Ramadhan Special Thread
Maswali: Qur-aan


Kusoma Qur-aan Kwa Maandishi Ya Kilatini Atapata Thawabu Sawa Na Mwenye Kusoma Qur-aan Kwa Kiarabu?



Alhidaaya.com



SWALI:



Assalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakatuh.

Sifa njema zote in za Allaah. Namshukuru Allah Subhannah Wataallah kuniongoza kujiunga na uanachama na AL HIDAAYA. Nimekuwa napata makala zenu kupitia kwa wenzangu kwa muda mrefu na nimefaidika sana kielimu katika dini yetu tukufu ya Kiislamu. Allaah Subhannah Wataallah awajaze kila la kheri wahusika wote wanaojitahidi kuelemisha jamii ya kiislam kupitia mtandao huu.



Nina swali naomba msaada maana mie sikujaliwa kusoma Qurani kwa Kiarabu ila naisoma sana kwa Kiswahili.



Mwisho, je sisi tunaosoma Kitabu hiki Kitukufu kwa Kiswahili au kiingereza tutapata thawabu kama anayekisoma kwa Kiarabu? Hasa wale ambao hata hawajui maana yake? Mie nina miaka zaidi ya 50 nashindwa kuimudu na kukariri isipokuwa sura fupi fupi ambazo zinaniwezesha kutimiza masharti ya swallah na duaah.



Jazaakum Allahu Khaira.





JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu wanaomilkiwa na mikono yetu ya kuume. Hakika ni kuwa Aayah hizi ambazo umezitaja zinatupatia sifa za Waumini wa kihakika.





Kuhusu kupata thawabu katika kusoma ni kusoma Qur-aan katika lugha yake ya asili nayo ni kwa Kiarabu. Hii ni kwa mujibu ya Hadiyth iliyonukuliwa na at-Tirmidhiy, ambamo Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



"Yeyote mwenye kusoma herufi moja ya Qur-aan anapata thawabu kumi wala sisemi Alif Laam Miym ni herufi, bali Alif ni herufi, Laam ni herufi na Miym ni herufi" [at-Tirmidhiy].



Hivyo, mwenye kusoma Alif Laam Miym anapata thawabu 30. Ama katika kusoma huko inafaa ieleweke kuwa inafaa tusiwe ni wenye kusoma kama kasuku bali tunahitajika kutilia maanani, kuzingatia, kujua maana na kufuata yaliyomo ndani. Ndio Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatueleza kuwa huenda tukawa tunasoma Qur-aan nayo inatulaani nasi hatuna habari kabisa.



Ama ukisoma Qur-aan kwa lugha nyingine hiyo haisemekani kuwa umesoma Qur-aan bali umesoma tafsiri ya Qur-aan. Kwa sababu hiyo tafsiri ni elimu utakuwa unapata thawabu ya kusoma mema na kusoma mambo mazuri. Tufahamu kuwa tunapata ujira kwa kusoma elimu na hakuna iliyo njema kama kusoma tafsiri ya Qur-aan.



Hata hivyo ndugu yetu tunakusihi bado unao muda wala hujakuwa mzee hivyo. Na lau utafanya bidii basi utaweza kusoma Qur-aan kwa Kiarabu bila ya matatizo yoyote kwa muda mfupi kabisa usiozidi hata miezi mitatu ikiwa utafanya bidii. Mfano mzuri ni hivi majuzi tu kulitoka habari za kuaminika za mama mwenye umri wa miaka 70 amekamilisha kuhifadhi Kitabu cha Allaah na habari hizo zikaenea kwenye tovuti mbalimbali za kuaminika, japo inaweza kuonekana kuwa hiyo ni kesi ya nadra, lakini hakuna kisichowezekana kwa uwezo wa Allaah na juhudi za mja. Kinachotakiwa ni wewe kuwa mkakamavu na mwenye bidii na hilo utaliweza bila ya shida. Kwa wakati huu wetu, zipo kaseti za Qur-aan nzima ikisomwa na wasomaji mahiri zenye kufunisha usomaji wa Qur-aan, zipo CD na njia nyingine za kuweza kujifunza, kinachotakiwa ni wewe kufanya bidii, kupanga muda, kufanya mazoezi ya kusoma na In shaa Allaah utaweza kufikia malengo na kufanikiwa.



Pia tufahamu kuwa kujifunza Lugha ya kiarabu ni jambo muhimu sana kwa Muislam na kuna fadhila kubwa katika hilo.





Na Allaah Anajua zaidi
 
Kuweka Milio Ya Miziki Kwenye Simu Za Mkononi

Au Qur-aan Inayosomwa Au Adhaana Au Du'aa



Alhidaaya.com









SWALI:



Namshukuru Allah aliye niwezesha kuuliza swali na Allaah atawalipa mema. Jee kuweka ring tone ktk simu ni vibaya? yaani ndio ikawa mlio wa simu. Shukran wajazaakumu-Allahul khayra. musinisahau nami kunijibu ktk email yangu nisome kiurahisi





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Twataraji kuwa majibu haya yatakayotolewa yatawafaidi wengi wenye tatizo . Awali ya yote tufahamu kuwa Mobile zimekuja na mazuri mengi kurahisisha mawasiliano baina ya watu. Lakini kama ilivyo vitu vizuri vingi huwa havikosi maafa na madhara vinapotumiwa kwa njia mbaya.





Ni hakika inayojulikana na kila mmoja kuwa vifaa hivi huwa vinaleta ghasia kubwa katika Misikiti na hivyo kuharibia unyenyekevu wa wenye kuswali wakati zinapoanza kulia na mbaya zaidi zinapokuwa na miziki. Jambo hili limepelekea katika Miskiti yetu kuwa Imaam baada ya tu kusema tengenezeni safu zenu, anakariri 'zimeni mobile zenu'. Hapo hapo tutakuta za wengineo zinalia watu wakiwa katika Swalaah. Haya yamekuwa ni maudhi na kero kubwa. Tufahamu kuwa Allaah Aliyetukuka Anatuambia:



وَالَّذِينَ يُؤْذُونَ الْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ بِغَيْرِ مَا اكْتَسَبُوا فَقَدِ احْتَمَلُوا بُهْتَانًا وَإِثْمًا مُّبِينًا ﴿٥٨﴾

Na wale wanaowaudhi Waumini wa kiume na Waumini wa kike bila ya kuwa wamechuma kosa, basi kwa yakini wamejibebea usingiziaji mkuu wa dhulma na dhambi bayana. [Al-Ahzaab: 58]





Hakuna maudhi kama kumuharibia mtu Swalaah yake, ambayo ni 'Ibaadah kubwa katika Uislamu.

Sana





Kwa hakika shaytwaan ametupambia njia zake mpaka tukaziona kuwa ni nzuri na hivyo kuziendea kwa njia moja au nyingine. Katika hizo shaytwaan ametufanya kuona kuwa muziki ni halali kabisa mbali na kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatuambia:



وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا ۚ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿٦﴾

6. Na miongoni mwa watu, yuko ambaye hununua maneno ya upuuzi ili apoteze (watu) njia ya Allaah bila elimu, na huichukulia mzaha. Hao watapata adhabu ya kudhalilisha.

[Luqmaan 31: 6]





'Abdullaah bin Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) aliapa kuwa maneno hayo ya upuuzi ni muziki na hivyo kuwa ni haramu kwa Muislamu, kusikiliza au yeye mwenyewe kuimba.

Na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameharamisha ala za muziki pale aliposema:



"Kutakuwa na watu miongoni mwa Ummah watakaohalalisha uzinzi, hariri, pombe na ala za muziki" [Al-Bukhaariy]

Hadiyth hii inatuashiria kwa kutujulisha kuwa ala za muziki ni haramu kwa kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametuambia kuwa wapo watu watakaoona kuwa zinaruhusiwa mbali na kuwa ni haramu. Pia ala hizo zimetajwa na vitu ambazo vinafahamika kuwa ni haramu uzinifu na pombe lau hazingekuwa haramu hazingetajwa pamoja navyo.



Inawezekana kuacha kitu hicho cha haramu kwa njia rahisi kabisa kwa kuweka mlio wa kawaida au mlio mwingine wowote ambao si wa muziki. Hakika ni kuwa mlio wa muziki aina yoyote hauruhusiwi kuwekwa katika simu za mkono (mobile phones).

Japokuwa muulizaji hakuuliza swali la kuweka sauti za wasomaji wa Qur-aan kuwa ndio mlio wa simu tungependa kuwatanabahisha ndugu zetu kwa kuwaambia yafuatayo:



Ni hakika isiyopingika kuwa Qur-aan ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ambayo yanafaa yaheshimiwe kwa kiwango cha juu kabisa na kila Muislamu. Qur-aan imeteremshwa kuwa ni uongofu kwa wanaadamu wote alivyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):



شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ ۚ

Mwezi wa Ramadhwaan ambao imeteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu na hoja bayana za mwongozo na pambanuo (la haki na batili). [Al-Baqarah: 185]





Qur-aan inafaa isomwe au isikilizwe kwa makini na kutafakari yaliyo ndani pamoja na kufuata.



Kuiweka tu kuwa ni mlio huwa umeitweza kwa kiasi kikubwa kwa kuwa inaweza kuwa inalia nawe unazumgumza bila kujali. Au inalia na wewe kwa kuwa una haraka kuipokea unafanya hivyo hata kabla ya Aayah yenyewe kukamilika. Na tufahamu kuwa simu hiyo inaweza kupigwa ukiwa chooni na hivyo kuikosea heshima kabisa kwani ikiwa jina la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) likiwa limeandikwa mahali hufai kuingia na kitu hicho chooni na pia ikiwa hufai kulitaja katika sehemu hiyo seuze sasa Aayah zake zikawa zinasomwa katika sehemu hiyo – chooni.



Pia wengine huweka mlio wa Adhaana au Du’aa kwenye simu zao, nayo pia haipasi kwani havikuletwa hivyo kwetu kwa ajili ya kumjulisha mtu kuwa anaitwa katika simu bali ni kwa ajili ya kujulisha wakati wa kuwadia Swalaah na kwa ajili ya kumwomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Vilevile huenda ikamshughulisha mtu kudhani wakati wa Swalaah umeingia kumbe bado na pia huenda ikalia wakati wa Magharibi na mtu amefunga akadhani ni wakati wa futari na kumsababishia mtu kufungua kabla ya wakati!



Tunamnasihi kila mmoja katika ndugu zetu asiwe ni mwenye kuweka sauti za usomaji wa Qur-aan au Adhaana au Du’aa kama mlio wa simu bali aweke mtikisiko au mtetemo (vibration) au ikibidi waweke mlio wa kawaida wa asili ile milio ya kizamani ya simu.



Na muhimu wenye kuweka sauti kwenye mobile zao wawe wanazima simu zao wanapoingia sehemu Msikitini, kwenye Madarsa ya Dini, au kwenye Mihadhara ili wasiharibu Swalaah au utulivu wa waliohudhuria kusikiliza mafunzo ya Dini katika sehemu hizo, na pia kuheshimu sheria za nyumba ya Allaah.



Na Allaah Anajua zaidi
 
haya mambo yaliandik
Kusikiliza Qur-aan Huku Unafanya Kazi Zako



Alhidaaya.com





SWALI



Jee unaweza kusikiliza Qur-an kwa makini huku unafanya kazi zako jikoni kama kupika au kukosha vyombo ingawa akili yako yote iko katika kile kisomo?





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Hii haina shaka kwani kusikiliza huko kwa makini ndiko kumesisitizwa zaidi. Na linalochukiza kwa baadhi ya ‘Ulamaa ni kuzungumza na huku Qur-aan inasomwa kwa ushahidi wa aya hii:



وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿٢٠٤﴾

Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na bakieni kimya (mzingatie) ili mpate kurehemewa. [Al-A'araaf: 204]



Hata hivyo pamoja na baadhi ya wanachuoni kusema kuwa aayah hiyo makusudio ni popote, ila wanachuoni wengi na wafasiri kama Ibn Kathiyr katika tafsiri yake kasema: "Maana yake ni ukiwa ndani ya Swala ya Jamaa'ah, pindi Imamu anaposoma kwa sauti (swala za Alfajiri, Maghrib na 'Ishaa') kama ilivyopokewa na Imaam Muslim kwenye Sahiyh yake kutoka katika hadithi ya Abu Muwsaa Al-Ash'ariy aliyesema: Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa Sallam) amesema: ((Imaam amewekwa ili afuatwe, kwa hivyo akisema: "Allaahu Akbar nanyi mfuateni kwa kusema kama yeye na akianza kusoma, nyinyi nyamazeni))



Vile vile akasema tena Ibn Kathiyr: Ibraahiym Ibn Muslim Al-Haajriy amepokea kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) aliyesema: Wao (Swahaba) walikuwa wakizungumza na hali ya kuwa wamo ndani ya swala, kwa hivyo ilipoteremshwa aya hii ... waliamrishwa wawe kimya.



Naye Imam At Twabariy kwenye tafsiri yake anasema kwamba Ibn Mas'uud amesema: Tulikuwa tukipeana salamu miongoni mwetu tukiwa ndani ya swala, kisha ikaja katika Qur-aan: Na isomwapo Qur-aan isikilizeni na nyamazeni.



Kwa hoja hizo inaonyesha aayah hiyo haihusiani na Qur-aan isomwayo maredioni na kwenye matelevisheni makompyuta au na watu nje ya swala, hata hivyo kwa kuyapa heshima maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni bora kunyamaza isomwapo au kuizima kama huwezi kusikiliza. Wa Allaahu A'alam



Nasiha Ya Kufuata Adabu Za Tilawa (Kusoma) Qur-aan;

Kwa hali yeyote ilivyo, ni bora kuipa heshima Qur-aan kwa kutimiza adabu za kusoma Qur-aan kwani ni maneno ya Allaah Subhaanahu wa Ta’aalaa na kuyatukuza ni wajibu. Nazo ni:



1) Kupiga mswaki

2) Kuwa na wudhuu

3) Kujifunika vizuri (mwanamke)

4) Kuelekea qibla

5) Kusoma kwa kutafakari

6) Kusoma kwa Tajwiid na kufuata sheria zake.





Na Allaah Anajua zaidi

haya mambo yaliandikwa > miaka 1500 iliyopita wakati dunia ikiwa haijapiga hatu kiteknologia kama leo hii, mfano mnaposema mwanamke akiwa hedhi siyo msafi kushika kitabu cha dini, lkn ukikiweka hicho kitabua unachomkataza mwanamke asikishike chini ya microscope utaona uchafu zaidi ya huo kuanzia bacterias, viruses na mpaka minyoo isiyoonekana kwa macho.

nachojaribu kusema ni kwamba mambo mengine yamepitwa na wakati kuweza kuyatumia leo hii, ndiyo maana hata ukienda gulf states kama uae, katar au hata saudia kuna mambo wameshalegeza, mfano uae huwezi kukutana na mwarabu wa uae kaoa wake 4 hata kama ni tajiri, huko mwanaume 1 mke 1 …
 
Kwa Nini Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatumia Neno 'Sisi',

Au 'Tuta....' Na Hali Yeye Hana Mshirika?



Alhidaaya.com





SWALI:



Asalam aleykum.



Mimi Nina Swali Kuhusu Mada Hii Mpya Ya Madhara Ya Chumo Laharam. Kama Ilivyoandikwa Kama “enyi Mlioamini Msiliane Mali Zenu Kwa Batili. Isipokua Iwe Biashara Ya Kuridhiana Baina Yenu. Wala Msijiue (wala Msiue Wenzenu) Hakika Allaah Ni Mwenye Kukuhurumieni. Na Atakae Fanya Hayo Kwa Uadui Na Dhulma Basi Huyo ''tuta Muingiza Motoni''.

Swali Langu Ni Hivi, Inakuaje Linatumika Neno ''tuta'' Kwa Wingi Wakati Allaah Ni Mmoja? Na Sio Mada Hii Pekee Inayosema Hivyo. Hata Ninaposoma Tafsir Za Kuran Huwa Nikikutana Na Neno Hilo Au Neno ''tuli'' Je Inamaanisha Vip?

Nitashukuru Mkiweza Kunielimisha Hapo. Allaah Awajaalie Kheri Ya Hapa Duniani Na Kesho Akhera Kwa Kazi Njema Mnayoifanya. Shukran



JIBU:





AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Ni kweli maneno hayo yanatumiwa na Allaah Aliyetukuka ndani ya Qur-aan yanayomaanisha wingi. Sasa wengi kati yetu tunakuwa na utata mkubwa, vipi Allaah Aliyetukuka hana mshirika lakini Anatumia wingi katika kauli Zake?



Hakika ni kuwa hakuna utata wowote katika hilo kwani ni tabia ya utumizi wa lugha nyingi ikiwemo Kiarabu, Kiingereza na hata Kiswahili. Wingi huu katika Lugha ya Kiarabu unaitwa Jam’u Litta’dhwiym (wingi wa utukufu na ukubwa). Wingi umegawanyika sehemu mbili – wingi kama wingi na wingi wa utukufu. Wingi unaotumika katika Qur-aan kwa Allaah Aliyetukuka ni huu wingi wa utukufu na ukubwa.



Katika lugha ya Kiingereza inaitwa The Majestic We. Mara nyingi wakubwa na watukufu kama Raisi, Mfalme, Malkia, Waziri mkuu anapoandika barua au anapohutubia watu husema sisi ilhali makusudio ni yeye peke yake. Sasa hawa sisi ni kina nani na ilhali ni yeye peke yake? Bila shaka ndiyo hayo hayo matumizi ya kutumia wingu wa utukufu.



Na katika Kiswahili, pia utamkuta mzee anasema akimwambia mtoto wa mtu mwengine, sisi tumekulea ilhali yeye hakumlea wala hakushirikiana na wazazi wa mtoto katika hilo. Huo ni wingi wa ule ukubwa wake wa umri.



Na ndivyo katika Qur-aan, Allaah Anatumia wingi huo wa utukufu Naye hakuna anayemfikia hata kumkaribia katika ukubwa na utukufu Wake.



Na Mara nyingine katika Qur-aan Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Hutaja hivyo pale kitendo kinapohusiana na Malaika wanapotumwa kufanya jambo. Mfano Anapotuma Malaika kuangamiza mji Anataja kwa wingi kwa maana Yeye Subhaanahu wa Ta’aala Ndiye Aliyetuma Malaika kufanya kitendo hicho kama ilivyo katika mifano ifuatayo:



فَكَذَّبُوهُ فَأَهْلَكْنَاهُمْ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣٩﴾

Wakamkadhibisha; basi Tuliwaangamiza. Hakika katika hayo pana Aayah (ishara, zingatio n.k.), lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. [Ash-Shu’araa: 139]



فَأَرْسَلْنَا عَلَيْهِمْ رِيحًا صَرْصَرًا فِي أَيَّامٍ نَّحِسَاتٍ لِّنُذِيقَهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَلَعَذَابُ الْآخِرَةِ أَخْزَىٰ ۖ وَهُمْ لَا يُنصَرُونَ﴿١٦﴾

Basi Tukawapelekea upepo wa dhoruba na mngurumo katika siku za mikosi ili Tuwaonjeshe adhabu ya hizaya katika uhai wa dunia; na bila shaka adhabu ya Aakhirah ni ya hizaya zaidi, nao hawatonusuriwa. [Fus-Swilat: 16]



Tufahamu kuwa Allaah Aliyetukuka Ameupiga vita ushirikina katika njia zake zote na Akafunga milango yote ambayo itampelekea kuja karibu na ushirikina huo. Ushirikina unaharibu ‘amali na unamuingiza sahibu wake Motoni. Hivyo, Akasema:



قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ ﴿١﴾

Sema: Yeye ni Allaah Mmoja Pekee. [Al-Ikhlaasw: 1]







Na Allaah Anajua zaidi
 
haya mambo yaliandik


haya mambo yaliandikwa > miaka 1500 iliyopita wakati dunia ikiwa haijapiga hatu kiteknologia kama leo hii, mfano mnaposema mwanamke akiwa hedhi siyo msafi kushika kitabu cha dini, lkn ukikiweka hicho kitabua unachomkataza mwanamke asikishike chini ya microscope utaona uchafu zaidi ya huo kuanzia bacterias, viruses na mpaka minyoo isiyoonekana kwa macho.

nachojaribu kusema mambo mengine yamepitwa na wakati kuweza kuyatumia leo hii …
Inaposemwa uchafu ndugu yangu sio uchafu huo unaosema wewe,huo ni uchafu upande wa dini,kwamba mwanamke akiwa katika hedhi au nifasi,ili awe tohara kwa ajili ya ibada basi anatakiwe aoge josho maalumu la kujisafisha

Kwakuwa tu huwa msomi biblia,hata huko inatakiwa mwanamke akoge akiwa katika hali hiyo

Dini sio historia useme kwamba ni ya zamani imepitwa na wakati,dini ni mfumo na sheria za Mwenyezi Mungu ambazo zinatakiwa zifuatwe
 
Inaposemwa uchafu ndugu yangu sio uchafu huo unaosema wewe,huo ni uchafu upande wa dini,kwamba mwanamke akiwa katika hedhi au nifasi,ili awe tohara kwa ajili ya ibada basi anatakiwe aoge josho maalumu la kujisafisha

Kwakuwa tu huwa msomi biblia,hata huko inatakiwa mwanamke akoge akiwa katika hiyo

Dini sio historia useme kwamba ni ya zamani imepitwa na wakati,dini ni sheria za mfumo na sheria za Mwenyezi Mungu ambazo zinatakiwa zifuatwe

lkn hedhi haitoki kwa kujisafisha tu maji kwani ipo ndani ya mwili wake isitoshe kama unavyosema dini siyo wakati ni kweli, kwa nini leo hawapigi mawe wahalifu mpaka kifo ?
 
Kwa Nini Uislamu Unataka Ushahidi Wa Wanawake Wawili Badala Ya Mmoja Kama Wanaume?



Alhidaaya.com



SWALI:



Assalam alaykum.

Mimi ni mwislamu na nimekabiliwa na swali ambalo linanitatiza mimi kwa sababu nimeulizwa na wengi wasiokuwa waislamu.Ijapokuwa nimejaribu kulijibu kwa elimu nilionayo naona bado hawajaridhika. Maswali ni mawili na ni yafuatayo:

1. Katika Qur'an tukufu wanaume waumini wamebashiriwa pepo na wameahidiwa wanawake wazuri ambayo hawajaingiliwa na binadamu yeyote wala jini. Je wananwake wamebashiriwa hayo? NA kuna maulama wanaosema waumini wa kiislamu waaume watafufuliwa na wake zao.

2. Utamwelezaje asiye muislamu kwa nini mwanamke kauli yake ni nusu ya mwanamume. Yaani ikiwa ni shahidi basi wanawake wanne wanatakikana au wanaume wawili.

Ninavyoamini mimi kila jambo la kiislamu tulioamrishwa kuna maana yake na alhamdulillah mengi nimetafuta maana na nikayapata.Ningependa kusikia mwislamu mwenzangu angejibu nini akiulizwa na asiyekuwa mwislamu maswali haya.

Shukran wa jazakAllaahu kheir.



JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.



Hakika ni kuwa Uislamu ulikuja kumtoa mwanmke katika minyororo aliyokuwa amefungwa nayo. Suala la mwanamke limezua mjadala mkubwa sana katika ulimwengu kwa sababu ya ujahili. Hata Waislamu wamekuwa katika njia panda kwa sababu hiyo hiyo. Mbali na ujahili, athari ya tamaduni za kimagharibi zimewafanya watu wasijue uhakika kuwahusu.



Mengi yamesemwa kuhusu hadhi na majukumu ya mwanamke wa Kiislamu. Yote haya yametokea kwa sababu ya nadharia zisizokuwa na msingi wowote wa dini. Wapotofu wa Kimagharibi mpaka sasa wana fikra chafu dhidi ya Uislamu. Hii ni dhahiri kulingana na makala ya mwandishi wa Woman in Islam (Mwanamke katika Uislamu): "Katika kipindi cha miaka 15 kuanzia nilipoingia katika Uislamu, nimeulizwa maswali mengi kuhusu maisha ya Muislamu na wasiokuwa Waislamu na marafiki zangu… wanauliza: Je, katika Uislamu, mnaamini kuwa mwanamke ana roho? Waislamu wanawake hawaswali au kwenda Makkah, je wanafanya hayo? Pepo ni kwa wanaume peke yao au sivyo?" Mengi ni kuwa mwanamke hana haki ya ilimu, kutoa rai, kuwa na akiba yake ya rasilmali au pesa, na kadhalika. Haya ni maswali ambayo yanaulizwa na yataendelea kuulizwa.



Ukitaja kujua neema ambayo Uislamu imempatia mwanamke soma kuhusu wanawake wanavyofanywa katika staarabu nyingine. Utakuta kuwa Uislamu umemuenzi mwanamke kwa kumpatia uhuru wa kumiliki atakacho, kuchuma, anashirikiana na mwanaume katika kunyanyua viwango vya maadili, kufanya Da'wah, kupata ilimu na kufundisha, kutoa rai na maoni, kushiriki katika Jihadi na mengineo mengi. Amepatiwa hadhi ya kijamii kama mama, mke, dada, binti, na kadhalika.



Hakika ni kuwa Pepo katika Uislamu na utukufu unategemea utendaji kazi na amali zake njema anazofanya. Wapo wanawake ambao wataingia motoni kama vile wanaume, na wapo wanawake ambao wataingia Peponi kama vile wanaume. Amali njema ni muhimu sana katika kufanikisha wepesi wa kuingia Peponi. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatueleza kuwa ubora mbele yake ni uchaji Mungu. Hivyo ikiwa mwanamke ana Imani na taqwa zaidi atakuwa karibu zaidi na Allaah kama Alivyosema Aliyetukuka:



يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَاكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَاكُمْ شُعُوبًا وَقَبَائِلَ لِتَعَارَفُوا ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّـهِ أَتْقَاكُمْ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ﴿١٣﴾

Enyi watu! Hakika Sisi Tumekuumbeni kutokana namwanamme na mwanamke, na Tukakujaalieni mataifa na makabila ili mtambuane. Hakika aliye na hadhi zaidi miongoni mwenu mbele ya Allaah ni mwenye taqwa zaidi kati yenu. Hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Al-Hujuraat: 13.]



Ama kuhusu kuingia Peponi Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) katika Ayah nyingi Anatufahamisha dhahiri shahiri:



مَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً فَلَا يُجْزَىٰ إِلَّا مِثْلَهَا ۖ وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ﴿٤٠﴾

Yeyote atakayetenda uovu, basi hatolipwa isipokuwa mfano wake; na yeyote atakayetenda mema kati ya mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Jannah wataruzukiwa humo bila ya hesabu. [Ghaafir: 40]



Pia,

فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ۖ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۖ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ ﴿١٩٥﴾

Basi Rabb wao Akawaitikia Hakika Mimi Sipotezi ‘amali za mtendaji yeyote yule miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, nyinyi kwa nyinyi. Basi wale waliohajiri na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa katika njia Yangu, wakapigana na wakauliwa; bila shaka Nitawafutia makosa yao na bila shaka Nitawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito, ni thawabu kutoka kwa Allaah. Na kwa Allaah kuna thawabu nzuri kabisa. [Aal- 'Imraan: 195]



Na Amesema:

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ﴿٩٧﴾

Mwenye kutenda mema miongoni mwa wanamume au wanawake naye ni Muumin, Tutamhuisha uhai mzuri, na bila shaka Tutawalipa ujira wao kwa mazuri zaidi ya yale waliyokuwa wakitenda. [An-Naml: 97]



Uislamu umetufanya sote, wanawake na wanaume kuwa ndugu moja kama Alivyosema:

إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ﴿١٠﴾

Hakika Waumini ni ndugu, basi suluhisheni baina ya ndugu zenu. Na mcheni Allaah ili mpate kurehemewa. [Al-Hujuraat: 10)]



Pia ifahamike kuwa maamrisho yote ya 'Ibadah yameamriwa kwa wanaume na wanawake bila kubagua. Vile vile mwanamke au mwanaume akifanya kosa wanapata adhabu sawa kabisa. Kwa mfano mwanamke au mwanaume akiiba, Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Amebaini adhabu zao:

وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا جَزَاءً بِمَا كَسَبَا نَكَالًا مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ حَكِيمٌ ﴿٣٨﴾

Mwizi mwanamume na mwizi mwanamke ikateni (kitanga cha) mikono yao; ni malipo kwa yale waliyoyachuma, ndio adhabu ya kupigiwa mfano kutoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-Maaidah: 38 ]



Vile vile anapozini mwanamke anapatiwa adhabu sawa na mwanamme, kama Alivyosema Aliyetukuka:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٢﴾

Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao mijeledi mia. Na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika hukmu ya Allaah mkiwa nyinyi mnamwamini Allaah na Siku ya Mwisho. Na washuhudie adhabu yao kundi la Waumini. [An-Nuwr: 2]



Katika Aayah moja, Allaah Aliyetukuka Amebaini matendo chungu nzima ambayo yanafaa yafanywe na jinsiya zote mbili. Hapo hapo akaahidi Aliyetukuka kuwa mwenye kufanya hayo basi atapata maghfira na ujira mkubwa. Allaah Anasema:

إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ وَالصَّادِقِينَ وَالصَّادِقَاتِ وَالصَّابِرِينَ وَالصَّابِرَاتِ وَالْخَاشِعِينَ وَالْخَاشِعَاتِ وَالْمُتَصَدِّقِينَ وَالْمُتَصَدِّقَاتِ وَالصَّائِمِينَ وَالصَّائِمَاتِ وَالْحَافِظِينَ فُرُوجَهُمْ وَالْحَافِظَاتِ وَالذَّاكِرِينَ اللَّـهَ كَثِيرًا وَالذَّاكِرَاتِ أَعَدَّ اللَّـهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا ﴿٣٥﴾

Hakika Waislamu wanaume na wanawake, na Waumini wanaume na wanawake, na watiifu wanaume na wanawake, na wasemao kweli wanaume na wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanawake, na watoao swadaqah wanaume na wanawake, na wafungao Swawm wanaume na wanawake, wanaojihifadhi tupu zao wanaume na wanawake, na wanaomdhukuru Allaah kwa wingi wanaume na wanawake; Allaah Amewaandalia maghfirah na ujira adhimu. [Al-Ahzaab: 35]



Hivyo, wanawake wamebashiriwa Pepo na neema nyingi sana. Wakati wa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwabashiria wanawake miongoni mwa Swahabiyah ishirini kuwa wataingia Peponi kulingana na Hadiyth kadhaa. Miongoni mwao ni Khadiyjah bint Khuwaylid, 'Aaishah bint Abubakar, Zaynab bint Jahsh, Hafswah bint 'Umar, Faatwimah bint Rasuul, Asmaa bint Abubakar, Umm Sulaym Rumayswaa' bint Milhaan, Asmaa bint Yaziyd, Nusaybah bint Ka'b, Sumayyah bint Khabbaat, Barakah bint Tha'labah na wengineo.



Hilo la kuwa wanaume watakaoingia Peponi wamebashiriwa wanawake ambao ni hurul 'ayn (wanawake wenye macho mazuri na makubwa) ni kweli kwani Aayah za Qur-aan zipo wazi kuhusu hilo. Zipo Aayah kadha kuhusu hili lakini inatosha kunukuu moja. Allaah Aliyetukuka Anatueleza:

فِيهِنَّ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ لَمْ يَطْمِثْهُنَّ إِنسٌ قَبْلَهُمْ وَلَا جَانٌّ ﴿٥٦﴾

Mna humo wanawake wenye staha wanaoinamisha macho, hajawabikiri binadamu kabla yao wala jini. [Ar-Rahmaan: 56]



Sehemu hii ya pili ambayo tumeipigia msitari imekaririwa tena katika surah hii hii aayah ya 74.



Wanawake Peponi watakuwa ni aina mbili. Aina ya kwanza ni wale wanawake wa duniani waliotenda matendo mema, Allaah Aliyetukuka Atawajazi na kuwaingiza Peponi pamoja na waume zao ikiwa walikuwa wema pia. Anasema Allaah Mtukufu:

إِنَّا أَنشَأْنَاهُنَّ إِنشَاءً ﴿٣٥﴾فَجَعَلْنَاهُنَّ أَبْكَارًا ﴿٣٦﴾عُرُبًا أَتْرَابًا ﴿٣٧﴾

Hakika Sisi Tunawaanzisha (huwrun-’iyn) uanzishaji. Tunawafanya mabikra. Wenye mahaba, ashiki na bashasha kwa waume zao, hirimu moja. [Al-Waaqi'ah: 35 – 37]



Pia,

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَاتَّبَعَتْهُمْ ذُرِّيَّتُهُم بِإِيمَانٍ أَلْحَقْنَا بِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَمَا أَلَتْنَاهُم مِّنْ عَمَلِهِم مِّن شَيْءٍ ۚ كُلُّ امْرِئٍ بِمَا كَسَبَ رَهِينٌ ﴿٢١﴾

Na wale walioamini na wakafuatwa na dhuriya wao kwa iymaan, Tutawakutanisha nao dhuriya wao na Hatutawapunguzia katika ‘amali zao kitu chochote. Kila mtu atawekewa rehani kwa yale aliyoyachuma. [Atw-Twuwr: 21]



Hizi Aayah zinaonyesha ikiwa mumeishi hapa duniani kama mume na mke kwa wema Allaah kwa rehema Yake Atawaungisha tena muishi pamoja lakini wakati huu nyote mtakuwa vijana hata kama mlikufa mkiwa wazee.



Wanawake aina ya pili ni wale walioumbwa na Allaah Aliyetukuka kwa ajili ya Pepo tu. Hawa watakuwa ni wenye kupewa wanaume waliowema kama jazaa yao. Kwa vile wanaume kimaumbile kuanzia hapa duniani ni wenye kuoa wake wengi Allaah pia Akhera Atawatunukia hadhi hiyo hiyo. Hekima ya hilo linajulikana na Allaah. Lakini kwa kuzingatia hekima ya mwanamume kuruhusiwa kuoa zaidi ya mke mmoja tutapata busara ya hilo ndilo hilo litakavyokuwa Peponi. Huku si kuwadunisha wanawake bali ni Muumba kuangalia maslahi na maumbile ya kila mmoja. Hapa leo ikiwa utamfanya mke mmoja awe na waume wanne basi utampatia shida na mtihani mkubwa mwanamke huyo, lakini kwa mwanaume ni jambo la kawaida tu.



Ama kuhusu swali lako la pili ni jambo ambalo liko wazi kabisa kwa udhaifu wa wanawake katika kukumbuka mas-ala ya nambari na hesabu.



Hakika ni kuwa kauli ya mwanamke si nusu. Inaonyesha hapa mmechanganya baina ya mambo mawili tofauti.



Suala la kwanza ni je, ushahidi wa mwanamke ni nusu wa ule wa mwanamme? Hakika jambo hili lipo wazi kabisa kwa kila mwenye kutaka ukweli bila ya kuwa na ubaguzi wala nadharia zake mwenyewe za awali. Kwa hukumu hii mwanamke hajadunishwa wala kudharauliwa. Hakika ni kuwa hukumu hii inakwenda sambamba na maumbile yake na saikolojia ya mwanamke inakuwa wazi kulingana na dondoo za wana-saikolojia, wataalamu wa magonjwa ya akili na tafiti za kitabibu.



Aayah hii ya Qur-aan:



يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا تَدَايَنتُم بِدَيْنٍ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى فَاكْتُبُوهُ ۚ وَلْيَكْتُب بَّيْنَكُمْ كَاتِبٌ بِالْعَدْلِ ۚ وَلَا يَأْبَ كَاتِبٌ أَن يَكْتُبَ كَمَا عَلَّمَهُ اللَّـهُ ۚ فَلْيَكْتُبْ وَلْيُمْلِلِ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ وَلْيَتَّقِ اللَّـهَ رَبَّهُ وَلَا يَبْخَسْ مِنْهُ شَيْئًا ۚ فَإِن كَانَ الَّذِي عَلَيْهِ الْحَقُّ سَفِيهًا أَوْ ضَعِيفًا أَوْ لَا يَسْتَطِيعُ أَن يُمِلَّ هُوَ فَلْيُمْلِلْ وَلِيُّهُ بِالْعَدْلِ ۚ وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ ۚ وَلَا يَأْبَ الشُّهَدَاءُ إِذَا مَا دُعُوا ۚ وَلَا تَسْأَمُوا أَن تَكْتُبُوهُ صَغِيرًا أَوْ كَبِيرًا إِلَىٰ أَجَلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ أَقْسَطُ عِندَ اللَّـهِ وَأَقْوَمُ لِلشَّهَادَةِ وَأَدْنَىٰ أَلَّا تَرْتَابُوا ۖ إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً حَاضِرَةً تُدِيرُونَهَا بَيْنَكُمْ فَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَلَّا تَكْتُبُوهَا ۗ وَأَشْهِدُوا إِذَا تَبَايَعْتُمْ ۚ وَلَا يُضَارَّ كَاتِبٌ وَلَا شَهِيدٌ ۚ وَإِن تَفْعَلُوا فَإِنَّهُ فُسُوقٌ بِكُمْ ۗ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ وَيُعَلِّمُكُمُ اللَّـهُ ۗ وَاللَّـهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٢٨٢﴾

Enyi walioamini! Mtakapokopeshana deni mpaka muda maalumu uliopangwa, basi liandikeni. Na aandike baina yenu mwandishi kwa uadilifu. Na wala asikatae mwandishi kuandika kama Allaah Alivyomfunza. Basi aandikishe kwa imla yule ambaye ana haki (mdai) na amuogope Allaah, Rabb wake, na wala asipunguze humo kitu chochote. Basi ikiwa yule ambaye ana haki amepumbaa kiakili au mnyonge, au hawezi kuandikisha mwenyewe, basi aandikishe msimamizi wake kwa uadilifu. Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. Na mashahidi wasikatae watapoitwa. Na wala msichukie kuliandika (deni) dogo au kubwa mpaka muda wake. Hivyo kwenu ndiyo uadilifu upasavyo mbele ya Allaah na ndio unyoofu zaidi kwa ushahidi; na ni karibu zaidi ili msiwe na shaka; isipokuwa itakapokuwa biashara taslimu mnayoiendesha baina yenu, basi si dhambi kwenu msipoiandika. Na shuhudisheni mnapouziana. Na wala asidhuriwe mwandishi wala shahidi; na mkifanya basi hakika huo ni ufasiki kwenu. Na mcheni Allaah, na Allaah Anakufunzeni, na Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.

[Al-Baqarah: 282] inazungumzia hitaji hilo la ushahidi kuhusu kukopeshana.


Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatoa muongozo kwa mambo yanayohusiana na majukumu ya pesa. Katika kipengele hiki, hitaji la kuandika mahusiano ya pesa limenukuliwa kwa mkazo, "Basi liandikeni". Baada ya hapo ayah inazungumzia kuhusu wajibu wa mwandishi au mhusika wa kutayarisha mkataba kwa ibara za kisasa. Ayah pia, inagusia ikiwa mhusika (mkopaji) ni mpumbavu au mnyonge au hawezi kuandikisha, basi walii wake awe ni mwenye kuchukua jukumu hilo kwa niaba yake na achague mashahidi wawili walio waadilifu. Ifahamike kuwa hili linatokea tu ikiwa mhusika hana uwezo wa kuandika mkataba. Kwa hiyo, mashahidi wanakuwa ndio wenye kuchunga kuwa haki lazima ifanyike.



Baada ya hapo ndio Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anaweka sharti la kuita mashahidi wawili wanaume na ikiwa hawapo basi mwanaume na wanawake wawili. Kisha Aayah inaelezea umuhimu wa kuandikiana ikiwa mkataba wenyewe ni mkubwa au mdogo. Qur-aan inazidi kutuelimisha kuwa kuwa si mara zote inawezekana kuandikiana mikataba hivyo, ikiwa haiwezekani basi kuwe na mashahidi wenye kushuhudia hilo.



Lengo hasa la kutoa utangulizi huo ni kuwavutia watu kwa ile hakika kuwa ushahidi wa wanawake hapa hauhusiani na hadhi yao bali ni juu ya mikataba ya kibiashara. Hapa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anatubainishia wazi kuwa wanaotakiwa ni mashahidi wanne bila kubagua kama ni wanawake au wanaume. Pale ambapo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anatulezea kuhusu ushahidi wa wanaume wawili au mwanaume na wanawake wawili ni katika mas-ala ya deni. Anasema Aliyetukuka:



وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ

Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. [Al-Baqarah: 282]



Ifahamike kuwa Allaah, Muumbaji, kwa hekima Yake isiyo kifani Anatoa maagizo ambayo yana manufaa tele kwa wanadamu. Yeye ndiye Muumbaji, hivyo, Anajua jambo ambalo litamsaidia mwanadamu mwenyewe. Katika mas-ala haya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa hekima Yake iliyo ya juu Ameweka hivyo kwa sababu ya kuwa wanawake si wazoefu katika mas-ala ya hesabu, hivyo wakiwa wawili wanaweza kukumbushana ikiwa mmoja wao ataghafilika. Wanawake hawakuwa ni wenye kujishughulisha katika biashara, hivyo kuwa jambo zito kwao na kwa kuwa halipo akili mwao anaweza kusahau mara moja.



Katika enzi hii ya sayansi tunaweza kupata umuhimu wa hukumu na sharia hii. Mengi yamevumbuliwa kuanzia wakati wa Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kila kukicha uvumbuzi mwingi zaidi unakuwa ni wenye kufanyika. Wanawake huwa wana duara la matatizo ya kisaikolojia kila mwezi. Alama za mfadhaiko zinakuwa ni zenye kuonekana mwanzo wa mimba, wakati wa mimba na baada yake, hali ya kukakita damu, shida ya kifiziolojia na saikolojia kwa ajili ya utasa na matatizo ya kisaikolojia baada ya kutisha (kuharibika mimba). Ni katika hali hizi ndio wanawake wanapata uchovu wa kisaikolojia ambao unaleta mfadhaiko, kukosa umakinifu, akili kuwa pole na ukosefu wa hifdhi kwa muda mfupi.



Utafiti unaonyesha kuwa wasichana kabla ya kupata ada yao ya mwezi wanapata mabadiliko ya kisaikolojia. Maelezo ni kama yafuatayo: "Tafiti nyingi zimeripoti kuwa kuna ongezo la athari hasi katika kipindi kabla ada ya mwezi. Katika hayo ni hisia nyingi ikijumlisha kusumbua, mfadhaiko, wasiwasi, huzuni, kujihisi kuwa hako salama, machofu, upweke, kudondokwa na machozi, kukosa utulivu na mabadiliko ya hali. Katika tafiti nyingi, watafiti wameona shida kutofautisha baina ya athari hasi…" (Psychological Medicine, Monograph Suppliment 4, 1983, Cambridge University Press, uk. 6).



Naye C. Shreeves ameandika: "Nguvu za umakinifu na hifadhi zinapungua ni jambo la kawaida katika kipindi kabla ya mwanamke kuingia katika ada yake. tatizo hili linaweza kutatuliwa tu ugonjwa wenyewe utatibiwa" (The Pre-Menstrual Syndrome).



Wakati wanawake wakiwa na mimba wanapata mfadhaiko na matatizo ya kiakili na hofu (Psychiatry in Practice, Oktoba-Novemba 1986, uk. 6). Matatizo kama haya yanaendelea mimba inapokua kubwa. Nako kukatika kwa damu ambako kunaanza katikati ya miaka thelathini hadi hamsini kunakuja na shida zake nyengine. Kuhusu hili Dkt. Jennifer al-Knopf anasema: "…Wanawake hawajui miili yao inawafanya nini.. Baadhi yao wanaripoti ishara ya udhoofu kwa kutokwa jasho usiku, kutopata usingizi, mwasho, mbadiliko wa hali, kupoteza hifdhi kwa muda, kuumwa na kichwa, kupatwa na kukojoa ambao si kawaida na kuongeza mwili. Mabadiliko haya yanapatikana kwa kupungua kwa hormoni za kike kama oestrogen na progesterone, ambazo zinatawala mduara wa uzazi" (Newsweek International, 25 Mei 1992)



Kuharibu mimba kwa mwanamke kunamletea mabadiliko mengine ya kisaikolojia na athari nyingine hasi. Wanawake wanakuwa na wasiwasi kwa asilimia kubwa zaidi kuliko wanaume pamoja na kuwa na hamu.



Kwa yaliyopatikana na wana-saikolojia, wataalamu wa akili na watafiti kama tulivyonukuu hapo juu tunaweza kuelewa kauli ya Aliyetukuka:



وَاسْتَشْهِدُوا شَهِيدَيْنِ مِن رِّجَالِكُمْ ۖ فَإِن لَّمْ يَكُونَا رَجُلَيْنِ فَرَجُلٌ وَامْرَأَتَانِ مِمَّن تَرْضَوْنَ مِنَ الشُّهَدَاءِ أَن تَضِلَّ إِحْدَاهُمَا فَتُذَكِّرَ إِحْدَاهُمَا الْأُخْرَىٰ

Na mshuhudishe mashahidi wawili wanaume miongoni mwenu. Na ikiwa hakuna wanaume wawili, basi mwanamme mmoja na wanawake wawili katika wale mnaowaridhia miongoni mwa mashahidi, ili kama mmoja wao hao wanawake wawili akikosea (akasahau), basi mmoja wao atamkumbusha mwengine. [Al-Baqarah: 282]



Ndio Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akatuusia: " Wafanyieni wema wanawake. Mwanamke ameumbwa na ubavu, na sehemu iliyopinda zaidi ni ya juu. Ukijaribu kuinyoosha itavunjika, na ukiiacha itabaki kama ilivyo. Kwa hiyo, watendeeni wema wanawake". Katika riwaya nyingine: " Ukijaribu kuunyoosha utamvunja na kumvunja ni kumtaliki" [Al-Bukhaariy na Muslim]



Maneno ya Aayah hii yaonyesha kwa uwazi kabisa kuwa msingi wa kanuni hii si kubagua baina ya jinsia lakini ni uwezo wa kuhifadhi wa wanawake. Aayah inatoa hakika ya kibayolojia – kuwa wanawake si wazuri katika kukumbuka vitu kama wanaume. Hii ndio sababu, ikiwa tutakubali ushahidi wa wanawake katika kesi za deni, ni lazima wawe wawili, ili kwa wakati wowote wa mustakbali, ikiwa wanahitajika kutoa ushahidi, mmoja wao ataweza kufidia udhaifu wa hifdhi wa mwenziwe.



Utafiti wa sasa kuhusu suala hili umeyakinisha ukweli huu wa Qur-aan, kuwa hifdhi na kumbukumbu za wanawake ni dhaifu kuliko za wanaume. Wanasayansi wa Urusi wametafiti hili kwa kina, na hitimisho lao lilichapishwa katika kitabu. Ufupisho wake ulitokea katika gazeti moja India ukiwa na anwani, "Uwezo wa Kuhifadhi S". "Wanaume wana uwezo mkubwa zaidi wa kuhifadhi na kufanyia kazi maalumati ya hesabu kuliko wanawake, lakini wanawake ni wazuri zaidi kwa maneno na kauli". Alisema mwanasayansi wa Urusi , "Wanaume wanatawala masomo ya hesabu kwa kuwa na sifa ya kuhifadhi ya kipekee" (Dr. Vladimir Konovalov, Memorising Ability, New Delhi edition of the Times of India, Januari 18, 1985).



Mbali na serikali ya Kenya kutaka kuona kuwa wasichana nao wanafanikiwa katika somo la hesabu pamoja na masomo ya sayansi utakuta kila matokeo yanapotoka yanakuwa ni kama yale ya miaka iliyopita. Ni wasichana wachache wanaofaulu katika mitihani hiyo kuliko wavulana.



Mas-ala ya pili ni kuwa, je ushahidi wa mwanamke ni sawa na wa mwanaume au wake ni duni zaidi? Hili lipo wazi kabisa katika Aayah kadhaa ila hii ya deni. Tunaposoma katika Suwrah An Nuwr pale ambapo Allaah Aliyetukuka Anatufahamisha:

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ الْمُحْصَنَاتِ ثُمَّ لَمْ يَأْتُوا بِأَرْبَعَةِ شُهَدَاءَ

Na wale wanaowasingizia wanawake watwaharifu kisha hawaleti mashahidi wanne.. [An-Nuwr: 4]



Pia tunasoma kuhusu mashahidi wa wasiya:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا شَهَادَةُ بَيْنِكُمْ إِذَا حَضَرَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ حِينَ الْوَصِيَّةِ اثْنَانِ ذَوَا عَدْلٍ مِّنكُمْ أَوْ آخَرَانِ مِنْ غَيْرِكُمْ إِنْ أَنتُمْ ضَرَبْتُمْ فِي الْأَرْضِ فَأَصَابَتْكُم مُّصِيبَةُ الْمَوْتِ ۚ

Enyi walioamini! Mauti yanapomfikia mmoja wenu wakati anapousia, basi chukueni ushahidi wa wawili wenye uadilifu miongoni mwenu; au wawili wengineo wasiokuwa nyinyi pale mnapokuwa safarini ukakufikeni msiba wa mauti. [Al-Maaidah: 106]



Pia:

وَالَّذِينَ يَرْمُونَ أَزْوَاجَهُمْ وَلَمْ يَكُن لَّهُمْ شُهَدَاءُ إِلَّا أَنفُسُهُمْ فَشَهَادَةُ أَحَدِهِمْ أَرْبَعُ شَهَادَاتٍ بِاللَّـهِ ۙ إِنَّهُ لَمِنَ الصَّادِقِينَ ﴿٦﴾

Na wale wanaowasingizia wake zao na hawana mashahidi isipokuwa nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa ni kushuhudia.. [An-Nuwr: 6]



Pia kuhusu talaka, anasema Aliyetukuka:

فَإِذَا بَلَغْنَ أَجَلَهُنَّ فَأَمْسِكُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ أَوْ فَارِقُوهُنَّ بِمَعْرُوفٍ وَأَشْهِدُوا ذَوَيْ عَدْلٍ مِّنكُمْ

Na watakapokaribia kufikia muda wao, basi wazuieni kwa wema, au farikianeni nao kwa wema, na mshuhudishe mashahidi wawili wenye uadilifu miongoni mwenu.. [Atw-Twalaaq: 2]





Na Allaah Anajua zaidi
 
kama unavyosema dini siyo wakati ni kweli, kwa nini leo hawapigi mawe wahalifu mpaka kifo ?
Ili sheria hizo ziweze kutekelezwa inabidi nchi husika iwe inatawaliwa na sheria za kiislamu

Sasa siku hizi kwa nchi nyingi hakuna utawala wa sheria za kiislamu,ndio maana ni vigumu kuteketeleza hizo sheria,mfano hapa Tanzania tu,tuliomba mahakama ya kadhi ili waislamu tuhukumiane maswala ya ndoa na mirathi lakini wewe ni shahidi jinsi kelele zilivyokuwa nyingi

Kule Afughstan chini ya Taliban wanaendesha kwa sheria za kiislamu,wanafanya hivyo,na Iran pia kama sikosei wanafanya hivyo
 
Maswali: Qur-aan


Mafunzo Kutoka Kisa Cha Nabiy Ayyuwb ('Alayhis-salaam)



Alhidaaya.com





SWALI:



Considering kisa of nabiy Zakariyyah (AS) and nabiy Ibrahiym (AS) who with ALLAHS grace has bestowed to them children at an old age and nabiy Ayyuwb (AS) got other children after a long illness. What are the lessons do we get from these kisaa of nabiy AS with this respect.

Thanks,





JIBU:



AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.




Kwanza tunakunasihi kutokufupisha maamkizi ya Kiislaam au Thanaa au kuwaombea Swalaah na Salaam Manabii, au kuwatakia Radhi Swahaba na mengineyo ambayo watu wanakosea kama hivyo. Jambo hilo limekemewa na ‘Ulamaa wetu. Bonyea viungo vifuatavyo upate faida:



Hukmu Ya Kufupisha Thanaa (Kumtukuza Allaah) Na Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Na Maamkizi Ya Kiislam
Al-Lajnah Ad-Daaimah: Haijuzu Kufupisha Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Katika Maandishi
Imaam Ibn Baaz: Kufupisha Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Kwa Mfumo Wowote Haijuzu




Hakika ni kuwa visa vyote vilivyotajwa na Allaah Aliyetukuka katika Qur-aan vina mazingatio kwa Ummah huu ikiwa ni visa vya watu wema na Manabii au watu wabaya. Visa vyote vinavyosimuliawa katika Qur-aan ni vizuri kama Anavyotueleza Aliyetukuka:



نَحْنُ نَقُصُّ عَلَيْكَ أَحْسَنَ الْقَصَصِ بِمَا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ هَـٰذَا الْقُرْآنَ

Sisi Tunakusimulia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) simulizi nzuri kabisa katika Tuliyokufunulia Wahy hii Qur-aan. [Yuwsuf: 3]



Ama kuhusu darsa na mafundisho tunayopata katika visa hivi Allaah Aliyetukuka Anasema:



لَقَدْ كَانَ فِي قَصَصِهِمْ عِبْرَةٌ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ۗ مَا كَانَ حَدِيثًا يُفْتَرَىٰ وَلَـٰكِن تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ كُلِّ شَيْءٍ وَهُدًى وَرَحْمَةً لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ ﴿١١١﴾

Kwa yakini katika visa vyao kuna mafunzo kwa wenye akili. Haikuwa (Qur-aan) hadithi zinazotungwa, lakini ni sadikisho la (vitabu) vya kabla yake na tafsili ya waziwazi ya kila kitu, na ni mwongozo na rahmah kwa watu wanaoamini. [Yuwsuf: 111]



Ama tukiangazia mafunzo tunayopata katika kisa cha baba wa Rusuli, Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-salaam) tunaona ya kwamba alijitolea mhanga kwa kiasi kikubwa mpaka Allaah Aliyetukuka Akamchagua kuwa Imaam kwa watu. Anasema Aliyetukuka:



إِنَّ إِبْرَاهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّـهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ الْمُشْرِكِينَ﴿١٢٠﴾

Hakika Ibraahiym alikuwa Imaam mtiifu kwa Allaah, aliyeelemea haki na wala hakuwa miongoni mwa washirikina. [An-Nahl: 120]



Alipita mitihani mikubwa yote aliyopatiwa kama Alivyoeleza Allaah Aliyetukuka kama ilivyo katika Suwrah Al-Baqarah: 124. Kwa wepesi aliokuja nao katika Dini ndio Allaah Aliyetukuka Akatuamuru tufuate mila hiyo yake [Al-Hajj: 78].



Ama Nabiy Zakariyyah ('Alayhis Salaam) alikuwa ni mnyenyekevu wa hali ya juu wala hakufa moyo akijua hakika kuwa Allaah Aliyetukuka yupo na Atamwitikia du’aa yake aliyoomba. Na tukisoma katika Suwrah Maryam mwanzoni tutapata hayo.



Ama tukija kwa Nabiy Ayyuwb ('Alayhis-salaam) naye pia tunapata mafunzo kemkemu kwani uvumilivu wake ni wa kuigwa na kupigiwa mfano kwa Ummah wote. Daraja yake kwa mpangilio tunapata katika Aayah ifuatayo:



إِنَّا أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ كَمَا أَوْحَيْنَا إِلَىٰ نُوحٍ وَالنَّبِيِّينَ مِن بَعْدِهِ ۚ وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَعِيسَىٰ وَأَيُّوبَ وَيُونُسَ وَهَارُونَ وَسُلَيْمَانَ ۚ وَآتَيْنَا دَاوُودَ زَبُورًا ﴿١٦٣﴾

Hakika Tumekufunulia Wahy (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) kama Tulivyomfunulia Wahy Nuwh na Manabii baada yake. Na Tumemfunulia Wahy Ibraahiym na Ismaa’iyl na Is-haaq na Ya’quwb na dhuriya, na ‘Iysaa na Ayyuwb na Yuwnus na Haaruwn, Na Sulaymaan. Na Tumempa Daawuwd Zabuwr. [An-Nisaa: 163]



Kuhusu madhara aliyopata Nabiy Ayyuwb ('Alayhis-salaam) na kuyavumilia hadi kumuomba Allaah Aliyetukuka Amuondoshee, na Aliyetukuka Akawa ni mwenye kumuondeshea hilo. Anasema Aliyetukuka:



وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ ﴿٨٣﴾فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِن ضُرٍّ ۖ وَآتَيْنَاهُ أَهْلَهُ وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَابِدِينَ ﴿٨٤﴾

Na Ayyuwb alipomwita Rabb wake: Hakika mimi imenigusa dhara, Nawe Ndiye Mbora zaidi wa kurehemu kuliko wengine wote wenye kurehemu. Tukamuitikia basi Tukamuondoshea dhara aliyokuwa nayo, na Tukampa ahli zake na mfano wao pamoja nao; ni rahmah kutoka Kwetu na ni ukumbusho kwa wanaoabudu (Allaah). [Al-Anbiyaa: 83 – 84]



Na Allaah Aliyetukuka Anamtaja Nabiy Ayyuwb ('Alayhis-salaam) kuwa ni mja Wake pindi alipomrudia Yeye baada ya kupata madhara na udhia kutoka kwa shetani. Haya yaliyotokea kwa kurudishiwa watu wake ni mawaidha kutoka kwa Allaah Aliyetukuka kwa wenye akili. Baada ya hapo tunaambiwa kuwa alikuwa mja mwenye kusubiri (38: 41 – 44). Kwa mwenye akili hakika atapata mawaidha makubwa sana katika maneno ya Allaah Aliyetukuka tuliyoyaeleza.

Kwa muhtasari tunapata fundisho katika maisha ya Nabii Ayyuwb ('Alayhis-salaam) la kusubiri, unyenyekevu, kumuomba Allaah Aliyetukuka katika matatizo, kuendelea kufanya Ibaadah katika hali zote na shetani hawezi kumghuri mja mwema, na kadhalika.





Na Allaah Anajua zaidi
 
lkn hedhi haitoki kwa kujisafisha tu maji kwani ipo ndani ya mwili wake isitoshe kama unavyosema dini siyo wakati ni kweli, kwa nini leo hawapigi mawe wahalifu mpaka kifo ?
Baada ya kumaliza hedhi ndio anakoga kujisafisha,au kama ni nifasi ile damu ya uzazi,baada ya kukatika au kuacha kutoka ndio anakoga
 
Baada ya kumaliza hedhi ndio anakoga kujisafisha,au kama ni nifasi ile damu ya uzazi,baada ya kukatika au kuacha kutoka ndio anakoga

i digress, unaweza kunielezea waislamu humaanisha nini wanaposema “mfumo Kristo” na waislamu wa watanzagiza wanajaribu kufanikisha nini kwa kupambana dhidi ya wanouita “mfumo Kristo” ?
 
i digress, unaweza kunielezea waislamu humaanisha nini wanaposema “mfumo Kristo” na waislamu wa watanzagiza wanajaribu kufanikisha nini kwa kupambana dhidi ya wanouita “mfumo Kristo” ?
Mfumo Kristo ni istilahi inayotumika kuelezea mfumo wa kijamii, kisiasa au kiutawala unaoathiriwa au kudaiwa kutawaliwa na fikra au misingi ya Ukristo, hasa katika maeneo yenye historia ya ukoloni au utawala wa kikristo.

Maana kwa muktadha tofauti:
1. Katika siasa au jamii:
Mfumo Kristo unaweza kumaanisha muundo wa utawala, sheria au taasisi zilizojengwa kwa misingi ya imani au maadili ya Kikristo — hata kama si wote ni Wakristo.

2. Katika historia ya Afrika:
Baadhi ya watu hutumia istilahi hii kuzungumzia mfumo wa kimfumo uliotokana na ukoloni ambapo dini, elimu na maadili vililetwa kupitia misheni za Kikristo, na kuchukua nafasi ya mila na utawala wa Kiafrika.

3. Katika mjadala wa kidini:
Inaweza pia kutumika kueleza namna baadhi ya jamii zinavyoegemea kwenye Ukristo hata katika masuala ya kiserikali au kielimu.

Hapo juu nimekuwekea inapozungumzwa mfumo kristo huwa inaamanisha nini

Sasa kwa muktadha wa hapa chini ni kwamba kuna mambo ambayo toka awali yaliwaweka nyuma waislamu katika nchi hii

Mfano mfumo wa elimu kipindi kile kabla hazijatumika namba wanafunzi wengi wa kiislamu waliathirika sana,kwa maana walikatwa ufaulu wao ili mradi wasiwe wengi kwenye elimu ya juu

Kadhia hii ilikuja kumalizwa na Waziri kigoma malima alipokuwa wizara ya elimu,ndio akatambulisha matumizi ya namba za mitihani

Tangia uhuru hakujawi kuwa na mkurugenzi muislamu baraza la mitihani Tanzania,sijui siku hizi sijafuatilia, je unadhani ilifanyika kwa bahati mbaya?

Ukija serikalini nafasi nyingi za uteuzi ni wasio waislamu,nadhan ni mwaka jana kuna wizara tulionywesha takwimu zake inaogopesha wakristo ni wengi mno kuliko waislamu,haya hayakufanywa kwa bahati mbaya

Kwahiyo kama unasikia waislamu wanataka mfumo ubadilishwe basi wana hoja ya msingi
 
Mfumo Kristo ni istilahi inayotumika kuelezea mfumo wa kijamii, kisiasa au kiutawala unaoathiriwa au kudaiwa kutawaliwa na fikra au misingi ya Ukristo, hasa katika maeneo yenye historia ya ukoloni au utawala wa kikristo.

Maana kwa muktadha tofauti:
1. Katika siasa au jamii:
Mfumo Kristo unaweza kumaanisha muundo wa utawala, sheria au taasisi zilizojengwa kwa misingi ya imani au maadili ya Kikristo — hata kama si wote ni Wakristo.

2. Katika historia ya Afrika:
Baadhi ya watu hutumia istilahi hii kuzungumzia mfumo wa kimfumo uliotokana na ukoloni ambapo dini, elimu na maadili vililetwa kupitia misheni za Kikristo, na kuchukua nafasi ya mila na utawala wa Kiafrika.

3. Katika mjadala wa kidini:
Inaweza pia kutumika kueleza namna baadhi ya jamii zinavyoegemea kwenye Ukristo hata katika masuala ya kiserikali au kielimu.

Hapo juu nimekuwekea inapozungumzwa mfumo kristo huwa inaamanisha nini

Sasa kwa muktadha wa hapa chini ni kwamba kuna mambo ambayo toka awali yaliwaweka nyuma waislamu katika nchi hii

Mfano mfumo wa elimu kipindi kile kabla hazijatumika namba wanafunzi wengi wa kiislamu waliathirika sana,kwa maana walikatwa ufaulu wao ili mradi wasiwe wengi kwenye elimu ya juu

Kadhia hii ilikuja kumalizwa na Waziri kigoma malima alipokuwa wizara ya elimu,ndio akatambulisha matumizi ya namba za mitihani

Tangia uhuru hakujawi kuwa na mkurugenzi muislamu baraza la mitihani Tanzania,sijui siku hizi sijafuatilia, je unadhani ilifanyika kwa bahati mbaya?

Ukija serikalini nafasi nyingi za uteuzi ni wasio waislamu,nadhan ni mwaka jana kuna wizara tulionywesha takwimu zake inaogopesha wakristo ni wengi mno kuliko waislamu,haya hayakufanywa kwa bahati mbaya

Kwahiyo kama unasikia waislamu wanataka mfumo ubadilishwe basi wana hoja ya msingi

lkn uchumi karibia wote wa tanzagiza umeshikiliwa na waislamu, hakuna kampuni hata moja kubwa ya maana inayomilikiwa na Christian, R.Mengi alikuwa ni wa mwisho na alipigwa vita sana na muslims akina manji, dewji &co. sasa labda nikuulize kati ya Muislamu wa tanzagiza na Mkristo yupi anayehitaji ukombozi?

utalalamikiaje khs “mfumo Kristo” kuwa hautendi haki kwa waislamu wakati nchi yote inamilikiwa na waislamu? je, unaweza nielezea hapo ? ubinafsishaji unaofanywa na serikali karibia wote unakwenda kwa muslims, kuanzia tourism, madini mpaka hata juzi wamegawa mwendokasi kwa waislamu, na sgr yetu pia iko karibia inaingia sokoni wamiliki waislamu, sijaongelea bongo flava, bongo movie yote muslim
owned, football clubs wamiliki wa yanga na simba wote waislamu iweje useme muslims ni victims?

hauoni kwamba anayehitaji ukombozi na upendeleo wa makusudi ili aweze kushiriki kwenye keki ya nchi hapa ni Christian?
 
lkn uchumi karibia wote wa tanzagiza umeshikiliwa na waislamu, hakuna kampuni hata moja kubwa ya maana inayomilikiwa na Christian, R.Mengi alikuwa ni wa mwisho na alipigwa vita sana na muslims akina manji, dewji &co. sasa labda nikuulize kati ya Muislamu wa tanzagiza na Mkristo yupi anayehitaji ukombozi?

utalalamikiaje khs “mfumo Kristo” kuwa hautendi haki kwa waislamu wakati nchi yote inamilikiwa na waislamu? je, unaweza nielezea hapo ? ubinafsishaji unaofanywa na serikali karibia wote unakwenda kwa muslims, kuanzia tourism, madini mpaka hata juzi wamegawa mwendokasi kwa waislamu, na sgr yetu pia iko karibia inaingia sokoni wamiliki waislamu, sijaongelea bongo flava, bongo movie yote muslim
owned, football clubs wamiliki wa yanga na simba wote waislamu iweje useme muslims ni victims?

hauoni kwamba anayehitaji ukombozi na upendeleo wa makusudi ili aweze kushiriki kwenye keki ya nchi hapa ni Christian?
Serikali ndio mwajiri mkuu,sector binafsi ndio ipo lakini nafasi za ajira ni finyu ukilinganisha na serikali

Lakini bado hao hao waislamu wenye kumiliki hizo biashara sio kwamba wanaajiri waislamu peke yake,bali na wakristo wapo pia

Lakini hatuwezi kupima ukandamizaji kupitia sekta binafsi,hao wana uhuru wao kuamua nini cha kufanya

Lakini hapa tunazungumzia serikali ambayo wananchi wote tunapaswa kupata keki ya taifa sawa bila kubaguana

Serikali ndio baba na mama mlezi wa wananchi hivyo awajibu wa moja kwa moja kuhakikisha watu wote wanapata haki stahiki hata kama sio kwa asilimia mia moja

Istoshe wote kwa namna moja au nyingine tunalipa kodi ambayo ndio inaendesha serikali,na sisi ndio waajiri kwa hiyo serikali,hapa utaona kwamba daraja la serikali na sekta binafsi ni umbali wa mbingu na ardhi

Hoja yako kwamba miradi mingi sijui wanapewa waislamu,hao ni wawekezaji ambao wanachangia pato la uchumi wa nchi hii,kwahiyo sijui uwepo wao unaingiliana vipi katika hoja ambayo ipo mbele yetu hapa
 
Serikali ndio mwajiri mkuu,sector binafsi ndio ipo lakini nafasi za ajira ni finyu ukilinganisha na serikali

Lakini bado hao hao waislamu wenye kumiliki hizo biashara sio kwamba wanaajiri waislamu peke yake,bali na wakristo wapo pia

Lakini hatuwezi kupima ukandamizaji kupitia sekta binafsi,hao wana uhuru wao kuamua nini cha kufanya

Lakini hapa tunazungumzia serikali ambayo wananchi wote tunapaswa kupata keki ya taifa sawa bila kubaguana

Serikali ndio baba na mama mlezi wa wananchi hivyo awajibu wa moja kwa moja kuhakikisha watu wote wanapata haki stahiki hata kama sio kwa asilimia mia moja

Istoshe wote kwa namna moja au nyingine tunalipa kodi ambayo ndio inaendesha serikali,na sisi ndio waajiri kwa hiyo serikali,hapa utaona kwamba daraja la serikali na sekta binafsi ni umbali wa mbingu na ardhi

Hoja yako kwamba miradi mingi sijui wanapewa waislamu,hao ni wawekezaji ambao wanachangia pato la uchumi wa nchi hii,kwahiyo sijui uwepo wao unaingiliana vipi katika hoja ambayo ipo mbele yetu hapa

kama serikali inawabagua waislamu, iweje wamiliki (waislamu) uchumi wa nchi huku Christians own nothing, na hata kidogo walicho nacho kinapigwa vita na kunyang’anywa?
 
kama serikali inawabagua waislamu, iweje wamiliki (waislamu) uchumi wa nchi huku Christians own nothing, na hata kidogo walicho nacho kinapigwa vita na kunyang’anywa?
Swala la biashara sio la waislamu wala wakristo, ingawa Mtume wetu Swalla aallahu alaih wa sallamu ametuhusia waislamu tufanye biashara kwani ina baraka

Sasa kwanini wakristo sio wafanyabiashara hilo ni swala lao binafsi

Unamaanisha nini unaposema kwamba wakristo hata hicho kidogo walicho nacho kinapigwa vita?

Na kipi walicho nacho kama serikali ni ya wote?
 
Swala la biashara sio la waislamu wala wakristo, ingawa Mtume wetu Swalla aallahu alaih wa sallamu ametuhusia waislamu tufanye biashara kwani ina baraka

Sasa kwanini wakristo sio wafanyabiashara hilo ni swala lao binafsi

Unamaanisha nini unaposema kwamba wakristo hata hicho kidogo walicho nacho kinapigwa vita?

Na kipi walicho nacho kama serikali ni ya wote?

swali zuri, ndiyo ujue kwamba hakuna kitu kama “mfumo Kristo” tanzagiza na kilichopo ni gaslighting tu, waislamu ndiyo wanaufaika wakuu katika hii nchi from get go, ila wanawa gaslight Christians kwamba ni victims, na lengo ni kuwafanya Christians waamini kwamba wao(Christians) ni privilleged na waislamu ni victims, wakati takwimu zote zinaonyesha tofauti.

lengo kuu ni total islamization ya tanzagiza na hii inaendelea polepole kuanzia uhuru, kuna sababu labda kwa nini ubinafsishwaji wanufaika wakuu au unafikiri imetokea tu kwamba ni waislamu kuanzia bandari, misitu carbon credits, vitalu, national
Parks wamasai wanaondolewa kupisha muslim investments, airports ya kia imeenda kwa muslims, huko mikoani misikiti inajengwa karibia kila kata hata ambazo ni Christian and so on.

sasa haya yanawezekana tu kwa kuwadanganya au kuwafanya Christians waamini kwamba wao ni privilleged na muslims wanalia kwamba ni victims wanaonewa lkn ni mbinu ya islamization of tanzagiza, ni insidious vinginevyo unawezaje kusema unaonewa kama una own everything na unayemshutumu kukuonea owns nothing ?

kwa kawaida anayeonewa siku zote ni masikini …
 
swali zuri, ndiyo ujue kwamba hakuna kitu kama “mfumo Kristo” tanzagiza na kilichopo ni gaslighting tu, waislamu ndiyo wanaufaika wakuu katika hii nchi from get go, ila wanawa gaslight Christians kwamba ni victims, na lengo ni kuwafanya Christians waamini kwamba wao(Christians) ni privilleged na waislamu ni victims, wakati takwimu zote zinaonyesha tofauti.

lengo kuu ni total islamization ya tanzagiza na hii inaendelea polepole kuanzia uhuru, kuna sababu labda kwa nini ubinafsishwaji wanufaika wakuu au unafikiri imetokea tu kwamba ni waislamu kuanzia bandari, misitu carbon credits, vitalu, national
Parks wamasai wanaondolewa kupisha muslim investments, airports ya kia imeenda kwa muslims, huko mikoani misikiti inajengwa karibia kila kata hata ambazo ni Christian and so on.

sasa haya yanawezekana tu kwa kuwadanganya au kuwafanya Christians waamini kwamba wao ni privilleged na muslims wanalia kwamba ni victims wanaonewa lkn ni mbinu ya islamization of tanzagiza, ni insidious vinginevyo unawezaje kusema unaonewa kama una own everything na unayemshutumu kukuonea owns nothing ?

kwa kawaida anayeonewa siku zote ni masikini …
Naona hapa unajaribu kuukwepa ukweli au hoja husika

Je,wakristo mmekatazwa kujenga makanisa kila sehemu?

Je wakristo mmekatazwa kufanya biashara au kuwekeza nanyi mkashiriki katika uwekezaji?

Je waislamu wameanza leo kuwekeza baada ya mama samia kuwa Raisi?

Waislamu wanalalamikia mambo ya msingi ya nchi hii,ila wewe unazungumzia mambo binafsi,kwasababu kujenga misikiti kila sehemu na biashara za waislamu ni mambo binafsi ambayo hata wakristo wanaweza kuyafanya

Hapa expert wangu tunazungumzia ni kwa kiasi gani serikali inajenga mfumo wa kuikandamiza dini nyingine

Mfano kuna memorundum of understanding,ambapo serikali imeingia mikataba na makanisa kujenga mashule na mahospitali,mfadhili mkuu ni serkali,je hii ni sawa?

Kwanini waislamu nao wasipate nafuu kama hiyo?

Huo ni mfano mmoja,mimi nazungumzia ni kiasi gani serikali imejitengenezea mfumo ambao unapendelea imani fulani,lakini wewe expert wangu unakuja na hoja ambazo za kibinafsi zaidi
 
Naona hapa unajaribu kuukwepa ukweli au hoja husika

Je,wakristo mmekatazwa kujenga makanisa kila sehemu?

Je wakristo mmekatazwa kufanya biashara au kuwekeza nanyi mkashiriki katika uwekezaji?

Je waislamu wameanza leo kuwekeza baada ya mama samia kuwa Raisi?

Waislamu wanalalamikia mambo ya msingi ya nchi hii,ila wewe unazungumzia mambo binafsi,kwasababu kujenga misikiti kila sehemu na biashara za waislamu ni mambo binafsi ambayo hata wakristo wanaweza kuyafanya

Hapa expert wangu tunazungumzia ni kwa kiasi gani serikali inajenga mfumo wa kuikandamiza dini nyingine

Mfano kuna memorundum of understanding,ambapo serikali imeingia mikataba na makanisa kujenga mashule na mahospitali,mfadhili mkuu ni serkali,je hii ni sawa?

Kwanini waislamu nao wasipate nafuu kama hiyo?

Huo ni mfano mmoja,mimi nazungumzia ni kiasi gani serikali imejitengenezea mfumo ambao unapendelea imani fulani,lakini wewe expert wangu unakuja na hoja ambazo za kibinafsi zaidi

ndiyo Christians walikatazwa kuown anything hapa tanzagiza na ndiyo sababu kuu ya hiyo economic disparities kati ya Christians na muslims, ndiyo maana Nyerere alijaribu sana kutaka kusawazisha leo hii kuna hata Christians wanaishi maeneo kama upanga, msasani, magomeni ambapo historically yalikuwa ni for muslims (only) wakati wa Nyerere alisaidia angalau kuwe na wafanyabiashara Christians ndiyo akina R.Mengi wakaibuka/ibuliwa, wahandisi walisaidiwa kulikuwa na Kampuni za Christians kwenye contructions ambapo walifanya kazi nzuri tu leo hii wote wamepigwa vita na muslims na kila kitu kapewa estim construction kazi na tenda zote za ujenzi za serikali estim amepewa na tumerudi kule kule.

swala la hospitali za misheni halihitaji hata mjadala kwani waislamu ni wanufaika wakubwa tu wa hizi hospitali pia mfano tumesoma juzi hapa Hashimu Rungwe kalazwa KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Center) kwani nini unafikiri hakwenda mawenzi hospital ambayo ni ya serikali ? na huo ni mfano mdogo tu huko vijijini kuna mahali hata serikali ni kama haipo na huduma pekee ni ya Kanisa.

kuhusu kujenga Kanisa ndiyo Christians wanakatazwa kujenga Kanisa popote hapa tanzagiza mfano pemba juzi kati wameandamana kupinga kujengwa Kanisa kwao wakati hakuna Christian aliyepinga tena kwa maandamano kujengwa kwa msikiti kwenye kata yao hata kama wakazi karibia wote ni Christians.

hivyo kama kuna yoyote anayehitaji ukombozi na kuwezeshwa kwa makusudi kabisa hapa tanzagiza ni Christians, na hakuna kitu kama “mfumo Kristo” hiyo ni reverse psychology inayotumiwa na muslims kujifanya victims ili waendelee kunufaika lkn labda “mfumo islam” upo na ni insidious …
 
Back
Top Bottom