Huyo Isa alikuwepo kabla ya ulimwengu kuwepo ? Na ana Baba ?
Yohana 17: 5 Sasa, Baba, nitukuze mbele yako kwa ule utukufu niliokuwa nao kabla ya kuumbwa ulimwengu.
Katika bibilia Kuna Yesu wawili
1) YESU AMBAYE NDIO ISA
UTABIRI WA MANABII KUHUSU UJIO WA YESU/ ISA
Mathayo 2:6
Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda, Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda; Kwa kuwa kwako atatoka mtawala Atakayewachunga watu wangu Israeli.
YESU / ISA ANATHIBITISHA UTABIRI UMETIMIA
Mathayo 15:24
Akajibu, akasema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli.
Yohana 17:3
Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma.
NABII MUHAMMAD KUPITIA QURAN ANAPIGILIA MSUMARI KUWA YESU / ISA ALITUMWA NA MUNGU KAMA MTUME KWA WANA WA ISRAEL
Quran 61:6
Na Isa bin Mariamu alipo sema: Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninaye thibitisha yaliyo kuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria kuja Mtume atakaye kuja baada yangu; jina lake ni Ahmad!
2) YESU AMBAYE SIO ISA ILA NI GALASA LILILOTENGENEZWA NA PAULO NA NDIO YESU WA WAKRISTO
Tito 2:13
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu;
Shida yako ipo wapi nimekuambia huyo Yesu GALASA mlilotengenezewa na Paulo wengine wanamuita Mungu mkuu ,wengine Mungu ,wengine sijui mwana wa Mungu
Nimekuambia nakubaliana na wakristo 100% huyu Yesu wenu sio Isa wa ndani ya Quran
Ila kama unamuongelea Yesu/ Isa alitajwa ndani ya Quran lete hoja zenye mashiko
Yesu/ Isa wa ndani ya Quran sifa zake ni hizi
Amezaliwa na Mariam bint Imran
Amepewa utume na Mungu Kwa ajili ya Wana wa Israel
Amepewa kitabu Cha Injili