Tofauti kati ya Yesu na Nabii Issa
Mimi nikiamua kujibu hakuna hoja hata moja ya nguvu uliyoitoa isipokuwa sikuwa na makusudio ya kuchangia mjadala huu, ila ukinitaka nichangie naweza na nitaanza kama ifuatavyo.

Bismillah, kwa ufupi mkubwa mijadala ya kumtofautisha issa mwana wa mwaryam alayhi ssalaam na yesu imekithiri siku za karibuni, na malengo ya mijadala hii ni kupindisha ukweli kwa makusudi baada ya kushindikana kuvunja hoja kuwa uislamu umemtukuza masihi issa alayhi ssalaam na kumpa heshima kubwa kuliko ukristo uliomtweza na kumfanya msulubiwa tena aliyedhalilishwa mbele za watu.

Jambo la pili, mijadala hii pia imekithiri baada ya kuwa kule kuonekana masihi issa amani juu yake ndio uzi mwembamba baina ya uislamu na ukristo hivyo wahafidhina wakaona bora kusema huyu si yule ili kuhafifisha hoja za wapinzani wao, maana tukikubaliana sio mwana wa mungu na tukikubaliana hajasulubiwa kama uislamu ulivyoeleza basi hakuna ukristo tena.

Tukirudi kwenye mada, binafsi sio muumini wa hearsay's hivyo mapenzi yangu ni kutoa hoja kutoka kwenye certified source ni mamoja iwe kutoka kwenye maneno ya allah yaani Qur'an au hadithi sahihi za mtume swala na salaam ziwe juu yake zilizoshuhudiliwa na wanawachuoni wakubwa wa fani ya hadithi juu ya usahihi wake, kwa sababu hiyo hoja za kutoka upande huu zitabaki zenye nguvu zaidi daima kutokana na usahihi wa kule zinapotoka.

Masihi issa mwana wa mariam ni mtume wa allah na ndie mtume wa pili kutoka mwisho na baina yake yeye na mtume muhammad swala na salaam ziwe juu yao ni miaka 600 takriban, yeye alitoa bishara ya kuja mtume muhammad na nabii ibrahiym alayhi ssalaam aliomba dua allah awapatie mtume pale alipoacha kizazi chake yaani mkewe haajar na mwanae ismail alayhi ssalaam, hivyo yeye mtume muhammad ni bishara ya ndugu yake issa mwana wa mariam na dua ya baba yake ibraahiym, manabii wote ni watoto wa baba mmoja na mama zao mbalimbali, juu yao swala na amani,

Turudi nyuma kidogo bila kurefusha sana maneno, nabii zakariyyah alayhi ssalaam alikosa mtoto kwa muda mrefu mpaka akafikia uzee na yeye ndio alikuwa mlezi na muangalizi wa mariam bint imraan mama yake na nabii issa, wakati fulani aliyaona mambo yasiyo ya kawaida kwa mariam na habari hii imeelezwa vizuri katika Qur'an pale allah aliposema.

"Hakika allah alimteua adam na nuhu na ukoo wa ibrahim na ukoo wa imran juu ya walimwengu wote."

"Ni kizazi wao kwa wao,na allah ni mwenye kusikia na mwenye kujua."

"Aliposema mke wa imran, mola wangu mlezi! nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu, basi nikubalie! hakika wewe ndiye mwenye kusikia mwenye kujua."

"Basi alipomzaa alisema: mola wangu mlezi! nimemzaa mwanamke! na allah anajua sana aliyemzaa, na mwanaume si sawa na mwanamke, na mimi nimemwita mariam, na mimi namkinga kwako, yeye na uzao wake, uwalinde na shetani aliyelaaniwa."

"basi mola wake mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya zakariyyah kuwa mlezi wake, kila mara zakariyyah alipoingia kwake alimkuta na vyakula, basi alimwambia: ewe mariamu! unavipata wapi hivi? naye akasema: hivi vinatoka kwa allah, na allah humruzuku amtakaye bila ya hisabu."

"basi hapo zakariyyah akamwomba mola wake, akasema: mola wangu mlezi! nipe kutoka kwako uzao mwema, hakika wewe ndiye mwenye kusikia maombi."

"Basi akamuita yeye malaika na hali ya kuwa amesimama akiswali kwenye mihrabu "hakika allah anakubashiria {kupata mtoto aitwae} yahya, atakayekuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa allah, ni bwana na mtawa na nabii kwa watu wema."


Qur'an 3:33-39

Mpaka mwisho wa habari hii, nimeleta aya hizi kwa makusudi kuonesha ufanano wa matukio ya zakariyyah, maryam, yahya na issa mwenyewe amani iwe juu yao, watu hawa kamwe haiwezekani kuwatenganisha kwasababu kwa uhakika hasa hilo haliwezekani.

Torati, injili, na zaburi vyote ni vitabu vimetoka kwa allah na ni maneno yake na si ya mwanadamu katu, ila tu hivyo vilivyotangulia vimeingiliwa na mikono ya watu wakayabadili mengine na mengine wakayafuta, na uwezekano wa kuyafuta yote ni mdogo ndio maana utaona tofauti ya majina ya kihebrania lakini yanawiana na yaliyotajwa kwenye Qur'an kwasababu yote ni majina ya kiajemi, na issa mwana wa mariam atarudi mwisho wa zama na atakufa kama wanavyokufa wanadamu wengine.

"Na mayahudi wanasema uzeir {ezra} ni mtoto wa allah, na wakristo wanasema, masihi {yesu} ni mtoto wa allah, hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao, wanayaiga maneno ya waliokufuru kabla yao, allah awaangamize! vipi wanageuzwa? {kuacha ukweli kuuelekea uongo}."

Qur'an 9:30

Nahofia kurefusha zaidi faida ikawa ndogo, tuanzie hapa.

Hapa nimeshuhudia maneno mengi ya kutaka kuaminiasha ujinga na wala hakuna hoja yoyote ya msingi uliyoitoa kujibu hoja za uzi,kimsingi maneno matupu na umepuyanga.
 
Hapana hakuna na baadhi ya maneno ndio hayo yako kwenye hiyo inaitwa biblia, na kwa kubadilishwa huku sisi tumetoshelezwa na Qur'an kwasababu imekuja kutueleza baadhi ya habari za torati na injili na zaburi pia, bali hizo zilikuwa sheria za wana wa israeli sisi ni umma na zama nyingine wala zisitufae tena, baadhi ni kama aya hii.

"Na hakika tulikwishaandika katika zaburi baada ya dhikr, ya kwamba ardhi watairithi waja wangu walio wema."

Qur'an 21:105

Na mfano wa habari hizo kwenye Qur'an ni nyingi tu, kwa ajili hiyo sisi tukafundishwa mtu akitujia na habari akadai ni sehemu katika torati au injili au zaburi basi tuseme sisi tumeamini yaliyoteremshwa kwenu na yaliyoteremshwa kwetu, ili tusije kukanusha kumbe ni sehemu katika hayo, na tusije kukubali kumbe ni yale yaliyobadilishwa.

Biblia imebadilishwa??tupe biblia ambayo ni kamili na haijabadilishwa ili tuweze kurefer na kujua wapi pamebadilishwa,tafadhari naomba hiyo biblia ambayo haijabadilishwa.
 
Alisema sisi tuna haki zaidi na mussa alayhi ssalaam kuliko wao hivyo akaamrisha tuifunge, na ni kweli sisi ndio tuna haki na mussa kuliko mayahudi kwasababu sisi tumemuamini yeye na mitume wote wa wana wa israeli, wakati wao walifikia kuwaua kabisa mitume wao.

Waliwauwa mitume gani?kumbe uislamu umeiba mitume wa wayahudi?
 
Robby,Issa kazaliwa miaka 600Anno Dominos.....Issa kazaliwa Madina kafia Makkah,Yesu kazaliwa Bethlehem zamani kabisaa huko enzi za za utawala wa Rumi kipindi Cha kina Ceisar Agustus na kina Herode,,,Issa kazaliwa Karne 6 baada ya Yesu...Sasa anakuwa vipi mtu mmoja,hakuna hoja hapa

Huyo issa hajawahi kuexist bali ni fiction character wa mudy,
 
Yesu na huyo issa ni fiction characters hawajawai kuwepo, hizo ni story tu za kutungwa

Bora haya Yesu anaweza kutetewa kwenye maandiko,ila issa wa kurwani yani hata ukijaribu kumtetea inashindikana mana ni character wa kubumba.
 
Yesu alizaliwa Nazareth, Huko Bethlehem ya Yuda nje ya Jiji la Yerusalem(Mji wa Daudi. Alizaliwa kwenye Usiku kwenye Hori la Ng'ombe, katika utawala wa Rumi Chini ya Herode.

Haya maelezo ukiwaomba wafuasi wa mudi wakueleze kuhusu isa alizaliwa wapi,lini na mji gani katika utawala gani wanaanza kutukana hovyo.
 
Yesu na huyo issa ni fiction characters hawajawai kuwepo, hizo ni story tu za kutungwa
[emoji849][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mzee baba unaleta mbango sasa.....miaka 2000 iliyopita si mingi sana kuweka historia.....kutoka sasa miaka 2000 mbele watakaokuwepo watajitokeza watu kama wewe watakaosema NYERERE hakuwa baba wa taifa la Tanzania/hakuwahi kuwepo mtu aitwaye Nyerere kabisaaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Haya maelezo ukiwaomba wafuasi wa mudi wakueleze kuhusu isa alizaliwa wapi,lini na mji gani katika utawala gani wanaanza kutukana hovyo.
Mkuu kwa hiyo Wayahudi nao waongo?!!!

Nionyeshe katika vitabu vyao vitakatifu/commentaries books wapi wametaja alipozaliwa Yesu kwani huyo ni ndugu yao wa damu zaidi....ama wameficha ili kutengeneza "conspiracy"?!!!
Kama ndivyo nitakushangaa vipi nawe mhehe/mndengereko kuwa hutengenezi "conspiracy attacks" dhidi ya hao waislamu ?!!!
 
Agano la kale katika Biblia limeandikwa miaka zaidi ya 3200 iliyopita wakati Agano Jipya limeandikwa miaka 2000.

Hiyo Quran imeandikwa miaka 1400 iliyopita.

Ukiwa na akili tu lazima ujuwe ni kipi kitabu cha ukweli.

Nakupongeza mtoa mada kwa kuonyesha gaps zilizopo kwenye Quran ambapo hawa wanayoiamini wanalazimisha kusema Issa wa kwenye kitabu chao ndiye Yesu Kristu wa kwenye Biblia.. Leo umewaumbua
Hoja ya miaka itakuangusha....

Dini ya Zoroastrianism na vitabu vyake ina miaka zaidi ya 3500 kuliko AGANO LA KALE....kwa hiyo wao ni wakweli zaidi ya wote hao waliofuata?!!![emoji1787][emoji1787]
 
Kwanza niseme inaonekana umesoma au umesimuliwa Quruani kama hadithi lakini siyo kwa kuielewa ndiyo maana hukuilewa,nitaanza na hapa uliposema Yesu atakuja kuwahukumu wanadamu,kwani Yeye ndiye aliyewaumba?Mwenye uwezo wa kuwahukumu Wanadamu ni Mungu peke yake ambaye ana sifa zote za Uungu,hakuzaliwa hafi,hana mwanzo wala mwisho

Kwa kutokujua hicho tu unaonekana mwenyewe elimu yako ni ndogo kiasi kwamba huna uwezo wa kumchambua Issa na Yesu

Tia facts acha porojo
 
Nauiza huyo Mudi aliyesema ameteremshiwa kitabu kilichokamilika kumbe alikuwa anaiga kwa wayahudi na wakristu yeye na wafuasi wake walikuwa wanafunga?
Unaweza kujadili hoja pasi na kuleta kejeli wala dharau hapa hatumjadili mpiga debe fulani pale mbezi mwisho, bali mtume miongoni mwa mitume so kama hutoweza kuwa mstaarabu mimi sitokujibu chochote.
 
Huna hoja kaa kimya,unaweza maliza umri hatq kwenye mambo ya kipuuzi.
Mtu asiye na hoja hujibiwa kwa hoja, na si mipasho au mikwara wewe umeleta hiyo hoja? ama kuhusu umri wangu kuhangaikia tafsiri ya kitabu hiki mimi nina uhakika nautumia vizuri na matunda yake nayaona kwenye maisha yangu, so hakuna shida mkuu wewe maliza kwenye simba na yanga mimi nitaumalizia huku, fainali yetu sote ni kwenye kifo.

"Na muabudu mola wako mlezi mpaka ikufike yaqini {mauti}."

Qur'an 15:99
 
Ina maana kitabu Cha Qur'an iliyotafsiriwa na Yusuf Ali haijakamilika?
Hoja zingine hizi
Yesu alikufa, Isa hakufa alafu unasema ni kama CCM na Chama Cha Mapinduzi.
Nionyeshe sehemu kwenye Biblia inayosema Yesu hakufa ndo tuamini usawa wa Yesu na Isa
Qur'an imeteremka kwa lugha ya kiarabu, tafsiri iliyokuja kwa lugha yeyote hutizamwa kama iko sahihi au laa, unaweza kuleta hoja kutoka kwenye tafsiri ya yusufu ali tukaijadili hakuna shida.

Ama kifo cha masihi issa mwana wa mariam alayhi ssalaam wewe huwezi kukithibitisha, kwasababu aliyemtuma ametuthibitishia hakufa kabisa bali walifananiziwa na yule msaliti akabeba adhabu yote yeye akapaa mbinguni, na hii ni habari inayohitaji hoja nzito.

Ama kutaka kufananisha Qur'an na biblia hii si sawa kabisa, kwa hoja kuwa ndani ya Qur'an hakuna herufi hata moja ambayo ni neno la mwanadamu awe mtume au swahaba au mtu mwingine yeyote bali ni maneno ya allah kwa ukamilifu wake! na yamedumu kwenye hali moja kwa zaidi ya miaka 1440+ sasa, hizo ni karne 14, je kuna kitabu chochote kilichobaki kwenye hali yake bila kubadilishwa herufi mpaka sasa zaidi ya Qur'an? ama ndani ya bible kuna maneno ya watu mengi tu, wachilia mbali watu wenye elimu bali hata watu wa zama za baadae sana ambao wala hawakumuona issa mwana wa maryam alayhi ssalaam, vipi utafananisha hoja za huku na huku kwa sura kama hii? utathibitishaje usahihi wa maneno yasiyojulikana msemaji wake na maneno ya allah?.

Katika uislamu kuna kitu kinaitwa sanad, huu ni mtiririko wa wapokezi wa habari, na neema hii allah ameupatia umma huu peke yake hakuna umma ulikuwa na utaratibu huu katu, na hii yote ni kuyahifadhi mafundisho ya uislamu pasi na kuingiliwa na uongo au mabadiliko yasiyohusika.

Kwa maana Qur'an imebaki pure vilevile tangu imeshuka mpaka leo na ni muujiza mkubwa kwa walimwengu lau kama watazingatia, sasa hoja ya kufa nabii issa imevunjwa vibaya sana katika Qur’an, vipi mimi nikose adabu niseme amekufa kwa hoja kutoka kwenye kitabu kingine ambacho wewe tu binafsi huwezi kunithibitishia usahihi wake kutokana na kuwa na versions nyingi sana, nyie wenyewe ni mashahidi mnabishana kila siku mara kitabu cha enoch kimefichwa, mara biblia sahihi iko vatican n.k tutaamini vipi? mnaweza kutukinaisha?.
 
Back
Top Bottom