Ramadhan Special Thread
Screenshot_20250618_162848_WhatsApp.jpg
 
Maswali: Qur-aan


Ninaweza Kuanza Kusoma Suwrah Katikati Ninaposwalisha?



Alhidaaya.com





SWALI:



S. Aleykum,



Nina swali,wakati mtu anaswalisha yuaweza kuanza kusoma suwrah popote anapotaka (yaani si lazima aanze mwanzo wa suwrah). Swali langu ni hili je kuna masharti yoyote ama mtu aweza kusoma atakavyo? Shukran





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho



Anaweza mtu kuanza kusoma popote katika Suwrah, ikiwa anaswalisha au anaswali mwenyewe, kwani kawaida katika Suwrah moja ya Qur-aan huwa ina maelezo mbali mbali, kwa hiyo hakuna kipingamizi kufanya hivyo.



Kuhusu sharti za kusoma katika Swaalah, ni vizuri kufuata adabu za Swaalah kama alivyokuwa akifanya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)



1. Kisomo cha Suwrah kinaweza kuwa kirefu mara nyingine na mara nyingine kifupi kutokana na hali ya mtu kama yuko katika safari, au anaumwa au kama mtoto analia.



2. Kisomo kinakuwa tofauti kutokana na hali ya Swaalah.



3. Kisomo cha Swalah ya Alfajiri ni kirefu kuliko Swaalah zote. Kisha kinafuatia kisomo cha Swaalah ya Adhuhuri, kisha Alasiri, kisha 'Ishaa na mwisho ni Magharibi.



4. Kisomo cha Swaalah ya usiku (Tahajjud) ni kirefu zaidi kuliko Swaalah zote hizo.



5. Ni Sunnah kufanya kisomo cha Raka'ah ya mwanzo kirefu kuliko Raka'ah ya pili.



6. Suwrahl Al-Faatihah ni fardhi katika kila Raka'ah.



7. Imaam haruhisiwi kusoma kisomo kirefu sana zaidi ya kilivyoelezwa katika Sunnah, kwa sababu kutowatia mashakani wanaoswali nyuma yake kama watu wazima, wagonjwa, na walio dhaifu.



Kisomo cha sauti na cha kimya:



1). Qur-aan isomwe kwa sauti katika Swaalah ya Alfajiri, Swaalah ya Ijumaa, Swaalah za 'Iyd, ya mvua, ya kupatwa jua na katika Raka'ah mbili za mwanzo kwenye Swaalah ya Magharibi na 'Ishaa.



2). Ni Sunnah kusoma Qur-aan kwa tartiyl, yaani kusoma inavyopaswa kusomwa kwa kufuata sheria zake za Tajwiyd, na kwa kuipendezesha sauti.





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Nini Hukmu Ya Sajdatut-Tilaawah (Sijda Ya Kisomo)



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalam alaykum. Kwanza napenda kumshukuru Allah kwa kunipa uzima na kuniwezesha kupata fursa hii ya kuuliza maswali Na kwa uhakika shukurani zote in zake. Na alafu napenda kuwashukuru maustadh wote ambao wamechangia kwa kuendesha hichi kiungo. Swali langu ni je tunatakiwa kusujudu wakati tukisikia Qur-aan? na kama ni kweli mbona jambo hili halifanywi katika jamii? Au ni bora kusujudu wakati mtu akisikia Qur-aan na si lazima? Sijawahi kusikia mtu au Swahaba kusujudu katika enzi za kipenzi chetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kusikia Qur-aan. Inawezekana maswahaba walikuwa wanasujudu lakini sijasikia mimi tu. kwahiyo inabidi sasa niulize je Swahaba walikuwa wakisujudu?. Na kama ni kweli basi naomba nielezelewe hivyo visa. Lakini nahisi kutokana na hizi aya kuwa waislam wanatakiwa kusujudu wakati wakisomewa Qur-aan lakini sina uhakika. Na kama hisia zangu ni sahihi mbona hili jambo halifanywi? na watu wanalinyamazia? Kama sikosei Aayah 21 ya Inshaqaaq inaelekea inawahusu makafiri ambalo wanaosikia Quran alafu hawasujudu wakajisalimisha kwenye Uislam. lakini na Aayah ya 15 ya suratul assajdah si inahusu waislam?



Aayah zenyewe ni zifuatazo:



وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩﴿٢١﴾

Na wanaposomewa Qur-aan, hawasujudu. [Al-Inshiqaaq: 21]



Na pia,



إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩﴿١٥﴾

Hakika wanaamini Aayaat Zetu wale wanapokumbushwa nazo huporomoka kusujudu, na wakasabbih kwa Himidi za Rabb wao, nao hawatakabari. [As-Sajdah 15]





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Sajdatut-tilaawa (Sijda ya kusoma Qur-aan) ni kitendo cha Sunnah, na kitendo chochote cha Sunnah humpatia mwenye kutenda thawabu. Ni bora zaidi kujitahidi kutimiza Sunnah ambazo nyepesi kama hizo ili kupata yafuatayo:



Thawabu kwa kutenda kitendo cha Sunnah.
Kupata fadhila za kufanya sijdah hiyo.
Kudhihirisha mapenzi ya Allaah na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kuzidumisha Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kujidhalilisha kwa Allaah (‘Azza wa Jalla) kwa kuweka kipaji chako cha uso chini kwenye ardhi na kusema:
سُبْـحانَ رَبِّـيَ الأَعْلـى

Ametakasika Rabb wangu Aliye juu



Aayah hizo ulizozitaja kama ulivyoona kwamba ya kwanza inawahusu makafiri na ya pili inawahusu Waumini, lakini hazileti tofauti katika hukmu ya kusujudu kwa ajili ya kusoma Qur-aan inapofika sehemu yenye alama ya kusujudu. Swahaba walikuwa wakifuata Sunnah za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hivyo na sisi ni vizuri kufuata nyendo zao.



Vile vile tutambue kuwa kila kitu kinamsujudia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) vilivyohai na visivyo hai, sasa vipi sisi wana Aadam tusimsujudie? Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



أَوَلَمْ يَرَوْا إِلَىٰ مَا خَلَقَ اللَّـهُ مِن شَيْءٍ يَتَفَيَّأُ ظِلَالُهُ عَنِ الْيَمِينِ وَالشَّمَائِلِ سُجَّدًا لِّلَّـهِ وَهُمْ دَاخِرُونَ﴿٤٨﴾

Je, hawaoni vile vitu Alivyoumba Allaah ambavyo vivuli vyake vinasogea huku na kule, kuliani na kushotoni vikimsujudia Allaah na huku vinanyenyekea?



وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ مِن دَابَّةٍ وَالْمَلَائِكَةُ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ﴿٤٩﴾

Na ni kwa Allaah pekee vinasujudia vyote vilivyomo mbinguni na ardhini katika viumbe vitembeavyo, na Malaika, nao hawatakabari.



يَخَافُونَ رَبَّهُم مِّن فَوْقِهِمْ وَيَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ ۩﴿٥٠﴾

Wanamkhofu Rabb wao Aliye juu yao, na wanafanya yale wanayoamrishwa. [An-Nahl: 48-50]



Pia katika Suwrah Ar-Ra’d Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



وَلِلَّـهِ يَسْجُدُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَظِلَالُهُم بِالْغُدُوِّ وَالْآصَالِ ۩﴿١٥﴾

Na kwa Allaah (Pekee) Humsujudia waliomo mbinguni na ardhini wakipenda wasipende na vivuli vyao pia (vinamsujudia) asubuhi na jioni. [Ar-Ra'd: 15]



Na katika Hadiyth ifuatayo:



حَدَّثَنَا مُحَمَّدُ بْنُ يُوسُفَ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ إِبْرَاهِيمَ التَّيْمِيِّ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ أَبِي ذَرٍّ ـ رضى الله عنه ـ قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم لأَبِي ذَرٍّ حِينَ غَرَبَتِ الشَّمْسُ ‏"‏ تَدْرِي أَيْنَ تَذْهَبُ ‏"‏‏.‏ قُلْتُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَإِنَّهَا تَذْهَبُ حَتَّى تَسْجُدَ تَحْتَ الْعَرْشِ، فَتَسْتَأْذِنَ فَيُؤْذَنَ لَهَا، وَيُوشِكُ أَنْ تَسْجُدَ فَلاَ يُقْبَلَ مِنْهَا، وَتَسْتَأْذِنَ فَلاَ يُؤْذَنَ لَهَا، يُقَالُ لَهَا ارْجِعِي مِنْ حَيْثُ جِئْتِ‏.‏ فَتَطْلُعُ مِنْ مَغْرِبِهَا، فَذَلِكَ قَوْلُهُ تَعَالَى ‏ ‏وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَهَا ذَلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ‏



Amesimulia Abuu Dharr (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aliniuliza wakati wa machweo: “Je, unajua jua linapokwenda (wakati wa kuzama kwake)?” Nikamjibu: “Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi.” Akasema: “Hakika linakwenda mpaka linasujudu chini ya ‘Arsh, na kutaka idhini kuchomoza tena, nalo linaruhusiwa. Na inachelewa kuwa (itafika wakati ambapo) litakaribia kusujudu lakini sijda yake haitokubaliwa, na litaomba idhini lakini litakataliwa (kutimiza mizunguko yake). Litaambiwa: ‘Rudi ulipotoka’. Hivyo, litachomoza Magharibi. Na hiyo ndiyo Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):



وَالشَّمْسُ تَجْرِي لِمُسْتَقَرٍّ لَّهَا ۚ ذَٰلِكَ تَقْدِيرُ الْعَزِيزِ الْعَلِيمِ ﴿٣٨﴾

“Na jua linatembea hadi matulio yake.[1] Hayo ni Takdiri ya Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mjuzi wa yote.” [Yaasiyn 36:38)- Hadiyth ameipokea Imaam Al-Bukhaariy]



Na pia,



عن ابن عباس قال: "جاء رجل فقال: يا رسول الله، إني رأيتني الليلة وأنا نائم، كأني أصلي خلف شجرة، فسجدتُ فسجَدَت الشجرة لسجودي، فسمعتُها وهي تقول:



اللّهُـمَّ اكْتُـبْ لي بِهـا عِنْـدَكَ أَجْـراً، وَضَـعْ عَنِّـي بِهـا وِزْراً، وَاجْعَـلها لي عِنْـدَكَ ذُخْـراً، وَتَقَبَّـلها مِنِّـي كَمـا تَقَبَّلْتَـها مِنْ عَبْـدِكَ دَاوُد



قال ابن عباس: فقرأ النبي صلى الله عليه وسلم سجدة ثم سَجَد، فسمعته وهو يقولُ مثلَ ما أخبره الرجل عن قول الشجرة. " رواه الترمذي، وابن ماجه، وابن حبّان في صحيحه



Ibn 'Abbaas (Radhwiya-Allaahu 'anhu) amehadithia: "Mtu moja alikuja na kusema: "Ee Rasuli wa Allaah, nilijiona katika ndoto jana usiku nikiswali nyuma ya mti. Niliposujudu na mti ukawa unasujudu. Kisha nikausikia unasema:



اللّهُـمَّ اكْتُـبْ لي بِهـا عِنْـدَكَ أَجْـراً، وَضَـعْ عَنِّـي بِهـا وِزْراً، وَاجْعَـلها لي عِنْـدَكَ ذُخْـراً، وَتَقَبَّـلها مِنِّـي كَمـا تَقَبَّلْتَـها مِنْ عَبْـدِكَ دَاوُد

Ee Allaah niandikie Kwako kwa sijdah hii malipo, na nifutie kwayo madhambi, na ijaalie kwangu mbele Yako ni akiba, na nikubalie kama Ulivyomkubalia mja wako Daawuwd.



Ibn 'Abbaas akasema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasoma Aayah inayotaja kusujudu kisha akasujudu na nikamsikia akisema maneno hayo hayo aliyosimulia mtu yaliyotajwa na mti." [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ibn Hibbaan katika Swahiyh yake]



Na ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:



أَلَمْ تَرَ أَنَّ اللَّـهَ يَسْجُدُ لَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ وَالنُّجُومُ وَالْجِبَالُ وَالشَّجَرُ وَالدَّوَابُّ وَكَثِيرٌ مِّنَ النَّاسِ ۖ وَكَثِيرٌ حَقَّ عَلَيْهِ الْعَذَابُ ۗ وَمَن يُهِنِ اللَّـهُ فَمَا لَهُ مِن مُّكْرِمٍ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ۩﴿١٨﴾

18. na mwezi na nyota, na majabali na miti na viumbe vinavyotembea, na wengi miongoni mwa watu? Na wengi imewastahiki adhabu. Na ambaye Allaah Amemdhalilisha, basi hatopata wa kumkirimu. Hakika Allaah Anafanya Atakavyo. [Al-Hajj: 18]



Hata makafiri walikuwa wakiathirika na Qur-aan walipokuwa wakiisikia hadi kwamba iliposomwa kwao Suwrah An-Najm Aayah za mwisho ambazo zimetaja kumsujudia Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) walisujudu bila ya kujijua. Aayah hizo ni zifuatazo:



أَفَمِنْ هَـٰذَا الْحَدِيثِ تَعْجَبُونَ ﴿٥٩﴾وَتَضْحَكُونَ وَلَا تَبْكُونَ ﴿٦٠﴾وَأَنتُمْ سَامِدُونَ ﴿٦١﴾فَاسْجُدُوا لِلَّـهِ وَاعْبُدُوا ۩﴿٦٢﴾

Je, mnastaajabu kwa Al-Hadiyth hii (ya Qur-aan)?Na mnacheka na wala hamlii? Na hali nyinyi mnaghafilika, mnadharau na kushughulika na anasa? Basi msujudieni Allaah na mwabuduni Yeye. [An-Najm: 59-62]



Zilipoteremshwa Aayah hizo za Suwrah An-Najm, zilkiwaathiri Makafiri wakasujudu bila ya kujijua. Habari zilienea kote hadi kuwafikia Swahaba waliokuwa Abisynia (Ethiopia) kuwa Maquraysh wameingia Uislaam. Swahaba wakarudi Makkah. Walipokuwa wanakaribia Makkah kwa muda wa msafara wa saa moja tu kutoka Makkah ikawadhihirikia ukweli kuwa Makafiri waliaathiriwa tu na Maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Baadhi ya Swahaba wakarudi Abisynia na wengine wao wakaingia kwa siri mjini Makkah [Ar-Rahiyq Al-Makhtuwm]



Kwa faida zaidi bonyeza kiungo kifuatacho:



Kusujudu Kwa Ajili Ya Kusoma Aayah





Na Allaah Anajua zaidi.
 
Nini Sababu Ya Kuteremshwa Suwrah At-Takaathur?



Alhidaaya.com







SWALI:



Naomba mnitumie tafsiri ya suratul alhaakum' takathuru pamoja na kisa chake.



JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Surwah At-Takaathur imeteremshwa Makkah kulingana na Mufassiriyn wengi. Hii ni Suwrah ambayo ina Aayah nane na katika Suwrah zilizoteremshwa mwanzoni katika kipindi cha Makkah.



Hatukuipata sababu ya kuteremshwa kwake katika Swahiyh Asbaab An-Nuzuwl.



Ila Ibn Abiy Haatim amenukuu kuwa Abuu Buraydah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Suwrah hii imeteremshwa kuhusiana na makabila mawili, Bani Haarithah na Bani al-Harth ambao walijifakharisha utukufu na matendo mazuri ya watu wao walio hai; bado ya hapo walikwenda makaburini na kujifakharisha na ‘amali tukufu na nzuri za waliofariki. Hapo ndipo Suwrah hii iliteremshwa.



At-Tirmidhiy, Ibn Jariyr na Ibn al-Mundhir wamepokea rai hii ya ‘Aliy bin Abi Twaalib (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: “Tulikuwa na shaka kuhusu adhabu ya kaburi mpaka Alhaakumut Takaathur ilipoteremshwa”.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Qur-aan Ina Roho? Imeumbwa?



Alhidaaya.com





SWALI:



Asalaam alaykum ama baada ya salaam anpenda kumshukuru Allah (SW) na kutakia rehma Mtume wetu Muhammad (SAW) na napenda kuwashuru waislam wote wanashiriki kujibu maswali yetu haya kwani hakutuna la kuwalipa bali Allah ndie atayewalipa inshaallah. Swali langu lipo hapa kuna baadhi wa watu wanasema Qur'an in roho. Je ni kweli ina roho au haina?



JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Nabiy, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'aalaa) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) baada ya kumtaja Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kiuvivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Swahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.





Kwa vile Qur-aan si kiumbe. Lakini kama unakusudia maana ya neno la 'ruwhan' ambalo kwa matamshi yetu ya Kiswahili husomeka kuwa ni 'roho' katika Aayah ifuatayo:



وَكَذَٰلِكَ أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ رُوحًا مِّنْ أَمْرِنَا ۚ مَا كُنتَ تَدْرِي مَا الْكِتَابُ وَلَا الْإِيمَانُ وَلَـٰكِن جَعَلْنَاهُ نُورًا نَّهْدِي بِهِ مَن نَّشَاءُ مِنْ عِبَادِنَا ۚ وَإِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٥٢﴾

Na hivyo ndivyo Tulivyokuletea Ruwh (Qur-aan) kutoka amri Yetu. Hukuwa unajua nini Kitabu wala iymaan, lakini Tumeifanya ni Nuru, Tunaongoa kwayo Tumtakaye miongoni mwa waja Wetu. Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka. [Ash-Shuwraa: 52]



‘Ulamaa Wafasiri wa Qur-aan, wamekhitilafiana kuhusu maana ya kauli hiyo. Kuna waliosema ni 'Unabiy, kama Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa). Wengine wamesema ni ima Qur-aan au Jibriyl au Wahyi. Wengine wamesea kuwa ni 'uhai' kwa sababu ni uhai unaofisha ujahili. [Al-Qurtwuby]



Hivyo fahamu kuwa Qur-aan si kiumbe ili kiwe na moyo. Kusema hivyo ni kinyumea na ‘Aqiydah wa Ahlus-Sunnah wal Jamaa’ah na ni kukufuru kama walivyosema ‘Ulamaa.



Kwa faida ziyada bonyeza viungo vifuatavyo:



Shaykh Fawzaan: Makundi Mengineyo Yanayodai Kwamba Qur-aan Imeumbwa

Imaam Atw-Twabariy: Qur-aan Ni Maneno Ya Allaah Hayakuumbwa
Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 01



Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa'ah Kuhusiana Na Qur-aan – 02



Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 03



Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 04



Itikadi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Kuhusiana Na Qur-aan – 05





Na Allaah Anajua zaidi
 
Qur-aan Ina Suwrah Ngapi Na Aayah Ngapi Jumla?



Alhidaaya.com







SWALI:



Qur ani ina aayah ngapi na mna suwrah ngapi





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Jumla ya Suwrah za Qur-aan ni 114 kuanzia Suwrah Al-Faatihah hadi Suwrah An-Naas. Majina yake na idadi zake imetajwa



katika kurasa za Mswahafu mwisho kabisa.





Ama idadi za Aayah, wengine wamesema ni 6666, lakini iliyo sahihi kabisa ni ya Aayah 6,236.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Qur-aan Inasemaje Kuruhusiwa Kufanya Utafiti

Wa Mas-ala Mbali Mbali?



Alhidaaya.com





SWALI:



Assalaam alaykum.

Qur-aan inasema nini kuhusu utafiti? Inatoa muongozo wowote kuhusu namna ya kufanya utafiti wa vitu mbali mbali? Kwa mfano kufanya utafiti wa chanzo cha tatizo fulani, au kujua jambo fulani, au utafiti wa chanzo cha ugonjwa fulani. Kuna utaratibu au muongozo wa namna ya kufanya utafiti wa mambo haya katika Qur'an? (Samahani, si utafiti wa Qur'an, bali Qur-aan inasema nini kuhusu kufanya utafiti wa mambo mbalimbali, utaratibu upi utumike.





JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho





Uislamu ni Dini ya pekee iliyohimiza utafiti katika masomo yote kwa kutumia akili na vifaa vinavyohitajika katika mazingira na maadili ya Kiislamu. Hivyo, katika Uislamu hakukupatikana wataalamu waliochomwa au kuuliwa kwa sababu ya nadharia zao kama ilivyotokea katika karne za kati huko Ulaya. Kina Galileo na wengineo ni mfano mzuri kwa hilo.



Allaah Aliyetukuka katika Qur-aan Tukufu Anabisha ndani ya nyoyo zetu kwa nguvu na kutupigia ukulele ili tuzindukane. Ibara kama amkeni! Tazameni pembezoni mwenu! Fikirieni! Kuweni na tafakuri! Yupo Muumbaji!



Allaah Aliyetukuka Anasema:

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ إِلَىٰ طَعَامِهِ ﴿٢٤﴾

Basi atazame mwana Aadam chakula chake. ['Abasa: 24]



Na tena,

فَلْيَنظُرِ الْإِنسَانُ مِمَّ خُلِقَ ﴿٥﴾

Basi na atazame mwana Aadam ameumbwa kutoka na kitu gani? [Atw-Twaariq: 5]



Na pia,

أَفَلَا يَنظُرُونَ إِلَى الْإِبِلِ كَيْفَ خُلِقَتْ ﴿١٧﴾

Je, hawamtazami ngamia namna walivyoumbwa? [Al-Ghaashiyah: 17]



Hizi ni baadhi ya Aayah, zinazomhimiza Muislamu atumie akili na hisia zake katika kufanya utafiti. Maurice Bucaille anaandika katika kitabu chake: The Bible, the Qur'aan and Science: "Hakuna Dini yoyote inayompwekesha Allaah inayoshutumu sayansi. Lakini hakika ni kuwa, kwa karne nyingi, ulimwengu wa Kikristo, ukuuzi wa kisayansi ulipingwa vikali sana. Kesi ya Galileo iko mbele ya kila mmoja wetu. Katika Uislamu mtazamo na msimamo wa sayansi ulikuwa tofauti. Qur-aan ilipokuwa inatuita kukuuza sayansi, yenyewe ina miono mingi ya kimaumbile, iliyo sambamba na maalumati ya kisayansi ya sasa".



Kwa hiyo, Uislamu unatuhimiza kufanya tafiti ili tuweze kuwahudumikia walimwengu kwa njia ya ufanisi na nzuri kabisa. Na hivi leo wasiokuwa Waislamu ndio wenye kufuata yaliyoelezwa katika Qur-aan na Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika zile zenye kuelezea mas-ala ya sayansi na utafiti na kuitilia maanani na kuitumia katika uvumbuzi na tafiti zao, na huku Waislam wameacha mafundisho hayo.



Qur-aan ina takriban Aayah 750 zinayoelezea kuhusu maalumati tofauti katika masomo ya kiutafiti na sayansi.





Na Allaah Anajua zaidi
 
🕌 Hutuba ya Ijumaa: Kuwatendea Wema Ndugu na Jamaa

Khutuba ya Kwanza:

Alhamdulillah, tunamshukuru Allah Subhaanahu Wata’ala kwa kutujaalia uhai na kutufikisha Ijumaa hii tukufu. Tunaswali na kumtakia rehema Mtume Muhammad ﷺ, familia yake, maswahaba wake na wote wanaomfuata kwa wema hadi Siku ya Qiyama.

Enyi Waja wa Allah,
Miongoni mwa maamrisho ya Uislamu ni kuwatendea wema ndugu na jamaa. Allah anasema:

"Na mpe jamaa yake wa karibu haki yake..." (Surah Al-Isra: 26)

Uislamu umetufundisha kuwa undugu wa damu ni neema, na kuwahudumia ni ibada. Mtume ﷺ amesema:

"Yeyote anayekata uhusiano wa jamaa hatopata pepo." (Bukhari na Muslim)

Jamaa ni wa kwanza katika ustawi wa jamii. Wenye shida wapewe msaada. Wenye huzuni wafarijiwe. Wenye makosa wasamehewe.

Khutuba ya Pili:

Ndugu wapenzi,
Kumtendea jamaa wema si kutoa mali tu. Bali ni:
  • Kuwatembelea,
  • Kuwaulizia hali,
  • Kuombeana dua,
  • Kuwasamehe,
  • Kutatua migogoro kwa hekima.

Mtume ﷺ aliulizwa: “Ni nini silat-ur-rahm (kuunga udugu)?” Akasema:
“Sio kulipa kwa kulipa, bali ni kuendeleza uhusiano hata kama wao wanakata.”

Ewe Muislamu, anza leo. Piga simu, tembelea ndugu, msamehe uliye na shida naye. Allah hupenda wanaojitahidi kuleta udugu.

Hitimisho:
Tuombe dua:
"Ee Allah, tujaalie kuwa miongoni mwa wanaowatendea wema jamaa zetu, tupatanishe waliogombana, na tulinde na moyo wa chuki."

Wassalaam Alaikum Warahmatullah.
 
01-Swalaah Ya Ijumaa Ni Fardhi Kwa Kila Mwanamme Haijuzu Kuiacha Kwa Sababu Ya Kazi Au Masomo n.k




Swalaah Ya Ijumaa Ni Fardhi Kwa Kila Mwanamume

Haijuzu Kuiacha Kwa Sababu Ya Kazi Au Masomo Na Kadhaalika




Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Swalaah ya Ijumaa ni Fardhw ‘Ayn (Fardhi kwa kila mtu mwanamme) wala haijuzu kuiacha kwa sababu ya kazi au masomo na sababu kama hizo.

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



“Na yeyote anayemcha Allaah; Atamjaalia njia ya kutoka (shidani).”





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/184)]
 
02-Swalaah Ya Ijumaa Ni Fardhi Kwa Kila Mwanamme Haijuzu Kuikhalifu Hata Ukikatazwa Na Mwajiri Wako



Swalaah Ya Ijumaa Ni Fardhi Kwa Kila Mwanamme

Haijuzu Kuikhalifu Hata Ukikatazwa Na Mwajiri Wako



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Swalaah ya Ijumaa ni fardhi kwa kila mwanamme mwenye kukafilika katika ‘Ibaadah, mkazi, wala haikupasi kuikhalifu kwa sababu ya kazi hata kama mwajiri wako atakukataza.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/185)]
 
03-Swalaah Ya Ijumaa: Wanaume Kuswali Ijumaa Misikitini Wanawake Nyumbani



Wanaume Kuswali Ijumaa Misikitini Wanawake Nyumbani



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Ni wajibu kwa wanaume kuswali Ijumaa pamoja na ndugu zao Waislamu katika nyumba za Allaah (Misikitini). Ama wanawake wao hawana Ijumaa na ni wajibu kwao kuswali Adhuhuri.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/196)]
 
04-Swalaah Ya Ijumaa: Haifai Kuzungumza Kamwe Pindi Khutba Ya Ijumaa Inapotolewa




Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Haifai kwa mtu anayekuweko Masjid kuongea na yeyote yule pindi khutbah ya Ijumaa inatolewa.

Ama Imaam, yeye anaweza kuongea inapombidi kwa lile analoliona lina maslahi.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/201, 202)]
 
05-Swalaah Ya Ijumaa: Kujuzu Swalaah Ya Ijumaa Hata Kama Idadi Ya Watu Ni Chini Ya Arubaini



Kujuzu Swalaah Ya Ijumaa Hata Kama Idadi Ya Watu Ni Chini Ya Arubaini



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Inajuzu kusimamisha Swalaah ya Ijumaa hata kama idadi imepunguka chini ya watu arubaini kutokana na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ

“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya Swalaah siku ya Ijumaa, kimbilieni kumdhukuru Allaah.” [Al-Jumu’ah: 9]





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/215)]
 
06-Swalaah Ya Ijumaa: Vipi Kuitikia Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)



Vipi Kuitikia Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam)



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Khatwiyb (wa Ijumaa) anapomswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), waitikie wanaomsikiliza (Maamuma) bila ya kupandisha sauti.



[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/217)]
 
07-Swalaah Ya Ijumaa: Hukmu Ya Anayepitwa Na Rakaa Ya Swalaah Ya Ijumaa



Hukmu Ya Anayepitwa Na Rakaa Ya Swalaah Ya Ijumaa



Al-Lajnah Ad-Daaimah



www.alhidaaya.com





Anayepitwa na Rakaa katika Swalaah ya Ijumaa, na akaipata Rakaa nyingine, basi aiswali ile Rakaa (iliyompita) na hivyo atakuwa amepata Ijumaa kwa sababu limesihi kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hilo.





[Al-Lajnah Ad-Daaimah (8/225)]
 
Back
Top Bottom