Ramadhan Special Thread
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com





14- Kusema Subhaana Allaah WalhamduliLLaah Wa Laa Ilaaha Illa Allaah Wa Allaahu Akbar Naipenda Zaidi Kuliko Kila Kilichoangaziwa Na Jua





عَنْ أبي هريرة رضي الله عنه: قَالَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم: ((لأَنْ أَقُولَ: سُبْحَانَ اللهِ، والحَمْدُ للهِ، وَ لاَ إَلَهَ إلاَّ اللهُ، واللهُ أَكْبَرُ، أَحَبُّ إَلَيَّ مِمَّا طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ)) مسلم



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Kusema kwangu: Subhaana-Allaah, WalhamduliLLaah, wa laa ilaaha illa Allaah, wa Allaahu Akbar (Utakasifu ni wa Allaah na Himdi Anastahiki Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila ni Allaah, na Allaah ni Mkubwa) naipenda zaidi kuliko kila kilichoangaziwa na jua)) [Muslim]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



15-Kutamka Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Miongoni Mwa Swadaqah





عن أبي ذَرٍّ رضي اللهُ عنه: أَنَّ ناساً من أَصْحابِ رسول الله صلى الله عليه وسلم، قالوا لِلنَّبيِّ صلى الله عليه وسلم: يا رسولَ اللهِ، ذَهَب أَهْلُ الدُّثورِ بالأُجورِ، يُصَلُّونَ كما نُصَلِّي، ويَصُومُونَ كما نَصُومُ، وَيَتَصَدَّقُونَ بِفُضُولِ أَمْوَالِهِمْ. قَالَ: ((أوَ لَيْسَ قَدْ جَعَلَ اللهُ لَكُمْ مَا تَصَدَّقُونَ ؟ إنَّ بكلِّ تَسْبيحَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَكْبِيرَةٍ صَدَقَةً، وكُلِّ تَحْمِيدَةٍ صَدَقَةً، وَكُلِّ تَهْلِيلَةٍ صَدَقَةً، وَأَمْرٍ بِالْمَعرُوفِ صَدَقَةً، وَنَهْيٍ عَنْ مُنْكَرٍ صَدَقَةً، وفي بُضْعِ أحَدِكُمْ صَدَقَةً)). قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ، أَيَأْتي أحَدُنَا شَهْوَتَهُ وَيَكُونُ لَهُ فِيهَا أجرٌ ؟ قَالَ: ((أَرَأَيْتُمْ لَوْ وَضَعَها في حَرَامٍ، أَكَانَ عَليْهِ وزْرٌ ؟ فَكَذلِكَ إذَا وَضَعَها في الْحَلاَلِ كانَ لَهُ أَجْرٌ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba: Watu katika Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walimwambia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ee Rasuli wa Allaah! Watu wenye mali wameondoka na thawabu nyingi; wanaswali kama tunavyoswali, na wanafunga kama tunavyofunga na wanatoa swadaqah kwa fadhila za mali zao. Akasema (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, kwani Allaah Hakukujaalieni njia ya kutolea swadaqah? Hakika kila (kutamka) Tasbiyh (Subhaana Allaah) ni swadaqah. Na kila Takbiyr (Allaahu Akbar) ni swadaqah. Na kila Tahmiyd (AlhamduliLLaah) ni swadaqah, na kila Tahliyl (Laa ilaaha illa Allaah) ni swadaqah. Na kuamarisha mema ni swadaqah. Na kukataza munkari ni swadaqah. Na mmoja wenu kujimai (na mkewe) ni swadaqah.” Wakasema: Ee Rasuli wa Allaah. Hivi mmoja wetu kujitoshelezea kwa shahawa yake atakuwa anapata thawabu? Akasema: “Mnaonaje kama atajitosheleza kwa njia ya haraam angelipata dhambi? Hivyo basi ikiwa atafanya kwa njia ya halaal, atapata thawabu.” [Muslim]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



16-Atakayekuwa Maneno Yake Ya Mwisho Ni Laa Ilaaha Illa Allaah Ataingia Jannah





عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ قَالَ : قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((مَنْ كَانَ آخِرُ كَلامِهِ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّةَ)) رواه أبو داود ( 3116 ) وحسَّنه الألباني في "إرواء الغليل" ( 3 / 149 ).



Kutoka kwa Mu’aadh bin Jabal (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Atakayekuwa maneno yake ya mwisho ni Laa ilaaha illa Allaah ataingia Jannah)). [Abuu Daawuwd, Ahmad na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Irwaa Al-Ghaliyl (3/149), Swahiyh Al-Jaami’ (6479), Swahiyh Abiy Daawuwd (3116)].
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



17-Kughufuriwa Makosa Japokuwa Ni Mfano Wa Povu La Bahari





Akitamka mtu: “Laa ilaaha illa Allaah …” kila baada ya Swalaah baada ya Adkhaar za Tasbiyh, Tahmiyd na Takbiyr mara thelathini na tatu kila moja na akamalizia kwa: “Laa ilaaha illa Allaah…” mara moja:



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ((مَنْ سَبَّحَ اللَّهَ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاةٍ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَحَمِدَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ وَكَبَّرَ اللَّهَ ثَلاثًا وَثَلاثِينَ فَتْلِكَ تِسْعَةٌ وَتِسْعُونَ وَقَالَ تَمَامَ الْمِائَةِ لا إِلَهَ إِلاّ اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ غُفِرَتْ خَطَايَاهُ وَإِنْ كَانَتْ مِثْلَ زَبَدِ الْبَحْرِ)) رواه مسلم



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakaye Sabbih (Subhaana Allaah) kila baada ya Swalaah mara thelathini na tatu, akaleta tahmiyd (AlhamduliLLaah) mara thelathini na tatu akaleta takbiyra (Allaahu Akbar) mara thelathini na tatu, akamalizia kwa: “Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah, Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr [Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu] ataghufuriwa makosa yake japokuwa ni mfano wa povu la bahari)). [Muslim (1/418) [597]]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



18-Atakayetamka Baada Ya Wudhu “Ash-hadu An Laa Ilaaha Illa Allaah...

Atafunguliwa Milango Minane Ya Jannah Aingie Autakao



عَنْ عُمَرَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم : ((مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ، فَيُسْبِغُ اَلْوُضُوءَ، ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الْجَنَّةِ الثَّمَانِيَةُ يَدْخُلُ مِنْ أَيِّهَا شَاءَ)) أَخْرَجَهُ مُسْلِم



Kutoka kwa ‘Umar (رضي الله عنه) amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakuna yeyote miongoni mwenu anayetawadha vizuri, kisha akasema: “Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, wa ash-hadu anna Muhammad ‘Abduhuu wa Rasuwluhu” (Nashuhudia kuwa hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Peke Yake, hana mshirika, na ninashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Rasuli Wake) ila atafunguliwa milango minane ya Jannah aingie wowote aupendao kati ya hiyo.” [Imetolewa na Muslim na At-Tirmidhiy]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



19-Maneno Bora Kabisa Waliyotamka Manabii Wote





عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما أن النَّبِيّ صلى الله عليه وسلم قال: ((خَيْرُ الدُّعَاءِ دُعَاءُ يَوْمِ عَرَفَةَ، وخَيْرُ مَا قُلْتُ أنَا وَالنَّبيُّونَ مِنْ قَبْـلِي: لَا إِلَهَ إِلاَّ اللهُ وَحْدَهُ لا شَرِيْكَ لَهُ، لَهُ الـمُلْكُ، ولَهُ الـحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيءٍ قَدِير)) روى الترمذي



Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin ‘Amr bin Al-‘Aasw (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Du’aa bora kabisa ni du’aa katika siku ya 'Arafah, na yaliyo bora kabisa niliyosema mimi na Manabii kabla yangu ni: “Laa Ilaaha illa Allaah Wah-dahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa Huwa 'alaa kulli shay-in Qadiyr” [Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Hana mshirika, ufalme wote ni Wake, na Himdi zote ni Zake, Naye ni Mweza wa kila kitu])) [Swahiyh At-Tirmidhiy (3/184), Silsilatu Al-Ahaadiyth Asw-Swahiyhah (4/6), Swahiyh At-Targhiyb (1536)]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



20-Atakayeamka Usingizi Akasema: ““Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu…” Atataqabaliwa

Du’aa Na Swalaah Yake.





عَنْ عُبَادَةُ بْنُ الصَّامِتِ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) عَنْ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((مَنْ تَعَارَّ مِنْ اللَّيْلِ فَقَالَ: لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَالْحَمْدُ لِلَّهِ وَلاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلاَ حَوْلَ ولاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِاللَّهِ. ثُمَّ قَالَ رَبِّ اغْفِرْ لِي أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ, فَإِنْ عَزَمَ فَتَوَضَّأَ ثُمَّ صَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ))



Kutoka kwa ‘Ubaadah bin Swaamit (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Atakayeamka usiku akasema: “Laa ilaaha illa-Allaah Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku wa-Lahul-Hamdu wa-Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr, wa Subhaana-Allaah wal-HamduliLLaah walaa ilaaha illa-Allaah wa-Allaahu Akbar walaa hawla walaa quwwata illa biLLaah” (Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Pekee Hana mshirika, Ufalme ni Wake na Himdi ni Zake Naye ni Mweza wa kila kitu. Ametakasika Allaah, na Himdi ni za Allaah, na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, Allaah ni Mkubwa kabisa, hapana uwezo wala nguvu ila za Allaah), kisha akasema: “Rabbigh-fir-liy” [ee Allaah, nighufurie] au akaomba, ataitikiwa. Na akiazimia kutawadha na kuswali atatakabaliwa Swalaah yake)). [Al-Bukhaariy na wengineo]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



21-Du’aa Anapopatwa Mtu Na Janga, Dhiki, Balaa



www.alhidaaya.com





عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضى الله عنهما قَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ عِنْدَ الْكَرْبِ ‏: ((لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ الْعَلِيمُ الْحَلِيمُ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ رَبُّ السَّمَوَاتِ وَرَبُّ الأَرْضِ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ))

Imepokelewa kutoka kwa ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema katika hali ya janga (balaa):



Laa ilaaha illa-Allaahul-‘Aliymul-Haliym. Laa ilaaha illa-Allaahu Rabbul-‘Arshil-‘Adhwiym. Laa ilaaha illa-Allaahu Rabbus-samawaati wa Rabbul-ardhwi wa Rabbul-‘Arshil-Kariym.



Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Aliye Mjuzi, Mvumilivu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Rabb wa ‘Arsh Adhimu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Rabb wa mbingu na Rabb wa ardhi na Rabb wa ‘Arsh tukufu. [Al-Bukhaariy (7/154) [6346], Muslim (4/2092) [2730]]
 
22-Thawabu Za Kuacha Huru Watumwa Kumi,

Kuandikiwa Mema Mia, Kufutiwa Maovu Mia,

Ni Kinga Ya Shaytwaan Kwa Siku Hiyo,

Na Hatakuwa Mtu Yeyote Mbora Kumshinda Ila Yule Aliyefanya Zaidi Yake

www.alhidaaya.com



عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ : ((مَنْ قَالَ : لاَ إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ المُلْكُ وَلَهُ الحَمْدُ، وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ، فِي يَوْمٍ مِائَةَ مَرَّةٍ ، كَانَتْ لَهُ عَدْلَ عَشْرِ رِقَابٍ ، وَكُتِبَتْ لَهُ مِائَةُ حَسَنَةٍ ، وَمُحِيَتْ عَنْهُ مِائَةُ سَيِّئَةٍ، وَكَانَتْ لَهُ حِرْزًا مِنَ الشَّيْطَانِ يَوْمَهُ ذَلِكَ حَتَّى يُمْسِيَ ، وَلَمْ يَأْتِ أَحَدٌ بِأَفْضَلَ مِمَّا جَاءَ بِهِ ، إِلَّا أَحَدٌ عَمِلَ أَكْثَرَ مِنْ ذَلِكَ)) البخاري ومسلم



Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema kwa siku mara mia,



لا إلهَ إلاّ اللّهُ وحْـدَهُ لا شَـريكَ لهُ، لهُ المُـلْكُ ولهُ الحَمْـد، وهُوَ على كُلّ شَيءٍ قَدير

Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lahu, Lahul-Mulku walahul-Hamdu wa Huwa ‘alaa kulli shay-in Qadiyr.



Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake, Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza, basi atapata sawa na thawabu za kuwaacha huru watumwa kumi na ataandikiwa mema mia moja na atafutiwa maovu mia moja, na atakuwa na kinga ya shaytwaan kwa siku hiyo yote hadi jioni na hatakuwa mtu yeyote mbora kumshinda ila yule aliyefanya zaidi yake)) [Al-Bukhaariy, Muslim]
 
www.alhidaaya.com



23-Unapohangaika Kupata Usingizi Sema Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar..





عن عائشة أم المؤمنين رضي الله عنها ان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم إذا تضوَّر مِن اللَّيلِ قال: ((لا إلهَ إلَّا اللهُ الواحدُ القهَّارُ ربُّ السَّمواتِ والأرضِ وما بينَهما العزيزُ الغفَّارُ))



Imepokelewa kutoka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akihangaika kupata usingizi usiku akisema:



لا إِلـهَ إِلاّ اللهُ الـواحِدُ القَهّـار، رَبُّ السَّـمواتِ وَالأرْضِ وَما بَيْـنَهـما، العَزيـزُ الغَـفّار

Laa ilaaha illa-Allaahul-Waahidul-Qahhaar. Rabbus-samawaati wal ardhwi wamaa baynahumaal-’Aziyzul-Ghaffaar.



Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Al-Waahid (Mmoja Pekee) Al-Qahhaar (Mshindi Mwenye kudhibiti na kudhalilisha). Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo kati yake, Al-’Aziyz (Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima) Al-Ghaffaar (Mwingi wa kughufuria)) [An-Nasaaiy katika As-Sunan Al-Kubraa (10700), Swahiyh Ibn Maajah (5530), Swahiyh Al-Jaami’ (4693), Al-Haakim na ameisahihisha Adh-Dhahabiy (1/540), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah (864) na Ibn As-Sunniy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah (757)]
 
www.alhidaaya.com



24-Atakayesema Laa Ilaaha Illa Allaah, Wa-Allaahu Akbar....

Allaah Humsadiki Na Akiwa Katika Ugonjwa Akafa Ameahidi Kuwa Moto Hautamla.





عن أَبي سعيد الخُدْرِيِّ وأَبي هريرة رضيَ اللَّه عنهما ، أَنهُما شَهِدَا على رسول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم أَنه قال: ((مَنْ قَالَ لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ ، صَدَّقَهُ رَبُّهُ فَقَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَأَنَا أَكْبَرُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَحْدَهُ لا شَرِيكَ لَهُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَحْدِي لا شَرِيكَ لِي ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ ، قَالَ اللَّهُ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا لِيَ الْمُلْكُ وَلِيَ الْحَمْدُ ، وَإِذَا قَالَ : لا إِلَهَ إِلا اللَّهُ وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِاللَّهِ ، قَالَ : لا إِلَهَ إِلا أَنَا وَلا حَوْلَ وَلا قُوَّةَ إِلا بِي)) وَكَانَ يَقُولُ: ((مَنْ قَالَهَا فِي مَرَضِهِ ثُمَّ مَاتَ لَمْ تَطْعَمْهُ النَّارُ))

Abu Sa’iyd Al-Khudriyy na Abu Hurayrah (رضي الله عنهما), wameshuhudia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Atakayesema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, na Allaah ni Mkubwa”, Rabb wake Amemsadiki, Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Nami ni Mkubwa”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Peke Yake”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Peke Yangu”. Na akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah Mpweke Hana mshirika”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi Peke Yangu Sina mshirika”. Na akisema; “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, ni Wake Ufalme na Himdi ni Zake”, Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi, Ufalme ni Wangu na Himdi ni Zangu”. Na Akisema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa kutoka kwa Allaah”. Allaah Husema: “Hapana mwabudiwa wa haki ila Mimi na hapana uwezo wala nguvu isipokuwa Zangu.”)) Na Alikuwa (Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Atakayesema hayo akiwa mgonjwa akafariki, moto hautamla)) [At-Tirmidhiy [3430], Ibn Maajah [3794], na ameisahihisha Al-Albaaniy. Taz. Swahiyh At-Tirmidhiy (3/152), Swahiyh Ibn Maajah (2/317), Swahiyh At-Targhiyb (3481)]
 
www.alhidaaya.com



25-Laa Ilaaha Illa Allaah Ni Nguzo Ya Kwanza Ya Kiislamu



عن أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: ((بُنَي الإسلامُ على خَمْسٍ: شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ، وصَوْمِ رَمَضَانَ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

Kutoka kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan Abdillaah bin 'Umar bin Al-Khattwaab (رضي الله عنه) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Uislamu umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba: Laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha Swalaah, kutoa Zakaah na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]
 
www.alhidaaya.com





26- Hakuna Anayeweza Kukizuia Alichokitoa Allaah Wala Kutoa Alichokizuia Wala Utajiri Wa Mtu Hautamsaidia Aliye Tajiri Mbele Ya Allaah





عَنْ وَرَّادٍ، كَاتِبِ الْمُغِيرَةِ قَالَ: كَتَبَ مُعَاوِيَةُ إِلَى الْمُغِيرَةِ: اكْتُبْ إِلَىَّ مَا سَمِعْتَ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم‏.‏ فَكَتَبَ إِلَيْهِ: إِنَّ نَبِيَّ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ يَقُولُ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلاَةٍ: (( لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ، وَحْدَهُ لاَ شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ، وَهْوَ عَلَى كُلِّ شَىْءٍ قَدِيرٌ، اللَّهُمَّ لاَ مَانِعَ لِمَا أَعْطَيْتَ، وَلاَ مُعْطِيَ لِمَا مَنَعْتَ، وَلاَ يَنْفَعُ ذَا الْجَدِّ مِنْكَ الْجَدُّ ‏))

Warraad (Mwandishi wa Al-Mughiyrah bin Shu'bah) amesema: Mu’aawiyah alimwandikia Al-Mughiyrah: Niandikie ambayo uliyasikia kutoka kwa Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم): Basi akamwandikia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akisema kila baada ya kumaliza Swalaah:



Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa-Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Allaahumma laa maani’a limaa A’-twayta, walaa mu’-twiya limaa mana’-ta, walaa yanfa’u dhal-jaddi Minkal-jaddu



Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye ni Muweza wa kila kitu. Ee Allaah, hakuna mwenye kukizuia Ulichokitoa, wala mwenye kutoa Ulichokizuia, na wala utajiri wa mtu haumnufaishi mwenye utajiri mbele Yako. [Al-Bukhaariy, Muslim na wengineo]



Tanbihi: Hii ni mojawapo wa Adhkaar za kila baada ya Swalaah.
 
www.alhidaaya.com



27- Laa Ilaaha Illa Anta Al-Ahadu Asw-Swamadu … Du’aa Inayotakabaliwa Ambayo Mna Jina Adhimu Kabisa





عن ‏عَبْدِ اللَّهِ بن بُرَيْدَةَ الأسْلَمِيِّ ‏عن‏ ‏أبِيهِ (رضي الله عنهما) ‏قال: ‏سَمِعَ النَّبِيُّ (‏صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ‏رَجُلاً يَدْعُو وَهُوَ يَقُولُ: "اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ‏ ‏كُفُوًا ‏‏أحَدٌ" فقال: ((وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَقَدْ سَألَ اللَّهَ بِاسْمِهِ الأعْظَمِ الَّذِي إذَا دُعِيَ بِهِ أجَابَ وَإذَا سُئِلَ بِهِ أعْطَى))

Kutoka kwa ‘Abdullaah bin Buraydah Al-Aslamiyy, kutoka kwa baba yake (رضي الله عنهما) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimsikia mtu akiomba:



اللَّهُمَّ إنِّي أسْأَلُكَ بِأنِّي أشْهَدُ أنَّكَ أنْتَ اللَّهُ لا إِلَهَ إِلاَّ أنْتَ الأحَدُ الصَّمَدُ الَّذِي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُنْ لَهُ‏ ‏كُفُوًا ‏‏أحَدٌ

(Ee Allaah, hakika mimi nakuomba kwa kushuhudia kwamba hakika Wewe ni Allaah, hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Wewe, Mmoja, Aliyekamilika sifa za kila aina ya utukufu Wake, Mwenye kukusudiwa kwa haja zote, Ambaye Hakuzaa na wala Hakuzaliwa, Na wala haiwi Awe na yeyote anayefanana na kulingana Naye) Akasema: ((Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, amemuomba Allaah kwa Jina Lake Adhimu kabisa Ambalo Anapoombwa kwalo [du’aa] Anaitikia na Anapotakwa kwalo [jambo] Hutoa)) [Swahiyh Ibn Maajah (3125) Swahiyh At-Tirmidhy (3475), Swahiyh Abi Daawuwd (1493), Swahiyh At-Targhiyb (1640)]
 
www.alhidaaya.com



28-Laa Ilaaha Illa Anta Khalaqatani Wa Anaa ‘Abduka….

Sayyidul-Istighfaar: (Du’aa Kubwa Kabisa Kuliko Zote Ya Kuomba Maghfirah)





Hadiyth ya Shaddaad bin ‘Aws (رضي الله عنه), Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema:

((مَنْ قَالَهَا مِنْ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ، وَمَنْ قَالَهَا مِنْ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ))

((Atakayesema mchana akiwa na yakini nayo, akafariki siku hiyo kabla kuingia jioni basi atakuwa mtu wa Jannah, na atakayesema usiku naye akiwa yakini nayo akafariki kabla hajafika asubuhi basi yeye ni mtu wa Jannah)) - Al-Bukhaariy (7/150) [2306]- Sayyid Al-Istighfaar:



اللّهـمَّ أَنْتَ رَبِّـي لا إلهَ إلاّ أَنْتَ، خَلَقْتَنـي وَأَنا عَبْـدُك، وَأَنا عَلـى عَهْـدِكَ وَوَعْـدِكَ ما اسْتَـطَعْـت، أَعـوذُبِكَ مِنْ شَـرِّ ما صَنَـعْت، أَبـوءُ لَـكَ بِنِعْـمَتِـكَ عَلَـيَّ وَأَبـوءُ بِذَنْـبي فَاغْفـِرْ لي فَإِنَّـهُ لا يَغْـفِرُ الذُّنـوبَ إِلاّ أَنْتَ

.

Allaahumma Anta Rabbiy laa ilaaha illaa Anta Khalaqtaniy wa ana ‘abduka wa anaa ‘alaa ‘ah-dika wawa’-dika mastatwa’-tu, a’uwdhu bika minsharri maa swana’-tu, abuw-u Laka bini’-matika ‘alayya waabuw-u bidhambiy, faghfirliy fainnahu laa yaghfirudh dhunuwba illaa Anta



Ee Allaah, Wewe ni Rabb wangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, umeniumba mimi na mimi ni mja Wako, nami niko juu ya ahadi Yako, na agano Lako, kiasi cha uwezo wangu, najikinga Kwako kutokana na shari ya nilichokifanya, nakiri Kwako kwa kunineemesha, na nakiri kwa madhambi yangu, basi nakuomba unighufurie kwani hakuna wa kughufuria madhambi ila Wewe .
 
www.alhidaaya.com



29-Allaahumma Inniy As-alauka Bianna Lakal-Hamdu Laa Ilaaha Illa Anta… (Du’aa Hutakabaliwa Kwa Kutajwa Jina Adhimu Kabisa La Allaah)





عَنْ أَنَسٍ أَنَّهُ كَانَ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ جَالِسًا وَرَجُلٌ يُصَلِّي ثُمَّ دَعَا: "اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَمْدُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ الْمَنَّانُ بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ يَا ذَا الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ" فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : ((لَقَدْ دَعَا اللَّهَ بِاسْمِهِ الْعَظِيمِ الَّذِي إِذَا دُعِيَ بِهِ أَجَابَ وَإِذَا سُئِلَ بِهِ أَعْطَى))



Imetoka kwa Anas bin Maalik Maalik (رضي الله عنه) kwamba alikuwa amekaa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na mtu mmoja alikuwa akiswali akaomba:



اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ بِأَنَّ لَكَ الْحَمْدُ لَا إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ الْمَنَّانُ بَدِيعُ السَّمَوَاتِ وَالْأَرْضِ يَا ذَا الْجَلَالِ وَالْإِكْرَامِ يَا حَيُّ يَا قَيُّومُ



Allaahumma inniy as-aluka bianna Lakal-Hamdu laa ilaaha illaa Anta Al-Mannaanu Badiy’us-samaawaati wal-ardhwi, yaadhal-Jalaali wal Ikiraami, yaa Hayyu yaa Qayyuwmu,



Ee Allaah hakika mimi nakuomba, kwa vile Himdi ni Zako, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe, Mwingi wa Kuneemesha, Mwanzishi wa mbingu na ardhi, Ee Mwenye Ujalali na Ukarimu, Ee Uliyehai daima, Msimamizi wa kila kitu.



Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((kwa yakini amemuomba Allaah kwa Jina Lake Tukufu ambalo Anapoombwa kwalo Anaitikia na Anapotakwa kwalo jambo hutoa)) - Ahlus-Sunan; Abu Daawuwd [1495], An-Nasaaiy (3/52), ibn Maajah [3858] na taz Swahiyh ibn Maajah (2/329)
 
www.alhidaaya.com



30-Allaahumma Rahmatika Arjwu Falaa Takilniy Ilaa Nafsiy….Laa Ilaaha Illa Anta Ni Miongoni Mwa Du’aa Wakati Wa Janga Na Balaa





عن نفيع بن الحارث الثقفي أبو بكرة رضي الله عنه قال: إنَّ رسولَ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّم قال كلماتُ المكروبِ: اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت



Kutoka kwa Nafiy’ bin Al-Haarith Ath-Thaqafiyy Abuu Bakrah (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وسلم) amesema: ((Miongoni mwa maneno (ya kuomba) katika kupatwa janga na balaa ni:



اللّهُـمَّ رَحْمَتَـكَ أَرْجـو فَلا تَكِلـني إِلى نَفْـسي طَـرْفَةَ عَـيْن، وَأَصْلِـحْ لي شَأْنـي كُلَّـه لَا إِلَهَ إِلَّا أنْـت



Allaahumma Rahmatika arjuw falaa Takilniy ilaa nafsiy twarfata ‘aynin, wa-Aswlih liy sha-aniy kullahu, laa ilaaha illaa Anta.



Ee Allaah, Rahma Zako nataraji, usinitegemeze kwenye nafsi yangu japo kwa muda wa upepesa jicho, na Unitengenezee mambo yangu yote, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe.

[Abuu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), Al-Albaaniy ameipa daraja ya Hasan katika Swahiyh Abiy Daawuwd (3/959), Swahiyh Al-Jaami’ (3388), Swahiyh At-Targhiyb (1823), pia Irwaa Al-Ghaliyl (3/356), Takhriyj Mishkaat Al-Maswaabiyh (2382)]
 
Hadiyth Kuhusu Fadhila Za Laa Ilaaha Illa Allaah



www.alhidaaya.com



31-Nyiradi Ya Baada Ya Kila Swalaah:



Laa Ilaaha Illa Allaah… Laa Hawla Walaa Quwwata Illa BiLLaah…







عن عبدالله بن الزبير قال: كان رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليه وسلَّمَ يُهَلِّلُ بهنَّ دُبُرَ كلِّ صلاةٍ:



لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون



Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah ibn Zubayr amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akitamka Tahliyl (laa ilaaha illa Allaah) kila baada ya Swalaah:



لا إلهَ إلاّ اللّه وحدَهُ لا شريكَ لهُ، لهُ الملكُ ولهُ الحَمد، وهوَ على كلّ شيءٍ قدير، لا حَـوْلَ وَلا قـوَّةَ إِلاّ بِاللهِ، لا إلهَ إلاّ اللّـه، وَلا نَعْـبُـدُ إِلاّ إيّـاه، لَهُ النِّعْـمَةُ وَلَهُ الفَضْل وَلَهُ الثَّـناءُ الحَـسَن، لا إلهَ إلاّ اللّهُ مخْلِصـينَ لَـهُ الدِّينَ وَلَوْ كَـرِهَ الكـافِرون



Laa ilaaha illa-Allaahu Wahdahu laa shariyka Lah. Lahul-Mulku wa Lahul-Hamdu wa Huwa ’alaa kulli shay-in Qadiyr. Laa hawla walaa quwwata illaa biLLaah. Laa ilaaha illa-Allaah. Walaa na’-budu illaa Iyyaahu. Lahun-Ni’-matu walahul-fadhwlu walahuth-thanaaul-hasan. Laa ilaaha illa-Allaah Mukhliswiyna Lahud-diyna walaw karihal-kaafiruwn



”Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah hali ya kuwa Peke Yake Hana mshirika, ni Wake Ufalme, na ni Zake Himdi, na Yeye ni Qadiyr (Muweza) wa kila kitu. Hapana uwezo wala nguvu ila kutoka kwa Allaah. Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, wala hatumwabudu ila Yeye, ni Zake neema, na ni Wake ubora, na ni Zake Sifa nzuri zote, Hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah, hali ya kumtakasia Dini Yake, ijapokuwa wanachukia makafiri.” [Muslim (1/415) [594]
 
www.alhidaaya.com





32-Allaahumma ‘Aafiniy Fiy Badaniy… Laa Ilaaha Illa Anta – Miongoni Mwa Adhkaar Za Asubuhi Na Jioni





عَبْدُ الرَّحْمَنِ بْنُ أَبِي بَكْرَةَ، أَنَّهُ قَالَ لأَبِيهِ يَا أَبَةِ إِنِّي أَسْمَعُكَ تَدْعُو كُلَّ غَدَاةٍ: ((اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ)) تُعِيدُهَا ثَلاَثًا حِينَ تُصْبِحُ وَثَلاَثًا حِينَ تُمْسِي‏.‏ فَقَالَ إِنِّي سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَدْعُو بِهِنَّ فَأَنَا أُحِبُّ أَنْ أَسْتَنَّ بِسُنَّتِهِ ‏



Kutoka kwa ‘Abdur-Rahmaan bin Abiy Bakrah (رضي الله عنه) ambaye amesema kuwa alimwambia baba yake: “Ee baba yangu, mimi nakusikia ukiomba hivi kila asubuhi:



اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَدَنِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي سَمْعِي اللَّهُمَّ عَافِنِي فِي بَصَرِي لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ



Allaahumma ‘aafiniy fiy badaniy, Allaahumma ‘aafiniy fiy sam-’iy, Allaahumma ‘aafiniy fiy baswariy, laa ilaaha illaa Anta. Allaahumma inniy a’uwdhu bika minalkufri walfaqri. Allaahumma inniy a’uwdhu bika min ‘adhaabil qabri laa ilaaha illaa Anta. (mara 3)



Ee Allaah, nipe ‘aafiyah (afya, siha, usalama, amani) ya mwili wangu, Ee Allaah, nipe ‘aafiyah ya masikio yangu, Ee Allaah, nipe ‘aafiyah macho yangu, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe. Ee Allaah, hakika mimi najikinga Kwako kutokana na ukafiri, na ufakiri, na najikinga Kwako kutokana na adhabu ya kaburi, hapana mwabudiwa wa haki ila Wewe)) Unaomba mara tatu asubuhi na jioni. Akasema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akitamka maneno hayo katika kuomba du’aa basi nami napenda kufuata Sunnah yake.” [Abuu Daawuwd (4/324) [5090], Ahmad (5/42), An-Nasaaiy katika ‘Amal Al-Yawm wal-Laylah [22], Ibn As-Sunniy [69], Al-Bukhaariy katika Adab Al-Mufrad na isnadi yake ameipa daraja ya Hasan Al-‘Allaamah Ibn Baaz (رحمه الله) katika Tuhfat Al-Akhyaaar (Uk. 26). Pia Swahiyh Abiy Daawuwd (5090).]
 
www.alhidaaya.com





33-Subhaanaka Allaahumma wa bihamdika … Ash-hadu Anlaa Ilaaha Illaa Anta – Du’aa Ya Kafara Kikao





عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا، قَالَتْ: مَا جَلَسَ رَسُولُ اللهِ مَجْلِسًا قَطُّ، وَلاَ تَلاَ قُرْآناً، وَلاَ صَلَّى صَلاَةً إِلاَّ خَتَمَ ذَلِكَ بِكَلِمَاتٍ، قَالَتْ: فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَرَاكَ مَا تَجْلِسُ مَجْلِساً، وَلاَ تَتْلُو قُرْآنًا، وَلاَ تُصَلِّي صَلاَةً إِلاَّ خَتَمْتَ بِهَؤُلاَءِ الْكَلِمَاتِ؟ قَال: ”نَعَمْ، مَنْ قَالَ خَيْراً خُتِمَ لَهُ طَابَعٌ عَلَى ذَلِكَ الْخَيْرِ، وَمَنْ قَالَ شَرّاً كُنَّ لَهُ كَفَّارَةً: سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، لاَ إِلَهَ إِلاَّ أَنْتَ، أَسْتَغْفِرُكَ وَأَتُوبُ إِلَيْكَ“. أخرجه النسائي في ”السنن الكبرى“ (9/123/10067) ، والسمعاني في ”أدب الإملاء والاستملاء“ (ص75)، وابن ناصر الدين في ”خاتمة توضيح المشتبه“ (9/282)، وصححه الألباني في ”السلسلة الصحيحة“ (7/495).





Imepokelewa kutoka kwa mama wa Waumini 'Aaishah (رضي الله عنها ) Amesema: “Hajapatapo kukaa Rasuli wa Allaah (kikao wala kusoma Qur-aan wala kuswali ila atamaliza na du'aa hii): “Subhaanaka Allaahumma wa bihamdika ash-hadu anlaa ilaaha illaa anta astagh-firuka wa atuwbu ilayka” Amesema mama wa Waumini 'Aaishah رضي الله عنها nikamuuliza “Ee Rasuli wa Allaah nakuona hukai kikao chochote wala husomi Qur-aan wala huswali Swalaah yoyote ile ila unaimalizia kwa kusoma maneno haya kwanini hasa? Akasema صلى الله عليه وسلم: “Ndiyo anayesema khayr amalize kwa khayr na anayesema shari yanakuwa maneno haya ni kafara kwake.” [An-Nasaaiy katika As-Sunan Al-Kubraa, na ameisahihisha Al-Albaaniy]
 
Back
Top Bottom