Mwande na Mndewa
JF-Expert Member
- Feb 26, 2021
- 949
- 2,865
Ikumbukwe wakati sheria ya kulinda rasilimali za taifa inatungwa mwaka 2017 Mh Waziri mkuu alikuwepo,Spika alikuwepo wakati huo alikuwa Naibu Spika,Rais alikuwepo wakati huo alikuwa Makamu wa Rais,Waziri wa fedha alikuwepo wakati huo alikuwa Waziri wa Sheria, na wabunge waliopitisha bungeni ni awa awa wa CCM, watu ni walewale na chama ni kilekile waliotaka na kuona kuna umuhimu wa kutunga sheria ya kulinda rasilimali za taifa lakini sasa ni haohao hawaitaki tena hiyo sheria, wanaona hamna haja ya kuwa na sheria hiyo tena ya kulinda rasilimali za taifa.!
Wananchi wanapiga kelele wanasema ibara ya 20 katika mkataba wa bandari ibadilishwe kwa kuwa inakwenda kinyume na kifungu cha 11 cha sheria ya mamlaka ya nchi kuhusiana na umiliki wa rasilimali na maliasili zetu,sheria ya mwaka 2017 aliyoipitisha Hayati Rais John Pombe Magufuli (The natural wealth and resources permanent sovereignty) act no 5 ya mwaka 2017 inayosema mgogoro wowote wa rasilimali na maliasili ya nchi utatatuliwa hapa hapa Tanzania na kwa sheria za Tanzania, sio kwenda nje ya nchi wakati rasilimali na maliasili ni zetu.
Kama kweli wanataka kufuta sheria hiyo aliyoipitisha Hayati Rais Magufuli, Swali langu ni hili.
Je wakati wanaitunga na kuipitisha hii sheria waliipitisha kwa kuwa walikuwa na uchungu wa rasilimali za taifa kutoka moyoni? Au walipitisha tu kwa sababu tu Rais alikuwa ni Magufuli?
#WatanzaniaTuipendeNchiYetu.