Bima ya afya iliyopo chini ya serikali (CHF, iCHF, NHIF) kufa rasmi(kumezwa), kuunganishwa (kuwa chini ya mwamvuli mmoja) au kuongezewa majukukumu makubwa zaidi. Hii ni sintofahamu kubwa.
5. Zipo dalili, taarifa na viashiria vya wazi kuwa, kupitia sheria hii serikali itakuwa imejiondoa kugharamia moja kwa moja matibabu ya wananchi wake na kulikabidhi jukumu hilo kwa mifuko ya Bima ya afya itakayoanzishwa. Jambo hilo kama litatokea ni hatari kubwa sana kwa wananchi wa vijijini, wenye vipato duni na wanatoka katika mazingira magumu.
MUDA NI MWALIMU MZURI, NGOJA TUSUBIRI KUONA.