Serikali imependekeza Sheria zinazolinda Maliasili na Kuikinga Nchi na Mikataba Mibovu zisitumike kwa DP World

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,107
IMG-20230704-WA0166(1).jpg

Serikali ya Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria kadhaa bungeni ili sheria zote za zamani zinazokinzana na mkataba na DP world zibadilishwe ili ziendane na hiyo IGA ya Dubai Ports World ‼️

Angalieni

Muswada wa The Written Laws (Misc Amendment) No. 2 Bill, 2023 umesomwa kwa mara ya Kwanza tr. 28 June 2023. Kamati ya Utawala Katiba na Sheria itauchambua kwenye vikao vya Kamati Mwezi wa Nane (Kuanzia 14 August).

Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria Tano ikiwemo :

1. Sheria ya Chuo cha
Bahari Dar es Salaam, Sura ya 253;

2. Sheria ya Mamlaka ya Nchi
Kuhusiana na Umiliki wa Mali na Rasilimali Asilia, Sura ya 449;

3. Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusu Utajiri na Maliasilia za Nchi (Mapitio ya
Mikataba na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi), Sura ya 450 na

Hii ni sawa na kutudharau wananchi
Wanasema “kwani watatufanya nini?”
Jamani mliokuwa mnamsifia eti ni msikivu mbona mko kimya? 🤣
#TutaelewanaTu lakini

=============

Taarifa hii ni kwa Kwa mujibu wa Muswada wa Marebisho ya Sheria Mbalimbali No. 2 wa mwaka 2023 uliosomwa kwa mara kwanza Bungeni Dodoma, Juni 28, 2023.

Muswada huo unapendekeza kutotumika kwa Sheria mbili zilizopitishwa na Bunge mwaka 2017 kwa madhumuni ya Kulinda Rasilimali zote za Tanzania katika Miradi ya Uendelezaji na Uboreshaji wa Bandari endapo itakuwa imesharidhiwa na Baraza la Mawaziri.

Katika mapendekezo ya mabadiliko hayo, Muswada unataka Sheria hizi zisitumike ili kuwezesha Bandari za Tanzania zifanye kazi kwa Viwango vya Kimataifa zikipata Meli kubwa za Mizigo mikubwa.

Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili. The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignity) Act, 2017

Sheria inaweka bayana kuwa Maliasili ni mali ya Watanzania na zinasimamiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba yao.

Inaeleza kuwa Mikataba yote ya Uwekezaji katika Maliasili inatakiwa kuidhiniswa na Bunge.

Sheria inaweka wazi kuwa makubaliano yoyote ya Uwekezaji lazima yazingatie Uhuru na Haki ya Umiliki wa Watanzania juu ya Maliasili yao.

Inazuia utoroshaji wa Fedha zinazopatikana katika Uwekezaji wa Maliasili.

Sheria ya Mapitia na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Mikataba ya Maliasili za Nchi. The Natural Wealth and Resorces Contracts (Review and Re-negotiations of Unconscionable Terms) Act, 2027

Sheria inalipa Nguvu Bunge kupitia Mikataba yote inayoingiwa na Serikali kuhusiana na Maliasili za Tanzania.

Sheria hii kwa kupitia vifungu vyake inaweza vigezo kuwa Serikali inaweza kupitia upya Mikataba na Makubaliano ambayo hayana Maslahi kwa Taifa.

Attachments

  • THE_WRITTEN_LAWS_MISCELLANEOUS_AMENDMENTS_NO_2_BILL,_2023_2.pdf
    429.3 KB · Views: 7
Yule aliwakebehi waliopeleka kesi mahakamani aje asome hii ndiyo atajua hajui…
In real sense haiwezi kutumika kwa mikataba yao coz imeendwa baada ya kesi kuwa mahakamani.
Kibaya zaidi serikali inazidi kumwaga mafuta kwenye moto….
 
View attachment 2678469
Serikali ya Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria kadhaa bungeni ili sheria zote za zamani zinazokinzana na

sifia eti ni msikivu mbona mko kimya? 🤣
#TutaelewanaTu lakini
Hilo bunge linakaa nyumbani kwenu? Kuna bunge sahivi? Hivi huoni aibu kuleta uzushi wa kipuuzi km huu? Acheni rais afanye kazi yake, km we unaihitaji subiri 2025 uchukue fomu.
 
View attachment 2678469
Serikali ya Samia imepeleka muswada wa mabadiliko ya sheria kadhaa bungeni ili sheria zote za zamani zinazokinzana na mkataba na DP world zibadilishwe ili ziendane na hiyo IGA ya Dubai Ports World ‼️

Angalieni

Muswada wa The Written Laws (Misc Amendment) No. 2 Bill, 2023 umesomwa kwa mara ya Kwanza tr. 28 June 2023. Kamati ya Utawala Katiba na Sheria itauchambua kwenye vikao vya Kamati Mwezi wa Nane (Kuanzia 14 August).

Muswada huu unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria Tano ikiwemo :

1. Sheria ya Chuo cha
Bahari Dar es Salaam, Sura ya 253;

2. Sheria ya Mamlaka ya Nchi
Kuhusiana na Umiliki wa Mali na Rasilimali Asilia, Sura ya 449;

3. Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusu Utajiri na Maliasilia za Nchi (Mapitio ya
Mikataba na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi), Sura ya 450 na

Hii ni sawa na kutudharau wananchi
Wanasema “kwani watatufanya nini?”
Jamani mliokuwa mnamsifia eti ni msikivu mbona mko kimya? 🤣
#TutaelewanaTu lakini
 
Attachments

  • IMG_1035.MP4
    13.1 MB
  • 455F5E30-0CDD-4014-BB86-6AFDD4C52E6C.jpeg
    455F5E30-0CDD-4014-BB86-6AFDD4C52E6C.jpeg
    71 KB · Views: 9

Back
Top Bottom