BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,393
8,161
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.
 
Ni sawa. Hakukuwa na haja ya kufanya hayo. Kwanza Sheria hizi hazihusiki na masuala ya uwekezaji wa Bandari
 
Back
Top Bottom