Haajar hakuwa mwanamke wa mtaani bali alikuwa kijakazi wake na sarah ndiye aliyemwambia amuoe ili wapate mtoto kutokana na yeye kuzeeka, ibrahim alayhi ssalaam ni mtume kamwe watu hawa hawafanyi makosa makubwa ya kutia aibu kama kuzaa nje ya ndoa, na wamekingwa na makosa.
Ni katika ukristo pekee utakuta mitume wanatukanwa kuwa ni walevi, mara wamezini na watoto wao wa kike, mara wameingiliwa kinyume na maumbile, mara wameiba wake wa majirani zao na matusi kama hayo, ibrahim ni mtume na ana heshima kubwa na ni kipenzi cha allah haimpasii yeye kuzaa nje ya ndoa.
Kuna swali nimekuuliza pale chini kwenye bandiko langu la juu nipatie majibu inshaallah.
Kijakazi hakuolewa ila Abraham alioa mke wapili ,Hivi ndivyo vizazi vya Ishmaeli, mwana wa Ibrahimu, ambaye Hajiri, Mmisri, mjakazi wa Sara, alimzalia Ibrahimu. Na haya ndiyo majina ya wana wa Ishmaeli, kwa majina yao, na kwa vizazi vyao. Mzaliwa wa kwanza wa Ishmaeli, ni Nebayothi, na Kedari, na Abdeeli, na Mibsamu, na Mishma, na Duma, na Masa, na Hadadi, na Tema, na Yeturi, na Nafishi, na Kedema. Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao,
Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake akiitwa Ketura. Akamzalia Zimrani, na Yokshani, na Medani, na Midiani, na Ishbaki, na Sua. Yokshani akamzaa Sheba, na Dedani; na wana wa Dedani walikuwa Waashuri na Waletushi, na Waleumi. Na wana wa Midiani walikuwa, Efa, na Eferi, na Hanoki, na Abida, na Eldaa. Hao wote walikuwa ni wana wa Ketura.
So elewe acha kukurupuka hii ni mwanzo:25:1-25