Ramadhan Special Thread
Assalaam alaikum warahmatullah wabrakatuh,,

Moja ya haki ambazo tutazipata kwa ALLAH ni kutodhulimiwa kwa jambo lolote lile,hapa duniani haki ya mtu hununuliwa,hubagazwa ,mwenye nacho ndio mwenye kunufaika na haki

Lakini kwa Allah hakika kuna uadilifu mkubwa mno,miongoni mwa uadilifu huo ni mja kutodhulumiwa amali zake au matendo yake,iwe amali za kheri ataziona na ima ni amali za uovu ataziona

Screenshot_20260203-133333_Msahafu wa Kiswahili Quran  .jpg

Hakika kila nafsi itapata haki yake,hata kama ni amali ndogo mfano wa punje ya mchanga iwe ya kheri au shari mja ataiona kwenye daftari lake,ndio maana tunaambiwa kwenye qur'an na Allah kwamba,kafir au waovu siku hiyo baada ya kupokea madaftar yao,watasema hili daftar lina nini haliachi kubwa wala dogo yote yamehudhurishwa hapo.

Kuna mambo ambayo kwa mtazamo wetu tunayaona ni madogo lakini hakika mbele ya Allah yana uzito wake,na yote hayo yapo kwenye records zetu

Kwahiyo ndugu zangu katika imani tutambue kila kitu tunachofanya kinadhibitiwa,hapa unaposoma andiko hili sasa unarekodiwa,kwahiyo tujue tupo ndani ya uangalizi wa Malaika waandishi ambao kutwa kucha wapo nasi wanapeana zamu tu,wakati wa Al asir inasemwa ndio hubadilishana shift,ndio maana hii swala ya Kati na kati imesisitizwa kuzingatiwa,ripoti zinapandishwa mbinguni kwamba mja wa Allah tumemuacha akiswali.

Allah tuongoze tuwe watu wenye kusikia maneno ya haki na kuyafuata,amiin
 
Nabii Musa Alayhi ssalaam alimuuliza Allah subhanahu wataala:

Yaa Rabbi! Umemuumba Adam kwa dhati yako. Ukampulizia roho kutoka kwako. Malaika walimsujudia kwa heshima uliyompa kutoka kwako. Na ukamuingiza kwenye pepo yako. Na uliikubali toba yake alipokukosea. Alikushukuru kwa namna gani kwa zote hizi neema ulizompatia?

"Faqaala lahullahu Yaa Musa! Yakfii min Adam annahu qaala Alhamdulillah rabbil alaamiin".

Allah akamwambia: Ewe Musa! Ilitosha kwa Adam, kwake yeye alisema Alhamdulillah rabbil alaamiin.

Hivyo, tusikose kumshukuru Mungu ama kutoa shukrani kwake. “Alhamdulillah rabbil alamin” ni ya kipekee kwa sababu imekusanya kumshukuru Allah kwa utukufu wake wote, inatambua udhibiti wake juu ya ulimwengu, inapanua shukrani kwa kila kiumbe, na ni msingi wa kila ibada ya kweli.
 
Ibilisi alisema kwa kumwambia Allah subhanahu wataala: "Nina apa kwa utukufu wako na kwa nguvu zako nitaendelea kuwapotosha waja wako kwa kadri roho zao bado zimo kwenye kiwiliwili chao (kwa maana; maadamu bado wapo hai nitaendelea kuwapotosha na hutapata wenye kukushukuru wewe)".

Akasema Allah rabbul izza: Nina apa kwa utukufu wangu na kwa nguvu zangu, nitaendelea kuwasamehe (waja wangu) mradi tu wataniomba msamaha wangu.
-------------------
Kuna nyakati huwa zinamfika binaadamu na kumsahau Allah. Katika kumsahau Mola wake binadamu huwa anafanya madhambi na wakati mwengine huwa anafikia kufanya kufru. Unapofika wakati anataka kurudi kwa Allah huwa anajihisi haya kwa madhambi aliyoyafanya. Anajiona haya hata kutaja jina la Mola wake.

Hakika ya Allah yeye alishasema: "Yeye ni arrahmani arrahiim". Yeye ni mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Ni mwenye kusamehe na kwake hilo lipo.

Mmoja katika watu alifika kwenye Kaaba na akisema; Ya Allah nimekukosea mimi, lakini naona aibu kukuelekea wewe kwa dhambi nilizofanya. Lakini ni nani nitakayemuomba zaidi ya wewe? Ninataka msamaha kutoka kwako ewe Mola wangu.

Mmoja katika watu qaumu ya Nabii Musa Alayhi ssalaam alikuwa ni mwenye kuabudu sanamu. Katika ibada zake alikuwa ni mwenye kusema; Ewe sanamu niponye, ewe sanamu niruzuku mimi, ewe sanamu nisamehe.

Siku hiyo ulimi wake uliteleza katika kufanya ibada yake. Alupotaka kutamka ya swanamu ukatamka ya Swamad, Allah subhanahu wataala akajibu kwa kuitikia "labbayka yaa abdi" (nipo hapa ewe mje mja wangu).

Nabii Musa Alayhi ssalaam akasema; "Ewe Mola wangu! Unajibu kwa kumwitikia wito wake wakati huyo mtu anaabudu usiyekuwa wewe?" Allah subhanahu wataala akamjibu akamwambia "Ewe Musa! Kuna Asswamad (tegemeo wa kila kitu ambaye hategemei chochote) mwengine zaidi yangu?"

Hivyo, tusikate tamaa kumuomba Allah msamaha. Allah ni mwenye huruma sana, tena sana. Halikadhalika, tusiwakatishe tamaa watu ambao wanataka kurudi kwa Allah subhanahu wataala.
 
Nabii Musa Alayhi ssalaam alimuuliza Allah subhanahu wataala:

Yaa Rabbi! Umemuumba Adam kwa dhati yako. Ukampulizia roho kutoka kwako. Malaika walimsujudia kwa heshima uliyompa kutoka kwako. Na ukamuingiza kwenye pepo yako. Na uliikubali toba yake alipokukosea. Alikushukuru kwa namna gani kwa zote hizi neema ulizompatia?

"Faqaala lahullahu Yaa Musa! Yakfii min Adam annahu qaala Alhamdulillah rabbil alaamiin".

Allah akamwambia: Ewe Musa! Ilitosha kwa Adam, kwake yeye alisema Alhamdulillah rabbil alaamiin.

Hivyo, tusikose kumshukuru Mungu ama kutoa shukrani kwake. “Alhamdulillah rabbil alamin” ni ya kipekee kwa sababu imekusanya kumshukuru Allah kwa utukufu wake wote, inatambua udhibiti wake juu ya ulimwengu, inapanua shukrani kwa kila kiumbe, na ni msingi wa kila ibada ya kweli.
🙏🏻🙏🏻🙏🏻🙏🏻
 
Nilikuwa naomba utupe darasa namna ya kutawaza na kuanza kuswali na hatua zake zote kama itapendeza utuandikie kwa kiarabu na utafsili kk wa kiswahili kwa asiyejua imraisishie kutamka natanguliza shukran kwa tunapo iendea Ramadhan
Ngoja aje kukupa muongozo.
 
Nilikuwa naomba utupe darasa namna ya kutawaza na kuanza kuswali na hatua zake zote kama itapendeza utuandikie kwa kiarabu na utafsili kk wa kiswahili kwa asiyejua imraisishie kutamka natanguliza shukran kwa tunapo iendea Ramadhan
Bismillahi Rrahmani Rrahiim

Sifa njema na shukrani za dhati zinamstahiki Mola ambaye amewapa ubora wanaadamu kwa elimu na matendo juu ya viumbe vyote.

Na rehma na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad Bwana/Kiongozi wa waarabu na wasiyo waarabu, na rehma na amani ziwe juu ya watu wa nyumbani kwake (familia yake) na sahaba zake ambao ni chemchemi za elimu na hekima.

Ijapokuwa ombi lilielekezwa kwa mtu mwengine ila si vibaya kusaidiana katika kheri. Kuhusu udhu tutakwenda hatua kwa hatua kama mtiririko wa vitabu vya fiqhi vilivyoanza kwa kuweka wepesi na mtu apate uelewa wa haraka kuhusiana na suala zima la udhu na kuendea ibada.

Kwenye udhu kuna vipengele vifuatavyo:
1)Furuudhul udhui (faradhi za udhu)
2)Sunanil udhui (sunna za udhu)
3)Nawaaqidhul udhui(vitenguzi vya udhu). Aidha, kuna;
4)Sharti za udhu.

I: FARDHI ZA UDHU
Fardhi za udhu zipo 6. Ya kwanza ni;
1)Nia
2)Kuosha uso
3)Kuosha mikono mpaka kwenye mirfaqi
4)Kupaka maji kichwani
5)Kuosha miguu mpaka kwenye vifundo vya miguu (kurefusha kiasi si mbaya)
6)Kufuata utaratibu.

I:1 UFAFANUZI NIA
Fardhi ina maanisha vitu vya lazima. Nia ni wakati unaosha uso kwa wakati mmoja. Ukipenda unaitamka ukipenda inakaa moyoni.

I:2 KUOSHA USO
Uso ki fiqhi wanaufafanuaje: Uso ni kuanzia maoteo ya nywele kutoka juu mpaka chini ya taya kwa urefu (na taya inaishia karibia na shingo). Sikio mpaka sikio kwa upana. Sehemu yote ya uso lazima ipate maji. Ikiwa una ndevu chache lazima zishike maji. Ikiwa una ndevu nyingi ni zishike maji kwa nje si lazima uzitifue zishike maji mpaka ndani.

I:3 KUOSHA MIKONO
Kuosha mikono ni mpaka kwenye mirfaqi (kifundo cha juu kuelekea sehemu yenye kigimbi). Ikiwa kama mtu alipata ajali kikabakia kiwiko basi aoshe sehemu iliyobaki. Ikiwa kama imekatika mpaka kwenye mirfaqi basi aoshe sehemu ya juu iliyobaki hata kama kwa udogo.

I:4 KUPAKA MAJI KICHWANI
Hapa faradhi ni kupaka maji sehemu ya kichwa tena mara moja, si kichwa kazima (sunna ndiyo kichwa kizima ila faradhi ni sehemu ya kichwa).

I:5 KUOSHA MIGUU
Kuosha miguu mpaka kwenye vifundo viwili vya miguu na kuhakikisha vidole navyo vinapata maji.

I:6 KUFUATA UTARATIBU
Nao ni kama ulivyoelezewa kwa mtiririko wa juu. Ikiwa uliosha uso na upo kwenye hatua ya kuosha miguu na ukagundua kuna sehemu ya uso haijapata maji, basi unatakiwa kuanzia hapo hapo kwenye uso na uhakikisha wote unapata maji na kisha unamalizia kwa utaratibu kama nilivyoelezea juu. Ikiwa ni mikono nayo ukagundua haikushika maji yqani hukuosha vizuri basi utaanzia hapo hapo kwenye mikono na kisha kuendelea na utaratibu.

II: SUNANIL UDHUI (SUNNA ZA UDHU)
Sunna za udhu ni zifuatazo: Kupiga mswaki, kusema bismillah, kuosha viganja viwili kabla ya kuingiza mikono kwenye chombo (ikiwa unatumia chombo), kusukutua, kupandisha maji puani, majosho kuyafanya mara tatu, na sunna ya kichwa kupaka maji kichwa kizima yaani chote. Kuesua vidole vya miguu kwa kutumia kidole kidogo cha mkono wa kushoto kwa kuanzia kidole kidogo cha mwisho wa mguu wa kulia mpaka kurudi nyuma kidole gumba cha mguu wa kulia na kisha kuanzia kidole gumba cha mguu wa kushoto mpaka kumalizia kabisa n.k Pia unasomo dua ya kumaliza kushika udhu.

NB: NAMNA YA KUTIA UDHU
Utaanza kwa kusema Bismillahi , kisha;
1)Utaosha viganja vyako mara 3, kisha
2)Utasukutua maji mdomoni mara 3
3)Kisha, utapandisha maji puani na kupenga × 3, kisha
4)Utaosha uso × 3 (kwa utaratibu wa juu kama ulivyofafanuliwa, na kwa wakati huo unaitamka Nia yako kwa maana moyo wako uwe dhahiri kuwa unatia udhu). Kisha,
5)Utaosha mikono ×3 (kurefusha mpaka juu yake si mbaya)Kisha
6)Utapaka maji kichwani kwa viganja vyako kushika maji kisha utapaka kwa kuanza mbele sehemu ya kichwa na mikono yako utairudisha nyuma ya kichwa na kisha unaipeleka mbele, na hali ya kuwa unamaliza tukio la mikono kumalizikia kwa mbele, vidole vyako vya shahada vyote viwili unasafisha masikio kwa ndani na vidole gumba vinasafisha kwa nje. Hili tukio unafanya mara moja.
7)Kisha, unamalizia kwa kuosha miguu (kurefusha mpaka juu yake si mbaya) kama utaratibu wa juu ulivyoelezewa
8)Baada ya hapo unamalizia dua ya kutia udhu.

Nayo ni hii: Ash hadu anlaa ilaha illallah wah daw laa shariika lah wa ash hadu anna muhammadan abduhu warasuuluh, Allahummaja-alnii minal mutatwahhirin waja-alnii min ibaadikas swaalihiin subhanakallahuma wabihamdika, ash hadu anlaa ilaha illa anta astaghfiruka wa-atuubu ilayka.

Utiaji udhu wa namna hii ni kwa mujibu wa mwenendo wa Imam Shafii.
 
Bismillahi Rrahmani Rrahiim

Sifa njema na shukrani za dhati zinamstahiki Mola ambaye amewapa ubora wanaadamu kwa elimu na matendo juu ya viumbe vyote.

Na rehma na amani ziwe juu ya Mtume Muhammad Bwana/Kiongozi wa waarabu na wasiyo waarabu, na rehma na amani ziwe juu ya watu wa nyumbani kwake (familia yake) na sahaba zake ambao ni chemchemi za elimu na hekima.

Ijapokuwa ombi lilielekezwa kwa mtu mwengine ila si vibaya kusaidiana katika kheri. Kuhusu udhu tutakwenda hatua kwa hatua kama mtiririko wa vitabu vya fiqhi vilivyoanza kwa kuweka wepesi na mtu apate uelewa wa haraka kuhusiana na suala zima la udhu na kuendea ibada.

Kwenye udhu kuna vipengele vifuatavyo:
1)Furuudhul udhui (faradhi za udhu)
2)Sunanil udhui (sunna za udhu)
3)Nawaaqidhul udhui(vitenguzi vya udhu). Aidha, kuna;
4)Sharti za udhu.

I: FARDHI ZA UDHU
Fardhi za udhu zipo 6. Ya kwanza ni;
1)Nia
2)Kuosha uso
3)Kuosha mikono mpaka kwenye mirfaqi
4)Kupaka maji kichwani
5)Kuosha miguu mpaka kwenye vifundo vya miguu (kurefusha kiasi si mbaya)
6)Kufuata utaratibu.

I:1 UFAFANUZI NIA
Fardhi ina maanisha vitu vya lazima. Nia ni wakati unaosha uso kwa wakati mmoja. Ukipenda unaitamka ukipenda inakaa moyoni.

I:2 KUOSHA USO
Uso ki fiqhi wanaufafanuaje: Uso ni kuanzia maoteo ya nywele kutoka juu mpaka chini ya taya kwa urefu (na taya inaishia karibia na shingo). Sikio mpaka sikio kwa upana. Sehemu yote ya uso lazima ipate maji. Ikiwa una ndevu chache lazima zishike maji. Ikiwa una ndevu nyingi ni zishike maji kwa nje si lazima uzitifue zishike maji mpaka ndani.

I:3 KUOSHA MIKONO
Kuosha mikono ni mpaka kwenye mirfaqi (kifundo cha juu kuelekea sehemu yenye kigimbi). Ikiwa kama mtu alipata ajali kikabakia kiwiko basi aoshe sehemu iliyobaki. Ikiwa kama imekatika mpaka kwenye mirfaqi basi aoshe sehemu ya juu iliyobaki hata kama kwa udogo.

I:4 KUPAKA MAJI KICHWANI
Hapa faradhi ni kupaka maji sehemu ya kichwa tena mara moja, si kichwa kazima (sunna ndiyo kichwa kizima ila faradhi ni sehemu ya kichwa).

I:5 KUOSHA MIGUU
Kuosha miguu mpaka kwenye vifundo viwili vya miguu na kuhakikisha vidole navyo vinapata maji.

I:6 KUFUATA UTARATIBU
Nao ni kama ulivyoelezewa kwa mtiririko wa juu. Ikiwa uliosha uso na upo kwenye hatua ya kuosha miguu na ukagundua kuna sehemu ya uso haijapata maji, basi unatakiwa kuanzia hapo hapo kwenye uso na uhakikisha wote unapata maji na kisha unamalizia kwa utaratibu kama nilivyoelezea juu. Ikiwa ni mikono nayo ukagundua haikushika maji yqani hukuosha vizuri basi utaanzia hapo hapo kwenye mikono na kisha kuendelea na utaratibu.

II: SUNANIL UDHUI (SUNNA ZA UDHU)
Sunna za udhu ni zifuatazo: Kupiga mswaki, kusema bismillah, kuosha viganja viwili kabla ya kuingiza mikono kwenye chombo (ikiwa unatumia chombo), kusukutua, kupandisha maji puani, majosho kuyafanya mara tatu, na sunna ya kichwa kupaka maji kichwa kizima yaani chote. Kuesua vidole vya miguu kwa kutumia kidole kidogo cha mkono wa kushoto kwa kuanzia kidole kidogo cha mwisho wa mguu wa kulia mpaka kurudi nyuma kidole gumba cha mguu wa kulia na kisha kuanzia kidole gumba cha mguu wa kushoto mpaka mpaka kumalizia kabisa n.k Pia unasomo dua ya kumaliza kushika udhu. Kuanza kwa upande wa kulia na kisha kumalizia wa kushoto n.k

NB: NAMNA YA KUTIA UDHU
Utaanza kwa kusema Bismillahi , kisha;
1)Utaosha viganja vyako mara 3, kisha
2)Utasukutua maji mdomoni mara 3
3)Kisha, utapandisha maji puani na kupenga × 3, kisha
4)Utaosha uso × 3 (kwa utaratibu wa juu kama ulivyofafanuliwa, na kwa wakati huo unaitamka Nia yako kwa maana moyo wako uwe dhahiri kuwa unatia udhu). Kisha,
5)Utaosha mikono ×3 (kurefusha mpaka juu yake si mbaya)Kisha
6)Utapaka maji kichwani kwa viganja vyako kushika maji kisha utapaka kwa kuanza mbele sehemu ya kichwa na mikono yako utairudisha nyuma ya kichwa na kisha unaipeleka mbele, na hali ya kuwa unamaliza tukio la mikono kumalizikia kwa mbele, vidole vyako vya shahada vyote viwili unasafisha masikio kwa ndani na vidole gumba vinasafisha kwa nje. Hili tukio unafanya mara moja.
7)Kisha, unamalizia kwa kuosha miguu (kurefusha mpaka juu yake si mbaya) kama utaratibu wa juu ulivyoelezewa
8)Baada ya hapo unamalizia dua ya kutia udhu.

Nayo ni hii: Ash hadu anlaa ilaha illallah wah daw laa shariika lah wa ash hadu anna muhammadan abduhu warasuuluh, Allahummaja-alnii minal mutatwahhirin waja-alnii min ibaadikas swaalihiin subhanakallahuma wabihamdika, ash hadu anlaa ilaha illa anta astaghfiruka wa-atuubu ilayka.

Utiaji udhu wa namna hii ni kwa mujibu wa mwenendo wa Imam Shafii.
Shukran sana kwa darasa mungu akuzishie ingependeza ungetupa pia darasa la namna ya kufanya Ibada,(kuswali) hatua kwa hatua
 
Shukran sana kwa darasa mungu akuzishie ingependeza ungetupa pia darasa la namna ya kufanya Ibada,(kuswali) hatua kwa hatua
Shukrani akhi; ningependelea kumalizia vitenguzi vya udhu kisha tutaingia kwenye suala la swala inshaallah.

VITENGUZI VYA UDHU

Vitenguzi vya udhu ni 4

1) Kutokwa na kitu chochote maumbile ya mbele au nyuma isipokuwa kutokwa na manii (nadhani hapa nimeeleweka).

2) Kutokwa na akili (aidha mtu awe amekumbwa au ana ugonjwa wa kifafa) au awe amelewa au kushikwa na usingizi ila isipokuwa kulala kwa kuambatisha makaadi kwenye ardhi.

3) Kumgusa mwanamke pasi na kizuizi

4)Kushika sehemu za siri za binadamu kwa matumbo ya viganja. Ziwe zako au za mwengine.

Mbeleni inshaallah tutaendelea na sharti za udhu. Ila kwa hapa tunaweza kuzungumzia suala la kuanza kuswali.

MLANGO WA SWALA
Kwanza kuna nguzo zake, zipo 17. Nazo;

1) Al qiyam (kusimama)

2)Nia (nako ni kutia nia)

3)Takbira ya kuhirimia (Allahu akbar)

4) Kusoma suratl fat-ha

5) Kurukuu

6) Kuwa na utulivu ndani yake

7)Kuitidali

8)Kuwa na utulivu ndani yake

9)Kusujudu (Mara 2)

10) Kuwa na utulivu ndani yake

11)Kitako baina ya sijida 2

12) Kuwa na utulivu ndani yake

13)Kukaa Tashahud ya kwanza

14) Kukaa tashahud ya mwisho

15) Kumswalia mtume kwenye tashahud

16)Kutoa salamu

17)Kufuatisha taratibu za nguzo

UFAFANUZI
1: QIYAM (KISIMAMO)

Kwenye swala ya fardhi ni lazima kusimama labda uwe na maradhi. Na sharti ya kusimama kwake ni lazima unyoke, yaani uti wa mgongo unyoke. Hata mtu akikona anasema yule amesimama. Usiwe umeelemea mbele wala nyuma. Ikiwa mtu amesimama tofauti haonekani mwenye kusimama na akiwa hana changamoto zozote za kimaumbile au maradhi basi kisimamo chake hakitoswihi. Kwa maana utakuwa umevunja nguzo ya swala hivyo swala nayo itakuwa imekwisha haribika.

2: NIA
Nia ni nguzo katika swala. Kwa mwenendo wa Imam Shafii kuna azma maana yake ni kuamua, kuna nia nako ni kukusudia kile ambacho unafanya. Umeazimia kuchimba mtaro lakini kitendo cha kuchimba ni kutimia kwa kusudi. Hivyo, nia ni nguzo ya pili. Nia inatekelezwa kwa namna mbili; Aidha kwa kuitamka au kwa kuidhihirisha moyoni.

3: TAKBIRA YA KUHIRIMIA (ALLAH AKBAR) YA KUFUNGULIA SWALA
Nayo ni Allahu Akbar! Itamkwe kama ilivyo. Isiwekwe madda mahali ambapo sipo na isizidishwe irabu mahali ambapo sipo. Ikitamkwa tofauti na kwa ni nguzo ya swala basi swala yako itakuwa haijaswihi. Pia, Ina sharti zake nazo 16. Tutaziongelea baadaye inshaallah.

4: KUSOMA SURAT FAT-HA
Suratul Fat-ha ni nguzo na bismillahi yake. Ina aya 7. Inasomwa kwa kila rakaa isipokuwa kwa rakaa kutorokwa, yaani; unafunga swala halafu kisha Imam anaingia kwenye rukuu hapa unatakiwa Kwenda sawa na Imam. Ina herufi 156 kwa Qiraa cha kurefusha MAA-kwenye Maaliki yawmiddin. Ukisoma kwa Qiraa cha MALIKI inakuwa na herufi 155. Ina shadda 14 kuanzia kwenye bismillahi mpaka waladhwaaliin. Na kusomwa kwake inabidi isomwe kwa kufululiza. Yaani usisome kisha ukafika aya Fulani halafu ukasimama bila sababu za msingi ( labda iwe kama kupiga myayo) n.k.

Kwenye usomaji wake ni lazima kila herufi itoke kwenye matoleo yake na idhirhirike kutamkwa kwake: Yaani; badala ya wala dhwaalin kuweka SWAD ukaweka DHWE, swala haitaswihi. Au badala ya IYYAKA ukasema IYAKA basi swala haitoswihi kwa maana; Iyaka maana yake ni mwangaza (nuru) na nuru ni kiumbe. Ukisema IYYAKA inamrejelea Mungu kwa maana wewe tu tunakuabudu ila ukitoa shadda inakuwa wewe mwangaza tunakuabudu. Kadhalika, kwa kila herufi inabidi ipatiwe haki yake. Na haijuzu wala herufi moja kupungua.

Ikiwa kama hajui kusoma suratul fat-ha ipasavyo ataleta aya 7 tofauti za sura nyengine kama anazijua. Ikiwa hajui kabisa basi ataleta dhikri kama tasbihi na tahlili. Ikiwa kama hajui sehemu yoyote ya Qur’an wala dhikri basi atakaa kimya kwa kuweka dhana ya kisomo cha fat-ha mpaka mwisho wake.

Kwa upande wa bubu anashurtishwa kutikisa midomo yake. Haishauriwi kusomwa kimoyoni hii sura yaani kimyakimya ukiwa kwenye ibada ya swala kwani kuifanya hivyo utapunguza baadhi ya herufi zake na baadhi ya matamko yake hayatatimilizwa kikamilifu isipokuwa kwa mdomo kucheza. UKIENDA TOFAUTI NA HAPO SWALA YAKO HAITASWIHI. Ni sunna baada ya kumaliza hii sura kusoma sura nyengine kama siku zote tunavyosikia misikitini wakiswalisha.

------------------------------------

Matendo mengineyo yanakwenda kwa picha. Nachelea wengine wanaweza wasielewe kurukuu ni nini, kuitidali ni nini n.k
 
14. Ulazima wa kuweka nia usiku katika swawm ya faradhi

Tambueni ya kwamba nia katika kufunga ni jambo la lazima na ni sharti la kusihi kwake, kama ilivyo sharti kwa kusihi kwa ´ibaadah zote. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika si vyengineyo matendo yanategemea nia na kila mmoja atalipwa kutokana na vie alivyonuia.”[1]

Nia hiyo ni kwamba mtu aitakidi mwanzoni mwa swawm kwamba anafunga Ramadhaan, anafunga deni, anafunga nadhiri au kafara.

Wakati wa nia ya swawm ya wajibu kwa aina zake zote ni usiku, ni mamoja iwe mwanzo wa usiku, katikati yake au mwisho wake. ad-Daaraqutwniy kwa cheni yake ya wapokezi kupitia kwa ´Amrah kutoka kwa ´Aaishah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambaye amesema:

“Yeyote asiyelaza [nia ya] swawm kabla ya kuchomoza kwa alfajiri basi hana swawm.”[2]

Ibn ´Umar amepokea kupitia kwa Hafswah ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote asiyelaza [nia ya] swawm kabla ya alfajiri, basi hana swawm.”

Imekuja katika tamko jengine:

“Yeyote asiyekusudia… ”

Kwa maana asiyefanya azma.

“… kufunga tangu usiku, basi hana swawm.”[3]

Kwa kuwa mchana wote unawajibika kufungwa. Ikipita sehemu ya mchana bila kuwepo nia basi swawm ya siku nzima haisihi, kwa sababu nia hairejei nyuma kwa yaliyopita.

[1] Muslim (1907).

[2] ad-Daaraqutwniy (02/172) na al-Bayhaqiy katika ”as-Sunan al-Kubraa” (04/202) ambaye amesema:

”Cheni yake ya wapokezi wote ni wenye kuaminika.”

[3] Ahmad (06/287), Abu Daawuud (2454) na at-Tirmidhiy (730).

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 22
Imechapishwa: 02/02/2026"

⤵️Ahl-ul-Hadiyth
 
15. Kutamka nia kwa sauti ni Bid´ah

Nia katika ´ibaadah zote mahali pake ni moyoni. Kwa msemo mwingine haijuzu kuitamka kwa sauti, kwa sababu hilo halikupokewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala kutoka kwa Maswahabah wake kwamba walikuwa wakisema:

”Nimekusudia kufunga.”

”Nimekusudia kuswali.”

Kwa hiyo kuitamka nia kwa sauti ni Bid´ah iliyozuliwa. Inatosha katika nia kula na kunywa kwa kusudia kufunga. Shaykh Taqiyy-ud-Diyn Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Yeye anapokula chakula cha usiku anakula chakula cha mtu anayekusudia kufunga, kwa sababu hiyo hutofautishwa kati ya chakula cha usiku wa ´iyd na chakula cha nyusiku za Ramadhaan.”

Amesema pia:

“Kila anayejua kuwa kesho ni Ramadhaan na anataka kuifunga, basi ameshaweka nia, jambo ambalo ndio kitendo cha waislamu wengi.”

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ithaaf Ahl-il-Iymaan bi Duruus Shahri Ramadhwaan, uk. 22
Imechapishwa:
05/02/2026"

⤵️Ahl-ul-Hadiyth
 
📲KUSAMBAZA MAUDHUI YA DINI

Kusambaza Nakala / Maudhui za Dini nako ni moja ya Matendo mema, na atakayefaidika kutokana na ulichokisambaza, na wewe utalipwa na malipo yake bila yeye kupunguziwa.
Kama Anavosema Allah ta’ala:
Mwenye kusaidia msaada mwema ana fungu lake katika hayo, na mwenye kusaidia msaada mwovu naye ana sehemu yake katika hayo. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye uweza na ujuzi juu ya kila kitu.
•{An-Nisaa 2:85}•
Pia Amesema Mtume ﷺ
“Yeyote atakayelingania watu kwenye uongofu, atapata thawabu sawa na thawabu za wale waliomfuata, bila kupunguziwa wao chochote katika thawabu zao. Na yeyote atakayelingania watu kwenye upotofu, atabeba dhambi sawa na dhambi za wale waliomfuata, bila wao kupunguziwa chochote katika dhambi zao.”
•{Ṣaḥīḥ Muslim, 2674}•

Hivyo ukumbusho wowote utakaoona humu na kwengine- Pupia katika kuusambaza, Namuomba Allah atuthibitishe katika njia yake.
 
📲KUSAMBAZA MAUDHUI YA DINI

Kusambaza Nakala / Maudhui za Dini nako ni moja ya Matendo mema, na atakayefaidika kutokana na ulichokisambaza, na wewe utalipwa na malipo yake bila yeye kupunguziwa.
Kama Anavosema Allah ta’ala:

•{An-Nisaa 2:85}•
Pia Amesema Mtume ﷺ

•{Ṣaḥīḥ Muslim, 2674}•

Hivyo ukumbusho wowote utakaoona humu na kwengine- Pupia katika kuusambaza, Namuomba Allah atuthibitishe katika njia yake.

Follow the WANAWAKE WA SUNNAH channel on WhatsApp: WANAWAKE WA SUNNAH
 
Back
Top Bottom