Mwanasheria Mkuu wa Serikali achia ngazi haraka sana, ni aibu kwa Serikali

JackisonDubai

JF-Expert Member
Mar 27, 2023
537
1,276
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
 
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.
dhui ya mapendekezo hayo.
Hii ya 2017 kipindi cha Magu mzalendo. Lazima sheria ilikuwa kwa manufaa ya nchi.Sasa wanafuta ili ziwe kwa manufaa ya wawekezaji.
 
Hawakutegemea kama pangekuwepo na huu upinzani toka kwa public, huyo mwanaaheria wa serikali unamuonea bure, yeye mwenyewe alitengwa ile siku wakiupitisha ule mkataba wa hovyo wa IGA, wabunge wakaimba jambo la mama yao lazima lipite.
 
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.
Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
AKIACHIA NGAZI NAJINYONGA PALE MNARA WA ASKARI POSTA SAA 4 ASUBUHI
 
Kwa mujibu wa katiba yetu mbovu mwanasheria anatumika tu kama toilet paper na mamlaka toka juu magogoni.

Huyu toilet paper siyo kwamba aliamua yeye kubadilisha hizo sheria bali ni yule mwenye toilet paper. Lkn kutokana na upepo kumwendea vibaya kaamua kughairi kwa muda.

Kumtaka huyu toilet paper ajiuzulu ni kumuonea tu
 
Back
Top Bottom