Kila kilichosainiwa na Hayati Magufuli kitaendelea, hatimae Bunge waigomea Serikali

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,755
15,234
Serikali imeyaondoa mapendekezo yaliyopelekwa Bungeni ya kufanya marekebisho ya sheria ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017 na Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 kuwa zisitumike katika miradi ya bandari.

Sheria hizo zilikuwa ni miongoni mwa sheria zilizojumuishwa katika Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 2 wa Mwaka 2023, uliokusudia kurekebisha, pamoja na sheria nyingine, sheria hizo mbili ili zisitumike katika uendeshaji wa miradi ya uendeshaji, uendelezaji na bandari.

Taarifa ya kuondolewa kwa marekebisho hayo ilitolewa leo Jumanne, Agosti 29, 2023, na Spika wa Bunge Tulia Ackson.

“Sehemu ya nne inafutwa ambayo inahusu mabadiliko kwenye sheria yetu ile ya marekebisho ya Sheria ya Mamlaka ya Nchi Kuhusiana na Umiliki wa Maliasili ya mwaka 2017, mapendekezo yaliyokuwa yameletwa yanafutwa yote,” alitamka Dk Ackson.

“Sehemu ya tano inahusu marekebisho ya Sheria ya Mapitio na Majadiliano Kuhusu Masharti Hasi Katika Maliasili ya nchi ya mwaka 2017 nayo inafutwa kwa maana ya kwamba Bunge halijaafiki,” aliongeza kiongozi huyo.

Hatua hii ya Bunge inakuja siku tano tangu The Chanzo iongee na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Masuala ya Kisheria, Joseph Mhagama, ambaye alieleza kuwa Kamati yake ilisitisha kupokea maoni juu ya mabadiliko haya yaliyopendekezwa na Serikali kwa sababu ilihitaji maelezo zaidi juu ya maudhui ya mapendekezo hayo.
 
Na Bunge lenyewe lilivyofubaa, mi sina muda wa kuunguza bando.

Bunge "mali" ni lile live la R.i.p Sitta lililomfurusha Lowasa.

Aah hilo!

Miye nilikuwa nashinda kwenye Tv hatua kwa hatua.

Anyway, ako ka clip nitakasamamba nijiridhishe na hiyo kauli
 
Back
Top Bottom