Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
Ushahidi wa unyanyasaji ulionea na mateso kutoka kwa mwanzilishi wa mojawapo ya makanisa makubwa ya kiinjili ya Kikristo duniani umefichuliwa na BBC.

Makumi ya waumini wa zamani wa Kanisa la Synagogue Church of all Nations - watano Waingereza - wanadai ukatili, ikiwa ni pamoja na ubakaji na utoaji mimba kwa lazima, uliofanywa na marehemu TB Joshua wa Nigeria.

Madai ya unyanyasaji katika eneo la siri la Lagos yamedumu kwa takriban miaka 20.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations halikujibu madai hayo lakini lilisema madai ya hapo awali hayana msingi.

TB Joshua, aliyefariki mwaka wa 2021, alikuwa mhubiri na mwinjilisti mwenye mvuto mkubwa na mwenye mafanikio makubwa ambaye alikuwa na wafuasi wengi duniani.

Matokeo ya BBC katika uchunguzi wa miaka miwili ni pamoja na:
  • Masimulizi mengi ya watu waliojionea matukio ya ukatili wa kimwili au mateso yaliyofanywa na Joshua, ikiwa ni pamoja na matukio ya unyanyasaji wa watoto na watu kuchapwa viboko na kufungwa minyororo.
  • Wanawake wengi wanaosema walinajisiwa na Joshua, huku baadhi wakidai kuwa walibakwa mara kwa mara kwa miaka mingi ndani ya boma hilo.
  • Tuhuma nyingi za kutoa mimba kwa lazima ndani ya kanisa kufuatia tuhuma za ubakaji na Joshua, akiwemo mwanamke mmoja ambaye anasema alitolewa mimba mara tano.
  • Simulizi nyingi za moja kwa moja zinazoelezea jinsi Joshua alivyodanganya kuhusu "uponyaji wake wa miujiza", ambao ulitangazwa kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote.
Mmoja wa waathiriwa, mwanamke wa Uingereza, anayeitwa Rae, alikuwa na umri wa miaka 21 alipoacha shahada yake katika Chuo Kikuu cha Brighton mnamo 2002 na kuandikishwa katika kanisa. Alitumia miaka 12 iliyofuata kama mmoja wa wale wanaoitwa "wanafunzi" wa Yoshua ndani ya boma lake la kifahari huko Lagos.

"Sote tulidhani tuko mbinguni, lakini tulikuwa katika hali inayofanana na ya kuzimu, na huko kunatokea mambo mabaya," aliiambia BBC.

Rae anasema alinajisiwa na Joshua na kuwekewa aina ya kifungo cha upweke kwa miaka miwili. Dhuluma hiyo ilikuwa kali sana, anasema alijaribu kujiua mara nyingi ndani ya boma hilo.

Kanisa la Synagogue Church of All Nations [Scoan] lina wafuasi wa kimataifa, wanaoendesha chaneli ya TV ya Kikristo iitwayo Emmanuel TV na mitandao ya kijamii yenye mamilioni ya watazamaji. Katika miaka yote ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000, makumi ya maelfu ya mahujaji kutoka Ulaya, Amerika, Kusini Mashariki mwa Asia na Afrika walisafiri hadi kanisani humo nchini Nigeria kumshuhudia Joshua akifanya "miujiza ya uponyaji".

Takriban wageni 150 waliishi naye kama wanafunzi ndani ya boma lake huko Lagos, wakati mwingine kwa miongo kadhaa.

Rae in a BBC studio interview, wearing glasses and black top

Maelezo ya picha: Rae alisalia kwa miaka 12 katika boma la Joshua

Zaidi ya "wanafunzi" 25 wa zamani walizungumza na BBC - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - wakitoa ushuhuda wenye nguvu wa kuthibitisha waliopitia ndani ya kanisa, pamoja na matukio ya hivi majuzi zaidi katika mwaka wa 2019. Waathiriwa wengi walikuwa katika ujana wao walipojiunga mara ya kwanza. Katika baadhi ya kesi za Uingereza, usafiri wao hadi Lagos ulilipwa na Joshua, kwa ushirikiano na makanisa mengine ya Uingereza.

Rae na waliohojiwa wengine wengi walilinganisha masaibu yao na kuwa katika dhehebu la itikadi kali .
Jessica Kaimu, kutoka Namibia, anasema masaibu yake yalidumu kwa zaidi ya miaka mitano. Anasema alikuwa na umri wa miaka 17 wakati Joshua alipombaka kwa mara ya kwanza, na kwamba matukio ya baadaye ya kubakwa na TB Joshua yalisababisha atoe mimba mara tano akiwa huko.

"Haya yalifanyika kisiri... matibabu tuliyokuwa tukifanyiwa... yangeweza kutuua," aliiambia BBC.
Wengine waliohojiwa wanasema walivuliwa nguo na kupigwa kwa nyaya za umeme na mijeledi ya farasi, na mara kwa mara walikoseshwa usingizi.
Katika kifo chake mnamo Juni 2021, TB Joshua alisifiwa kama mmoja wa wachungaji wenye ushawishi mkubwa katika historia ya Afrika.

Akiinuka kutoka kwa umaskini, alijenga himaya ya kiinjilisti ambayo ilijivunia makumi ya viongozi wa kisiasa, watu mashuhuri na wanasoka wa kimataifa kati ya washirika wake.

Hata hivyo, alizua utata wakati wa uhai wake wakati nyumba ya wageni ya mahujaji wa kanisa ilipoporomoka mwaka wa 2014, na kuua watu wasiopungua 116.Uchunguzi wa BBC, ambao ulifanywa na jukwaa la kimataifa la vyombo vya habari vya Open Democracy, ni mara ya kwanza watu wengi wa zamani wa makanisa kujitokeza kuzungumza juu ya rekodi hiyo. Wanasema wametumia miaka mingi kujaribu kupaza sauti lakini wamenyamazishwa kwa ufanisi.

Baadhi ya mashahidi wetu nchini Nigeria wanadai walishambuliwa kimwili, na katika kisa kimoja walipigwa risasi, baada ya awali kujitokeza kupinga unyanyasaji huo na kuchapisha video zenye madai kwenye YouTube.

Wafanyakazi wa BBC ambao walijaribu kurekodi picha za boma la kanisa hilo Lagos kutoka mtaa wa umma mnamo Machi 2022 pia walipigwa risasi na usalama wa kanisa hilo, na walizuiliwa kwa saa kadhaa.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi wetu. Haikuwajibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.
"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," iliandika.

Raia wanne wa Uingereza waliozungumza na BBC wanasema waliripoti unyanyasaji huo kwa mamlaka ya Uingereza baada ya kutoroka kanisani. Wanasema hakuna hatua zaidi zilizochukuliwa.

Anneka pictured in BBC studio interview, wearing white jumper

Maelezo ya picha: Anneka anasema anaamini kuna waathiriwa wengi ambao bado hawajazungumza

Zaidi ya hayo, mwanamume Muingereza na mkewe walituma barua pepe kwa mashahidi waliojionea ushahidi wao wa mateso na video - ikiwa ni pamoja na rekodi za kushikiliwa kwa mtutu wa bunduki na wanaume wanaojiita polisi ambao pia ni wanachama wa Scoan - kwa Ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria mnamo Machi 2010 baada ya kukimbia kanisa hilo. Katika barua pepe yake, mwanamume huyo alisema mke wake alishambuliwa kingono mara kwa mara na Joshua. Aliionya ubalozi huo kuwa raia wengine wa Uingereza bado wako ndani ya boma hilo wakikabiliwa na ukatili.

Pia anasema hakuna hatua zilizochukuliwa. Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza haikujibu madai haya, lakini iliambia BBC kwamba inachukulia ripoti zote za uhalifu, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya raia wa Uingereza nje ya nchi, kwa uzito mkubwa.

Scoan inaendelea kustawi leo, chini ya uongozi wa mjane wa Joshua, Evelyn. Mnamo Julai 2023, aliongoza ziara ya kwenda Uhispania.

Anneka, ambaye aliondoka Derby nchini Uingereza na kujiunga na Scoan akiwa na umri wa miaka 17, aliambia BBC kuwa anaamini kuna waathiriwa wengine wengi ambao bado hawajazungumza. Anatumai hatua zaidi zitachukuliwa kufichua vitendo vya Joshua.

"Ninaamini Kanisa la Synagogue Church of All Nations linahitaji uchunguzi wa kina ili kujua ni kwa nini mtu huyu aliweza kufanya kazi kwa muda mrefu kama alivyofanya," alisema.

Ripoti ya ziada ya Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward
Kwa usaidizi na taarifa kuhusu unyanyasaji wa kingono, tafadhali wasiliana na Mtandao huu wa BBC Actionline nchini Uingereza. Na kwa habari zaidi juu ya madhehebu, tafadhali tazama The Family Survival Trust

BBC
Pia soma: BBC imepanga kutoa video inayoonesha Unabii Feki wa TB Joshua
 
Wacha wapigwe si wanajipendekeza wenyewe, Mwanamke anaeamini sana hawa viongozi wa dini mchunguze utagundua mengi mfano hai ni hao waliobakwa na kufungiwa leo ndio inajulikana ila alipokuwepo hawakuweza sema wakiamini ni mtumishi wa Mungu kumbe fix tu
 
Upuuzi mtupu. Hakuna uchunguzi wowote wala kitu cha maana, ni siasa tu za umiliki wa mali za kanisa kati ya Mke wa TB Joshua na Baraza la Wazamini wa Kanisa kwani mama aliwashinda waliokuwa wanategemea kujichotea manoti ya kanisa baada ya jamaa kufa. Sasa wanapambana kuona namna gani wataliyumbisha kanisa mbele ya jamii.

Hapa hakuna uchunguzi wa maana na huo uchunguzi ni aibu kwa BBC. Uchunguzi ungetakiwa usiwe wa maneno tu bali uwe na ushahidi tosha kama:

1. Taarifa za kidaktati zinazoonesha namna hao waathirika waliathiriwa na Nabii.

2. Case zilizofunguliwa Mahakamani na mashtaka yaliyopelekwa polisi.

3. Namna Balozi za UK,NAMIBIA na nchi nyingine zilipokea malalamiko na kurespond kuhusu malalamiko ya waathiriwa.

4. Picha na vielelezo toka kwa waathirika.

Simtetei TB Joshua kwani naye ni Bunadamu na alikuwa na mapungufu ila hiki walicholeta BBC ni blah blah na hadithi tu, kwanini wasingechunguza na kuja na hizo blah blah muhusika akiwa hai?

Blah blah hizi zinahusu mtu aliyekufa direct asiyejitetea na hazihusu taasisi. Wajunga wasiojitambua wala wenye uwezo wa kufikiria kizazi cha 1990's to 2000's ndio mtashadadia ila kwa mtu mwenye utulivu wa kiakili, hakuna kitu cha maana hapa.
 
Mbona kama ushahidi hauna nguvu, mtu yoyote anaweza kuzungumza.

N.B MIMI SI MFUASI WA TB JOSHUA
Utaambiwa wewe ni mfuasi wa Mitume na u mfuasi wa TB JOSHUA ila hapa hakuna kitu bro.

Pale Kanisani kuna fukuto la umiliki wa mali za kanisa baada ya jamaa kufariki na walishapelekana mahakamani na mke wa jamaa kushinda kesi.

Baada ya Jamaa kufariki, waliokuwa wajumbe wa baraza la wadhamini walipendekeza mtu wao awe mkuu au mmiliki na mali za kanisa kwani ile ni taasisi sasa. Kulitokea kashfa ya watu kukwapua mabilioni ya kanisa mpaka wakapelekana mahakamani ndipo mke akawa kidedea. Hiki kinachoitwa uchunguzi ni muendelezo wa siasa baada ya kuona mama anaendelea na kanisa linaendelea kusonga mbele. Kinachotafutwa hapa ni kukosekana kwa imani dhidi ya kanisa katika jamii na hakuna lolote la maana.

Vijana wa kuponda wenye mapepo na low IQ watakuja kushambulia lakini hakuna la maana hapa.
 
Back
Top Bottom