Qur'an imeteremka kwa lugha ya kiarabu, tafsiri iliyokuja kwa lugha yeyote hutizamwa kama iko sahihi au laa, unaweza kuleta hoja kutoka kwenye tafsiri ya yusufu ali tukaijadili hakuna shida.
Ama kifo cha masihi issa mwana wa mariam alayhi ssalaam wewe huwezi kukithibitisha, kwasababu aliyemtuma ametuthibitishia hakufa kabisa bali walifananiziwa na yule msaliti akabeba adhabu yote yeye akapaa mbinguni, na hii ni habari inayohitaji hoja nzito.
Ama kutaka kufananisha Qur'an na biblia hii si sawa kabisa, kwa hoja kuwa ndani ya Qur'an hakuna herufi hata moja ambayo ni neno la mwanadamu awe mtume au swahaba au mtu mwingine yeyote bali ni maneno ya allah kwa ukamilifu wake! na yamedumu kwenye hali moja kwa zaidi ya miaka 1440+ sasa, hizo ni karne 14, je kuna kitabu chochote kilichobaki kwenye hali yake bila kubadilishwa herufi mpaka sasa zaidi ya Qur'an? ama ndani ya bible kuna maneno ya watu mengi tu, wachilia mbali watu wenye elimu bali hata watu wa zama za baadae sana ambao wala hawakumuona issa mwana wa maryam alayhi ssalaam, vipi utafananisha hoja za huku na huku kwa sura kama hii? utathibitishaje usahihi wa maneno yasiyojulikana msemaji wake na maneno ya allah?.
Katika uislamu kuna kitu kinaitwa sanad, huu ni mtiririko wa wapokezi wa habari, na neema hii allah ameupatia umma huu peke yake hakuna umma ulikuwa na utaratibu huu katu, na hii yote ni kuyahifadhi mafundisho ya uislamu pasi na kuingiliwa na uongo au mabadiliko yasiyohusika.
Kwa maana Qur'an imebaki pure vilevile tangu imeshuka mpaka leo na ni muujiza mkubwa kwa walimwengu lau kama watazingatia, sasa hoja ya kufa nabii issa imevunjwa vibaya sana katika Qur’an, vipi mimi nikose adabu niseme amekufa kwa hoja kutoka kwenye kitabu kingine ambacho wewe tu binafsi huwezi kunithibitishia usahihi wake kutokana na kuwa na versions nyingi sana, nyie wenyewe ni mashahidi mnabishana kila siku mara kitabu cha enoch kimefichwa, mara biblia sahihi iko vatican n.k tutaamini vipi? mnaweza kutukinaisha?.