Jinsi binti yake TB Joshua alivyokabiliana na baba yake kwa kufichua maovu yake

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
th

10 Januari 2024
Na Charlie Northcott, Helen Spooner & Tamasin Ford
BBC Africa Eye

BBC inafichua jinsi kiongozi wa kanisa kuu marehemu TB Joshua, ambaye anatuhumiwa kwa uhalifu wa kingono kwa wingi, alimfungia bintiye mwenyewe na kumtesa kwa miaka kadhaa kabla ya kumwacha bila makao katika mitaa ya Lagos, Nigeria.
Onyo: Ina maelezo ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kuhuzunishwa nayo
"Baba yangu alikuwa na woga, hofu ya mara kwa mara.

Aliogopa sana kwamba mtu angezungumza," anasema mmoja wa binti za mhubiri, Ajoke - mfichua ukweli wa kwanza kufikia BBC kuhusu unyanyasaji alioshuhudia katika kanisa la babake,Kanisa la Sinagogi la Mataifa Yote (Scoan).

TB Joshua, aliyefariki mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 57, anatuhumiwa kwa unyanyasaji na mateso yaliyoenea kwa takriban miaka 20.

Sasa ana umri wa miaka 27, Ajoke anaishi mafichoni na ameacha jina lake la ukoo "Joshua" - BBC haichapishi jina lake jipya.

Machache yanajulikana kuhusu mama mzazi wa Ajoke, ambaye aliaminika kuwa mmoja wa washirika wa TB Joshua. Ajoke anasema alilelewa na Evelyn, mjane wa Joshua, tangu mapema anapokumbuka.

Hadi umri wa miaka saba, Ajoke anasema alikuwa na maisha ya furaha sana, akienda likizo na familia ya Joshua katika maeneo kama Dubai.

Lakini siku moja kila kitu kilibadilika. Alifukuzwa shule kwa kosa, na mwandishi wa habari wa eneo hilo aliandika makala akimtaja kama mtoto wa nje wa TB Joshua. Alitolewa shuleni na kupelekwa katika boma la Scoan huko Lagos.

"Nililazimishwa kuhamia kwenye chumba cha wanafunzi. Sikujitolea kuwa mfuasi. Nililazimishwa kujiunga," anasema.

Wanafunzi walikuwa kundi la wasomi wa wafuasi waliojitolea ambao walimtumikia TB Joshua na waliishi naye ndani ya muundo wa kanisa.

Walikuja kutoka duniani kote, wengi walikaa kwenye boma hilo kwa miongo kadhaa.

Waliishi chini sheria kali: Marufuku kulala kwa zaidi ya saa chache kwa wakati mmoja, kupigwa marufuku kutumia simu zao wenyewe au kupata barua pepe zao za kibinafsi, na kulazimishwa kumwita TB Joshua "Daddy".

"Wanafunzi walikuwa wamepewa mafunzo ya itikadi kali na walikuwa wawezeshaji wa madhila katika kanisa hilo. Kila mtu alikuwa akiigiza tu kwa kufuata amri - kama zombi.

Hakuna aliyekuwa akihoji chochote," anasema.

Akiwa mtoto tu, Ajoke hangefuata sheria kama wanafunzi wengine: alikataa kusimama wakati mchungaji alipoingia chumbani na kuasi amri kali za kulala.

Unyanyasaji ulianza hivi punde.
Muda mfupi baada ya kufika, akiwa na umri wa miaka saba, anakumbuka alipigwa kwa sababu ya kukojoa kitanda na kisha kulazimishwa kuzunguka kiwanja hicho na alama shingoni yake ikisema "Mimi hukojoa kitandani'

"Ujumbe kuhusu Ajoke ulikuwa kwamba alikuwa na pepo wabaya sana ambao walihitaji kufukuzwa," anasema mwanafunzi mmoja wa zamani wa kike.

"Kuna wakati katika mikutano ya wanafunzi - yeye [Joshua] alisema watu wanaweza kumpiga. Mtu yeyote katika bweni la kike angeweza tu kumpiga na nakumbuka kuona tu watu wakimpiga makofi walipokuwa wakipita," anasema.

Tangu wakati Ajoke alipohamia kanisani katika kitongoji cha Ikotun huko Lagos, alichukuliwa kama mtu aliyetengwa.

"Alikuwa, kama, aliyeitwa kondoo mweusi wa familia," anasema Rae, kutoka Uingereza, ambaye kwa miaka 12 aliishi kanisani kama mfuasi. Kama wanafunzi wengi wa zamani waliohojiwa na BBC, alichagua kutumia jina lake la kwanza pekee.

Rae anakumbuka wakati Ajoke alilala kwa muda mrefu sana, na Joshua akamfokea ainuke.

TH

CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Ajoke anasema baada ya kuteswa kwa miaka mingi alipoteza hofu yake kwa baba yake akiwa na umri wa miaka 17

Mwanafunzi mwingine alimpeleka kuoga na "kumchapa kwa waya ya umeme na kisha kuwasha maji ya moto", anasema.

Akikumbuka tukio hilo, Ajoke anasema: "Nilikuwa nikipiga kelele kwa sauti ya juu, na waliacha tu maji yakipita kichwani mwangu kwa muda mrefu sana."

Unyanyasaji kama huo haukuisha, anasema.

"Tunazungumza kuhusu miaka na miaka ya unyanyasaji.

Unyanyasaji wa mara kwa mara.

Kuwepo kwangu kama mtoto kutoka kwa mama mwingine kulidhoofisha kila kitu ambacho [TB Joshua] alidai kuwakilisha."
Unyanyasaji huo uliongezeka kwa kiwango tofauti alipokuwa na umri wa miaka 17 na kumkabili baba yake kuhusu "simulizi, za moja kwa moja, za watu ambao walifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia".

"Niliwaona wanafunzi wa kike wakipanda chumbani kwake. Walikuwa wakienda kwa masaa mengi. Nilikuwa nikisikia mambo: 'Loh hii ilinipata.

Alijaribu kulala nami.' Watu wengi walikuwa wakisema kitu kimoja, "anasema.

BBC ilizungumza na zaidi ya wanafunzi 25 wa zamani - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - ambao walitoa ushuhuda wenye nguvu wa kufanyiwa au kushuhudia unyanyasaji wa kingono.
"Sikuweza kuvumilia zaidi.

Niliingia ofisini kwake moja kwa moja siku hiyohiyo. Nilipiga kelele kwa sauti kuu: '

Kwa nini unafanya hivi?

Kwa nini unawaumiza wanawake hawa wote?'

"Nilikuwa nimepoteza kila chembe ya hofu kwa mtu huyu. Alijaribu kuniangalia kwa ukali, lakini nilikuwa nikimtazama machoni," anasema.

Emmanuel, ambaye alikuwa sehemu ya kanisa kwa miaka 21 na alikaa zaidi ya muongo mmoja akiishi katika boma hilo akiwa mfuasi, anakumbuka siku hiyo waziwazi.

"Yeye [TB Joshua] alikuwa mtu wa kwanza kuanza kumpiga… kisha watu wengine wakajiunga," anasema.

"Alikuwa akisema: 'Je, unaweza kufikiria anachosema kunihusu?' Hata walivyokuwa wakimpiga, bado alikuwa akisema hayo hayo."

Ajoke anasema alitolewa nje ya ofisi yake na kuwekwa katika chumba mbali na waumini wengine wa kanisa, ambapo aliishi katika kifungo cha kijamii kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ni aina ya adhabu ndani ya Scoan inayojulikana kama "adaba", jambo ambalo Rae pia alipitia kwa miaka miwili.

Wakati huu Ajoke anasema mara kwa mara alipigwa na mikanda na minyororo, mara nyingi kila siku.

"Nashangaa jinsi nilivyoishi nyakati hizo. Sikuweza hata kusimama kwa siku kadhaa baada ya vipigo hivi. Sikuweza hata kuoga.

Alikuwa akijaribu sana kuwazuia watu kunisikiliza."

Siku moja Ajoke alipokuwa na umri wa miaka 19, anasema alisindikizwa hadi kwenye lango la mbele ya kanisa na kuachwa hapo. Walinzi wa kanisa, ambao walikuwa na silaha, waliambiwa asiruhusiwe kamwe kurudi ndani. Hii ilikuwa miaka sita kabla ya baba yake kufariki.

"Nilijipata bila makao. Sikuwa na mtu wa kufikia. Hakuna ambaye angeniamini. Hakuna kilichonitayarisha kwa maisha hayo," anasema.

Akiwa msichana asiye na pesa, Ajoke alifanya alichoweza ili kuishi na aliishi miaka mingi mitaani.

Aliwasiliana na BBC kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 baada ya kutazama ufichuzi wa BBC Africa Eye - na hivyo kuanza uchunguzi mrefu wa BBC kufichua unyanyasaji wa Scoan.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi huu. Haikuibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.

"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," ilisema.

Kwa usaidizi wa wanafunzi wa zamani na baadhi ya marafiki wa karibu, hivi majuzi Ajoke aliweza kuondoka mitaani.

Lakini imesababisha vipindi ambapo amekuwa na shida na afya yake ya akili.

Hata hivyo baada ya kila kitu ambacho amepitia, amebakia kuamua kusema ukweli kuhusu baba yake.

"Kila nilipopigwa, kila nilipodhalilishwa, ilinikumbusha tu kwamba kulikuwa na shida kwenye mfumo," anasema.

Wanafunzi wa zamani wameambia BBC kwamba kuona Ajoke akimpinga mwanamume huyu ilikuwa mojawapo ya sababu kuu za kuanza kutilia shaka imani yao kwa TB Joshua.

"Alituweka sote katika utumwa, utumwa kamili," anasema Emmanuel.

"Ajoke alikuwa na ujasiri wa kukabiliana naye. Ninamwona kama shujaa."

Ukweli, Ajoke anasema, ni jambo muhimu zaidi kwake: "Nilipoteza kila kitu, nyumba yangu, familia yangu, lakini kwangu, ukweli ndilo jambo la msingi.

"Na kwa muda mrefu kama kuna pumzi ndani yangu, nitatetea hilo, hadi mwisho."

Ndoto zake ni siku moja arudi shule na kumaliza elimu yake ambayo ilikatizwa.

Uchunguzi huu wa Africa Eye ulifanywa na Charlie Northcott, Helen Spooner, Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward. chanzo. BBC
 
Bwanae huna habari zingine tofauti na hii? Tumekuchoka pimbi wewe
 
Tutaaminije story za upande mmoja? Nadhani wanafunzi wa Tb Kishua bado wapo ataje hata mtu mmoja kwamba fulani alinipiga ili ashitakiwe, kumbe anadai Tb Joshua ni baba yake, watoto wa pembeni ni vimeo, anataka mpunga ili na yeye awe sehemu ya mali za Tb Joshua
 
hata kama jamaa ni mbaya kweli ila hizi stori kwa sasa hazisaidii kitu maana ni za upande mmoja tu
 
Alishikwa na mapepo tu huyo Akoje. Na ni muongo kama BBC.

Sijui Akoje!

Masaliti haya ya Afrika
 
Kama ni kweli aisee mzee halikiwa hatari mnoo
"Katika siku ile Mungu atakapozihukumu SIRI ZA WANADAMU, sawasawa na injili yangu, kwa Kristo Yesu". WARUMI 2:16. NB: sisi wanadamu tunazo siri zetu. Twaweza kumwona kwa nje mtu ni mstaarabu kumbe jambazi, au anazini nk nk. Toba ya kweli ni kule kutubia mambo yetu ya siri na kuamua kuyaacha.
 
th

10 Januari 2024
Na Charlie Northcott, Helen Spooner & Tamasin Ford
BBC Africa Eye

BBC inafichua jinsi kiongozi wa kanisa kuu marehemu TB Joshua, ambaye anatuhumiwa kwa uhalifu wa kingono kwa wingi, alimfungia bintiye mwenyewe na kumtesa kwa miaka kadhaa kabla ya kumwacha bila makao katika mitaa ya Lagos, Nigeria.
Onyo: Ina maelezo ambayo baadhi ya wasomaji wanaweza kuhuzunishwa nayo
"Baba yangu alikuwa na woga, hofu ya mara kwa mara.

Aliogopa sana kwamba mtu angezungumza," anasema mmoja wa binti za mhubiri, Ajoke - mfichua ukweli wa kwanza kufikia BBC kuhusu unyanyasaji alioshuhudia katika kanisa la babake,Kanisa la Sinagogi la Mataifa Yote (Scoan).

TB Joshua, aliyefariki mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 57, anatuhumiwa kwa unyanyasaji na mateso yaliyoenea kwa takriban miaka 20.

Sasa ana umri wa miaka 27, Ajoke anaishi mafichoni na ameacha jina lake la ukoo "Joshua" - BBC haichapishi jina lake jipya.

Machache yanajulikana kuhusu mama mzazi wa Ajoke, ambaye aliaminika kuwa mmoja wa washirika wa TB Joshua. Ajoke anasema alilelewa na Evelyn, mjane wa Joshua, tangu mapema anapokumbuka.

Hadi umri wa miaka saba, Ajoke anasema alikuwa na maisha ya furaha sana, akienda likizo na familia ya Joshua katika maeneo kama Dubai.

Lakini siku moja kila kitu kilibadilika. Alifukuzwa shule kwa kosa, na mwandishi wa habari wa eneo hilo aliandika makala akimtaja kama mtoto wa nje wa TB Joshua. Alitolewa shuleni na kupelekwa katika boma la Scoan huko Lagos.

"Nililazimishwa kuhamia kwenye chumba cha wanafunzi. Sikujitolea kuwa mfuasi. Nililazimishwa kujiunga," anasema.

Wanafunzi walikuwa kundi la wasomi wa wafuasi waliojitolea ambao walimtumikia TB Joshua na waliishi naye ndani ya muundo wa kanisa.

Walikuja kutoka duniani kote, wengi walikaa kwenye boma hilo kwa miongo kadhaa.

Waliishi chini sheria kali: Marufuku kulala kwa zaidi ya saa chache kwa wakati mmoja, kupigwa marufuku kutumia simu zao wenyewe au kupata barua pepe zao za kibinafsi, na kulazimishwa kumwita TB Joshua "Daddy".

"Wanafunzi walikuwa wamepewa mafunzo ya itikadi kali na walikuwa wawezeshaji wa madhila katika kanisa hilo. Kila mtu alikuwa akiigiza tu kwa kufuata amri - kama zombi.

Hakuna aliyekuwa akihoji chochote," anasema.

Akiwa mtoto tu, Ajoke hangefuata sheria kama wanafunzi wengine: alikataa kusimama wakati mchungaji alipoingia chumbani na kuasi amri kali za kulala.

Unyanyasaji ulianza hivi punde.
Muda mfupi baada ya kufika, akiwa na umri wa miaka saba, anakumbuka alipigwa kwa sababu ya kukojoa kitanda na kisha kulazimishwa kuzunguka kiwanja hicho na alama shingoni yake ikisema "Mimi hukojoa kitandani'

"Ujumbe kuhusu Ajoke ulikuwa kwamba alikuwa na pepo wabaya sana ambao walihitaji kufukuzwa," anasema mwanafunzi mmoja wa zamani wa kike.

"Kuna wakati katika mikutano ya wanafunzi - yeye [Joshua] alisema watu wanaweza kumpiga. Mtu yeyote katika bweni la kike angeweza tu kumpiga na nakumbuka kuona tu watu wakimpiga makofi walipokuwa wakipita," anasema.

Tangu wakati Ajoke alipohamia kanisani katika kitongoji cha Ikotun huko Lagos, alichukuliwa kama mtu aliyetengwa.

"Alikuwa, kama, aliyeitwa kondoo mweusi wa familia," anasema Rae, kutoka Uingereza, ambaye kwa miaka 12 aliishi kanisani kama mfuasi. Kama wanafunzi wengi wa zamani waliohojiwa na BBC, alichagua kutumia jina lake la kwanza pekee.

Rae anakumbuka wakati Ajoke alilala kwa muda mrefu sana, na Joshua akamfokea ainuke.

TH

CHANZO CHA PICHA,AFP
Maelezo ya picha,
Ajoke anasema baada ya kuteswa kwa miaka mingi alipoteza hofu yake kwa baba yake akiwa na umri wa miaka 17

Mwanafunzi mwingine alimpeleka kuoga na "kumchapa kwa waya ya umeme na kisha kuwasha maji ya moto", anasema.

Akikumbuka tukio hilo, Ajoke anasema: "Nilikuwa nikipiga kelele kwa sauti ya juu, na waliacha tu maji yakipita kichwani mwangu kwa muda mrefu sana."

Unyanyasaji kama huo haukuisha, anasema.

"Tunazungumza kuhusu miaka na miaka ya unyanyasaji.

Unyanyasaji wa mara kwa mara.

Kuwepo kwangu kama mtoto kutoka kwa mama mwingine kulidhoofisha kila kitu ambacho [TB Joshua] alidai kuwakilisha."
Unyanyasaji huo uliongezeka kwa kiwango tofauti alipokuwa na umri wa miaka 17 na kumkabili baba yake kuhusu "simulizi, za moja kwa moja, za watu ambao walifanyiwa unyanyasaji wa kijinsia".

"Niliwaona wanafunzi wa kike wakipanda chumbani kwake. Walikuwa wakienda kwa masaa mengi. Nilikuwa nikisikia mambo: 'Loh hii ilinipata.

Alijaribu kulala nami.' Watu wengi walikuwa wakisema kitu kimoja, "anasema.

BBC ilizungumza na zaidi ya wanafunzi 25 wa zamani - kutoka Uingereza, Nigeria, Marekani, Afrika Kusini, Ghana, Namibia na Ujerumani - ambao walitoa ushuhuda wenye nguvu wa kufanyiwa au kushuhudia unyanyasaji wa kingono.
"Sikuweza kuvumilia zaidi.

Niliingia ofisini kwake moja kwa moja siku hiyohiyo. Nilipiga kelele kwa sauti kuu: '

Kwa nini unafanya hivi?

Kwa nini unawaumiza wanawake hawa wote?'

"Nilikuwa nimepoteza kila chembe ya hofu kwa mtu huyu. Alijaribu kuniangalia kwa ukali, lakini nilikuwa nikimtazama machoni," anasema.

Emmanuel, ambaye alikuwa sehemu ya kanisa kwa miaka 21 na alikaa zaidi ya muongo mmoja akiishi katika boma hilo akiwa mfuasi, anakumbuka siku hiyo waziwazi.

"Yeye [TB Joshua] alikuwa mtu wa kwanza kuanza kumpiga… kisha watu wengine wakajiunga," anasema.

"Alikuwa akisema: 'Je, unaweza kufikiria anachosema kunihusu?' Hata walivyokuwa wakimpiga, bado alikuwa akisema hayo hayo."

Ajoke anasema alitolewa nje ya ofisi yake na kuwekwa katika chumba mbali na waumini wengine wa kanisa, ambapo aliishi katika kifungo cha kijamii kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Ni aina ya adhabu ndani ya Scoan inayojulikana kama "adaba", jambo ambalo Rae pia alipitia kwa miaka miwili.

Wakati huu Ajoke anasema mara kwa mara alipigwa na mikanda na minyororo, mara nyingi kila siku.

"Nashangaa jinsi nilivyoishi nyakati hizo. Sikuweza hata kusimama kwa siku kadhaa baada ya vipigo hivi. Sikuweza hata kuoga.

Alikuwa akijaribu sana kuwazuia watu kunisikiliza."

Siku moja Ajoke alipokuwa na umri wa miaka 19, anasema alisindikizwa hadi kwenye lango la mbele ya kanisa na kuachwa hapo. Walinzi wa kanisa, ambao walikuwa na silaha, waliambiwa asiruhusiwe kamwe kurudi ndani. Hii ilikuwa miaka sita kabla ya baba yake kufariki.

"Nilijipata bila makao. Sikuwa na mtu wa kufikia. Hakuna ambaye angeniamini. Hakuna kilichonitayarisha kwa maisha hayo," anasema.

Akiwa msichana asiye na pesa, Ajoke alifanya alichoweza ili kuishi na aliishi miaka mingi mitaani.

Aliwasiliana na BBC kwa mara ya kwanza mwaka wa 2019 baada ya kutazama ufichuzi wa BBC Africa Eye - na hivyo kuanza uchunguzi mrefu wa BBC kufichua unyanyasaji wa Scoan.

BBC iliwasiliana na Scoan na madai hayo katika uchunguzi huu. Haikuibu, lakini ilikanusha madai ya awali dhidi ya TB Joshua.

"Kutoa tuhuma zisizo na msingi dhidi ya Nabii TB Joshua si jambo geni... Hakuna madai yoyote yaliyowahi kuthibitishwa," ilisema.

Kwa usaidizi wa wanafunzi wa zamani na baadhi ya marafiki wa karibu, hivi majuzi Ajoke aliweza kuondoka mitaani.

Lakini imesababisha vipindi ambapo amekuwa na shida na afya yake ya akili.

Hata hivyo baada ya kila kitu ambacho amepitia, amebakia kuamua kusema ukweli kuhusu baba yake.

"Kila nilipopigwa, kila nilipodhalilishwa, ilinikumbusha tu kwamba kulikuwa na shida kwenye mfumo," anasema.

Wanafunzi wa zamani wameambia BBC kwamba kuona Ajoke akimpinga mwanamume huyu ilikuwa mojawapo ya sababu kuu za kuanza kutilia shaka imani yao kwa TB Joshua.

"Alituweka sote katika utumwa, utumwa kamili," anasema Emmanuel.

"Ajoke alikuwa na ujasiri wa kukabiliana naye. Ninamwona kama shujaa."

Ukweli, Ajoke anasema, ni jambo muhimu zaidi kwake: "Nilipoteza kila kitu, nyumba yangu, familia yangu, lakini kwangu, ukweli ndilo jambo la msingi.

"Na kwa muda mrefu kama kuna pumzi ndani yangu, nitatetea hilo, hadi mwisho."

Ndoto zake ni siku moja arudi shule na kumaliza elimu yake ambayo ilikatizwa.

Uchunguzi huu wa Africa Eye ulifanywa na Charlie Northcott, Helen Spooner, Maggie Andresen, Yemisi Adegoke na Ines Ward. chanzo. BBC
Kama ni ukweli basi 'this was a cult not a church '..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom