Uchaguzi 2020 Special Thread: Taarifa za Kampeni za Wagombea Urais kupitia CCM, Dkt. John Pombe Magufuli na Samia Suluhu

Yuko vizuri, Sera zake zinaeleweka kamanda, sio lazima kila mgombea aongee kama Lissu. CCM mbele kwa mbele, CCM tano tena.
 
 
Hapo ndipo huwa ananiacha hoi. Inakuwaje mtu unatumia muda na nguvu nyingi kupigania kitu cha kukitesa wakati kwako una miradi na mazingira ya kukuwezesha kujipumzisha tu! Yaani unaishi bila shaka lolote?!
 
Kwakweli CCM imejiimalisha sana. Kuna watu wanaponda mfumo wa kampeni za kuambatana na wasanii lakini ukweli ni kwamba wanaumia kimoyomoyo.

Kampeni za CCM ni raha, burudani mda mwingi, mtu unasikiliza sera huku ukiburudika.
Kuna watu wanasema kazi na bata, hii ya ccm ni kampeni na bata wakubwa wakubwa.

Hongereni sana wasanii na ccm kwa ujumla. Tuko nanyi kila sehemu.
 
.. Salaaam

Kumekuwa na Sintofahamu juu ya chama cha CCM na mgombea wake Dr John Pombe Magufuli juu Upatikanaji wa Tume Huru na Katiba Mpya.

Tofauti na vyama vingine Kama CHADEMA, ACT WAZALENDO N.K Ambao wao katika Ilani na Sera zao wameipa Kipaumbele KATIBA MPYA NA TUME HURU YA UCHAGUZI, Tena wameenda mbali na kusisitiza kuwa Litakuwa jambo la kwanza kulifanya Tena kwa Haraka kupitia Rasimu ile ya JAJI WARIOBA.

Chama cha CCM wao hawana muda Kabisa na Katiba Mpya na Tume Huru Tena katika Miaka mitano (5) ya Magufuli aliipinga vikali wakati ni hitaji la Watanzania.

Sasa kwa kuwa Hawa ccm wanajifanya kuikwepa Katiba na Tume Huru hatuna haja ya kuchagua watu wanaopenda Katiba ya KUTUTAWALA badala ya KUTUONGOZA.


Tundu Lissu Anatosha ndugu zangu.
 
Necccm ndo inayowabakiza madarakani ccm na katiba iliyopo ndo inayowaweka watoto wa dada kwenye vitengo nyeti...
 
Ulipozungumzia ilani umenikosha sana maana tokea kampeni zimeanza nimekua naitafuta ilani ya uchaguzi ya chadema bila mafanikio. Naomba unisaidie kuiweka hapa comrade nipate kuisoma.
 
Ulipozungumzia ilani umenikosha sana maana tokea kampeni zimeanza nimekua naitafuta ilani ya uchaguzi ya chadema bila mafanikio. Naomba unisaidie kuiweka hapa comrade nipate kuisoma.

Hatuwezi kuchagua chadema hawana ilani tuachagua CCM wanayo ilani nzuri
 
Hujui kuwa baba wa familia ndio anapanga chochote juu ya watoto pamoja na mkewe au mke ndio huwa anakupangia wewe kipi cha kufanya ndugu...!
Nchi sio familia ndugu... Huwezi kuongoza nchi Kama unavyoongoza mkeo gheto.

Hili ni Taifa
 
Ndugu mimi kama kawaida natumia platform kama hii nikiamini kipenzi changu mh ataona

Mh nilikuwepo leo pale Gymkana mjini Bukoba na nilishangaa kuona maaskari wakiwakamata sijui waliozomea kuwa hawakutaki baada ya ww kuwauliza kama wanakutaka. Sasa mh hili jambo la hasira ulipunguze tubaki kunadi sera zetu maana hata Yesu kunawaliompinga na pia hili jambo limeleta hasira kwa baadhi ya wana Bukoba mpaka kwa baadhi ya wana CCM wenzetu huku tukizokewa baada ya ww kuondoka hapa.

Sasa sisi watafuta kura tutapata wakati mgumu kuwafikia hawa wapga kura maana walishaanza kutengeneza na kuamini maneno atupashayo huyu kilema wa mguu Lissu. Rekebisha sana hasira mh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…