Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
Yesu/Isa hana baba mimba yake imeingia Kwa uwezo wa Mungu

Na ndio maana hapa anasema Baba yake ndio baba yetu ambaye ni Mungu na Mungu wake ndio Mungu wetu kama hauliamini hili andiko sema

Yohana 20:17
Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu

Kuhusu Alikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo hapo shida ni umbumbu wenu kuhusu maandiko ya Mungu roho zote Mungu aliziumba siku Moja hata wewe roho yako ilikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo hata binaadam watakao zawaliwa miaka laki Moja ijayo roho zao zipo Kwa Mungu ila mda wao wa kuja duniani ndio bado haujafika
Bwana yesu Kristo NI MUNGU kasome isaya 9:6
 
Quran imeandikwa na watu na uandishi wake ulikuwa na makosa mengi sana. Tukisema tuamgalie usahihi wa kihistoria,kisayansi na kinabii hakuna mtu atakayebisha usahihi wa Bible na upungufu wa Quran.

Kwa maana hiyo basi kama Biblia zaidi ya mara 100 inamtaja Yesu kama Mungu hakuna namna huyu jamaa asiwe Mungu. Na hata hiyo Quran sometimes inajicontradict na kumtambua Yesu kama Mungu,iko hivyo unless tukubaliane na mtoa mada kuwa Issa sio Yesu Kristu.
Labda kwa kukusaidia kama hujui,Quruani imekuja kuisahihisha Biblia, Wakati biblia imeandikwa kwa stairi ya kukusanya hadithi kwa stairi ya kusimuliana kutoka kizazi kilichokuwa hakijui kuandika mpaka kizazi kilichojua kuandi maana yake imepita kwa watu wengi,

Lakini Quruani imeteremshwa kwa mtu mmoja tu, Yaani kutoka kwa Mungu kupitia kwa Malaika jibrir au Gabriel mpaka kwa mtume Muhammad (S.A.W) na Mungu ameahidi kukilinda kitabu chake maana yake hamna wa kukichakachua, ndiyo maana Quruani lazima kwanza iandikwe kwenye Lugha yake ya kiarabu ndiyo iende kwenye lugha zingine.


Na hata tunaposali Dunia nzima tunasali kwa lugha moja yaani ukiwa China au Marekani mpaka Tanzania Adhana ni ileile ya kipindi cha Mtume Muhammad (S.A.W) na stairi ya kuswali vitendo na maneno ni yaleyale ya miaka 1440 iliyopita, je wewe unachoabudu leo kwa vitendo na maneno ndiyo alichofanya Yesu?
 
Tukuelewe vipi? Mara Yesu siyo Isana mara Yesu ni Isa
Haujanielewa Kwa sababu Kuna comments zangu haujasoma

Soma hapo utaelewa nilicho amanisha

Katika bibilia Kuna Yesu wawili

1) YESU AMBAYE NDIO ISA

UTABIRI WA MANABII KUHUSU UJIO WA YESU/ ISA

Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

YESU / ISA ANATHIBITISHA UTABIRI UMETIMIA

Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

NABII MUHAMMAD KUPITIA QURAN ANAPIGILIA MSUMARI KUWA YESU / ISA ALITUMWA NA MUNGU KAMA MTUME KWA WANA WA ISRAEL

Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad!

2) YESU AMBAYE SIO ISA ILA NI GALASA LILILOTENGENEZWA NA PAULO NA NDIO YESU WA WAKRISTO

Tito 2:13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu


Manabii 3 wa Mungu maelezo Yao yanafana kuhusu Yesu/Isa

Huyo Yesu wa Paulo ndio wenu na hilo ni GALASA ambalo halijawahi kuwepo hapa duniani
 
Sasa sijui ulichojibu ni nini?kiukweli wakristo wengi elimu yao ya kujua mambo ya Dini ni ndogo sana,ndiyo maana wanadanganywa kirahisi na kubaki kuamini miujiza
Nilichokujibu Mimi NI kwamba Yesu Kristo ni MUNGU. Na andiko nimekupa, ukitaka elimu sasa ndo uwende kwenye ulimwengu ambapo kunapatikana elimu. Ila yesu Kristo NI MUNGU na inabaki kua hivyo
 
Umenena ila woote hao kama unavotaka kuwatenganisha hakuna kati yao aliewahi sema kwa mdomo wake sio mtu amsemee,mimi ni Mungu mniabudie.
Luka 20:41-47 BHN

Yesu akawauliza, “Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’ Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?”
 
Haujanielewa Kwa sababu Kuna comments zangu haujasoma

Soma hapo utaelewa nilicho amanisha

Katika bibilia Kuna Yesu wawili

1) YESU AMBAYE NDIO ISA

UTABIRI WA MANABII KUHUSU UJIO WA YESU/ ISA

Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.

YESU / ISA ANATHIBITISHA UTABIRI UMETIMIA

Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.

Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.

NABII MUHAMMAD KUPITIA QURAN ANAPIGILIA MSUMARI KUWA YESU / ISA ALITUMWA NA MUNGU KAMA MTUME KWA WANA WA ISRAEL

Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad!

2) YESU AMBAYE SIO ISA ILA NI GALASA LILILOTENGENEZWA NA PAULO NA NDIO YESU WA WAKRISTO

Tito 2:13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu


Manabii 3 wa Mungu maelezo Yao yanafana kuhusu Yesu/Isa

Huyo Yesu wa Paulo ndio wenu na hilo ni GALASA ambalo halijawahi kuwepo hapa duniani
Umemaliza mjadala.Umefafanua vizuri.
 
Kwani Mariamu alikuwa na dini gani ?? na haruni alikuwa na dini gani ?? tuanzie hapa
Mariamu alikuwa MYAHUDI wa kabila la Yuda.
Haruni alikuwa Mwebrania wa kabila la Lawi, Kuhani Mkuu, enzi za Haruni na Musa , Wana wa Israeli walitambuliwa kama Hebrews(WAEBRANIA) ila nyakati za Yesu , wale makabila ya Yuda na Benyamini walitambuliwa kama Wayahudi Ili kuwatofautisha na WASAMARIA waliokuwa na mchanganyiko wa damu ya WAEBRANIA na watu wa mataifa mengine.
 
Mtanziko!!.. abracadabra siyo!!..yeah,ndo Imani yenu ilivyo,ukiichimba kidogo tu sharti upate kizunguzungu..ndiyo maana wazungu wameachana na dini wanasema hakuna Mungu maana vitu havieleweki...endelea kujificha kwenye hicho kichaka ulichoamua kujificha badala ya kujibu hoja
Kosa langu ni nini wakati we umequote Biblia ikisema Yesu akilia msalabani ?
Kama ingekuwa Imani ya hovyo mngeacha kuquote kutoka kwenye Biblia mkastick na Qur'an tu.
Maana Yesu wa ndani ya Biblia ni tofauti na Isa so hamna Mamlaka ya KUMFANANISHA Wala kutumia Biblia kama reference ya KUMFANANISHA.
 
Issa aliweza kujiokoa asiuliwe msalabani,baada ya kumuomba Mungu wake,hawakumsulubu:,wala hawakumuua,alipaa akaenda mbinguni.Hakufa,mpaka leo yuko hai.
Yesu alikamatwa,akadhihakiwa,akapigwa,akasulubiwa,akauliwa,akazikwa,alimuomba Mungu wake amuepushe na kikombe hiki,lakini hakujibiwa maombi yake.Na mwanafunzi wake,aliyemsaliti,Yuda Iskariote,mpaka tunamwita msaliti,kwa kupewa vipande vya fedha,huyu alitakiwa asifiwe,kwa kutusaidiasisi, kukombelewa na kusamehewa dhambi zetu,kwa kufanikisha kusulubiwa kwa Yesu.
 
Labda nikuulize swali moja dogo sana,hata mtoto wa chekechea anaweza kujibu, kama Yesu ni Mungu, je Mama yake bikira Maria wakati akiwa mdogo alikuwa anamuitaje?

Na kama Yesu akiwa ni mwana wa Mungu, je bikira Maria Mungu atamuitaje? Ni hayo machache tu, ukishinndwa kujibu muombe mwanao akusaidie
Mm nakujibu hivi

Luka 20:41-47 BHN

Yesu akawauliza, “

Yasemekanaje kwamba Kristo ni mwana wa Daudi? Daudi mwenyewe anasema katika Zaburi: ‘Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia mpaka niwaweke maadui zako kuwa kiti cha kuwekea miguu yako.’ Ikiwa Daudi anamwita yeye, ‘Bwana,’ basi, atakuwaje mwanawe?” Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote, “
 
Kosa langu ni nini wakati we umequote Biblia ikisema Yesu akilia msalabani ?
Kama ingekuwa Imani ya hovyo mngeacha kuquote kutoka kwenye Biblia mkastick na Qur'an tu.
Maana Yesu wa ndani ya Biblia ni tofauti na Isa so hamna Mamlaka ya KUMFANANISHA Wala kutumia Biblia kama reference ya KUMFANANISHA.
Issa hakusulubiwa,hakuuliwa,hakudhihakiwa,hakufa,hakuzikwa,alipaa kwenda mbinguni,:yupo hai.Alimuomba Mungu wake,wasimuuwe,wale wsbaya wake,mmoja akafananishwa na Issa,ndio wakamsulubu.
Yesu alikamatwa,akadhihakiwa,akasulubiwa,akauliwa,akazikwa,alimuomba Mungu wake,kikombe hiki kimuepuke,lakini hakujibiwa maombi yake.Na aliyefanikisha haya,Yuda Iskariote,twamwita msaliti,kwa kupewa vipande vya fedha,wakati katenda jambo jema,la ukombozi na kusamehewa dhambi zetu.
 
Kuhusu Alikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo hapo shida ni umbumbu wenu kuhusu maandiko ya Mungu roho zote Mungu aliziumba siku Moja hata wewe roho yako ilikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo hata binaadam watakao zawaliwa miaka laki Moja ijayo roho zao zipo Kwa Mungu ila mda wao wa kuja duniani ndio bado haujafika[/B]
Weka andiko linalosema tulikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo
 
JINA LA ISA MAANA YAKE NINI?Katika Qurani yenye jumla ya juzuu 30; Surah 114; aya 6236; maneno yenye kutamkia 76,440; herufi 322,373; jina Isa linatamkwa lisa au Aysi limetajwa mara 25. Isa pia ameitwa masihi mara 93. Lakini tunaposoma Qurani iliofarsiriwa/tafsiriwa na Imam Baidawi Vol 1 Ukurasa 160 ameeleza kuwa Isa jina la Kiarabu maana yake ni Wekundu unaozidiana na weupe. Hii ndio maana ya Jina la Isa wa Quran. Je, Yesu wa Biblia maana yake nini?



JINA LA YESU MAANA YAKE NINI?JINA Yesu linatokana na lugha ya Kiebrania ‘Yehoshua’ katika lugha ya Kigiriki wanasema ‘lesous’ inatamka ‘Yesous’ yaani Yesu. Katika lugha ya Kiarabu wanasema ‘Yasu’, kwa kiingereza ni “Jesus” maana yake ‘Bwana anaokoa au Bwana ni Mwokozi’ Isaya 43:6, 10-11.

Katika Biblia ambayo ina jumla ya Sura 1189; aya 31,102; vitabu 66 – Agano la kale vitabu 39 na agano Jipya vitabu 27; Neno Mwokozi kwa Kiingereza wanasema ‘Saviour’ limetajwa mara 55. Ikumbukwe kwamba katika agano jiypa jina Yesu au Yehoshua (kwa Kiebrania) limetajwa mara 1275 katika aya zipatazo 1226.



Zingatia pia kuwa agano jipya lina jumla ya aya 7930 na sura 260 hivyo hapa tunaona jina Yesu maana yake ni Mwokozi na jina Isa ni wekundu uliozidiana na weupe. Kwa kuwa maana ya haya majina tofauti bila shaka Isa sio Bwana Yesu.
 
Back
Top Bottom