Ramadhan Special Thread
Maswali: Hukmu Za Swalah
Anaweza Kuswali Katika Nyumba Ya Asiye Muislamu?





SWALI:



Assalaam aleikum.



Kwanza nimefurahi sana kuipata website hii mola awabariki.

swali langu ni hili.mimi nafanya kazi za nyumbani katika nyumba za wazee wasiokua waisilamu,wakati wakuswali huswali katika nyumba hio.je yafaa kuswali au haifai hata kama hapana najisi kwa vile mwenye nyumba hio simuislamu na ameridhika ni swali bila tabu?



JIBU:



AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.





Unaweza kuswali katika nyumba hiyo ikiwa una dharura na madamu tu ni mahali pasafi hakuna najsi na hakuna picha au misalaba mbele yako.





Kwa maelezo zaidi bonyeza kiungo kifuatacho:



Swalah Katika Kanisa Inafaa?





Na Allaah Anajua zaidi
 
Naam ndugu zangu katika imani,kama unafuatilia vizur post humu ndani utaona kwamba hakika hakuna sababu ya mtu kuacha kuswali

Yani leta ujanja wote unaojua wewe lkn bila ya swala hatutoboi ng'o

Tushikamane na Swalaa

Baadae tutasoma mambo mengine inshaallah
 
WATU SIKU YA KIAMA TUTAKUWA MAKUNDI MATATU KAMA ALLAH ANAVYOSEMA KATIKA SURATIL AL WAAQIAH

Screenshot_20250426_194506_Quran Swahili.jpg

Screenshot_20250426_194600_Quran Swahili.jpg

Screenshot_20250426_194918_Quran Swahili.jpg
 
Afanyeje Ili Aweze Kumrudia Mke Aliyemuacha Kwa Kukataa Kwake Kusilimu Sasa Anataka Kusilimu??
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:

Assalam Alleykum. Natoa pongezi kwenu kwa kutupa elimu ya dini ya kiislam katika masuala mbalimbali.

Mimi ni muislamu ambaye nilifunga ndoa ya kiserikali na kuishi na mwanamke ambaye si muislam kwa muda wa miaka 6. Tulifanikiwa kupata watoto wawili. Nilimuacha mke wangu baada ya kujaribu kumshawishi abadili dini na yeye kuwa mzito katika hilo. Niliamua kuoa mwanamke mwingine ambaye ni muislam. Katika kipindi cha takribani miezi 4 iliyopita mwanamke niliyemuacha amekuwa akiniomba msamaha na kusema yupo tayari kusilimu na kuwa mke mwenza. Nipo katika mkakati wa kumrudia. Je ni mambo gani ambayo kwa taratibu za kislam ninapaswa kuyafuata na ambayo sistahili kuyafuata kuweza kumrudia na kuishi katika ndoa ya kiislam? Wabilah Tawfiq



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.





Shukrani kwa swali lako kuhusu kumuoa mwanamke uliyeishi naye kwa miaka sita akiwa si Muislamu.

Awali ya yote inatakiwa kwako kurudi kwa Allaah Aliyetukuka na kuomba msamaha kwa kuishi na mwanamke asiyekuwa Muislamu bila ya ndoa. Uazimie kabisa kuwa hutorudia tena kufanya kosa hilo maishani mwako kabla ya kumrudia huyo mwanamke uliyekuwa naye.

Kisha baada ya wewe kuomba msamaha huo kwa Allaah Aliyetukuka, jaribu kumshawishi mwanamke huyo kuingia katika Uislamu mwanzo. Usiichukue kauli yake kuwa yeye anataka kusilimu tu, jambo hilo linatakiwa litiwe katika matendo ambayo ndio muhimu zaidi kwa maslahi yake. Baada ya kusilimu, muingize katika madrasah au markaz inayofundisha Dini inavyotakiwa na Uislamu. Kufanya hivyo utaweza kujilinda wewe na kumlinda na kizazi chenu kutokana na mitihani yanayowakumba wengi miongoni mwa wenye kuoa waliosilimu bila ya kuwapatia msingi wa Dini yenyewe.

Kisha pia, hakikisha kuwa mwanamke huyo hana mimba na utaweza kujua kuwa hana mimba kwa kuwa utakuwa umechukua miezi kama 6 hadi mwaka katika kipindi cha yeye kusoma. Ukiona kuwa ameshika Dini endelea na mipango ya kumuoa na Allaah Aliyetukuka Atawatilia tawfiki na baraka.

Kwa kuwa lengo la kumuoa ni Da’wah jaribu kushirikisha wazazi wake ambao si Waislamu katika ndoa japokuwa idhini haitotoka kwao ikiwa si Waislamu. Kuwashirikisha huko kutaweza kukupatia wewe fursa ya kuweza kuwaonyesha uzuri wa Uislamu na kuwavutia katika Uislamu. Na ujira wako kwa kufanya hivyo utaupata kwa Allaah Aliyetukuka.

Yatakapotekelezeka yote hayo na akasilimu kikwelikweli mwanamke huyo baada ya kuujua Uislamu na ukaweza kumuoa, fanya uadilifu baina ya wake zako na dhihirisha Uislamu kwa mke wako aliyesilimu ili aweze kuipenda Dini hii ya Uislamu.

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na manufaa zaidi:



Amemuoa Mkristo Bila Kufuata Sheria Za Kiislamu Hataki Kuingia Katika Uislamu Nini Hukmu Yake Na Watoto Watakaozaa?





Kumsilimisha Kafiri Na Hukmu Ya Kuoana





Na Allaah Anajua zaidi
 
Amemrudia Mke Aliyeritadi Na Ambaye Alikuwa Akimhubiria Aingie Ukiristo
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:



Assalaam aleykum.



Jamaa yangu alimsilimisha mwanamke akamuoa. Bahati mbaya wakaachana na yule mwanamke akasema kwa kutamka kuwa amerudi dini yake ya Ukristo baada ya kuachwa manake yeye alisilimu kwa kutaka kukaa na huyu bwana tu. Akawa anamletea huyu bwana makala za kumhubiria ili nae aingie ukristo. Baadae yule mwanamke akasema hajarudi dini yake ile ilikuwa ni kumfanya huyu bwana amrudie tu. Na huyu bwana amemuoa tena. Jee nini hukumu yake?



JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kumrudia mke aliyeritadi baada ya kumuacha.



Suala hili la kuoa mke au kuolewa na mume aliyesilimu na baada ya hapo ikafanywa Nikaah huwa yapo matatizo mengine. Tumetahadharisha sana suala hilo kwani baada ya ndoa huwa kunapatikana matatizo mengi sana kwa kuwa ndoa yenyewe haina ikhlaasw inayotakiwa katika Ibadah ya aina yoyote ile.



Ni nasaha kwa sote tufuate maagizo ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kuchagua mchumba. Miongoni mwa maagizo ni kutafuta mke aliyeshika Dini na mwenye maadili mema. Mwanamke amesilimu leo na kesho kuolewa Dini yake imejulikana wakati gani? Shida zinazopatikana zinakuwa nyingi zisizokuwa na hesabu ya aina yoyote ile. Inatakiwa tuwe waangalifu sana katika uchaguzi wa mchumba ili tusiwe tunafanya kazi ya bure. Ni nasaha yetu ya dhati kuwa kabla ya kumuoa msichana kama huyo afunzwe Dini kwa muda usiopungua mwaka ili kuweza kupima Dini yake na ukakamavu wake katika kufuata Dini hii ya Kiislamu. Baada ya hapo unaweza kuchukua uamuzi muafaka baada ya kuswali Swalah ya Istikhaarah.



Wengi wanachukua ruhusa iliyotolewa kuwaoa wanawake wa Kiyahudi na Kikristo, lakini hata hivyo Allaah Aliyetukuka Ameweka sharti muhimu sana kabla ya sisi kuchukua hatua hiyo nyeti. Sharti lililowekwa ni wanawake hao wawe wema na bila kufanya nao uzinzi kabla ya kuingia nao katika ndoa ya halali. Mbali na hilo ni muhimu tuzibe paa zetu kwani wanawake wetu wataolewa na nani ikiwa kila mmoja kwa maslahi yake anaoa Mkristo.



Ikiwa mwanamke huyo baada ya kupatiwa talaka aliritadi hakutakuwa na ndoa baina yao mpaka arudi katika Uislamu kwa ajili ya kutaka Dini na sio kuolewa. Hivyo kama wamerudiana basi waachane haraka hadi mwanamke asilimu kikweli kisha huyo mwanamke kama anautaka Uislam kikweli, basi aanze kwanza kupewa mafunzo ya Uislam maana yaonyesha kuwa huyo mke hakupatiwa mafunzo ya Dini hapo kabla. Inatakiwa kwa wakati huu apatiwe vitabu kuhusu Uislamu awe ni mwenye kusoma apate ufahamu mzuri na kusomeshwa kabla ya kurudiwa. Ikiwa kweli atarudi katika Dini kwa kuomba msamaha na kujirekebisha pamoja na kusoma Uislamu kutakuwa hakuna tatizo lolote la wanandoa hao kurudiana.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Amemuoa Mkristo Bila Kufuata Sheria Za Kiislamu Hataki Kuingia Katika Uislamu Nini Hukmu Yake Na Watoto Watakaozaa?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:



kama mtu atakuwa kaowa mwanamke wa kinasara nakuowa yenyewe sio kwa kiislam ni kwa kupitia marage regester office, kwa mfano kama hapa England. Swali langu ni hili je mke kama huyu inafaa mtu kusema au kuhisabiwa kaowa? Na kama utazaa nae hukumu yake itakuwaje kidini? Na vile vile kama kakataa kuufata uislam anataka kubakia na unasara wake mwanamke kama huyu je inafaa kuendelea kukaanae? Nitashukuru nikipata majibu kutoka kwenu ndugu zangu. Asalam alaikum warahmatullah wabarakatu.






JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu swali lako la kuoa mwanamke wa kinasara. Uislamu umemruhusu mwanamme kumuoa mwanamke wa kinasara. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Aliyetukuka:



"Na mmehalalishiwa kuwaoa wanawake wema wa Kiislamu na wanawake wema katika wale waliopewa Kitabu kabla yenu. Ni halali kwenu kuwaoa mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila kufanya uzinzi wala kuwaweka kinyumba" (5: 5).



Katika Aayah iliyo juu tunapata mafunzo mazuri na mema katika kuoa wanawake waliopewa Kitabu. Miongoni mwayo ni:

Wanawake hao ni lazima wawe ni wema, waliojihifadhi ambao hawana tabia ya uzinifu wala kuzungunga zunguka.
Mfunge nao ndoa kwa njia ya Kiislamu.
Msifanye nao uzinzi kabla ya kuwaoa.
Msiwaweke kinyumba kabla ya ndoa.
Ikiwa mwanamke atakuwa na sifa hiyo ya kujihifadhi na kuwa mwema basi itaruhusiwa kwako kisheria kumuoa. Ikiwa hatakuwa na sifa hiyo basi hujapatiwa idhini ya kumuoa bali inafaa utafute Muislamu.



Nukta ya pili ndio ni jibu la swali lako, haifai kwa Muislamu kufunga ndoa na Mnasara Kanisani au kwa Marriage Register Office kwani ndoa hiyo haitambulikani kisheria. Bali inafaa ufunge kwa njia ya Kiislamu ambayo inakuamuru wewe umfanyie wema wa hali ya juu wala usimlazimishe kuingia katika Uislamu na umpatie mahari yake.



Ikiwa haikufungwa kwa njia ya Kiislamu aliyeoa kwa Ofisi ya Registrar, hatakuwa ni mkewe kisheria, hivyo watoto atakaozaa naye hawatambulikana kisheria kuwa ni wake. Hapa tungependa kuwatanabahisha ndugu zetu wasiwe ni wenye kuoa wanawake wa Kinasara au Kiyahudi kwani tukifanya hivyo, mwanzo wasichana wetu wataolewa na nani? Je, tunataka waolewe na John na Joseph au ni vipi? Kisha yapo matatizo mengi ambayo tunakumbana nayo pindi kunapotokea talaka kwa sababu tuko katika nchi ambazo sheria zake si za Kiislamu watoto ima anapewa mama au wanachukuliwa na serikali hivyo kuongeza idadi ya wasiokuwa Waislamu kwa nguvu na juhudi zetu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Ameoa Mwanamke Asiye Muislamu Baada Ya Kuzaa Naye Nje Ya Ndoa, Naye Bado Hakubadili Dini Wala Hana Niyah, Nini Hukmu Yake?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:



Assalam aleykum warahmatullah taaala wabarakatu!



Napenda kuuliza swali hili kwa niaba ya kaka yangu wa kiislamu ambaye yuko katika ndoa ambayo kwamba hana uhakika inaswihi au haiswihi kwa mwanamme wa kiisalam. Kwanza kaka huyu aliishi na mwanamke wa kikatoliki bila kumuoa kwa zaidi ya mwaka, wakajaaliwa kupata mtoto na hapo ndipo alipochukua hatua yakumuoa mwanake huyo,je ndoa hii katika uislamu inakubalika? Na kama haikubaliki au inakubalika naomba unipe ufafanuzi nipate kuelimika na nukumuelimisha kaka yangu juu ya swala hili.



Pia mwanake huyu ambaye kaka yangu anaamini ni mke sasa wamekuwa pamoja kwa zaidi ya mwaka lakini bado hajawa mislamu na wala katika kipidi kitakatifu kama hiki hafungi wala kuswali. Je mwanamme wa kiislamu anaruhusiwa kuoa mwanamke wakikirsto nakuendelea kuishi nae muda wote hata kama hatobadili dini nakuwa muislamu?





Allah (Subhanahu wataala) akupe wepesi katika kujibu swali hili





JIBU:



Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumuoa mwanamke wa Kikristo katika sheria.

Awali ya yote tunataka kukunasihi kuwa mwanzo umpe nasaha kaka yako kwa yaliyopita katika maisha yake. Uzinifu katika Uislamu ni dhambi kubwa ambalo kusamehewa linahitaji aliyefanya atubie kwa Mola wake Mlezi toba ya sawa na kikweli. Kisha inafaa aelewe kuwa yule mtoto wake wa kwanza si wake kisheria, na mmoja akifa hawarithiani kabisa. Pia umetueleza kuwa kaka yako baadaye alimuoa huyo mwanamke bila kutueleza kama alimuoa Kiislamu, Kikatoliki au kimila? Ni ndoa ya Kiislamu tu ndio inayokubalika kisheria.



Uislamu umetupatia muongozo kuhusu kuwaoa watu wa Kitabu (Mayahudi na Wakristo). Ruhusa hiyo imetolewa lakini kwa kuwekewa sharti ambalo linahitajika lipatikane kusihi hiyo ndoa. Allaah Aliyetukuka Anatuambia: “Na ni halali kuwaoa wanawake wema walio waumini na wema miongoni mwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu nyinyi ikiwa mtawapatia ujira wao (mahari) mkafunga nao ndoa, bila kufanya uzinzi wala kuwaweka wanawake wa kinyumba” (5: 5). Kwa kuwa kaka yako alikaa naye kinyumba hiyo inaondoa sifa ya mwanamke mwema miongoni wa waliopewa Kitabu.



Hata ikiwa mwanamke wa Kikristo ni mwema anayejitunza muruwa maadili na tabia yake itakuwa si katika maslahi kwa Waislamu kuwaoa kwani ikiwa kila Muislamu atakimbilia Mkristo, wasichana wetu wataolewa na nani? Itabidi wasichana wetu nao wachukuliwe na Wakristo hivyo kuleta maafa makubwa sana kwa jamii. Ndio baadhi ya madhehebu wana msingi wa sheria unatambuka kama maslahi.



Imepatikana pia katika maeneo mengi katika nchi kadhaa kwa watoto wanaozaliwa kuingizwa katika Dini za mama zao. Au ikiwa kunatokea ugomvi unaopelekea wanandoa hao kuachana, nchi nyingi inampatia haki ya ulezi mama. Na ikiwa mama ni Mkristo basi inatarajiwa kuwa na mtoto naye atakuwa wa Dini hiyo.



Hivyo, inatakiwa tutahadhari sana juu ya suala hilo tusije tukaingia katika balaa ambayo haitakuwa na mwisho mzuri kwa jamii.



La kufanya ni kumnasihi kaka yako na umjulishe kuwa misingi sahihi ya kuishi na huyo mwanamke ilikiukwa tokea mwanzoni na anatakiwa afanye Tawbah ya kweli kweli na afuate taratibu sahihi ikiwa atataka kuishi na huyo mwanamke. Na kisha akitaka amfanyie Da‘wah huyo mwanamke ili apate kusilimu na kisha afundishwe Dini ili ajikite katika hilo kwa ufanisi wake huyo mtoto hapa duniani na kesho Akhera.



Kwa hivi sasa ni bora umnasihi ajitenge naye ikiwa kweli anamuogopa Allaah, na atekeleze kwanza hayo tuliyoyaeleza hapo juu.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Amesilimu Kwa Sababu Ya Kutaka Kuoa lakini anakiri kuwa yeye ni Mkristo, Je, Ndoa Inaswihi?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina



SWALI:

Bismilahi rahmani rahim,, namshukuru alwa kwa neema zake na nguvu zake za kusimamisha mbingu na ardhi..na kuindeleza website ili iidi kuulingania uislam uzidi kusonga mbele..............

Swali, kuna mtu mmoja..Alitokea kumpenda sana binti mmoja alikuwa ndani ya dini ya kiislam...lakini yeye yupo ndani ya ukristu.. sasa akapeleka ujumbe wa kutaka kumuoa ktk familia ya yule binti..yule bwana akajibiwa ya kwamba haitowezekana ,,kwa sababu ya dini yako...

alicho kifanya yeye ni kwenda kwa shekh kusilim,,lakini sio kwa kupenda ila ni kama wale wazazi wajue ni kweli amesilim ili wampe mke...na kweli baada ya hapo akapewa mke.. kilicho fuatia mpaka sasa yeye nusu mkristu nusu mu islam.......kanisani haendi wala masjid..lakini yeye mpaka sasa anakiri kabisa kama yeye ni mkristu.....na kwa mkewe anamwabia yeye ni muislam...lakini ndugu zake wa najua yeye ni mkristu...sasa mtihani unakuja hapa mtu kama huyu akifa azikwa vipi au ktk dini ipi................. wakwe wanajua ni muislam ..... sasa huu si utata.................................






JIBU:


Sifa zote njema Anastahiki Allah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allahu 'Alayhi Wa Aalihi Wasallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'Anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu jambo hili nyeti. Hakika ni kuwa hili ni tatizo kubwa kwa Waislamu wanaoishi katika Afrika Mashariki na hasa kwa ndoa kama ambazo zinaleta utata mkubwa katika familia. Hivyo, ni nasaha yetu kuwa ikiwa mume si Muislamu na amempenda binti basi apatiwe muda baada ya Kusilimu kabla ya kuozwa binti. Muda utakuwa wa kumsomesha Dini na kumfundisha mpaka jamii ihakikishe kuwa kweli amekuwa Muislamu wa utekelezaji.

Hapa tunakumbuka kisa baina ya Mzungu mmoja aliyekwenda Mombasa wakati Sheikh Muhammad Qaasim Mazrui ndiye Qadhi Mkuu wa Kenya. Huyu bwana alipendana na msichana wa Kiislamu naye akaambiwa kuwa hawezi kumuoa mpaka asilimu, naye akasema kuwa ikiwa ni hivyo basi yu tayari. Wazazi walitaka ushauri kwa Sheikh Muhammad, naye akawaambia wamlete. Sheikh alimwambia ya kwamba wazazi wanaona wapatiwe muda kabla ya harusi hivyo yeye asilimu mwanzo na yule Mzungu akasema kama ni hivyo basi sina haja ya kusilimu.

Katika Uislamu mtu anatakiwa aingie mzima mzima na wala sio nusu nusu

((Enyi mlioamini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za shetani; hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi )) [AL-Baqarah 2: 208]



Hawezi mtu kuwa ni Muislamu na hapo hapo ni Mkristu, ima utakuwa Muislamu au Mkristu na ikiwa yeye aliingia katika Dini kisha akatoka atakuwa ni murtadi na hivyo ndoa ya hao wawili inavunjika. Na ikiwa yeye mwenyewe anakiri si Muislamu basi amejitoa mwenyewe na ni lazima familia ijulishwe na hiyo ndoa ivunjwe kwani sasa wanakuwa wanazini.

Ikiwa yeye mwenyewe anajijua kuwa si Muislamu hilo linakuwa ni jambo sahali kwani akifa atazikwa na watu wake Kikristu.

Tusiwe wepesi kuwaoza watu kama hawa kwani kisha huleta matatizo mengi katika ndoa na familia. Tuwe waangalifu na tahadhari katika mas-ala mazito kama ya ndoa.

Na Allaah Anajua zaidi.
 
Anataka Kusilimu Lakini Anataka Kwanza Aonyeshwe Wapi Kwenye Qur-aan Kuna Amri Kumi Za Muusa, Na Kwa Nini Waislam Wanaswali Ijum
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:

Assalam alaikum.kuna rafiki yangu anataka kusilimu. Yeye ni msabato, na amekuwa karibu miezi miwili anajifunza uislamu. Mambo yanayomtatiza anataka aoneshwe wapi kwenye quran wameandika amri kumi alizopewa nabii Musa (as). Na kwa nini waislamu wanasali ijumaa badala ya jumamosi. Naomba mnisaidie majibu



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.




Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta'ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea au kivivu. Pia hiyo ni ibada, na ibada inatakiwa ifanywe kwa namna iliyofundishwa na haifai kugeuza, kuongeza au kupunguza. Hali kadhalika Maswahaba walikuwa wakiandikiana barua na hakuna aliyekuwa akikatisha Salaam, wala kumswalia Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wala kumtukuza Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwenye barua zao. Tuige na tufuate nyendo zao tusalimike.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu amri kumi za Nabii Musa (‘Alayhis Salaam) katika Qur-aan na kuswaliwa Swalah ya Ijumaa.

Kwanza amri hizi kumi ambazo zipo katika Agano la Kale zinapatikana katika ‘Kutoka’ 20: 1 – 17 na ‘Kumbukumbu la Sheria’ 5: 7 – 21. Bila shaka Uislamu ukiwa ni mfumo kamili wa maisha ya mwanadamu, amri hizo zilizo nzuri zinapatikana katika machimbuko muhimu ya Uislamu nayo ni Qur-aan na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Nasi tutajibana katika Aayah za Qur-aan kuhusu amri hizo kumi. Nazo ni kama zifuatazo:

1. Usiwe na miungu mingine:

2. Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga:

3. Usivisujudie wala kuvitumikia:

Hizi nukta tatu za juu zinahusiana na ushirikina ambao umepigwa vita vikali sana. Muislamu anafaa amuabudu, kumsujudia, kutofanya masanamu ya kuchonga au mengine na kutomshirikisha. Kumshirikisha Mwenyezi Mungu ni miongoni mwa madhambi makubwa sana katika Uislamu ambayo inafanya amali zako zote ziharibike. Miongoni mwa Aayah kuhusu hilo ni kama zifuatazo:

a. Amepitisha Mola wako Mlezi usimuabudu ila Yeye (17: 23).

b. Muabuduni Allaah wala msimshirikishe Yeye na chochote (4: 36).

c. Na miongoni mwa watu wapo wenye kuchukua miungu washirika wanaowapenda kama kumpenda Allaah. Na wale Waumini wanampenda Allaah zaidi (kuliko yeyote mwengine)” (2: 165).

d. Na hakika Tumewatuma kwa kila Ummah Mitume, na Tukawaambia: Muabuduni Allaah tu na mjiepushe na Twaaghuuti (anayeabudiwa asiyekuwa Allaah) {16: 36}.

e. Sema: Allaah ni Mmoja tu. Allaah ndiye Mwenye kukusudiwa. Hakuzaa wala Hakuzaliwa na hakuna anayefanana Naye (112: 1-4).

f. Mwenyezi Mungu Hasamehe dhambi ya kushirikishwa (4: 48, 116)



4. Waheshimu baba na mama yako: Kuwaheshimu wazazi imekuja katika Qur-aan baada ya kumuabudu Allaah. Kutowaheshimu wazazi ni katika madhambi makubwa.

a. Anasema Aliyetukuka: Na kuwafanyia wema wazazi. Na wanapofikia uzee mmoja wao au wote wawili, usiwaambie uff (neno ndogo hata kusema ah!) ... na uwaambie maneno mema (17: 23-24).

b. Wafanyie wema wazazi wako (4: 36).

c. Mnishukuru Mimi na wazazi wako. Na wakikulazimisha kunishirikisha kwa usilokuwa nalo elimu usiwatii (wazazi wako) lakini suhubiana nao duniani kwa wema (31: 14 – 15).



5. Usizini: Uzinzi ni dhambi kubwa katika Uislamu kiasi ambacho mwenye kuzini akiwa ameoa au hajaoa au kuolewa ana adhabu kali. Mwenyezi Mungu anatuamuru hata tusije karibu na zinaa (17: 32).

6. Usiue: Kuua pia ni katika madhambi makubwa ambayo anapata adhabu mwenye kufanya kitendo hicho. Mwenyezi Mungu Asema kuwa yeyote mwenye kuua nafsi moja ni kama ambavyo ameua walimwengu wote na kuhuisha nafsi moja ni kama ambavyo amehuisha walimwengu wote (5: 32). Na pia msiue watoto wenu kwa kuhofia ufakiri (17: 31).



7. Usiibe: Kuiba ni katika dhambi kubwa na mwenye kufanya hilo inabidi aadhibiwe na sheria ya Kiislamu. Na mwizi mwanamme na mwanamke, kateni mikono yao kama malipo kwa wanayochuma (5: 38). Kufanya hivyo ni kumkwaza anayetaka kuiba asiwe ni mwenye kutenda tendo hilo baya.

8. Usimshuhudie jirani yako uongo: Jirani ni mtu muhimu katika jamii. Uislamu umehimiza sana ujirani mwema. Zipo heshima na adabu ambazo majirani wawili kila mmoja analazimika kumfanyia mwenzake na kumpa haki zake zikiwa kamili. Na kutomshuhudia jirani uongo ni miongoni mwa adabu. Na Allaah Anasema: “Na kuwafanyia wema wazazi wawili … jirani ndugu na jirani asiye ndugu” (4: 36). Na Mtume (Swalla Allaah ‘alayhi wa sallam) amesema: “Anayemuamini Allaah na siku ya Mwisho basi amkirimu jirani yake” (Muslim, Ahmad).



9. Usimtamani mke wa jirani yako wala vitu vyake: Kufanya hivyo ni kutoka katika ujirani mwema na kuvunja ujirani mwema. Maelezo tayari tumeyaandika hapo juu. Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Na kumwekea mshirika wakati Yeye ndiye Aliyekuumba, kumuua mwanao ili asile nawe na kuzini na mke wa jirani yako” (al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaa’iy).



10. Adhimisha siku ya Sabato: Sabato ya Waislamu ni siku ya Ijumaa wala sio Jumamosi. Hiyo ni kuwa siku ya Ijumaa ni siku bora na tukufu hapa duniani. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Siku bora iliyochomoza jua ni Ijumaa, kwani ndani yake aliumbwa Aadam (‘Alayhis salaam) na siku hiyo aliingizwa Peponi na kwayo alitolewa, na Qiyaamah hakitasimama ila Ijumaa” (Muslim). Siku hii ni sikukuu ya Waislamu ulimwenguni. Hiyo ni siku ambayo inafaa kwa Muislamu kuiheshimu, hivyo kwenda Msikitini mapema na kufanya Ibadah. Japokuwa sikukuu kwa Muislamu anaruhusiwa kufanya kazi kabla ya Ibadah hiyo mahsusi au baada yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “Na itakapokwisha Swalah, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Allaah, na mkumbukeni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu” (62: 10).

Ama kuhusu kipengele cha pili cha swali lako kuhusu kwa nini Waislamu huswali Ijumaa, ni kuwa sisi Waislamu tunaswali siku ya Ijumaa badala ya Jumamosi kwa kuwa tumeagiziwa hilo na Muumba wetu, Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala). Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema:

“Enyi Mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Swalah ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Allaah na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu ikiwa mnajua” (62: 9).

Na Allaah Anajua zaidi
 
Asiye Muislam Anataka Kusilimu Kwa Kunioa, Nikikataa Itahesabikaje?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina


SWALI:





Ningependa kuuliza suala kama ifuatavyo

mimi ni msichana mwenye umri wa karibia miaka 25, ninaesoma nje ya nchi . huko ninakaa peke yangu. nimejitahidi kufuata dini kwa kadri ninavyoweza kwa kipindi chote nilichokuwepo huku masomoni kwa bahati mbaya au nzuri, ametokea mtu ambae si muislam kunipenda na kutaka kuniona (hatujawahi kufanya kitendo kibaya chochote), jee nini uhalali wa ndoa pamoja na yeye ikiwa atasilimu? Na ikiwa nitakataa kuolewa naye, nitahesabika kuwa nimemumzuilia mtu nafasi ya kuingia kwenye usilam?

naomba majibu yenu



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.






Shukrani za dhati kwa dada yetu aliyeuliza swali kuhusu jambo muhimu katika maisha yetu hapa ulimwenguni. Hasa ikiwa suala hilo likiwa ni mahusiano ya kijamii baina ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu.


Mwanzo kabisa tunakupatia hongera zetu kwa kushikilia Dini yako katika nchi ya ugeni ambapo wengi wanapotea kwa kutoweza kushikilia jambo hilo. Hiyo inatokana ima na kutopata malezi mazuri kutoka kwa wazazi, au kuwa na marafiki wabaya na pengine wasiokuwa Waislamu, kujiona kujitambulisha kwako na Uislamu ni kujitweza au kuona kuwa ugenini unaweza kufanya lolote kulingana na msemo 'When in Rome do as the Romans do' - "Don't set your own rules when you are someone's guest” - (Ukiwa Roma fanya kama Warumi). Huu ni msemo ambayo unakwenda kinyume kabisa na maadili ya Kiislamu. Na ni msemo ambao asili yake ni wa mmoja wa wakuu wa kikrsto aitwaye Saint Ambrose (340-397), ambaye alimshauri Saint Augustine kwa kumwambia: Si fueris Romae, Romano vivito more; si fueris alibi, vivito sicut ibi ('When you are in Rome live in the Roman style; when you are elsewhere live as they live elsewhere') – Ukiwa Roma ishi kwa mtindo wa maisha ya ki-Roma, na ukiwa pengine, ishi kama wanavyoishi huko”



Ni msemo unaotumiwa na Waislam wengi kwa kuiga na wengine huufan yia kazi kabisa kimaisha, na hali ni msemo unaopingana kabisa na Dini yetu na unaogongana na Uislam kama ndio sehemu ya maisha yetu katika kila Nyanja na katika kila sehemu na kila wakati. Utakapoufuata msemo huo kama ambavyo tunaona kwa wengi wanaoishi Ulaya baada ya kutoka na maadili yao mazuri kutoka Tanzania, Zanzibar, Kenya na kwengineko kwa kufuata utamaduni wa ki-Magharibi wa kuwa na ‘boy friends’ na ‘girl friends’ n.k, basi utakuwa umejivua na sifa za Uislam na kuelekea kwenye hizo sifa za nasaha za kina Saint Ambrose na mwisho wake utakuwa ni mtu aliyebakiwa na jina la Kiislam lakini matendo ya kikafiri.


Nasaha yetu ya kwanza kwa dada yetu ni kuwa upate marafiki wa kike wa Kiislamu walio wema ili upate kukabiliana na changamoto za huko. Ikiwa unaishi karibu na Msikiti na ipo sehemu ya wanawake ya masomo ya Dini ujiunge nao. Ikiwa hakuna Msikiti lakini zipo sehemu ambazo Waumini wanakutana ima siku za wikiendi utafute njia ya kuweza kuwa nao. Hii ni kuwa, kusikiliza mawaidha kunamsaidia Muislamu kuweza kukabiliana na mitihani kama hiyo yako kwani utakuwa na wenzi wako watakaokusaidia kwa nasaha, fikra na mengineyo.


Ile hali ya kuwa mpaka sasa hamjafanya chochote kibaya ni dalili ya kuwa unaweza kukumbana na vishawishi katika maisha. Baada ya kusema hayo inahitajia uwe mkakamavu zaidi kwani mara nyingi wasichana kwa ujumla wao wanakuwa rahisi kudanganywa na kushawishiwa kuingia katika tendo la mapenzi kabla hata ya kuolewa.


Pindi atakaposilimu ndoa yenu ikiwa itatimiza masharti mengine itakuwa halali. Lakini swali la kujiuliza ni: Je, huyu mvulana anataka kuingia katika Uislamu kwa sababu ya kunipata mimi au kwa kuipenda Dini yenyewe? Hivyo, hapana budi kumfanyia mtihani na kujua uhakika wake. Jambo kama hili liliwahi kutokea katika wakati wa Shaykh Muhammad Qaasim Mazrui akiwa Qaadhi mkuu wa Kenya. Alitakwa shauri na mzazi ambaye binti yake aliposwa na Mzungu aliyekuwa tayari kusilimu. Shaykh Muhammad Qaasim alimwambia bwana huyo kuwa wazazi wa binti wameghairi katika suala hilo la ndoa lakini yeye anaweza kuendelea kusilimu. Aliposikia hayo bwana huyo alimaka kwa kusema ikiwa ni hivyo basi hana haja ya kusilimu tena.


Ni juu yako kama Muislamu mwanzo kabisa kumchunguza kuhusu ukweli wake au ni kuwa anakutaka wewe na kusilimu ni chambo tu. Katika mas-ala ya mtu kusilimu isiwe tunafanya haraka kumuozesha kabla ya kupata tamkini na uhakika wa kusilimu kwake. Yapo matatizo mengi yanayotokea kwa mtu kusilimu na kisha kuoa bila ya kupatiwa mafunzo ya aina yoyote. Mara nyingi ndoa hizo hazidumu kwani mkikosana kidogo tu huyo mume atarudi katika dini yake ya awali na huenda ikiwa mmeshazaa naye na hivyo kuna hatari hata ya kuja kukimbia na mtoto. Vilevile udhaifu wa binti kwa kiasi fulani huwafanya na wao pia wakaritadi jambo ambalo ni hasara kubwa kwa Waislamu.


Ikiwa umeona ya kwamba huna budi kuoana naye basi itabidi umwambie wazi kuwa ndoa haiwezi kuwa moja kwa moja baada ya kusilimu kwake. Ni juu yake mwanzo ajifunze Dini ya Uislamu kwa muda usiopungua miezi sita. Katika kipindi hicho unaweza kutathmini uhakika wake wa kuingia katika Dini. Katika hilo ikiwa utakuwa na ndugu wa Kiislamu wakupatie ushauri baada ya hayo na hasa mwalimu wake anayemfundisha. Huna budi pia kuwajulisha wazazi wako kwa hatua hiyo ambayo umeiona kuwa inakufaa katika maisha yako na Imani yako. Ikiwa wazazi hawana pingamizi basi ni juu yako kuswali Swalah ya kumtaka ushauri Allaah Aliyetukuka (Swalatul-Istikhaarah Swalah ya Istikhaarah ) ambayo ni rakaa mbili naye Allaah Atakuongoza kwa lililo la kheri nawe katika Dini yako, maisha na hatima yako atakufanyia sahali.



Ikiwa wazazi wameridhia hasa baba ambaye ni walii wako basi ndoa itakuwa halali kwani Mtume Muhammad (Swalla Alaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuwa hapana ndoa bila walii. Hii ina maana hata ikiwa umekubaliana na huyo bwana huwezi kujiozesha mpaka upate idhini ya walii wako.


Kipengele cha mwisho katika swali lako ni kuwa kukataa kwako kuolewa na huyo bwana hata baada ya kuwa amesilimu na akawa ni Muislamu mzuri hutakuwa na makosa wala dhambi aina yoyote. Ikiwa yeye amesilimu kwa sababu ya Dini yenyewe au anataka kusilimu kwa sababu hiyo hatatishwa kukataa kwako kwani lengo lake si wewe bali kufika katika njia nyoofu. Hata pindi unapokataa kuolewa naye, naye akakataa kusilimu au akaritadi basi wewe hutakuwa na dhima yoyote wala dhambi. Kosa litakuwa kwake kwani atakuwa tayari amejua ukweli wa Uislamu. Wewe hutakuwa umemzuia kuingia katika Uislamu bali amejizuia mwenyewe. Mtu huyo anaingia katika ile Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliposema:


“…na ambaye kuhama kwake ni kwa ajili ya kuupata ulimwengu au mwanamke wa kumuoa, basi kuhama kwake ni kwa lile alilohamia”



(Ahmad, al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaaiy na Ibn Maajah). Usibabaike kwa hilo bali mtegemee Allaah Aliyetukuka naye Atakuongoza katika njia iliyonyooka.


Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akupatie subra, utulivu, umakini, usighurike kwa chochote wala lolote na Akupe lililo na kheri nawe hapa duniani na Kesho Akhera pamoja na kukuweka katika Imani thabiti.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Binti Yangu Amezaa Na Mkristo Tumekubali Posa Kwa Sharti Abadili Dini, Sasa Anakataa Tufanyeje?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI

Assalaal Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh.

BINTI YANGU AMEZAA NA MKIRISTO, TUMEKUBALI POSA NA KUWA ATABADILI DINI SASA ANAKATAA TUFANYEJE

Ndugu zangu nina mtihani mkubwa naombeni msaada na ushauri mapema.

Tuna binti huko UK anasoma tukakuta ana rafiki kijana Mkiristo. Tukamshauri kuwa ni haramu kuishi na kijana mkiristo na tutam-disown kama ataolewa naye abadili dini. Tukamjulisha na kijana kuwa kama anataka kumuoa binti lazima abadili dini awe Muislamu. Nimekuwa nawapelekea makala nyingi za dini na msahafu wenye tafsiri niliwapa muda mrefu. Binti akatuambia kijana amekubali kubadili dini lakini bahati mbaya sasa wamezaa mtoto. Kijana akaleta posa na tukaikubali kwa sharti letu la kuwa atamuoa tu akiwa amependa dini yetu na abadili dini awe Muislamu ndoa ifungwe ya Kiislamu. Wazazi ndio tumepanga kuonana kupanga kuhusu harusi mwezi ujao.

Sasa leo binti ananiambia kuwa anaona kijana hajapenda sana kubadili dini na hataki kumlazimisha. Wamepanga wafungie ndoa huko UK ambapo watapewa cheti cha serekali.

Kufuatana na hukmu ya dini tunatakiwa tum-disown binti kabisa kwa hii tabia haramu?. Je Turudishe posa au tumshawishi abadili wafunge ndoa ya Kiislamu?? Sitaki kumuasi Mwenyezi Mungu kwa makosa ya binti ambaye ni mtu mzima.

Mwenyezi Mungu awabariki na kuzidi kuwaongoza katika kazi hii njema ya kuelimisha umma wa Kiislamu.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.



‘Kijana kaleta posa na tukaikubali’ Asli katika uchumba na kupelekea kukubali posa ni kuwa muhimu sana kwa wazazi kumkubalia kwa mtoto wao yule aliyewashauri Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pekee tumkubalie, kama kweli ni katika wenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho na kufuata aliyowapa Muhammmad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kuacha na aliyowakataza kama inavyotuelekeza na kutusisitiza Qur-aan kwa kusema:

“ … Na anachokupeni Mtume chukueni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho. Na mcheni Allaah. Hakika Allaah ni Mkali wa kuadhibu” Al-Hashr: 7.

Kwani Muhammmad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndio dira na kiongozi wa Waumini, yeye ni kiongozi pekee anayewapendelea wafuasi wake kila lenye kheri katika maisha yao yote, ndio akawa yanamhuzunisha yanayowataabisha; anawahangaikia sana, anapata dhiki kwa madhara yanayo wasibu, ana hamu tuongoke, tena basi ni mwingi wa huruma na rehema kwetu Waumini; ushauri wake katika posa ni kuwa tumkubali mtu wa namna moja tu, mtu aliye na muelekeo wa kuweza kwa tawfiki yake ar-Rahmaan kumsaidia katika kumpelekea kutekeleza yenye kutarajiwa kumfikisha Peponi na huyo ni yule aliyekubali kwa ridhaa yake. Na kuyathibitisha hayo kwa vitendo vyake kuwa kuna Mungu mmoja ambaye Pekee ndiye mwenye haki ya kuabudiwa na huyo ndiye mnayetakiwa kuipokea posa yake sio mshirikina; kwani Mkiristo ni mshirikina bila ya shaka yoyote ile, vyenginevyo ni uharibifu katika ardhi kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

“Amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Atakapokujieni mtayeridhika na tabia yake na dini yake (kwa posa) basi muozesheni, vyenginevyo itakuwa fitna katika ardhi na ufisadi mkubwa” Imepokelea na Al-Haakim.

Hivyo basi kosa lililotendeka kwanza ni kwenda kinyume na ushauri bali amri ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa kukubalia posa ya uliyesema, ‘kijana Mkiristo akaleta posa na tukaikubali’, kwa kukubali posa yake mlikuwa mmeridhika na nini? Tabia zake?! Tabia ya kuishi na mtoto wenu na kumzalisha! Dini yake?! Kumshirikisha Allaah kwa kusema kuwa ana mtoto au kuabudu masanamu! Kuna ushirikina zaidi ya huu?! Kipi mlichoridhika nacho?

Jengine ni kuwa umekwenda kinyume na ushauri bali pia ni amri ya Allaah kwani Ametukataza kuwaoa au kuwaozesha watoto wetu washirikina; kwa kuipokea posa ni kama ushakata shauri la kuwa tayari kumuozesha mtoto wenu kama ulivyosema, ‘Wazazi ndio tumepanga kuonana kupanga kuhusu harusi mwezi ujao’

na Qur-aan inakushauri na kukuamrisha hivi:

“Wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini. Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Wala msiwaoze (binti zenu) wanaume washirikina mpaka waamini. Na mtumwa mwanamume Muumini ni bora kuliko mshirikina hata akikupendezeni. Hao wanaitia kwenye Moto, na Allaah Anaitia kwenye Pepo na maghafira kwa idhini yake…” Al-Baqarah: 221.

Umesema, ‘Tuna binti huko UK anasoma’, katika makosa ambayo yanafanywa tena kwa wingi ni huku Waislamu kutomsikiliza na kushikamana na ushauri wake wanaedai kuwa wanampenda na kumtukuza, Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kumpeleka mtoto wa kike masomoni tena Uingereza ambako hakuna neno haramu katika kamusi la jamii yao, huko ni kumtelekeza na kumuangamiza mtoto, watoto wa kiume hupotea achila mbali wa kike.

Wazazi wenye kipato huonelea ni vyema kuwasomesha mtoto wao nchi za nje (sio vibaya kama kinachotakiwa hakipo katika nchi zao) ila tu wanahitaji waulize nini ametushauri Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kusafiri mwanamke kama ilivyothibiti katika Hadiyth ya Abu Sa’iyd Al-Khudriy amesema: amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Si halali kwa mwanamke (katika riwaya): - Kwa hakika hakai pekee mwanamume na mwanamke isipokuwa yuko Mahram wa huyo mwanamke - , mwenye kuamini Allaah na Siku ya Mwisho kusafiri safari ya siku tatu na ziada isipokuwa anakuwa pamoja naye baba yake au mtoto wake au mume wake au ndugu yake au Mahram wake” Imepokelewa na Muslim, kitabu cha Hijja, mlango safari ya mwanamke pamoja na Mahram wake Hajj na kwengineko.

Kama katika kesi yetu hii palifuatwa ushauri huu wa kusafiri na kuishi na Mahram wake huko UK, basi kusingekuwepo neno lako la ‘tukakuta ana rafiki kijana Mkiristo’, haya pengine yasingelitokea; na kubwa zaidi ni kuwa kama tulimuandaa na kumsomesha mapema kuhusu dini yake na kumuelewesha lipi ni halali na lipi ni haraam kabla ya safari yake na kuhakikisha kuwa akili yake ni yenye kuelewa na kufanya kazi sawa sawa na imani ipo katika moyo wake na kuelewa kuwa dini yake ni ya haki na ndio ya kufuatwa na kila mtu, ilikuwa yeye mwenyewe huyo mtoto wenu kama anamtaka na kumpenda kikweli kweli awe baba wa watoto wake; alitarajiwa kama ni Muislamu yeye mwenyewe awe na uwezo wa kumueleza na sio nyinyi kumueleza huyo kijana kama ulivyosema, ‘Tukamshauri kijana’; kama alivyomueleza Ummu Saliym Abu Twalhah alipotaka kumuoa, kisa chake ni sawa sawa na cha mtoto wenu kama anavyosimulia Anas (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwa kusema:

“Alileta posa Abu Twalhah kutaka kumuoa Ummu Saliym; Ummu Saliym akamwambia: Wa Llaahi (kwa kula kiapo) haiwezekani kwa mtu kama wewe Abu Twalhah kuoana na mimi, kwani wewe ni kaafir (mkiristo) na mimi ni Muislamu na si halali kwangu kuolewa na wewe; utaposilimu (ukibadili dini na kuwa Muislam) basi huko kusilimu kwako ndio kutakuwa mahari yako kwangu na sitotaka zaidi ya hilo; basi Abu Twalhah alisilimu na ikawa ndio mahari yake; Thaabit amesema: Sikuwahi kusikia kwa mwanamke yeyote aliyewahi kupata mahari bora na mazuri kuliko Ummu Saliym kwani mahari yake yalikuwa Uislam…” Imepokelewa na An Nasaaiy, kitabu cha ndoa ,mlango wa kuolewa kwa sababu ya Uislamu.

Hivyo basi kama mtoto wenu ni Muislam, alitarajiwa kuwa na msimamo kama huu wa Ummu Saliym wa kumueleza kuwa ni muhali bali ni haramu kuolewa na mkiristo na ukisilimu basi huko kusilimu kwako ndio kutakuwa mahari yako kwangu na sitotaka zaidi ya hilo kwani dini kwangu ndio uti wa mgongo wa maisha yangu.

Kisha umesema, ‘Tukamjulisha kijana kuwa kama anataka kumuoa binti lazima abadili dini awe Muislamu. kwa sharti letu la kuwa atamuoa tu akiwa amependa dini yetu na abadili dini awe Muislamu ndoa ifungwe ya Kiislamu’. Asli, haya yalikua yatokee kwa mtoto wenu kama ni Muislamu na yalikuwa yaje kwa njia nzuri ya kumlingania na njia iliyokuwa nzuri ya kumlingania kwani kwa kijifedhehesha kwake sasa wamezaa mtoto, kutokuwa yeye mwenyewe Muislam na kumthibitishia kivitendo kuwa hakuna haja ya kubadili dini wala kufunga ndoa Kiislamu. Kisha umesema, ‘anaona kijana hajapenda sana kubadili dini na hataki kumlazimisha. Wamepanga wafungie ndoa huko UK ambapo watapewa cheti cha serekali’, hakika huo ndio mchango wa mtoto wenu kumpelekea kijana abakie kama alivyo; kwani kuna usemi sio mzuri lakini hapa ni pahala pake unaosema: “kuna haja gani ya kununua ngo’mbe ikiwa unapata maziwa kwa kawaida kama apatavyo mmiliki wa ngo’mbe,” na haya ndio aliyokuwa nayo kijana katika akili yake ya nini kubadili dini na ya nini kuoana Kiislamu kwani kila nikitakacho chenye kuitwa maisha ya ndoa baina ya mke na mume ninakipata bila ya kuoa wala kubadili dini na ushahidi wake sasa wamezaa mtoto.

Umesema, ‘Sitaki kumuasi Mwenyezi Mungu kwa makosa ya binti ambaye ni mtu mzima’. Kwa hakika tushamuasi Mwenye nguvu na Mwenye adhabu iliyo chungu! Kwani tulitakiwa tujilinde nafsi zetu na ahali zetu (akiwemo huyo mtoto wetu) na Moto wa Jahannam, na kujilinda kwenyewe ni kutekeleza kila litaloweza kwa tawfiki yake Allaah kukupelekea kutokwenda kinyume na amri za Allaah na haya huja kwa kumuelimisha kama ulivyosema ‘Nimekuwa nampelekea makala nyingi za dini na msahafu wenye tafsiri’ yepi halali kwake na yepi haraam na kule kumpeleka UK bila ya Mahram kumechangia yote nako ni kwenda kinyume na amri ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) , hivyo basi mumemtelekeza na kumsukumiza mtoto wenu katika Moto, bila shaka yoyote ile mumeasi na mumekwenda kinyume na mafundisho ya Qur-aan, kwani Qur-aan inasema:



“Enyi mlioamini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia Malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa Anayowaamrisha, na wanatenda wanayo amrishwa” At-Tahriym: 6.

Tunatumai kuwa hii itakuwa funzo kwa wazazi wengine pia wasije kufanya kosa kama hili kwa watoto wao wa kike.

Umesema, ‘Kufuatana na hukmu ya dini tunatakiwa tum-disown binti kabisa kwa hii tabia haramu?’ Nyinyi wazazi mna makosa yenu na mtoto ana yake; na lilio wazi ni kuwa yeye ni mzinifu na zinaa ni haraam katika Uislamu na kama atakuwa anaona na kuitakidi kuwa zinaa ni halali na sio haraam basi atakuwa amehalalisha kilichoharamishwa na Allaah hivyo atakuwa ametoka nje ya duara la Uislamu kwa kuhalalisha aliyoharamisha Allaah; hukumu ya mzinifu kama inavothibitisha Qur-aan ni kupigwa mboko mia (100), hakuna pa kutekelezwa hayo; lakini hayo yatamthibitikia Siku ya Malipo kama hatotubia na kuacha kuzini; Qur-aan inasema:

“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini.” An-Nuur: 2.



Umesema tena, ‘Je Turudishe posa,’ kwa hakika ndugu yetu hapo hakuna posa, kwani aliyeleta posa hana haki ya kumuoa mtoto wenu kama mnaamini Allaah na Siku ya Mwisho na kutarajia aliyoyaandaa kwa wenye imani hiyo; kwani mtoto wenu kama ni Muislamu si halali kuolewa na huyo kijana Mkiristo kama ilivyoashiria Qur aaan kwa kusema:



“….Wanawake hao (Waumini) si halali kwa hao makafiri, wala hao makafiri hawahalalikii wanawake Waumini. Na wapeni hao wanaume mahari waliyotoa….” al Mumtahinah aya ya 10.



Hivyo basi kurudisha posa na kutorudisha hakutosaidia kitu, kwani kilichotakiwa na wote wawili kinapatikana kila wanapotaka; hivyo basi kinachotakikana ni kumuaidhi na kumnasihi kwa kumueleza mtoto wenu kuwa anazini na Allaah Ameiharamisha na kutahadharisha kwa kuikaribia zinaa, yeye analala na kuamka nayo, bali ndio maisha yake, pia kumuelewesha kuwa huenda yeye kwa kumkubalia ayatakayo akawa miongoni au sababu tosha ya kumpelekea huyo Mkiristo kuona kuwa Uislamu si lolote bali ni kama Ukiristo kwani wao kama wanavyodai kuwa ni mafundisho ya dini yao huishi na kuzaa kisha wakaja kufunga ndoa miaka mingi bada ya kupata watoto kama watataka.



Kisha ukasema, ‘tumshawishi abadili wafunge ndoa ya Kiislamu??’ Ndoa ya Kiislamu haifungwi isipokuwa baina ya Waumini wawili na hapa hakuna hilo, bali haliruhusiwi kwa muozeshaji kumuozesha Muislam kwa asiye Muislamu hata kama wao wataridhiana na mtoto wako anayaelewa hayo ndio akakutaarifuni kuwa ‘Wamepanga wafungie ndoa huko UK ambapo watapewa cheti cha serekali.’



Tunamuombea Allaah (Subhaana wa Ta’ala) Amuongoze mtoto wenu Amuonyeshe haki na atoke katika maasi hayo kabla hayajazidi madhara kwake, na tunawaombea watoto wetu wote wa Kiislamu Allaah Awaongoze katika Njia iliyonyooka. Aamiyn.



Na Allaah Anajua zaidi
 
Dada Anayetaka Kusilimu, Watoto Awafanye Nini Ili Wasichukuliwe Na Baba Yao Asiyetaka Wawe Na Mama Yao?
Maswali: Ahlul-Kitaab-Washirikina
SWALI:



Asalamu Aleikum Warahmatullah Wabarakatu,

Kwa hakika nina furaha sana kwa mtandao wenu na kwa kadri munavyo yajibu mswali kwa ustadi na umakinifu, Inshalla Mungu atawawezesha muwe na moyo huo huo kwani sikazi ndogo munayo ifanya kuwaelisha umaa. Allaha bariq fee.

Suala langu ni, Kuna dada mmoja mkristo alijaaliwa kuwa na toto wa 3 na alikua akiishi na mumu wake Mkristo, kwa sasa hivyo wame kosana na mumuwe kwa matatizo yao yakinyumbani, mke amempeleka mume kortini ili amuachie watoto na ampe talaka, Sasa dada kama huyu ana sema yeye sasa anataka kusilimu na aolewe na muislamu kinacho msumbua zaidi ni watoto kwa sababu yeye akisilimu je watoto itakuaje? Kwa sababu anaogop baba ya watoto anaweza kuja kuchuka watoto na awapeleke kwa familia yake (Baba) ili waepukane na mama yao kwa sababu amesilimu, je jambo kama hili utampa dada huyu Ushauri gani? Naomba jibu kadri ya uwezo wenu.

Shukran.



JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani kwa swali lako kuhusu dada anayetaka kusilimu.

Mwanzo jambo la kusilimu halifai kucheleweshwa kabisa, inafaa mumsilimishe mwanzo na auweke Uislamu wake kuwa ni siri huku akingojea uamuzi wa mahakama ili umkabidhi yeye watoto.

Akishakabidhiwa watoto, afanye juhudi ya kuwapeleka kwa haraka katika Madrasah nzuri au amuite mwalimu nyumbani kuwafundisha. Watoto hao wakipata elimu ya Uislamu pamoja na kuingiwa na Imani itakuwa si rahisi kwa baba kuweza kuwachukua kwani watoto wenyewe hawatokubali kabisa jambo hilo.

Na hata baba akiweza kuwachukua watoto wake, hilo halitakuwa katika uwezo wake yey huyo dada na hivyo hatoadhibiwa na Allaah kwa hilo bali atapata thawabu kwa juhudi zake.

Fanyeni hima katika hilo na kwa ajili ya Niyah yenu na yake njema Allaah Aliyetukuka Atakuwa pamoja naye.



Na Allaah najua zaidi
 
Back
Top Bottom