Ramadhan Special Thread
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



021-Kufuga Ndevu



Alhidaaya.com







Hukmu ya kufuga ndevu



Kufuga ndevu ni lazima kwa wanaume, na hii ni kwa Hadiyth zifuatazo:



1- Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuzifuga. Agizo hili ni la wajibu, kwani hakuna kiashirio chochote chenye kulipindisha na kulifanya liwe ni la Sunnah. Kati ya maagizo hayo ni neno lake Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):



((خالفوا المشركين: وفروا اللحى وأحفوا الشوارب))

((Khalifianeni na washirikina. Fugeni ndevu na punguzeni masharubu)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (5892) na Muslim (259)].



Na neno lake:

((جزوا الشوارب، وأرخوا اللحى، خالفوا المجوس))

((Kateni masharubu, ziachilieni ndevu, khalifianeni na wamajusi)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (260)].



1- Anayezinyoa, anajifananisha na makafiri kama ilivyotangulia katika Hadiyth hizo mbili.

2- Anayezinyoa, anabadili Umbile la Allaah na anamtii shaytwaan aliyesema:



(( وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّهِ ))

((Na kwa hakika, nitawaamrisha, na wao bila kusita, watalibadilisha Umbile la Allaah)). [An-Nisaa (4:119].



3- Anayezinyoa, anajifananisha na wanawake. Na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amewalaani wanaume wanaojifananisha na wanawake. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (5885) na At-Tirmidhy (2935)].



Na kwa ajili hiyo, Sheikh wa Uislamu anasema: “Ni haramu mtu kunyoa ndevu zake”. [Al-Ikhtiyaarat Al-Fiqhiyyah cha ‘Alaaud Diyn Al Baaly (uk 10). Angalia pia Al-Furu’u cha Ibn Muflih (1/291)].



Ibn Hazm na wengineo, ameinukuu Ijma’a ya Maulamaa kwamba ni haramu kunyoa ndevu. [Maratibul Ijma’a na Raddul Mukhtaar (2/116)].



Je, Inajuzu Kunyoa Ndevu Zilizozidi Mkamato Wa Mkono?



Baadhi ya Maulamaa wanaona kwamba inajuzu kuzikata ndevu zilizozidi mkamato wa mkono kwa kigezo cha Hadiyth ya Ibn ‘Umar ya kwamba alipokuwa anahiji au kufanya ‘Umrah, alikuwa akikamata ndevu zake, na zile zinazozidi, huzikata.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (5892) na Muslim (259)].



Wanasema: “Yeye ndiye mpokezi wa Hadiyth inayoamuru kufuga ndevu, na kwa hivyo, anayajua zaidi madhumuni yake”.



Hujja ya Maulamaa hawa haina mashiko katika athari hii kutokana na haya yafuatayo: [Ameyaelezea haya Sheikh Al-Habiyb Wahiyd ‘Abdus Salaam Baaly – Allaah Ainyanyue hadhi yake – katika kitabu cha Al-Ikliyl].



1- Ibn ‘Umar (Radhwiya Allaahu Anhu) alikuwa akilifanya hilo wakati anapojifungua na ihram ya Hijjah au ya ‘Umrah. Lakini wao wanalijuzisha hilo katika hali zote.



2- Kitendo hiki cha Ibn ‘Umar, kinatokana na yeye kuliawilisha Neno Lake Allaah Mtukufu:

((مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمْ وَمُقَصِّرِينَ))

((Mkinyoa vichwa vyenu na mkipunguza)).[Al-Fat-h (48:27].



..kuwa ni katika amali ya Hijjah. Kunyoa ni kwa kichwa, na kupunguza ni kwa ndevu. [Angalia Sharhul Kirmaany Al-Bukhaary (21/111)].



3- Swahaba akisema au akifanya kinyume na aliyoyasimulia, basi kinachoangaliwa ni kile alichokisimulia, si ufahamu wake wala kitendo chake. Kinachoangaliwa ni kile alichokisema Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) moja kwa moja.



Kutokana na vigezo hivi, la sahihi ni kuwa kufuga ndevu ni wajibu na kuzikata haijuzu kwa msingi wa kuyafuata maagizo jumuishi yaliyokuja kwenye Hadiyth nyingi Swahiyh kama wanavyoona Jamhuri ya Maulamaa. Allaah Ndiye Mjuzi
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



022-Twahara Za Kihukmu



Alhidaaya.com







Aina Za Maji



Maji juu ya kutofautiana sampuli zake, hayatoki nje ya aina mbili:



1- Maji Mutwlaq (Maji Twahara)



Ni yale yenye kubakia kwenye asili ya maumbile yake. Na haya ni maji yoyote yaliyochimbuka toka ardhini au yaliyoteremka toka mbinguni. Allaah Mtukufu Anasema:



((وَيُنَزِّلُ عَلَيْكُمْ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً لِيُطَهِّرَكُمْ به))

((Akakuteremshieni maji kutoka mbinguni ili Akusafisheni kwayo)). [Al-Anfaal (8:11)].



Katika aina hii, yanaingia maji ya mito, theluji, mvua barafu, na visima, hata kama yatabadilika kwa kukaa sana au kwa kuchanganyika na kitu twahara ambacho ni vigumu kuepukana nacho. Vile vile maji ya bahari, kwani Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoulizwa kuhusu maji ya bahari alisema:



((هو الطهور ماؤه الحل ميتته))

((Maji yake ni twahara na mfu yake ni halali)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (83), At-Tirmidhy (69), An-Nasaaiy (1/176) na Ibn Maajah (386)].



Maji haya yote yanafaa kutawadhia na kuogea bila hitilafu yoyote kati ya Maulamaa, na hata kama yatachanganyika kidogo na kitu twahara yataendelea kubeba jina la maji. Katika Hadiyth ya Ummu Haani ni kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alioga yeye na Maymunah katika kijibeseni kimoja chenye athari ya kinyunya. [Imefanyiwa “ikhraaj” na An Nasaaiy (240) na Ibn Maajah (378)].



Na (ushahidi mwengine ni) kwa amri ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam kwa wanawake waliomwosha binti yake Zaynab alipowaambia:



((اغسلنها ثلاثا بماء وسدر واجعلن في الآخرة كافورا))

((Mwosheni mara tatu; kwa maji na mkunazi, na osho la mwisho fanyeni kwa kafuri)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (1253) na Muslim (939)].



Ama kama yatachanganyika na kitu twahara kikaondosha jina la maji na kuwa jina jingine kama chai kwa mfano, basi haijuzu kujitwaharisha nayo. Aidha, haijuzu kujitwaharisha hadathi kwa kutumia vimiminika vilivyokamuliwa toka vitu twahara kama maji ya waridi na mfano wake, kwani hayo si maji halisi.



Ibnu Al-Mundhir anasema: “Maulamaa wote tuliohifadhi kauli zao, wamekubaliana kwa kauli moja kuwa wudhuu haufai kwa maji ya waridi, maji ya miti na maji ya m-’asfara. Na haifai kujitwaharisha ila kwa maji “mutwlaq” yenye jina la maji..” [Al-Mughny (1/11) na Al-Muhallaa (1/199)].





2- Maji yaliyonajisika



Ni maji yaliyochanganyika na najsi ikaathiri moja kati ya sifa zake kwa kubadilisha harufu yake, au rangi yake au ladha yake, kwa namna ambayo mtu akiyatumia, ataona kwa yakini kwamba anatumia najsi (badala ya maji).



Haijuzu kutawadhia kwa maji haya kwa vile yenyewe ni najsi.
 
Tunakumbushana jambo muhimu sana,kwa wale tunaotarajia kwenda kuswali swala ya eid kesho au kesho kutwa

Basi usiende kuswali kama umefunga bali ni sunna uende ukiwa umekula chochote,hata funda la maji linatosha

Ila kwa swala ya eid kubwa eid ya kuchinja ni sunna kwenda kuswali ukiwa hujala kitu
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



023-Kutawadha Kwa Maji Yanayochuruzika Toka Viungo Vya Wudhuu



Alhidaaya.com





Maji yanayochuruzika toka kwenye viungo vya mwenye kutawadha na mfano wake, huitwa “maji yaliyotumika”. Na bila shaka Maulamaa wamehitalafiana kuhusu maji hayo kama yanapoteza sifa ya kuwa ni yenye kutwaharisha au la.



Rai yenye nguvu ni kuwa maji hayo yanabakia ni yenye kutwaharisha madhali hayajapoteza jina la maji “mutwlaq” na wala hayajachanganyika na najsi ikaathiri moja kati ya sifa zake.



Haya ndio madhehebu ya ‘Aliy bin Abi Twaalib, Ibn ‘Umar, Abuu Umaamah na watangu wema wengi. Ni mashuhuri pia katika madhehebu ya Maalik. Aidha, ni moja kati ya riwaya mbili zilizopokelewa toka kwa Ash-Shaafi’iy na Ahmad. Pia ni madhehebu ya Ibn Hazm na Ibn Al-Mundhir. Mwelekeo huu pia umekhitariwa na Shaykh wa Uislamu (Ibnu Taymiyah). [Al-Mughny (1/31), Al-Majmuu (1/205), Al-Muhallaa (1/183), Majmuu Al-Fataawaa (20/519) na Al-Awswat (1/285)].



Kauli hii inatiliwa nguvu na dalili zifuatazo:



1- Kwamba asili ni kuwa maji ni twahara wala hayanajsiwi na chochote. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

((الماء طهور لا ينجسه شيئ))

((Maji ni twahara, hayanajsiwi na chochote)).[Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (266), At-Tirmidhy (66) na An-Nasaaiy (1/173)].



Isipokuwa kama sifa yake moja itabadilika au yakapoteza jina la maji “mutwlaq” kwa kuchanganyika na kitu twahara.



2- Imethibiti kwamba Maswahaba walikuwa wakitumia mabaki ya maji aliyotawadhia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). (Hii ni kwa dalili zifuatazo):





(a) Imepokelewa toka kwa Abuu Juhayfah akisema:

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitutokea mchana wa jua kali, akaja na maji ya kutawadhia kisha akatawadha. Hapo watu wakaanza kuchukua mabaki ya maji aliyotawadhia na kujipangusa nayo”.[Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (187)].



Al-Haafidh katika “Al-Fat-h” (1/353) anasema: “Inawezekana kuwa walichukua yale yaliyochuruzika toka kwenye viungo vya wudhuu vya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na hii ni dalili wazi kuwa maji yaliyotumika ni twahara.





(b) Na katika Hadiyth ya Al-Masuur bin Makhramah: “…na anapotawadha Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), walikuwa wakikaribia kupigana kugombea maji aliyotawadhia”.[Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (189)].





(c) Imepokelewa na Abuu Musa Al-Ash’ary kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliagizia bilauri ya maji. Akaoshea mikono yake na uso wake humo na akatema. Kisha akamwambia yeye (Abuu Muusa) na Bilaal:

(( إشربا منه، وأفرغا على وحوهكما ونحوركما))

((Kunyweni humo, na yamiminieni kwenye nyuso zenu na shingo zenu)).[Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (188)].





3- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), wanaume na wanawake walikuwa wakitawadha wote pamoja”. [Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (193), Abuu Daawuud (79), An-Nasaaiy (1/57), na Ibn Maajah (381). Riwaya baada yake ni ya Abuu Daawuud kwa Sanad Swahiyh].



Na katika riwaya: “Katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), tulikuwa sisi na wanawake tukitawadha katika chombo kimoja tukiingiza mikono yetu ndani”.





4- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiogea kwa mabaki (ya maji) ya Maymunah. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (323). Iko kwenye Swahiyh Mbili kwa tamko lisemalo: “Walikuwa wakiogea chombo kimoja”].





5- Imepokelewa toka kwa Al-Rubayi’i bin Mu’awwadh kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipangusa kichwa chake kwa mabaki ya maji yaliyokuwa mkononi mwake. [Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (130) na Ad Daaraqutwny (1/87)].





6- Ibn Al-Mundhir katika Al-Awswaat (1/288) amesema: “Na katika Ijma’a ya Maulamaa ni kwamba matone tone yaliyobakia katika viungo vya mwenye kutawadha au mwenye kuoga, na yale maji yaliyotona kwenye nguo zao, hayo yote ni twahara. Na hii ni dalili kuwa maji yaliyotumika ni twahara. Na kama ni twahara, basi hakuna maana kuzuia kutawadhia maji hayo bila ya hoja wanayoirejelea wale wenye rai tofauti na kauli”.



Inafaa kueleza hapa kwamba kundi la baadhi ya Maulamaa wamesema: “Haijuzu kutawadhia maji yaliyotumika”. Yamesemwa haya na Maalik, Al-Awzaa’iy, Ash-Shaafi’iy – katika riwaya moja kati ya mbili – na Abuu Haniyfah na wenzake. [Al-Istidhkaar (1/253), At-Tamhyid (4/43), Al-Mughny (1/19), na Al-Awswat (1/285)].



Maulamaa hawa hawana dalili yakinifu za kuridhisha. Mwenye kutaka, azirejee katika rejea tajwa.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



024- Inajuzu Kwa Mwanaume Kuogea Kwa Mabaki Ya Maji (Aliyojitwaharishia Mwanamke)



Alhidaaya.com





'Ulamaa wana mielekeo miwili katika hukmu ya mtu kujitwaharisha kwa maji yaliyobakia baada ya mwanamke kutawadhia au kuogea.



Mwelekeo Wa Kwanza:



Haijuzu kwa mwanaume kujitwaharisha kwa mabaki ya mwanamke. Na haya ni madhehebu ya Ibn ‘Umar, ‘Abdullaah bin Sarjas, Mama wa Waumini Juwayriyah bint Al-Haarith, Al-Hasan, Ahmad bin Hanbal, Is-haaq, Ash-Sha’abiy na Daawuud Adh-Dhaahiriy. [Al-Awswat (1/292) na Al-Mughny (1/282)].



Hoja yao ni:



1- Yaliyopokewa toka kwa Al-Hakam bin ‘Amr kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mtu kutawadhia mabaki ya maji aliyojitwaharishia mwanamke. [Maulamaa wameitia ila. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (82), At-Tirmidhiy (64), An-Nasaaiy (1/179), Ibn Maajah (373) na Ahmad (5/66). Al-Bukhaariy, Ad-Daarqutwniy na An-Nawawy wameitia dosari pia. Ama Ibn Hajar na Al-Albaaniy, wao wamesema ni Swahiyh katika “Al-Irwaai (1/43)].



2- Imepokelewa toka kwa Humayd Al-Humayriy akisema: “Nilikutana na mtu aliyesuhubiana na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa miaka minne kama alivyosuhubiana Abu Hurayrah. Alisema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza mwanamke kuogea mabaki ya mwanaume, au mwanaume kuogea mabaki ya mwanamke. (wachote wote kwa pamoja)”.[Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (81), An-Nasaaiy (1/130) na Al-Bayhaqiy (1/190)].



3- Ni yale yaliyopokelewa toka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ahli wake, walikuwa wakiogea chombo kimoja, na haogei mmoja wao kwa mabaki ya mwenzake”.[Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (1/133)].



Mwelekeo Wa Pili:



Inajuzu mtu kujitwaharisha kwa mabaki ya mwanamke. Yamesemwa haya na “Umar, Abu Hurayrah, ‘Abdullah ibn ‘Abbaas, Ibn ‘Umar, Sa’ad bin Abiy Waqqaas, mjumuiko wa watangu wema, Abu ‘Ubayd na Ibn Al-Mundhir. Haya pia ndio madhehebu ya Hanafi, Maalik, Ash-Shaafi’iy na riwaya ya Ahmad. [Muswannaf ya ‘Abdur-Razzaak (1/110), Ibn Abi Shaybah (1/38), Al-Awswat (1/297), At-Twahuwr cha Abu ‘Ubayd (236), Al-Mabsutw (1/61), Al-Ummu (1/8) na Al-Mughny (1/283)].



Wametoa hoja kwa haya yafuatayo:



1- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiogea kwa mabaki ya Maymuunah. [Hadiyth Swahiyh. Imeshafanyiwa “ikhraaj” hapo nyuma].



2- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Ahli mmoja wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliogea kwenye beseni. Na Rasuli alipokuja alimwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Mimi nilikuwa na janaba. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

(( إن الماء لا ينجس))

((Hakika maji hayapati janaba)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (68), At-Tirmidhiy (65), An-Nasaaiy (1/173) na Ibn Maajah (370). Baadhi ya Maulamaa wameitia ila kwa riwaya ya Simaak toka kwa ‘Ikrimah. Riwaya hii imekorogeka. Lakini Al-Haafidh katika kitabu cha Al-Fat-h amewajibu kwamba Shu-’ubah amepokea toka kwake, na yeye hapokei toka kwa Mashaykh zake isipokuwa Hadiyth Swahiyh.. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi].



3- Imepokelewa toka kwa Mama wa Waumini ‘Aaishah aliyesema: “Nilikuwa mimi na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tukioga katika chombo kimoja nailhali wote tuna janaba)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (299) na Muslim (321)].

Na katika riwaya nyingine: ((…wote tunachota humo)).





Lenye Nguvu:



Lenye kuridhisha na kuondosha shaka katika dalili za mwelekeo wa kwanza ni Hadiyth ya mtu aliyesuhubiana na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa miaka minne (ingawa Al-Bayhaqiy ameitia ila) pamoja na dalili zote za mwelekeo wa pili. Na dalili hizo zinaweza kuoanishwa kwa moja ya mawili: [Fat-hul Baary (1/300- Al Ma-’arifah), Subulus Salaam (1/28), na Naylul Awtwaar (1/26)].

1- Hadiyth zinazokataza zichukuliwe juu ya maji yanayochuruzika toka kwenye viungo, na Hadiyth za kujuzisha zichukuliwe juu ya maji yenye kubaki ndani ya chombo. Hivi ndivyo Al-Khatwaabiy alivyooanisha.



2- Katazo lichukuliwe juu ya ukaraha pamoja na kujuzu yote mawili.



Ninasema: “Na huenda hili la pili ndilo bora zaidi. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi".
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



025-Wudhuu Taarifu Yake Na Dalili Ya Usharia Wake



Alhidaaya.com







Ama kiistilahi (kitaaluma), ni kutumia maji kwenye viungo maalumu; uso, mikono miwili, kichwa na miguu miwili, ili kuondosha kwayo kinachozuia kuswali na mfano wake.

Uthibiti wake umeashiriwa na Qur-aan, Hadiyth na Ijma’a. Ama katika Qur-aan, Allaah Mtukufu Anasema:



((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ ۚ))

((Enyi walioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah, basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni)). [Al-Maaidah (5:6)].





Ama katika Hadiyth, tunakuta kama vile:



1- Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake) aliyesema: “Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):



((لا تقبل صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ))

((Haikubaliwi Swalaah ya yeyote kati yenu anapokuwa na hadathi mpaka atawadhe)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (135), Muslim (225) na wengineo].

2- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Umar akisema: “Hakika nilimsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:



((لا يقبل الله صلاة بغير طهور، ولا صدقة من غلول))

((Allaah Haikubali Swalaah bila twahara, wala swadaqah ya mali haramu)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (224).





3- Imepokelewa toka kwa Ibn ‘Abbaas akisema: “Amesema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((إنما أمرت بالوضوء إذا قمت إلى الصلاة))


((Hakika mimi nimeamrishwa kutawadha ninaposimama kuswali)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhy (1848), Abuu Daawuud (3760) na An-Nasaaiy ((1/73). Angalia kitabu cha Swahyhul Jaami’i (5761)].





4- Imepokelewa toka kwa Abuu Sa’iyd kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((مفتاح الصلاة الطهور، وتحريمها التكبير، وتحليلها التسليم))

((Ufunguo wa Swalaah ni kujitwaharisha, uingio wake ni Takbiyr, na utokaji wake ni kusema “Assalaamu ‘alaykum wa RahmatuLlaah”)). [Hadiyth Hasan Lighayrih. Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhy (3), Abuu Daawuud ((60) na Ibn Maajah (275). Al- Albaany katika Swahiyhul Jaami’i ameizingatia kama ni Swahiyh].





Ama Ijma’a, ni kuwa Maulamaa wa Ummah wamekubaliana kwamba Swalaah haikamiliki ila kwa twahara kama itakuwa ni wepesi kufanya hivyo. [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (1/107)].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



026-Fadhla Za Wudhuu



Alhidaaya.com







1- Ni kama nusu ya iymaan:





Ni kama katika Hadiyth ya Abuu Maalik Al-Ash‘ariy (Radhi za Allaah ziwe juu yake) aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:



((الطهور شطر الايمان))



((Twahara ni nusu ya iymaan)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (223) na wengineo.]





2- Hufuta madhambi madogo madogo:





(a) Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((إذا توضأ العبد المسلم – أو المؤمن – فغسل وجهه خرج من وجهه كل خطيئة نظر إليها مع قطر الماء – أو مع آخر قطر الماء-، فإذا غسل يديه خرجت من يديه كل خطيئة كان بطشتها يداه مع الماء – أو مع آخر قطر الماء – فإذا غسل رجليه خرجت كل خطيئة مشتها رجلاه مع الماء – أو مع آخر قطر الماء – حتى يخرج نقيا من الذنوب))

((Anapotawadha mja Muislamu – au Muumini – akauosha uso wake, hutoka katika uso huo pamoja na matone ya maji kila kosa la kuangalia – au pamoja na tone la mwisho la maji - , na anapoosha mikono yake miwili, hutoka katika mikono hiyo pamoja na maji, kila kosa ambalo mikono yake imetumilia nguvu – au pamoja na tone la mwisho la maji - , na anapoosha miguu yake miwili, hutoka pamoja na maji kila kosa ambalo miguu yake ililiendea – au pamoja na tone la mwisho la maji, mpaka hutoka akiwa ametakasika kabisa na madhambi)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (244) na wengineo].



(b) Imepokelewa toka kwa ‘Uthmaan (Radhi za Allaah ziwe juu yake) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((من توضأ هكذا غفر له ما تقدم من ذنبه، وكانت صلاته ومشيه إلى المسجد نافلة))

((Mwenye kutawadha hivi, husamehewa dhambi zake zilizopita, na Swalaah yake na kwenda kwake Msikitini huwa ni thawabu ziada. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (229) na wengineo].





Fadhila na thawabu hizi hupatikana kwa uhakika zaidi kwa mwenye kuswali moja kwa moja Swalaah ya faradhi au ya Sunnah baada ya kutawadha.



(c) Katika Hadiyth ya ‘Uthmaan akizungumzia namna wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ulivyo, anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:



((من توضأ مثل وضوئي هذا ثم قام فصلى ركعتين لا يحدث فيهما نفسه، غفر له ما تقدم من ذنبه))

((Mwenye kutawadha kama ninavyotawadha mimi hivi, kisha akasimama akaswali rakaa mbili, haizungumzishi nafsi yake ndani yake, ila hufutiwa dhambi zake zilizotangulia)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (6433), Muslim (226) na wengineo].





3- Hunyanyua daraja za mja:



Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((ألا أدلكم على ما يمحو الله به الخطايا ويرفع به الدرجات؟)) قالوا: بلى يا رسول الله! قال: ((إسباغ الوضوء على المكاره، وكثرة الخطا إلى المساجد، وانتظار الصلاة بعد الصلاة، فذلكم الرباط، فذلكم الرباط، فذلكم الرباط))

((Je, niwaambieni lile ambalo kwalo Allaah Huyafuta makosa na Hunyanyua kwalo daraja? Wakasema: “Tuambie, ee Rasuli wa Allaah! Akasema: Kutawadha kikamilifu pamoja na kuwepo uzito na ugumu, kukithirisha hatua kwenda Msikitini, na kusubiri Swalaah baada ya Swalaah, basi hayo ni mambo ya mtu kujifunga nayo, basi hayo ni mambo ya mtu kujifunga nayo, basi hayo ni mambo ya mtu kujifunga nayo)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (251) na wengineo].





4- Ni njia ya kuelekea peponi:



(a) Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Allaah iwe juu yake) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Bilaal:



(( يا بلال! حدثني بأرجى عمل عملته فى الاسلام، إني سمعت دف نعليك بين يدي في الجنة)). قال : ((ماعملت عملا أرجى عندي من أني لم أتطهر طهورا في ساعة من ليل أو نهار إلا صليت بذلك الطهور ما كتب لي أن أصلى))

((Ee Bilaal! Nielezee amali yenye matarajio zaidi uliyoifanya katika Uislamu, kwani mimi nimesikia mtaharuki wa viatu vyako mbele yangu huko peponi)).

Bilaal akasema: “Sikufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa kwangu zaidi ya kuwa sikupata kujitwaharisha wakati wowote wa usiku au mchana, ila huswali kwa twahara hiyo kile nilichoandikiwa kukiswali”. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (1149), Muslim (2458) na wengineo].





(b) Imepokelewa toka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (Radhi za Allaah ziwe juu yake) akisema: “Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:



((من توضأ فأحسن الوضوء ثم صلى ركعتين، يقبل عليهما بقلبه ووجهه، وجبت له الجنة))

((Mwenye kutawadha, akaukamilisha vyema wudhuu wake kama inavyotakikana, kisha akaswali rakaa mbili, akafanya khushui kwa moyo wake na uso wake (viungo vyake), basi ni lazima aingie peponi)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (234) An-Nasaaiy (1/80) na wengineo].





(5) Utakuwa ni alama itakayoupambanua Ummah huu wakati wa kupita kwenye hawdh:





Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikwenda makaburini akasema:



((السلام عليكم دار قوم مؤمنين وإنا- إن شاء الله- بكم عن قريب لاحقون، وددت لو أنا قد رأينا إخواننا)) قالوا: أو لسنا إخوانك يا رسول الله؟ قال: ((أنتم أصحابي، وإخواننا الذين لم يأتوا بعد)) فقالوا: كيف تعرف من لم يأت من أمتك يا رسو ل الله؟ قال: (( أرأيت لو أن رجلا له خيل غر محجلة بين ظهري خيل دهم بهم ألا يعرف خيله؟)) قالوا: بلى يا رسول الله، قال: ((فإنهم يأتون غرا محجلين من الوضوء، وأنا فرطهم على الحوض، ألا ليذادن رجال عن حوضى كما يذاد البعير الضال أناديهم ألا هلم فيقال: إنهم قد بدلوا بعدك، فأقول: سحقا سحقا))



((Amani iwe juu yenu nyumba ya jamaa ya Waumini. Na sisi bila shaka Apendapo Allaah tutakuwa nanyi hivi karibuni. Ningependa lau sisi tungeliwaona ndugu zetu)). Wakasema: “Ee Rasuli wa Allaah! Je, sisi sio ndugu zako”? Akasema:

((Nyinyi ni Maswahaba zangu. Ama ndugu zangu, hao ni wale ambao hawajakuja bado)). Wakasema: “Ni vipi utamtambua yule ambaye bado hajakuja katika umati wako ee Rasuli wa Allaah?”. Akasema: ((Niambieni, lau kama mtu ana farasi wenye alama usoni na miguuni wakawa baina ya farasi weusi wasio na mabaka, je hawezi kuwatambua farasi wake?)). Wakasema: “Ndio, atawatambua ee Rasuli wa Allaah”. Akasema: ((Basi wao watakuja nailhali wana nuru nyusoni, miguuni na mikononi kutokana na wudhuu. Na mimi ndiye nitakayewatangulia kwenye hawdh. Basi jueni kwa yakini kwamba watu watazuiliwa na kufukuzwa wasije kwenye hawdh langu kama wanavyozuiliwa ngamia wasio na mchunga. Nitawaita: Haya njooni! Patasemwa: “Hakika hao walibadili baada yako”. Nitawaambia: Poteleeni mbali kabisa)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (234), An-Nasaaiy (1/80) na wengineo].





(6) Ni nuru kwa mja siku ya Qiyaamah:



Imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake) akisema: “Nimemsikia Kipenzi changu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:



((تبلغ الحلية من المؤمنين حيث يبلغ الوضوء))

((Nuru ya Waumini itafikilia pale wudhuu unapofikilia)).







(7) Unafungua kifundo cha shaytwaan:



Imepokelewa toka kwa Abuu Hurayrah (Radhi za Allaah ziwe juu yake) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((يعقد الشيطان على قافية رأس أحدكم إذا هو نام ثلاث عقد يضرب كل عقدة: عليك ليل طويل فارقد، فإن استيقظ فذكر الله انحلت عقدة، فإن توضأ انحلت عقدة، فإن صلى انحلت عقدة، فأصبح نشيطا طيب النفس، وإلا أصبح خبيث النفس كسلان))

((Anapolala mmoja wenu, shaytwaan hufunga kisogoni mwake vifundo vitatu. Hupiga kila kifundo (kumwambia): Umebakiwa na usiku mrefu, basi lala. Anapoamka akamtaja Allaah, kifundo kimoja hufunguka. Anapotawadha, hufunguka kingine, na anaposwali cha tatu hufunguka. Hapo huwa mchangamfu na mwenye nafsi nzuri, na kama si hivyo, huwa na nafsi mbaya na mvivu)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (1142) na Muslim (776)].
 
TUENDELEZE YALE MAZURI AMBAYO TUMEYAFANYA KATIKA MWEZI MZIMA WA RAMADHANI

Naam ndugu zanga katika imani hatuna budi kumshukuru Allah azza wa jallah kwa kutuwezesha kumaliza salama mfungo wa Ramadhani,kuna ambao tuliokuwa nao lkn leo hii hawapo tena katika mgongo wa ardhi

Kuwepo kwetu hai si kwamba tunampendeza sana Allah au ni wacha mungu sana,na wale walio tangulia mbele ya haki si kwamba ni wenye dhambi sana au walimkosea Allah,laa! Ila wakati wao ulifika ikabidi waende kwa Allah

Nasi huenda leo au kesho au kesho kutwa tukawa katika hiyo safar ambayo hakuna ambaye ataikwepa,je tumebeba zawadi gani kwa ajili ya Allah? Hakika kila nafsi inajua inayoyachuma kwa ajili ya akhera yake

Kikubwa tushikamane na Sala tano,tufanye dhikri kwa wingi na ibadati nyingine mbali mbali ambazo zitatuweka karibu sana na Allah mtukufu na kujiwekea akiba ya matendo mazuri ambayo yatakuwa ni sababu ya kupata rehma ya Allah mtukufu

Tukumbuke sana kikata starehe ambayo ni mauti, je tutakufa katika namna ipi na hali ipi? Ni juu yetu kuandaa akhera yetu

Allah anasema "enyi mlioamini msife hali ya kuwa ni waislamu"
Hapa haimaanishi ufe na jina lako la kiislamu laa,ila ufe hali ya kuwa unafuata maamrisho yote ya Allah na kuacha makatazo yake

Eid Mubarak!
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



027-Sifa Ya Wudhuu Uliokamilika (Kiujumla)



Alhidaaya.com





Imepokelewa toka kwa Humraan mwachwa huru wa ‘Uthmaan kwamba alimwona ‘Uthmaan bin ‘Affaan akiagiza chombo, kisha akamimina juu ya viganja vyake mara tatu na kuviosha. Kisha akauingiza mkono wake wa kuume kwenye chombo, akasukutua na kupaliza maji puani. Kisha akaosha uso wake mara tatu, na mikono yake hadi kwenye viwiko mara tatu. Halafu akapukusa kichwa chake, kisha akaosha miguu yake mara tatu hadi kwenye vifundo, kisha akasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

(( من توضأ نحو وضوئي هذا، ثم صلى ركعتين لا يحدث فيهما نفسه، غفر له ما تقدم من ذنبه))

((Mwenye kutawadha mfano wa wudhuu wangu huu, kisha akaswali rakaa mbili, haizungumzishi nafsi yake ndani yake, hughufiriwa madhambi yake yaliyopita)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (158) na Muslim (226)].





Na kutokana na Hadiyth hii na nyinginezo zitakazokuja kuzungumziwa kwa ufafanuzi, tunaweza kuiweka sifa ya wudhuu katika haya yafuatayo:





1-Atanuwia wudhuu kwa ajili ya kuondosha hadathi.



2-Atalidhukuru Jina la Allaah Mtukufu.



3-Ataviosha viganja vyake mara tatu.



4-Atateka maji kwa mkono wake wa kuume, kisha atayaweka mdomoni na puani kwa teko moja, atasukutua na kupaliza.



5-Atapenga kwa kutumia mkono wake wa kushoto. Atafanya hivi mara tatu.



6-Ataosha uso wake wote mara tatu pamoja na kupachanyisha ndevu.



7-Ataiosha mikono yake miwili – wa kulia kisha wa kushoto – mpaka juu ya viwiko viwili pamoja na kupachanyisha vidole vya mikono miwili.



8-Atapukusa kichwa chake chote kwenda nyuma na mbele mara moja.



9-Atapukusa masikio yake mawili nje na ndani.



10-Ataosha miguu yake miwili pamoja na vifundo vyake viwili - wa kulia kisha wa kushoto - pamoja na kupachanyisha vidole vya miguu miwili.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



028-Niya Ni Sharti Ya Kuswihi Wudhuu



Alhidaaya.com





[Sharti ni jambo ambalo kutokuwepo kwake hulazimisha kutokuwepo, na kuwepo kwake hakulazimishi kuwepo au kukosekana kwa dhati yake. Sharti ni lazima iwepo kabla ya kitendo nje ya uhalisia wake].



Ili wudhuu uwe sahihi, ni lazima pawepo niya. Niya ni kuazimia kwa moyo juu ya kufanya tendo la kutawadha kwa ajili ya kufuata Maagizo ya Allaah Mtukufu na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama ilivyo kwenye ‘ibaadah nyinginezo za kisharia. Allaah Mtukufu Anasema:

(( وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ))

(( Na hawakuamrishwa isipokuwa kumwabudu Allaah huku wakimtakasia Dini na kuwa mbali na shirki)). [Al Bayyinah (98:5)]





Na Rasuli ((Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

(( إنما الأعمال بالنيات، وإنما لكل امرء ما نوى...))

((Hakika matendo ni kwa niya, na kila mtu ni kwa lile alilolinuwiya..)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (1) na Muslim (1907)].



Huu ndio msimamo walioukhitari Maalik, Ash Shaafi’iy, Ahmad, Abuu Thawr na Daawuud. [“Bidaayatul Mujtahid” (1/6), “Al-Majmuu” (1/374), na “At-Tamhiyd” (22/100,101)].



Lakini Abuu Haniyfah msimamo wake ni kuwa niya si sharti kwa ajili ya wudhuu, kwa kuwa wudhuu ni ‘ibaadah ya kidhahania na wala haikusudiwi kwa dhati yake. [Badaai’u Asw Swanaai-’i” (1/19 – 20)].



Mfano wake ni kama kutwaharisha uchafu. Kauli ya Jamhuri ya Maulamaa ndio sahihi kwa kuwa matni inatutaarifu kuwa thawabu zinapatikana katika kila wudhuu, na kwamba thawabu hazipatikani kwa kisichonuwiliwa kwa Ijma’a, na kuwa wudhuu ni ‘ibaadah ambayo haijulikani ila kwa sharia. Na kwa ajili hiyo, niya imekuwa ni sharti. [Al-Furu’u” cha Muflih (1/111)].



Mahala Pa Niya Ni Moyoni



Shaykh wa Uislamu (Allaah Amrehemu) anasema: [Majmuuat Ar-Rasaail Al-Kubraa (1/234)].

“Mahala pa niya ni moyoni na si katika ulimi kwa makubaliano ya Maimamu wa Kiislamu katika ‘ibaadah zote; twahara, Swalaah, Zakaat, Swaum, Hajji, kuacha huru mtumwa, Jihaad na kadhalika”.



Hakuna usharia ya kuitamka kwa sauti au kuikariri. Aliyezoea kufanya hivyo na hususan kama anawaudhi watu, inatakikana atiwe adabu au afanyiwe izari lakini baada ya kueleweshwa. Mwenye kuitamka niya, ni mkosa, na lau kama ataitakidi kwamba kuitamka ndio dini na ‘ibaadah kwa Allaah, basi huyo amezua. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba Zake hawakuwa wakiitamka niya kabisa, na hilo halikurekodiwa kutoka kwao. Na lau kama lingekuwa ni jambo la kisharia, basi Allaah Angelibainisha kupitia kwa Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Mbali ya hivyo, hakuna haja ya kuitamka niya, kwa kuwa Allaah Anaijua. [Angalia Zaadul Ma’aad (1/196), Ighaathat Al-Lahafaan (1/134), Badaai’ul Fawaaid (3/186), Al-Furu’u (1/111) na Sharhul Mumti-’i (1/159)].



Faida



1- Shaykh wa Uislamu anasema:

“Lau kama atatamka kwa ulimi wake kinyume na alichonuwia moyoni, kinachozingatiwa ni kile alichokinuwia na si alichokitamka. Na lau kama atatamka kwa ulimi bila kunuwia moyoni, basi hilo halitosihi kwa makubaliano ya Maimamu wa Kiislamu, kwa kuwa niya ndio makusudio na azima yenyewe”.





2- Hadathi zinazowajibisha kutawadha zikikusanyika pamoja kama mtu kwenda haja ndogo, kisha kubwa, halafu akalala, ikiwa atanuwia kuondosha moja tu kati ya hizo, basi zote zitaondoka – kwa kauli sahihi – kwa kuwa hadathi wasifu wake ni mmoja ingawa sababu zake ni tofauti. [Angalia Al-Majmu’u (1/385) na Ash Sharhul Mumti’i (1/165)].





3- Ni vyema kwa mwenye kutawadha anuwie kuondosha hadathi tu ili kuepukana na mahitilafiano ya Maulamaa katika kujuzisha baadhi ya picha za niya pasina nyinginezo. Picha hizi ni kunuwia kuondosha hadathi, au kunuwia twahara kwa lililo wajibu kwake, au kunuwia twahara kwa lililo sunna kwake, au kunuwia kujadidisha wudhuu kulikosuniwa. [Angalia namna Maulamaa walivyokhitilafiana katika masuala haya katika kitabu cha Al-Majmu’u (1/385)].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



029-Nguzo Za Wudhuu







Nguzo za wudhuu ni mambo ambayo uhakika wake unajengekea kwayo kwa namna ambayo ikikosekana nguzo yoyote kati yake, basi wudhuu unabatilika na unakuwa hauzingatiwi kisharia. Nguzo hizo ni:



1- Kuosha uso wote:



Uso ni sehemu ya makabiliano. Na mpaka wake ni kutokea kwenye mapindio ya kipaji cha uso (au tokea kwenye maoteo ya kawaida ya nywele) mpaka kwenye mashukio ya ndevu na kidevu kwa urefu, na tokea kwenye sikio hadi sikio jingine kwa upana.

Kuosha uso ni nguzo kati ya nguzo za wudhuu. Wudhuu hautoswihi bila ya nguzo hii kwa neno Lake Subhaana:

((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ ))



(( Enyi walioamini! Mnaposimama kuswali, basi osheni nyuso zenu)). [Al Maaidah 5:6]

Kila aliyehadithia sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), amethibitisha kuoshwa uso. Na Maulamaa wote wamekubaliana juu ya hili.



Ni Lazima Kusukutua Na Kupaliza:



Kusukutua ni kusafisha mdomo na kuyazungusha maji ndani yake. Na kupaliza, ni kuyafikisha maji mpaka ndani ya pua na kuyavuta kwa pumzi hadi mwisho wake. Ama kupenga, ni kuyatoa maji puani (kwa mpumuo) baada ya kuyapaliza.



Kusukutua na kupaliza maji, ni mambo ya lazima wakati wa kutawadha kwa mujibu wa kauli sahihi zaidi za Maulamaa. Na hii ni kwa dalili zifuatazo:



1- Ni kwamba Allaah Mtukufu Ameamuru kuosha uso kama ilivyotangulia. Na pua na mdomo ni sehemu ya uso, na wala hakuna chenye kuwajibisha kuhusisha nje yake bila ndani yake, kwani vyote hivyo viwili vinaitwa “uso” katika Lugha ya Kiarabu. Na kama utasema: “Tundu ya pua ina jina lake na pua ina jina lake, na hivyo haviitwi uso katika Lugha ya Kiarabu”, tunajibu tukisema: “Vilevile vitefute viwili, kipaji, mgongo wa pua, nyusi mbili na sehemu nyingine za uso, zina majina yake, na hivyo haviitwi uso! Huku ni kujikwaa kubaya, kwa kuwa kutamaanisha kwamba si lazima kuosha uso”. [Angalia Naylul Awtwaar (1/174) chapa ya Al-Jiyl na Ahkaamul Qur-aan cha Ibnul ‘Araby (2/563)].





2- Ni kwamba Allaah Mtukufu Ameamuru kuosha uso kiujumla, na Rasuli alilifasiri hilo kwa kulifanya kivitendo na kulifundisha. Akasukutua na akapaliza maji katika kila wudhuu aliotawadha. Na hakuna yeyote aliyenukulu kuwa aliacha kufanya hayo pamoja na kufupishia kwake juu ya kichache chenye kutosheleza. Na ikiwa kitendo chake kimefanyika kwa ajili ya kufuata amri, basi hukmu yake inakuwa ni hukmu ya jambo hilo katika kuhukumia ulazima. [Sharhul ‘Umdah cha Ibn Taymiyah (1/178) na At-Tamhiyd cha Ibn ‘Abdul Barri (4/36)].





3- Amri ya kupaliza na kupenga imethibiti kutokana na neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((من توضأ فليستنثر))

((Mwenye kutawadha, basi apenge)).



Na katika riwaya nyingine:



((إذا توضا أحدكم فليجعل في أنفه ماء ثم ليستنثر))

((Anapotawadha mmoja wenu, basi aingize maji puani mwake kisha apenge)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (161), Muslim (237) na wengineo].



Na kauli yake:



(( إذا توضأ أحدكم فليستنشق..))

((Anapowatadha mmoja wenu, basi apalize maji puani)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (237)].



Na kauli yake:



(( وبالغ في الاستنشاق إلا أن تكون صائما..))

((na ubalighishe katika kupaliza isipokuwa kama umefunga)).[Hadiyth Swahiyh. Itakariri mara nyingi].



Shaykh wa Uislamu anasema: “…Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoa amri maalumu ya kupaliza, hakumaanishi kwamba ni muhimu zaidi kuliko kusafisha mdomo. Itawezekana vipi nailhali mdomo ndio sehemu tukufu zaidi ya kufanyia dhikri na kusoma, na mara nyingi hubadilika na kuwa na harufu mbaya?! Lakini kinachofananishwa hapa - na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi – ni kuwa, mdomo ulipowekewa usharia wa kupigwa mswaki na jambo hilo likasisitizwa, na pia kuuosha kabla na baada ya kula, itakuwa imejulikana kuwa Allaah Mtukufu Ametoa kipaumbele zaidi cha kuusafisha kinyume na pua ambayo imetajwa kwa ajili ya kubainisha hukmu yake ili isipuuzwe…”. [Sharhul ‘Umdah (1/179 – 180)].





4- Ni kwamba amri ya kusukutua imekuja vile vile katika Hadiyth nyinginezo zenye uhakika zaidi. Ni kama Hadiyth ya Laqyt bin Swabrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



(( إذا توضأت فمضمض))

((Ukitawadha, basi sukutua)).



Ninasema: “Na lau kama mtu atasema kwamba dalili za kuwajibisha kusukutua na kupaliza zimegeuzwa na kuelekezwa katika Sunnah kutokana na Hadiyth ya Rifa’a bin Raafi’i katika kisa cha mwenye kuswali vibaya ambaye Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia:



(( إنها لا تتم صلاة أحدكم حتى يسبغ الوضوء كما أمره الله تعالى، فيغسل وجهه ويديه إلى المرفقين ويمسح رأسه ورجليه إلى الكعبين...))

((Hakika haikamiliki Swalaah ya mmoja wenu mpaka akamilishe wudhuu wake kama Alivyoamrisha Allaah. Aoshe uso wake na mikono yake miwili hadi kwenye vifundo, na apake kichwa chake, na (aoshe) miguu yake miwili hadi kwenye vifundo…)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (859), At Tirmidhy (302), An Nasaaiy (2/20, 193) Ibn Maajah (460) na wengineo].



Hapa hakutaja kusukutua au kupaliza katika hayo ambayo Allaah Amemwamuru, na kwa hivyo amekwenda sawa na Aayah Tukufu. Hoja hii pia ni madhubuti na makinifu. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi".





Faida



Fahamu kwamba Wanazuoni wamehitalifiana juu ya hukmu ya kusukutua na kupaliza katika wudhuu na kuoga katika kauli nne. [Ikhtilaaful ‘Ulamaa cha Al-Muruuziy (uk. 23-24), At-Tamhiyd (4/34), Al-Awsatw (1/379), At-Tahqiyq cha Ibn Al-Jawziy (1/143) na Al-Muhalla (2/50)].



Kauli ya kwanza:



Ni wajibu kusukutua na kupaliza wakati wa kuoga tu, lakini kwa wudhuu haipasi. Yamesemwa haya na Ath-Thawriy, Abu Haniyfah na wenzake na wengineo.



Kauli ya pili:



Ni Sunnah wakati wa kuoga na kutawadha. Haya yamesemwa na Maalik, Ash-Shaafi’iy, Al-Layth, Al-Awzaa’iy na jama‘ah.



Kauli ya tatu:



Yote mawili ni wajibu wakati wa kuoga na kutawadha. Haya yamesemwa na ‘Atwaa, Ibn Jurayj, Ibn Mubarak, Is-Haaq na riwaya iliyonukuliwa toka kwa Ahmad. Suala hili ni mashuhuri katika madhehebu ya Hanbali.



Kauli ya nne:



Kupaliza ni wajibu wakati wa kuoga na kutawadha, lakini kusukutua ni Sunnah. Yamesemwa haya na Ahmad katika riwaya, Abu ‘Ubayd, Abu Thawr na jopo la Maulamaa wa Hadiyth. Ibn Al-Mundhir ameichagua kauli hii.



Kuosha Ndevu Na Nywele Nyingine Za Uso



[Sharhu Fat-hil Qadiyr (1/12), Al-Mughniy (1/87) na Al-Majmuu’i (1/380)].

Ikiwa nywele zilizoota usoni (ndevu, masharubu, kilambamchuzi, kope na nyusi) ni nyingi kiasi ambacho ngozi inakuwa haionekani, basi itatosheleza kuosha juu yake tu. [Kilambamchuzi ni nywele zinazoota kati ya mdomo wa chini na kidevu].



Na kama ngozi inaonekana, basi itabidi ipate maji. Na ikiwa baadhi ni ndogo na nyingine ni nyingi, basi ni lazima ngozi ya nywele ndogo ipate maji na yenye nywele nyingi ioshwe juu tu.

Ama ndevu refu za singa, si lazima kuziosha zile zilizoshuka, bali inatosheleza kuosha zile tu zilizo katika mpaka wa uso, kwa vile kinachokusudiwa katika uso ni ngozi basi. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Abuu Haniyfah na riwaya toka kwa Ahmad.



Ama kwa mujibu wa Ash-Shaafi’iy na madhehebu ya Ahmad, ni lazima kuosha nywele singa vyovyote zitakavyokuwa zimeshuka, kwani nywele hizo zimeota katika mahali pa faradhi, na kwa ajili hiyo zinaingia katika wigo wa vyenye kuonekana. Na rai hii ina nguvu zaidi. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.





2- Kuosha mikono miwili hadi kwenye vifundo



Allaah Mtukufu Anasema:



(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلاةِ فاغْسِلُواْ وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ))

(( Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah, basi osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka vifundoni )).[Al Maaidah (5:6)].



Maulamaa wamekubaliana kwa sauti moja kuwa ni lazima kuosha mikono miwili wakati wa kutawadha.



Fahamu kuwa herufi ya )) (( إلىkatika Neno Lake Allaah Mtukufu:



(( أَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ ))

mikono yenu mpaka vifundoni



..ina maana ya “pamoja” kama ilivyo katika Neno Lake Allaah Mtukufu:



((وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَهُمْ إِلَىٰ أَمْوَالِكُمْ ))

(( Na wala msile mali zao pamoja na mali zenu)). [An Nisaa (4:2)].



Na Neno Lake:



((وَيَزِدْكُمْ قُوَّةً إِلَىٰ قُوَّتِكُمْ))

(( Na Atawaongezeeni nguvu pamoja na nguvu zenu)). [Huud (11:52].



Al Mubarrid amesema: “Ikiwa mpaka unatokana na jinsi ya chenye kuwekewa mpaka, basi nao huingia”.



Na kwa ainisho hili, ni lazima vifundo viwili vijumuishwe wakati wa kuosha mikono. Na haya ndio madhehebu ya Jamhuri ya Maulamaa kinyume na baadhi ya wafuasi wa madhehebu ya Maalik. [Al-Mabswuut (1/6), Bidaayatul Mujtahid (1/11), Al-Majmu’u (1/389), na Al-Mughny (1/90)].



Msimamo huu wa Jamhuri ya Maulamaa unatiliwa nguvu na kitendo cha Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Imenukuliwa toka kwa Abuu Hurayrah kwamba yeye alitawadha, akaosha mikono yake hata akaingia katika kipanya, na akaosha miguu yake mpaka akaingia katika miundi miwili. Kisha alisema: “Hivi ndivyo nilivyomwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitawadha.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (246)].



Kisha kaida ‘qaaidah’ (kanuni) inasema: “Lile ambalo wajibu hautimu ila kwalo, basi linakuwa ni wajibu”. Na kuosha mkono kikamilifu hakutojulikana ila kwa kuyazungusha maji kwenye vifundo viwili. [Ikhtiyaarat Ibn Qudaamah cha Al-Ghaamidiy (1/164)].





3- Kupaka kichwa



Allaah Mtukufu Anasema:



(( وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ ))

(( Na pakeni vichwa vyenu)). [Al Maaidah (5:6)]

.

Maulamaa wamekubaliana kwa sauti moja kuwa kupaka maji kichwani ni lazima. Lakini hata hivyo wamehitalifiana juu ya kiasi kinachotosheleza upakaji huo katika kauli tatu:



Kauli ya kwanza:



Ni lazima kupaka kichwa chote maji sawasawa kwa mwanamke au kwa mwanamume.

Haya ni madhehebu ya Maalik na Dhwaahir. Pia ni madhehebu ya Ahmad na kundi la wenzake, Abu ‘Ubayd na Ibn Al-Mundhir. Na Ibn Taymiyah ameuridhia msimamo huu. [Al-Mudawwanah (1/16), Al-Mughniy (1/92), Atw-Twahuur (uk. 358), Al-Awsatw (1/399) na Majmuu’i Al-Fataawa (21/123)].



Ushahidi wao ni haya yafuatayo:



1- Ni Neno Lake Allaah Mtukufu:



((وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ))

((Na pakeni vichwa vyenu))



Hapa “ب baa” ni ya kuambatisha (si ya usehemu). Kwa hiyo makadirio ya Aayah yanakuwa ni:



((وَامْسَحُوا رُءُوسِكُمْ))

Hii ni kama kuosha uso katika tayammum, kwani vyote katika Qur-aan Tukufu vimekuja kwa tamko moja. Allaah Anasema:



((فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُم))

((Na mwoshe nyuso zenu)). [Al Maaidah (5:6)] yaani uso wote.





2- Ni kwamba jambo hili limefasiriwa na Sunnah iliyonukuliwa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ni kuwa, yeye alipotawadha, alikuwa akipaka kichwa chake chote. Na kati ya yanayothibitisha hili, ni Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zayd aliyesema: “Alitujia sisi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tukamtolea maji katika ndoo ya shaba. Akatawadha; akaosha uso wake mara tatu, akaosha mikono yake mara mbili hadi katika vifundo, akapaka maji kichwani kwa kupeleka mkono mbele na nyuma na akaosha miguu yake miwili”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (185) na Muslim (235)].



Na katika tamko jingine “akapaka kichwa chake chote”.





3- Ni Hadiyth ya Al-Mughiyrah bin Shu’ubah aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha, akapukusa juu ya khufu zake, mbele ya utosi wake na juu ya kilemba chake”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (275), Abuu Daawuud (150) na At-Tirmidhy (100). Hadiyth hii imejadiliwa sana. Na Al-Albaany Allaah Amrehemu, amesema kuwa ni Swahiyh].



Na lau kama ingetosheleza kupukusa mbele ya utosi, basi asingelipukusa juu ya kilemba. Kwa hivyo, hilo limeonyesha kuwa ni lazima kueneza (kichwa kizima).





Kauli ya pili:



Inatosheleza kupaka sehemu ya kichwa.



Ni madhehebu ya Abu Haniyfah na Ash-Shaafi’iy. [Al-Mabswuut (1/8), Al-Majmu’u (1/399), na Al-Mughny (1/92)].



Lakini pamoja na hivyo, wao wamehitalifiana juu ya kiasi kinachotosheleza. Wamesema ni nywele tatu, au robo ya kichwa au nusu!! Na hoja yao ni:



1- Kwamba “ب baa” katika Neno Lake Allaah Mtukufu:



((وَامْسَحُوا برُءُوسِكُمْ))

((Na pakeni vichwa vyenu)),

ni ya sehemu na si ya kuambatisha.



2- Yale yaliyopokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kuwa alipaka katika utosi wake.





Kauli ya tatu:



Ni lazima kupaka kichwa chote kwa mwanamume tu, si kwa mwanamke.



Ni riwaya iliyonukuliwa toka kwa Ahmad. Amesema: “Ninataraji kupaka maji kichwani kwa mwanamke kuwe ni sahali zaidi. ‘Aaishah (Allaah Amridhie) alikuwa akipaka mbele ya utosi wake.





Ibn Qudaamah anasema: “Na Ahmad ni katika mabingwa wa Hadiyth. Na hatolei dalili kwa tukio la kitu ila kama limethibiti kwake kwa Uwezo wa Allaah”. [Al-Mughny (1/93)].



Ninasema: “Ninaloliona lenye nguvu katika hayo yaliyotangulia ni kuwa ni lazima kupaka maji kichwa chote wakati wa kutawadha kutokana na nguvu ya hoja zake. Ama wale waliosema kuwa “ب baa” katika Aayah ni ya usehemu, basi hilo Siybawayhi amelikanusha katika sehemu kumi na tano katika kitabu chake. Na Ibn Burhan amesema: “Mwenye kudai kwamba “ب baa” inaonyesha usehemu, basi atakuwa amewaletea mabingwa wa Lugha jambo wasilolijua. [Naylul Awtwaar (1/155) na Al-Mughny (1/87)].



Mbali ya hivyo, hakuna Hadiyth yoyote Swahiyh toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayoeleza kuwa yeye alifupishia kupaka baadhi ya kichwa chake tu. Lililothibiti ni kuwa yeye alipokuwa akipaka utosi wake, alikamilishia juu ya kilemba. [Majmu’u Al-Fataawa (21/122), Ahkaam Al-Qur-aan cha Ibn Al-‘Arabiy (2/571) na Subul As-Salaam (1/107)].



Ama mwanamke, mimi siijui dalili yoyote ya kumbagua yeye na mwanamume katika hilo. Lakini inajuzu kwake kupaka maji juu ya mtandio wake. Na lau kama amepaka utosi wake pamoja na mtandio wake, basi hilo litakuwa ni bora ili kuepukana na mvutano. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi”.



Faida



Ikiwa kichwa kimepakwa hina ghafi au mfano wake, itajuzu kupaka maji juu yake. Kwani imethibiti toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba yeye alikuwa akikipaka kichwa chake hina akiwa katika ihramu yake na hakuwa akijisumbua kuitoa kwa ajili ya wudhuu (kama itakavyokuja katika mlango wa Hijjah). Hii ni kwa vile kilichowekwa kichwani kinakuwa ni sehemu ya kichwa. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.





4- Kupaka masikio mawili:



Ni lazima kupaka masikio mawili pamoja na kichwa, kwani masikio ni sehemu ya kichwa. Imepokelewa toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba amesema:



(( الأذنان من الرأس ))

((Masikio mawili ni sehemu ya kichwa )). [Hadiyth Dhwa’iyf: Ina njia nyingi na zote zina kasoro. Pia pamekhitalifiwa katika kuifanya ni Hadiyth Hasan kwa vikundi vyake. Na Mwanachuoni Mweledi Al-Albaaniy Allaah Amrehemu katika Kitabu chake cha Asw-Swahiyhah amesema kuwa huenda Hadiyth hii ikapanda kufikia ngazi ya Hadiyth Mutawaatir kwa baadhi ya Maulamaa!! Shaykh wetu (Allaah Amhifadhi), ameitolea maelezo ya kichambuzi katika Al-Nadhwaraat na akatilia nguvu udhwaifu wake, nalo ni jambo sawa kabisa. Na Shaykh Mash-huur Hasan (Allaah Amhifadhi) amesema kuwa ni Dhwa’iyf baada ya utafiti wa kina alioufanya pambizoni mwa Kitabu cha Al-Khilaafiyyaat kilichotungwa na Al-Bayhaqiy (1/448)].





Hadiyth hii ni Dhwa’iyf Marfu’u kwa kauli yenye nguvu. Lakini hata hivyo imethibiti kwa watangu wema wengi akiwemo Ibn ‘Umar. [Isnadi yake ni Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-Daar Qutwniy (1/98), Ibn Abuu Shaybah (1/28) na wengineo].



Na kuna Hadiyth zinazolitolea hilo ushahidi. Ni kama ile inayoashiria kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipaka kichwa chake na masikio yake mara moja. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (133), At-Tirmidhiy (36), An-Nasaaiy (1/74), Ibn Maajah (439) na wengineo. Ina njia mbalimbali za kuifanya kuwa Swahiyh zilizonukuliwa toka kwa Ibn ‘Abbaas. Na asili yake iko kwa Al-Bukhaariy (157) kwa ufupi. Pia ina ushahidi toka kwa Hadiyth ya Ar-Rubayi’i binti Mu’awwidh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (126), At-Tirmidhiy (33) na Ibn Maajah (418). Vilevile imenukuliwa toka kwenye Hadiyth ya Al-Miqdaam].



Hadiyth hizi ni nyingi zilizonukuliwa toka kwa ‘Aliy, Ibn ‘Abbas, Ar-Rubayyi’i na ‘Uthmaan. As-Swan-’aaniy anasema: “Wote wamekubaliana kuwa kuyapaka masikio na kichwa ni mara moja tu”, yaani kwa maji hayo hayo kama inavyoonekana kutokana na tamko la “mara moja”. Kwa vile, lau kama masikio yangekuwa yanatekewa maji mapya, basi kusingelithibitishwa ya kuwa “yeye alipaka kichwa na masikio mara moja”. Na kama itachukulika kwamba mapendeleo ni kuwa yeye hakukariri kuyapaka bali aliyatekea maji mapya, basi huo ni uwezekano wa mbali”. [Subulus Salaam (1/49)].



Ninasema: "Na kama atateka maji mengine ya kupaka masikio, basi hapana ubaya. Kwani hilo limethibiti toka kwa Ibn ‘Umar". [Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdur Razzaaq (29) na Al-Bayhaqiy (1/65).]



Angalizo



Hakuna usharia wowote wa kuosha shingo wakati wa kutawadha, kwa vile hakuna Hadiyth yoyote Swahiyh iliyopokelewa toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ikiligusia hilo. [Majmu'u Al-Fataawa (1/56) na Zaad Al-Ma’ad (1/49). Tizama As-Silsilat Adh-Dhwa’iyfah (69-744)].





5- Kuosha miguu miwili pamoja na vifundo



Vifundo viwili ni mifupa miwili iliyochomoza katika pambizo mbili za mguu. Kuosha miguu miwili ni lazima kwa Jamhuri ya Maulamaa wa Ahlus-Sunnah kutokana na Neno Lake Allaah Mtukufu:



((وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ))

((Na miguu yenu hadi kwenye vifundo viwili)). [Al Maaidah (5:6)].



Ni kwa kuweka “fat-hah” juu ya “arjulakum” kuunganishia kwenye viungo vinavyooshwa.

Na kila aliyehadithia sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amethibitisha kwamba aliosha miguu miwili hadi kwenye vifundo viwili. Na kati ya yaliyoelezewa ni yale yanayomhusu ‘Uthmaan yanayosema: “..Kisha akaosha miguu yake miwili hadi katika vifundo mara tatu….”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (158) na Muslim (226)].



Na vifundo viwili hujumuishwa katika kuoshwa, kwani ikiwa mpaka unatokana na jinsi ya chenye kuwekewa mpaka, basi nao huingia kama ilivyotangulia. Na Hadiyth ya Ibn ‘Amri (Allaah Amridhie) inaonyesha juu ya haya. Anasema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikawia nyuma katika safari. Kisha alituwahi nailhali alasiri imekurubia kumalizika wakati wake. Tukaanza kutawadha huku tukipaka miguu yetu. Hapo akanadi kwa sauti kubwa:



((ويل للأعقاب من النار))

((Ole wao na moto kwa (kutoosha) visigino)).

Alisema mara mbili au tatu. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (161) na Muslim (241)].





Ama yale yaliyopokelewa ya kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipaka (miguu) katika wudhuu wake, linalochukuliwa ni kupaka juu ya khufu mbili, nalo ni jambo ambalo yeye aliliruhusu. Suala hili Maraafidha na Mashia wengi wamekwenda kinyume nalo wakisema kuwa ni lazima kupaka miguu miwili badala ya kuosha. Na lililo sahihi kutumiwa ni la kwanza. ‘Abdur-Rahmaan bin Abi Layla anasema: “Maswahaba wote wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wamekubaliana juu ya kuosha miguu miwili”. [Fat-hul Baariy (1/266) na Al-Mughniy (1/120)].





6-Kupachanyisha vidole vya miguu na mikono:



Vidole na sehemu zilizo kati yake, ni sehemu ya mahala pa faradhi. Kwa hiyo ni lazima zioshwe. Na kama haitowezekana kuoshwa ila kwa kupachanyishwa, basi ni lazima kufanya hivyo. Na kama itawezekana, basi itapendeza kama itakavyokuja.





7- Kupangilia:



Ni kuvitwaharisha viungo vya wudhuu kimoja baada ya kingine kwa mpangilio ambao Allaah Ameamrisha katika Aayah Tukufu. Ataosha uso, kisha mikono miwili, kisha atapaka kichwa, halafu ataosha miguu miwili. Mpangilio huu ni wajibu katika kauli sahihi zaidi kati ya kauli mbili za Maulamaa. Na hayo ndiyo madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, Hanbali, Abu Thawr, Abu ‘Ubayd na Adh-Dhwaahiriyya. [Al-Majmu’u (1/433), Al-Mughny (1/100), na Al-Muhalla (2/66)]. Wajibu huu wameutolea hoja kwa haya yafuatayo:





1- Ni kwamba Allaah Mtukufu Ametaja katika Aayah ya faradhi za wudhuu kimpangilio pamoja na kutenganisha miguu miwili na mikono (ambavyo ni lazima vioshwe) kwa kichwa ambacho ni lazima kipakwe. Na Waarabu hawakitenganishi kitu na chenziye ila kwa faida fulani. Na hapa Aayah inaashiria ulazima wa kupangilia. [Kama hivyo katika Al-Mughny (1/100)].





2- Ni kwamba kila aliyehadithia kuhusu wudhuu wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), ameuelezea ukiwa umepangika. [Maswahaba 20 wamehadithia sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakinukulu toka kwake. Wote wameuelezea kwa mpangilio isipokuwa katika Hadiyth mbili Dhwa’iyf ambazo Al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika kitabu cha Tamaam Al-Minnah (uk.85)].

Na kitendo chake hicho kinafasiri Kitabu cha Allaah Mtukufu.





3- Ni kwa yale yaliyohadithiwa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha kimpangilio kisha akasema:



(( هذا وضوء لا يقبل الله الصلاة إلا به))

((Huu ndio wudhuu, Allaah Haikubali Swalaah ila kwao)).



Lakini Hadiyth hii ni Dhwa’iyf. [Hadiyth Dhwa’iyf. Angalia Al-Irwaa (85)].



Lakini Maalik, Ath-Thawriy na Abuu Haniyfah na wenzake, wao wanasema kuwa kupangilia ni jambo lililosuniwa na wala si wajibu. [Al-Mudawwanah (1/14), Al-Mabsuwtw (1/55), na Sharhu Fat-hil Qadyr (1/30)].



Hoja yao ni:



1- Kwamba kiunganishi kihusishi “و waw” katika Aayah, hakihukumii mpangilio. Jibu la haya, liko katika yaliyotangulia.



2- Ni yale yaliyopokelewa toka kwa ‘Aliy na Ibn Mas-’oud kwamba wamesema: “Haijalishi ni kwa kiungo gani nilichoanzia”. [Athar ya ‘Aliy. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad katika kitabu cha Al-’Ilal (1/205), Ibn Abiy Shaybah (1/55) na Ad-Daarqutwniy (1/88), Sanad yake ni Dhwa’iyf. Pia athar ya Ibn Mas-’oud iliyofanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy katika kitabu cha Al-Taariykh (1650) na Abu ‘Ubayd katika At Twahuur (325) kwa Sanad Hasan kwa tamko la: “Akitaka ataanza kushoto kwake katika wudhuu kama alivyosema Imaam Ahmad].



Hili linajibiwa kwa kauli ya Al- Imam Ahmad kama ilivyo katika “Masuala ya mwanawe ‘Abdullaah” aliposema (27-28):

“Bila shaka ina maana ya kushoto kabla ya kulia. Na hakuna ubaya kuanza kwa kushoto kwake kabla ya kulia kwake, kwani matoleo yake toka katika Qur-aan ni mamoja. Allaah Mtukufu Anasema:

((فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ))

(( Basi osheni nyuso zenu na mikono yenu hadi kwenye vifundo, na mpake vichwa vyenu, na (mwoshe) miguu yenu)). [Al Maaidah (5:6)].



Kwa hiyo, hapana ubaya kuanza kushoto kabla ya kulia”.



Ninasema: “Na ingawa ubora ni kuanzia kulia kwa ajili ya kufuata Sunnah. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi".





8- Kuandamisha:



Ni kufuatilizia uoshaji wa viungo vya wudhuu kwa namna ambayo kisikauke kiungo kabla hajaingia kiungo kingine katika muda wa wastani.



Ash-Shaafi’iy katika kauli yake ya zamani na Ahmad katika Al-Mash-hur wanasema kuwa ni lazima kuandamisha. Pia Maalik anasema hivyo hivyo isipokuwa yeye ametofautisha kati ya aliyekusudia kutoandamisha na kati ya mwenye udhuru. Na haya ndiyo aliyoyachagua Shaykh wa Uislamu. [Al-Ummu (1/30), Al-Majmu'u (1/451), Kash-Shaaf Al-Qina’i (1/93), Al-Mudawwanah (1/15), Al-Istidhkaar (1/267) na Majmu'u Al-Fataawaa (21/135)].



Ulazima wa kuandamisha unaashiriwa na Hadiyth ya ‘Umar bin Al-Khattwaab kwamba mtu mmoja alitawadha akaacha sehemu ndogo ya kucha katika miguu yake. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwangalia kisha akamwambia:

(( إرجع فأحسن وضوءك ))

(( Rejea ukatawadhe vizuri)).



Akarejea, kisha akaswali. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (232), Ibn Maajah (666) na Ahmad (1/21). Hadiyth hii imetiwa baadhi ya dosari, lakini ina vithibitisho vyake vinavyoifanya kuwa Swahiyh bila ya shaka yoyote. Angalia katika At-Talkhiysw (1/95) na Al-Irwaa (86)].





Na katika riwaya iliyopokelewa na baadhi ya Maswahaba wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwona mtu mmoja akiswali nailhali juu ya mguu wake kuna sehemu nyeupe ya ukubwa wa dirham haikupata maji. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamrisha atawadhe upya na aswali tena. [Al-Albaaniy amesema ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (175) na Ahmad (3/424) kupitia kwa Buqayyah bin Al-Waliyd toka kwa Bahiyr aliyepokea toka kwa Khaalid. Buqayyah ameeleza kwamba amesikia toka kwa Bahiyr kwa mujibu wa yaliyoandikwa na Ahmad, na ambaye amesema kwamba Isnadi yake ni Hasan. Na kwa ajili hiyo, Al-Albaaniy katika Al-Irwaa (86), amesema ni Swahiyh. Ninasema: “Ni Hadiyth Hasan lau si kuhofiwa kumwadilisha Buqayyah. Hakueleza kwamba Bahiyr amesikia toka kwa Khaalid!”].



Abu Haniyfah na Ash-Shaafi’iy katika madhehebu mapya wanasema kuwa kuandamisha si lazima. Nayo ni riwaya iliyopokelewa toka kwa Ahmad, na pia ni madhehebu ya Ibn Hazm. [Al-Mabsuwtw (1/56), Al-Ummu (1/30), Al-Majmuu’ (1/451) na Al-Muhalla (2/70)].





Wamesema:



1- Kwa vile Allaah Mtukufu Amewajibisha kuosha viungo, hivyo basi, mwenye kuviosha, atakuwa amefanya wajibu wake, ni sawa awe ameviosha kiholela bila mpangilio au akaviosha kwa mpangilio uliopangika.





2- Ni kwa aliyoyahadithia Naafi’i kwamba Ibn ‘Umar alitawadha sokoni, akaosha uso wake na mikono yake na akapaka kichwa chake. Kisha aliitwa kwenda kuswalia maiti, akaingia Msikitini, kisha akapaka juu ya khufu zake na akaswali. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Maalik (48) na kutoka kwake akapokea Ash-Shaafi’iy (16) na Al-Bayhaqiy katika Al-Ma’arifah (99)].





3- Hadiyth yenye amri ya kutawadha na kuswali upya, wanaizingatia kwamba ni Dhwa’iyf.





4- Wameliawilisha neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ((Rejea ukatawadhe vizuri)) kwamba makusudio yake ni kukamilisha kuosha sehemu ambayo haikupata maji mguuni.





Ninasema: “Hukmu ya mvutano wa yaliyotangulia ni Hadiyth ya Khaalid bin Mi’idaan yenye amri ya kutawadha tena na kuswali upya aliyoinukuu toka kwa baadhi ya Maswahaba wa Rasuli. Aliyeifanya kuwa ni Swahiyh, amesema ni lazima, na kama si hivyo, basi hoja zilizobakia zina uwezekano wa hili au lile. Ninaloliona mimi kuwa ni sawa, ni ulazima wa kuandamisha kutokana na Hadiyth hii. Pia, ni kwa vile wudhuu ni ‘ibaadah moja, isitenganishwe. Ama athar ya Ibn ‘Umar, inavyoonekana ni kuwa hiyo ni katika hali ya udhuru na kulazimika, na kwa hivyo, haipimiwi na hali ya kawaida. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi. Lakini ikiwa patatokea mtengano kidogo katika kuosha viungo, basi hakuna ubaya. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.”
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



030-Sunnah Za Wudhuu



Alhidaaya.com







1- Kupiga mswaki:



Jambo hili limekwishadokezwa kuwa linapendeza katika mlango wa “Sunnah za hulka asili”.







2- Kupiga Bismillaah mwanzoni:



Kiilivyo, kupiga Bismillaahi ni jambo zuri la kisharia katika mambo yote. Kuna Hadiyth dhwa’iyf zilizopokelewa kuhusu kupiga bismillaahi wakati wa kutawadha ingawa baadhi ya Maulamaa wamesema kuwa Hadiyth ni Swahiyh. Kati ya Hadiyth hizo ni ile isemayo:



((ولا وضوء لمن لم يذكر اسم الله عليه))

((Hana wudhuu asiyelitaja Jina la Allaah)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (101), At-Tirmidhiy (25), Ahmad (2/418) na wengineo. Lenye nguvu ni kuwa Hadiyth hii ni Dhwa’iyf. Shaykh Al-Albaaniy Allaah Amrehemu katika kitabu cha Al-Irwaai”(1/122), amesema kuwa ni Hadiyth Hasan. Shaykh Mtukufu Abuu Is-Haaq Al Huwayny – Allaah Amhifadhi – amechangia kidogo katika kuupitisha uswahiyh wake. Uswahiyh wake uko karibu zaidi. Allaah Ndiye Mjuzi zaidi].



Na kuna Hadiyth nyingine Dhwa’iyf sana zisizofaa kabisa kutegemewa kwa hoja. Na kwa ajili hiyo, Imaam Ahmad amesema: “Siijui Hadiyth yoyote katika mlango huu yenye Isnadi Hasan”.



Ninasema (Abuu Maalik): “Linalotilia nguvu kutokuwepo ulazima wa kupiga bismillaahi ni kuwa watu walioelezea sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hawakutaja kuhusu bismillaahi. Na haya ni madhehebu ya Ath-Thawriy, Maalik, Ash-Shaafi’iy na Abuu Haniyfah na wenzake. Ni riwaya toka kwa Ahmad. [Vitabu vya Fat-hul Qadiyr (1/22), Mawaahib Al-Jaliyl (1/266), Majmu'u (1/385) na Al-Insaaf (1/128)].





3- Kuosha viganja viwili mwanzoni:



Ni kwa yale yaliyomo katika Hadiyth ya ‘Uthmaan katika sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). ‘Uthmaan anasema: “Akamiminia katika viganja vyake mara tatu, akaviosha…”[Hadiyth Swahiyh Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (159) na Muslim (226)].





4- Kusukutua na kupaliza maji mara tatu kwa teko moja:



Ni kwa yale yaliyomo katika Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zayd alipokuwa akifundisha namna Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa akitawadha: “Kwamba yeye (Rasuli) alisukutua na akapaliza kwa teko moja. Akafanya hivyo mara tatu”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (235), At-Tirmidhy (28) na Ibn Maajah (405)].





5- Kuyakomeza maji hadi mwisho wakati wa kusukutua na kupaliza kwa ambaye hakufunga:



Ni kwa Hadiyth Marfu’u ya Laqiyt bin Swabrah:

وبالغ في الاستنشاق إلا أن تكون صائما

((Na komeza maji hadi mwisho isipokuwa kama umefunga)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (142), An-Nasaaiy (1/66), Ibn Maajah (407) na Ahmad (4/33)].





6- Kutanguliza kulia kabla ya kushoto:



Katika Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas kuhusu sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “…kisha alichukua teko la maji akaosha kwalo mkono wake wa kulia, kisha akachukua teko jingine akaosha kwalo mkono wake wa kushoto, kisha alipaka kichwa chake maji, kisha alichukua teko la maji, akanyunyizia kwalo mguu wake wa kulia mpaka akauosha, kisha alichukua teko jingine akaosha kwalo mguu wake, yaani wa kushoto….”[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (140)].



Na imepokelewa toka kwa ‘Aaishah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akipenda kuanza kwa upande wa kulia wakati wa kuvaa viatu, kutembea, kujitwaharisha na katika kila jambo lake alilolifanya. [Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (168) na Muslim (268)].





7- Kuviosha viungo mara tatu:



Imepokelewa Hadiyth Swahiyh toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ya kwamba alitawadha (akiviosha viungo) “mara moja moja”, [Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (156) toka kwa Ibn ‘Abbaas.]…na kwamba aliviosha “mara mbili mbili”. [Hadiyh Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (157) toka kwa ‘Abdullaah bin Yaziyd]. Na ukamilifu na utimilifu zaidi wa wudhuu ni kuviosha viungo mara tatu kama alivyofanya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mujibu wa ilivyoelezewa katika Hadiyth za ‘Uthmaan na ‘Abdullaah bin Zayd. Hadiyth hizi zimekwisha zungumziwa.





Zindushi mbili



(a) Kupukusa kichwa ni mara moja tu:



Asipukuse mara mbili au tatu kulikoelezewa kiujumla katika Hadiyth za sifa ya wudhuu wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ama riwaya zinazoelezea kuwa kupukusa kichwa ni mara tatu, riwaya hizo si Swahiyh. Ama zile zinazoelezea kwamba Rasuli alipukusa mara mbili, basi hiyo ni tafsiri ya neno lake:

((فأقبل بهما وأدبر))

((Ipeleke mbele na nyuma)), kama alivyosema Ibn ‘Abdul Barri. [Al-Khilaafiyyaat cha Al-Bayhaqiy (1/336). Kimetolewa maelezo na maoni na Shaykh Mash-huur Aali Salmaan. Angalia pia At-Twahuwr cha Abu ‘Ubayd (uk 359)].



Kuipelekea mikono miwili mbele na nyuma wakati wa kupukusa kichwa, hakuzingatiwi kama ni kukariri, kwa kuwa kukariri kunakuwa ni kwa kuchukua tena maji upya. Kisha kukariri, kumestahabiwa tu kwa viungo vinavyooshwa na si kwa vile vinavyopukuswa. [Muqaddimaat Ibn Rushd Alal Mudawwanah (uk 16)].



Na kati ya dalili imara zinazoonyesha kwamba kichwa hakipukuswi zaidi ya mara moja, ni Hadiyth ya bedui aliyekwenda kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumuuliza namna ya kutawadha. Rasuli akamwonyesha kila kiungo mara tatu tatu, kisha akasema:

(( هذا الوضوء، فمن زاد على هذا فقد أساء وتعدى وظلم))

((Huu ndio wudhuu. Atakayezidisha zaidi ya hivi, basi amefanya ubaya, amepetuka mipaka, na amedhulumu)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na An Nasaaiy (1/88), Ibn Maajah (422) na Ahmad (2/180)].



Al Haafidh katika “Al Fat-h” (1/298) anasema: “Riwaya ya Sa’iyd bin Mansour, ina kiashirio kwamba alipukusa kichwa chake mara moja tu, hivyo basi, inaonyesha kwamba kupukusa kichwa zaidi ya mara moja, si jambo mustahabu. Yaliyokuja kwenye Hadiyth zinazoelezea kupukusa mara tatu – kama zitakuwa ni Swahiyh – yanaweza kuchukulika kama ni kwa lengo la kukipukusa kichwa chote kikamilifu, na si kwamba kila mpukuso na hesabu yake. Na hii ni kwa ajili tu ya kuoanisha kati ya dalili”.





Ninasema: “Haya ni madhehebu ya Abuu Haniyfah, Maalik na Ahmad (katika Swahiyh kutoka kwake) kinyume na Ash Shaafi’iy Allaah Awarehemu”. [Al-Mabsuwtw (1/5), Haashiyat Ad-Dusuwqy (1/98), Al-Mughny (1/127) na Al-Umm (1/26)].





(b) Ni karaha kuzidisha zaidi ya mara tatu kwa aliyeosha viungo kikamilifu:



Kuosha mara tatu viungo vya wudhuu, ndio wudhuu uliokamilika na uliotimia. Ni karaha kuzidisha zaidi ya mara tatu kutokana na Hadiyth:

((فمن زاد على هذا فقد أساء وتعدى وظلم))

((Atakayezidisha zaidi ya hivi, basi amefanya ubaya, amepetuka mipaka, na amedhulumu)).

Mahala pa maneno haya, ni pale ziada inapofanywa si kwa ajili ya kukamilisha upungufu. Na kama viungo vyake vitaosheka kikamilifu mara tatu au chini yake, itakuwa ni karaha kuongeza zaidi ya mara tatu. Haya hayana mabishano kabisa. [At-Tamhiyd cha Ibn ‘Abdul Barri (20/117) kwa mfano wake kwa muhtasari].





8- Kuziasulia ndevu nyingi:



Tumekwisha eleza kwamba kama ndevu ni nyingi zilizoficha ngozi, basi itatosha kuosha nje yake tu. Na hapa tunaongeza kusema kuwa imesuniwa kuziasulia kwa maji kutokana na Hadiyth ya Anas isemayo kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kutawadha, alikuwa akichukua teko la maji, kisha huliingiza chini ya kaakaa na kuasulia kwalo pia. Kisha Rasuli husema:

((هكذا أمرني ربي عز وجل))

((Hivi ndivyo Mola wangu Ázza wa Jalla Alivyoniamuru)). [Hadiyth Swahiyh Lighayrih. Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (145), Al-Bayhaqy (1/54) na Al-Haakim (1/149). Angalia Al-Irwaa (92).



Na jambo hili linageuzwa kuwa Sunnah kutokana na Hadiyth iliyotangulia hapo kabla ya Rifa’a bin Raafi’i inayozungumzia kisa cha mwenye kuswali vibaya.





9- Kusugua viungo:



Ni kwa Hadiyth ya ‘Abdullaah bin Zubayr aliyesema: “Nilimwona Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitawadha, na kisha akaingia kuisugua mikono yake miwili”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Hibaan (1082) na Al-Bayhaqy (1/196)].





10- Kuasulia vidole vya mikono na miguu:



Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((أسبغ الوضوء، وخلل الأصابع، وبالغ في الاستنشاق إلا ان تكون صائما))

((Tawadha wudhuu kamili, asulia vidole, na ubalighishe katika kupaliza maji, isipokuwa kama umefunga)).[Hadiyth Swahiyh. Imetajwa nyuma kidogo].



Na kama vidole na sehemu za kati yake haviosheki ila kwa kuasulia, basi wakati huo itakuwa ni lazima kufanya hivyo kama tulivyotangulia kusema.





11- Kuosha zaidi ya mpaka wa faradhi:



Imesuniwa kutawadha kikamilifu, kurefusha kuosha uso hadi katika ncha ya utosi, na kuosha juu zaidi ya vifundo viwili na visigino. Katika Hadiyth ya Abu Hurayrah, Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:



((إن أمتي يأتون يوم القيامة غرا محجلين من آثار الوضوء))

((Hakika umati wangu utakuja siku ya Qiyaama hali ya kuwa nyuso zao, mikono yao na miguu yao inang’ara kutokana na athari za wudhuu)).



Abu Hurayrah anasema: “Basi yeyote kati yenu atakayeweza kurefusha kuosha uso, basi na afanye”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (36) na Muslim (246)].



Na imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba alitawadha, akaosha mikono yake hadi akaingia kuosha vipanya vyake, akaosha miguu yake miwili hadi akaingia kuosha miundi yake. Kisha alisema: “Hivi ndivyo nilivyomwona Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitawadha”.[ Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (246).



Na imepokelewa tena toka kwake akisema: Nimemsikia kipenzi changu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:



((تبلغ الحلية من المؤمن حيث يبلغ الوضوء))

((Nuru ya Muumini inafikia pale wudhuu unapofikia)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (250)].







12- Kutumia maji kwa uangalifu:



Ni kwa Hadiyth ya Anas aliyesema: “Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiogea maji ya lita 2 hadi lita 2½, na akitawadha kwa maji ya ½ lita”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (198) na Muslim (325)].





13- Du’aa baada ya kutawadha:



Imepokelewa toka kwa ‘Umar amesema: Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((ما منكم من أحد يتوضأ فيسبغ ثم يقول: أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأشهد أن محمدا عبده ورسوله إلا فتحت له أبواب الجنة الثمانية يدخل من أيها شاء))

((Hakuna yeyote kati yenu anayetawadha akautimiza vilivyo wudhuu wake, kisha akasema: “Nashuhudia ya kwamba hapana mola mwingine isipokuwa Allaah Aliye Peke Yake na Asiye na mshirika, na nashuhudia ya kwamba Muhammad ni Mja Wake na Rasuli Wake, isipokuwa hufunguliwa milango minane ya pepo aingie wowote autakao)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (234)].





Imepokelewa na Abu Sa‘iyd kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((من توضأ فقال: سبحانك اللهم وبحمدك، أشهد أن لا إله إلا أنت، أستغفرك وأتوب إليك، كتب فى رق ثم طبع بطابع فلا يكسر إلى يوم القيامة))

((Mwenye kutawadha akasema: “Umetakasika ee Mola na kwa Himdi Yako, ninashuhudia ya kwamba hapana mola mwingine ila Wewe, nakuomba maghfirah na ninatubia Kwako”, huandikwa katika karatasi nyeupe, kisha hutiwa chapa, halafu haichanwi mpaka Siku ya Qiyaamah)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa ”Ikhraaj” na An Nasaaiy katika kitabu cha Al-Kubraa (9909), na Al-Haakim (1/564). Kuna Hadiyth kama hii iliyopokelewa na Swahaba mwingine].





14- Kuswali rakaa mbili baada ya kutawadha:



Ni kwa Hadiyth ya ‘Uthmaan aliyesema: “Nilimwona Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akitawadha kama hivi ninavyotawadha akasema”:



((من توضأ نحو وضوئي هذا، ثم صلى ركعتين لايحدث فيهما نفسه، غفر له ما تقدم من ذنبه))

((Mwenye kutawadha kama wudhuu wangu huu, kisha akasimama akaswali rakaa mbili haizungumzishi nafsi yake, basi husamehewa madhambi yake yaliyotangulia)).[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (6433) na Muslim (226)].





Na imepokelewa toka kwa Abu Hurayrah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia Bilaal wakati wa Swalaah ya alfajiri:



(( يا بلال! حدثني بأرجى عمل عملته فى الاسلام، إني سمعت دف نعليك بين يدي في الجنة)). قال : ماعملت عملا أرجى عندي من أني لم أتطهر طهورا في ساعة من ليل أو نهار إلا صليت بذلك الطهور ما كتب لي أن أصلى))

((Ee Bilaal! Nielezee amali yenye matarajio zaidi uliyoifanya katika Uislamu, kwani mimi nimesikia mtaharuki wa viatu vyako mbele yangu huko peponi)).

Bilal akasema: “Sikufanya amali yoyote yenye matarajio makubwa kwangu zaidi ya kuwa sikupata kujitwaharisha wakati wowote wa usiku au mchana, ila huswali kwa twahara hiyo kile nilichoandikiwa kukiswali”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (1149) na Muslim (2458)].







Inajuzu Kukausha Viungo Baada Ya Kutawadha Kwa Kutopokelewa Lolote La Kuzuia Hilo



Na asili ni kufaa hilo. Na kama itasemwa kuwa imethibiti kwamba Maymuunah (Allaah Amridhie) alimletea Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kitambaa cha kujifutia baada ya kuoga, na yeye hakujifutia nacho, na akaondoka na ilhali anakung’uta mikono yake miwili.. [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (270)]…..basi tunasema: “Tukio hili lina mwelekeo wa kuwa na mambo kadhaa. Inawezekana kuwa alikirejesha kitambaa hicho kutokana na sababu inayohusiana nacho kama kutokuwa kisafi, au kuhofia kukilowesha na maji au sababu nyingine. Kisha Bi Maymuunah kumletea Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kitambaa hicho, inaonyesha kuwa ilikuwa ni mazoea yake. [Faida zaidi zipo kwenye Ash Sharhul Mumti’i (1/181). Angalia Kitabu cha Zaadul Maad (1/197)].





Kujuzu huku kunatiliwa nguvu na yaliyopokelewa kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitawadha, akaligeuza juba la sufi alilokuwa nalo, kisha akajifuta nalo.” [Isnadi yake iko karibu na Hadiyth Hasan. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (468, 3564)].





At-Tirmidhiy (54) anasema: “Baadhi ya Maswahaba wasomi wa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na wa baada yao, wameruhusu kujifuta kwa kitambaa baada ya kutawadha. Na mwenye kulifanya hilo kuwa makruhu, basi amefanya hivyo kwa yale yaliyosemwa kuwa “wudhuu hupimwa”.





Wudhuu Haufai Kwa Aliyepaka Kucha Rangi [Yamenukuliwa kutoka kitabu changu cha Fiqhus Sunnah Lin Nisaa (uk 39)].



Kwa vile hilo huzuia maji kupenya na kufika sehemu ya faradhi. Ama rangi nyingine ya kawaida kama vile hina na mfanowe, hiyo haiathiri. Lakini hata hivyo ni vizuri kuiondosha kabla ya kutawadha na kuswali kwa kauli ya Ibn ‘Abbaas: “Wake zetu hujipaka hina bora kabisa. Hujipaka baada ya Swalaah ya ‘Ishaa na huiondosha kabla ya Alfajiri”. [Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibnu Abi Shaybah (1/120)].



Na imepokelewa kuwa Ibraahiym An-Nakh’iy aliulizwa kuhusu mwanamke anayepaka mikono yake hina bila ya kuwa na wudhuu kisha wakati wa Swalaah ukafika. Alijibu akisema: “Ataondosha vilivyomo mkononi mwake kama atataka kuswali”. [Isnadi yake ni Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bayhaqy (1/77, 78)].
 
Naam darsa la fiqh linaendelea hakika faida kubwa inapatikana,tenga mda kusoma mafundisho ya dini yako ili ufanye ibada zako vizur kabisa

Wanawake nawakumbusha najua mnapenda kunukia vizur na ni jambo zuri lkn fanya hivyo ukiwa nyumbani kwako na si mabarabarani na sehemu ya public

Kwenu nyinyi inaleta fitina na kuhamasisha machafu,ikiwa mna mcha Allah na mfanye hivyo
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



031-Yanayotengua Wudhuu



Alhidaaya.com







1- Ni kutoka mkojo, au kinyesi, au upepo katika moja ya njia mbili (utupu wa mbele au wa nyuma)



Ama mkojo na kinyesi, ni kwa Neno Lake Subhaana:

أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِّنكُم مِّنَ الْغَائِطِ

((Au mmoja wenu ametoka chooni)). [Al Maaidah (5:6)]



“Al-Ghaait” ni kinaya cha kukidhi haja ndogo au haja kubwa. Wanachuoni wote wamekubaliana kuwa wudhuu unatenguka kwa kutoka kinyesi au mkojo toka moja ya njia mbili (mbele au nyuma). [Al-Ijma’a (uk 17), na Al-Awsatw (1/147) cha Ibn Al-Mundhir].

Ama ikiwa vitatoka sehemu isiyo ya mbele au nyuma kama kutoka kwenye jeraha la kwenye kibofu au tumbo, hapa wanachuoni wamevutana. Wanachuoni wenye kukizingatia kile tu kinachotoka (kiini chenyewe) kama Abu Haniyfah, Ath-Thawriy, Ahmad na Ibn Hazm, hao wamesema: “Wudhuu unatenguka kwa kila najsi inayobubujika toka mwilini iliyotokea sehemu yoyote”. Ama wale wenye kuyazingatia matokeo mawili (nyuma na mbele) kama Ash-Shaafi’iy, hao wamesema: “Unatenguka kinapotoka kitu chochote toka sehemu hizo mbili hata kama si najsi kama kijiwe na mfanowe”. [Al-Muhalla (1/232), Bidaayat Al-Mujtahid (1/40) na Al-Awsatw (1/137)].





Ama upepo, ikiwa utatoka kwa nyuma, kwa sauti au bila sauti, basi unatengua wudhuu. Hii ni kwa Ijma’a ya Maulamaa na kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

لا يقبل الله صلاة أحدكم إذا أحدث حتى يتوضأ

((Allaah Haikubali Swalaah ya mmoja wenu akipata hadathi mpaka atawadhe)).



Mtu mmoja toka Hadhramawt akauliza: “Ni nini hadathi ee Abu Hurayrah? Akajibu: “Ni ushuzi wa kimya kimya au wa sauti ”. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (135) na Muslim (135), lakini kwake bila kauli ya Abu Hurayrah].



Na ikiwa upepo utatokea utupu wa mbele, Jamhuri ya Maulamaa wamesema unatengua. [Bidaayat Al-Mujtahid (1/40) na Al-Ummu (1/17)].



Lakini Abu Haniyfah aliyeungwa mkono na Ibn Hazm amesema upepo huo hautengui wudhuu kwa vile ushuzi wa kimya na ushuzi wa sauti ni majina mawili ambayo hayaitwi upepo ila tu kama utatokea kwa nyuma. [Al-Muhalla (1/232) na Al-Mabsuwtw (1/83)].



Ninasema: “Ikiwa mtu atauhisi upepo unaojulikana (kwa harufu yake), basi utatengua wudhuu sawasawa ukiwa umetoka kwa mbele au kwa nyuma. Na ikiwa hauna harufu, basi ni ule tu unaotoka nyuma”.





Tanbihi



Mwanamke anaweza kuhisi kitu kinachofanana na upepo kikitoka kwenye utupu wake wa mbele. Hiki si kingine bali ni mjazo na mtaharuki wa ndani kwa ndani na wala si ushuzi unaotoka. Huo hautengui wudhuu wake, kwani ni kama kuteuka na mfano wake. Lakini ikiwa mwanamke huyo ni yule ambaye njia yake ya haja ndogo na kubwa zimeingiliana, basi atatawadha kiakiba tu kwa kuwepo uwezekano wa kuwa pengine upepo huo umetokea nyuma. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi.





2- Kutoka manii, wadii na madhii:



Kutoka manii kunatengua wudhuu kwa ijmai ya Wanazuoni na kunawajibisha kuoga kama itakavyokuja. [Al-Ifswaah (1/87) na Al-Ijma’a (uk 31)].



Na kila lile lenye kupasisha kuoga, basi linabatilisha wudhuu kwa Ijma’a ya Wanazuoni.



Na madhii nayo inatengua kwa Hadiyth ya ‘Aliy bin Abiy Twaalib Allaah Amridhie aliyesema: “Nilikuwa ni mtu ninayetokwa sana madhii. Nikamwamuru mtu mmoja amuulize Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na hishma ya binti yake. Akamwuliza, naye akasema:

توضأ واغسل ذكرك

((Tawadha na uoshe utupu wako)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (269) na Muslim 303)].



Madii pia ni hivyo hivyo. Ni wajibu mtu aoshe utupu wake na atawadhe.



Ibn ‘Abbaas anasema: “Manii, wadii na madhii; ama manii, ni yale ambayo inapasa kuoga kwa kutoka. Ama wadii na madhii, akasema: Osha utupu wako, au nyuchi zako, na utawadhe wudhuu wako wa Swalaah”.[Isnadi yake ni Swahiyh: Al-Bayhaqy (1/115)].



Faida



Aliyepata bahati mbaya ya kusumbuliwa na kichocho cha mkojo au cha madhii, au akawa mara kwa mara anatokwa na kimoja ya viwili hivyo vilivyotangulia kutokana na kasoro ya kimwili mpaka ikawa ni uzito kwake, basi huyo ataosha nguo yake na mwili wake, na atatawadha kwa kila Swalaah kama mwanamke mwenye damu ya istihaadhwah (maelezo yatakuja). Kisha hakitakuwa na neno kitakachomtoka akiwa ndani ya Swalaah au kati ya wudhuu wake na Swalaah yake.





3- Usingizi mzito wa kutojifahamu:



Athar zilizokuja kuhusu kutawadha baada ya mtu kulala zimetofautiana, na maana zake kama zinavyoonekana zimegongana. Kuna Hadiyth ambazo maana zake kama zinavyoonekana, huonyesha kuwa kimsingi hakuna kutawadha kwa sababu ya kulala (usingizi), wakati ambapo kuna nyingine maana yake ya nje inalazimisha kuwa kulala ni hadathi (kunatengua). Kwa hivyo basi, Maulamaa katika suala hili, wameelekea mielekeo miwili: Madhehebu ya kukusanya na Madhehebu ya kutilia nguvu.



Maulamaa wa madhehebu ya kutilia nguvu, hawa ima wameliondosha kabisa suala la kutawadha baada ya kulala wakisema kuwa (kulala) si hadathi, au ima wameliwajibisha hilo moja kwa moja wakisema kuwa kulala ni hadathi. Ama Maulamaa wa madhehebu ya kukusanya, hawa wamesema kuwa kulala si hadathi bali ni kwa kuzoeleka kuwa hupelekea katika hadathi. Maimamu hawa wamehitalifiana kuhusu namna ya ulalaji unaowajibisha kutawadha.



Na kutokana na mielekeo hii mitatu ya Maulamaa hawa, pamechipuka kauli nane. [Ziangalie katika vitabu vya Al-Muhalla (1/222-231), Al-Istidhkaar (1/191), Al-Awsatw (1/142), Fat-h Al-Baariy (1/376), Sharhu Muslim cha An-Nawawiy (370) na Nayl Al-Awtwaar (1/241)].



Nazo ni:



Kwanza: Kulala hakutengui wudhuu kabisa



Haya yameelezewa yakinukuliwa toka kwa kundi la Maswahaba akiwemo Ibn ‘Umar na Abu Musa Al-Ash‘ariy. Nayo ni kauli ya Sa‘iyd bin Jubayr, Mak-huul, ‘Ubaydah As-Salmaaniy, Al-Awzaa‘iy na wengineo. Hoja yao ni:



(a) Hadiyth ya Anas bin Maalik (Allaah Amridhie) aliyesema: “Swalaah ilikimiwa nailhali Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anazungumza chemba na mtu fulani. Basi aliendelea kuzungumza naye mpaka Maswahaba zake wakalala. Halafu alikuja, akawaswalisha”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (6192) na Muslim (376), na tamshi ni lake].





(b) Imenukuliwa toka kwa Qataadah akisema: “Nilimsikia Anas akisema: “Maswahaba wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walikuwa wakilala, kisha wanaswali wala hawatawadhi”. Akasema: Nikasema: Je, umesikia toka kwa Anas? Akasema: Ndiyo, naapa kwa Allaah”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (376) na At-Tirmidhy (78)].





Na tamko jingine lasema: “Wakingojea Swalaah, wakasinzia mpaka vichwa vyao vikajigonga (vikainamia chini), kisha husimama wakaswali”.





(c) Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliyesema: “Nililala kwa mama yangu mdogo Maymuunah. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasimama, nami nikasimama upande wake wa kushoto. Akauvuta mkono wangu akanisimamisha upande wake wa kulia. Nikawa kila ninaposinzia, hunivuta ndwele ya sikio. Aliswali rakaa 11”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (117) na Muslim (763), na tamshi ni lake].





(d) Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas wakati alipolala kwa Maymuunah. Anasema: “…kisha Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilala mpaka nikasikia mkoromo wake, kisha alitoka akaenda kuswali”.[Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (117), Muslim (184), na Ahmad (1/341)].



Na katika tamko jingine: “Kisha alisimama, akaswali na wala hakutawadha”.





Pili: Kulala kwa hali yoyote kunatengua wudhuu



Hakuna tofauti kati ya kulala kidogo au kulala sana. Haya ni madhehebu ya Abu Hurayrah, Abu Raafi’i, ‘Urwa bin Zubayr, ‘Atwaa, Al-Hasan Al-Baswriy, Ibn Al-Musayyib, Az-Zuhriy, Al-Mazniy, Ibn Al-Mundhir na Ibn Hazm. Ni chaguo la Al-Albaaniy. Ni kwa hoja zifuatazo:





(a) Ni kwa Hadiyth ya Swafwaan bin ‘Assaal. Amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akituamuru tunapokuwa safarini, tupukuse (tupanguse kwa maji) juu ya khofu zetu na wala hatuzivui kwa muda wa siku tatu hata kama tutakwenda haja kubwa au ndogo au kulala, ila kwa janaba”. [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1/32), At-Tirmidhiy (3535) na Ibn Maajah (478). Angalia pia kitabu cha Al-Irwaai (104)].



Wamesema: “Hapa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amechukulia kiujumla usingizi wote wala hakuhusisha usingizi hafifu au mzito, wala hali hii kwa ile, na akaufanya sawa na haja kubwa na ndogo”.



(b) Ni kwa yaliyohadithiwa toka kwa ‘Aliy bin Abi Twaalib (Allaah Amridhie) aliyepokea toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((العينان وكاء السه، فمن نام فليتوضأ))

((Macho mawili ni kizibo cha tundu la haja kubwa. Basi mwenye kulala, atawadhe)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (203), Ibn Maajah (477) na wengineo. Ni dhwa’iyf kwa kauli yenye nguvu. Al-Albaaniy amesema ni Hadiyth Hasan].



"السه" ni tundu la nyuma la haja kubwa, na "الوكاء"ni uzi unaofungiwa mdomo wa kiriba. Kwa hiyo kuwa macho kwa jicho, kumefanywa ni kama kizibo cha kiriba. Na jicho linapolala, kifuniko hicho huchopoka na hadathi huwa.



(c) Ni kwa Hadiyth ya ‘Aaishah kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((إذا نعس أحدكم وهو يصلي فليرقد حتى يذهب عنه النوم، فإن أحدكم إذا صلى وهو ناعس لا يدري لعله يستغفر فيسب نفسه))

((Anaposinzia mmoja wenu wakati anaswali, basi alale mpaka usingizi umwishe, kwani mmoja wenu anaposwali hali ya kuwa anasinzia, hajui pengine yeye anaona kuwa anaomba maghfirah huku kumbe anajitukana mwenyewe)). [Hadiyth Swahiyh. Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaary (212) na Muslim (222)].



Katika “Swahiyh yake”, Al-Bukhaariy ameitolea dalili Hadiyth hii juu ya ulazima wa kutawadha baada ya kulala. Lakini ninaloliona mimi ni kuwa kuna kijinukta cha kukizungumzia katika utoaji dalili kwa kutumia Hadiyth hii. Ikiwa ataifanya sababu ya kuikatiza Swalaah kutokana na usingizi ni kuchelea kujiombea mwenyewe vibaya, au kusoma asichokijua, au kutouhudhurisha moyo wake kukawa hakuna khushui, basi haya hayana uhusiano na kutawadha baada ya kulala. Bali huenda wenye kusema kuwa wudhuu hautenguki kwa usingizi wameitumia dalili hii kuthibitishia hoja yao. Basi atazame.



(d) Wamesema: "Maulamaa wote wamekubaliana kwamba ni lazima kutawadha kwa mtu aliyeondokewa na akili kwa wendawazimu au kupotewa na fahamu kwa hali yoyote iwayo. Pia aliyelala".





Tatu: Usingizi mzito unatengua kwa hali yoyote, na mwepesi hautengui



Hii ni kauli ya Maalik, riwaya ya Ahmad, Az-Zuhriy Rabi‘ah na Al-Awzaa‘iy!! Wameichukulia Hadiyth ya Anas ya kulala Maswahaba kuwa ni usingizi hafifu. Na pia wametolea dalili kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah:

من استحق النوم فقد وجب عليه الوضوء

((Mwenye kustahiki kulala, basi lazima atawadhe)). [Hadiyth Swahiyh Mawquwf. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Abi Shaybah (1/158) na ‘Abdur-Raaziq (481) ikiwa Mawquwf kwa Sanad Swahiyh. Na imepokelewa ikiwa Marfu’u. Na si Swahiyh, kama alivyosema Ad-Daara Qutwniy katika Al’Ilal (8/954). Angalia Adh-Dhwa’iyfah (954)].





Lililo sahihi ni kuwa Hadiyth hii ni Mawquwf. Na Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas:

((وجب الوضوء على كل نائم إلا من خفق رأسه خفقة أو خفقتين))

((Ni lazima kutawadha kwa kila aliyelala, isipokuwa kwa yule aliyegonga kichwa mara moja au mara mbili)). [Hadiyth Dhwa’iyf Mawquwf Marfu’u. Imefanyiwa “ikhraaj” na ‘Abdur Raaziq (479), na Al- Bayhaqiy (1/119). Angalia ‘Ilal Ad Daaru Qutwniy].





Nne: Kulala hakutengui ila kama atalala kwa ubavu au kwa kuegemea



Mwenye kulala kwa umbo lolote kati ya maumbo ya Swalaah kama kwa staili ya mwenye kurukuu, au mwenye kusujudu, au mwenye kusimama, au mwenye kukaa, basi wudhuu wake hautenguki, sawasawa akiwa katika Swalaah au nje ya Swalaah. Hii ni kauli ya Hammaad, Ath-Thawriy, Abu Haniyfah na wenzake, Daawuud na Ash-Shaafi’iy. Na hoja yao ni:



(a) Ni yale yaliyohadithiwa toka kwa ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake aliyepokea toka kwa babu yake ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

ليس على من نام جالسا وضوء حتى يضع جنبه

((Hakuna kutawadha kwa aliyelala kwa kukaa mpaka aweke ubavu wake)).

[Hadiyth Munkar: Imefanyiwa “ikhraaj” na ibn ‘Uday katika Al-Kaamil (6/2459), Ad-Daara Qutwniy (1/160) na At-Twabaraaniy katika Al-Awsatw..



Ni Hadiyth Dhwa’iyf, haifai.



(b) Ni Hadiyth ya Anas toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliyesema:



((إذا نام العبد في سجوده باهى الله تعالى به الملائكة يقول: أنظروا إلى عبدي روحه عندي وجسده في طاعتي))

((Anapolala mja katika sijda yake, Allaah Hujifaharisha kwake kwa Malaika Akiwaambia: “Mwangalieni Mja Wangu; roho yake iko Kwangu na mwili wake uko katika kunitii Mimi)). [Hadiyth Dhwa’iyf: Angalia kitabu cha As-Silsilat Adh-Dhwa’iyfah (953).



Na wamevipimia vipambo vingine vya mwenye kuswali kwa sijda.





Ninasema: “Hadiyth hii Sanad yake ni Dhwa’iyf. Al-Bayhaqiy amesema: “Kisha hakuna linaloashiria kuwa hatoki kwenye Swalaah yake. Na makusudio ya yaliyoelezwa - kama yatakuwa ni sawa - ni kumsifia mja anayedumu katika Swalaah mpaka usingizi ukamlemea”.





Tano: Hakutengui ila kwa aliyelala kwa umbo la kurukuu au kusujudu



An-Nawawiy ameinasibisha kauli hii kwa Ahmad. Na huenda mwono wake ni kuwa mwinamo wa kurukuu na kusujudu ulivyozoeleka, hupelekea kutenguka wudhuu.





Sita: Hakutengui ila kwa aliyelala kwa umbo la kusujudu



Kauli hii imepokelewa vilevile toka kwa Ahmad.





Saba: Usingizi ndani ya Swalaah hautengui kabisa, lakini nje ya Swalaah hutengua



Kauli hii imepokelewa na Abu Haniyfah kwa mujibu wa Hadiyth iliyotangulia katika kauli ya nne.





Nane: Wudhuu hautenguki kama atalala kwa kuambatisha barabara makalio yake chini, sawasawa ikiwa ni ndani ya Swalaah au nje yake, usingizi ukiwa mzito au mwepesi.





Haya ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, kwa vile kwa mujibu wa anavyoona yeye ni kuwa usingizi wenyewe si hadathi, bali ilivyozoeleka ni kuwa hupelekea kwenye hadathi. Anasema Ash-Shaafi’iy: “Kwa vile mwenye kulala, hujiambatisha barabara na ardhi na hakiwezi kutoka chochote isipokuwa hukishtukia”. Ash-Shawkaaniy ameichagua kauli hii.





Ninasema: “Wenye kuisema kauli hii, wameichukulia Hadiyth ya Anas ya kulala Maswahaba juu ya kuwa walikuwa wamekaa. Al-Haafidh katika kitabu chake cha “Al-Fat-h” (1/251) amelijibu hilo kwa kusema: “Lakini katika musnadi ya Al-Bazzaar kwa Sanad Swahiyh katika Hadiyth hii (panaelezwa): “Wakaweka ubavu wao, wengine wakilala, kisha hunyanyuka wakaswali”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bazzaaz. Na kama hiyo hiyo, imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud katika kitabu cha Masaail Ahmad (uk.318). Na Isnadi yake ni Swahiyh kwa sharti ya Mashaykh Wawili. Tazama pia katika Tamaam Al-Minnah (uk.100)].





Lenye Nguvu



Usingizi mzito wa kutojifahamu kiasi ambacho mtu hawezi kusikia sauti, au kuhisi kudondoka kitu toka mkononi mwake, au kutokwa na udenda na mfano wa hayo, bila shaka usingizi huo unatengua wudhuu, kwani ilivyozoeleka hupelekea hadathi. Ni sawasawa ikiwa mtu amesimama, au amekaa, au amelala ubavu, au amerukuu au amesujudu, hakuna tofauti kati ya milalo hiyo.



Na ikiwa wenye kauli ya kwanza wanamaanisha usingizi wa aina hii, basi sisi tuko nao. Na kama si hivyo, basi usingizi mwepesi wa kusinzia ambao mtu huhisi yanayopita, hautengui wudhuu kwa hali yoyote iwavyo. Ni kwa Hadiyth ya kulala kwa Maswahaba mpaka vichwa vyao vikajigonga (vikainama). Pia kwa Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas aliposwali na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).



Na kwa haya, zinakusanyika dalili zote zilizokuja katika mlango huu.



Ni Zake Allaah Himdi na Ihsaan.



Faida



Ilivyokuwa usingizi umezoeleka kuwa hupelekea kwenye hadathi yenye kuwajibisha kutawadha, basi kutenguka kwake kutategemezewa kwa mwenye wudhuu kwa mujibu wa mwenyewe alivyolala na kwa jinsi dhana yake itakavyopondokea. Na ikiwa atafanya shaka kama alivyolala kunatengua au la, basi lililo na nguvu ni kuwa asihukumie kutenguka wudhuu wake, kwa vile twahara ni yenye kuthibiti kwa yakini na haiondoki kwa shaka. Na hili ndilo alilolichagua Shaykh wa Uislamu katika kitabu cha Al-Fataawaa (21/230).





4- Kuondokewa na akili kwa kulewa au kupoteza fahamu au wendawazimu:



Hili linatengua wudhuu kwa makubaliano ya Maulamaa wote. [Al-Awsatw cha Ibn Al-Mundhir (1/155)].

Na kupatwa na mfadhaiko au mshtuko kuna uzito zaidi kuliko kulala.





5- Kugusa utupu bila kizuizi sawasawa ikiwa ni kwa matamanio au bila ya matamanio

Maulamaa wana kauli nne kuhusu kugusa utupu baada ya kutawadha. Kauli mbili kwa kutilia nguvu na kauli mbili kwa kukusanya.





Kauli ya kwanza:



Kugusa utupu hakutengui kabisa wudhuu.



Ni madhehebu ya Abuu Haniyfah na riwaya moja toka kwa Maalik. Pia kauli hii imepokelewa toka kwa kikundi cha Maswahaba. [Al-Badaai-’i (1/30), Sharhu Fat-hil Qadiyr (1/37), Al-Mudawwanah (1/8-9) na Al-Istidhkaar (1/308 na baada yake)].

Hoja zao ni haya yafuatayo:



(a) Ni Hadiyth ya Twaliq bin ‘Aliy kwamba mtu mmoja alimwuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu mtu anayegusa utupu wake baada ya kutawadha. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

هل هو إلا بضعة منك

((Hakika hiyo ni sehemu tu ya mwili wako)). [Isnadi yake ni Tepetepe: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (182), At-Tirmidhiy (85) na An-Nasaaiy (1/101). Maulamaa wamekhitalifiana juu ya kuwa ni Swahiyh au la. Kauli yenye nguvu ni kuwa Hadiyth hii ni Dhwa’iyf kwa ajili ya Qays bin Twaliq. Lakini Al-Albaaniy ameipasisha kuwa ni Swahiyh. Kwa hiyo kila mmoja na mwono wake. Na sisi hatuubani wasaa. Na Allaah Ndiye Mwelewa zaidi].



Na katika kauli nyingine, mwenye kuuliza alisema: “Wakati nikiwa katika Swalaah, niliingia kukuna paja langu na mkono wangu ukagusa dhakari yangu”. Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:

إنما هو منك

((Hiyo ni sehemu ya mwili wako)). [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Dawuud (183), Ahmad (4/23), Al-Bayhaqiy (1/135) na wengineo].

(b) Wamesema: Wote wanakubaliana kwamba dhakari ikiligusa paja, basi hakuwajibishi kutawadha, na hakuna tofauti kati ya mkono na paja. Hakuna mahitilafiano yoyote kati ya Maulamaa katika suala hili. Na wameizungumzia Hadiyth ifuatayo ya Bisarrah inayogusia amri ya kutawadha kwa kuugusa uume. [Al-Awsatw (1/203). Na tizama pia Sharhu Ma’aaniy Al-Aathaar (1/71-79)].



Kauli ya pili:



Kugusa utupu kunatengua wudhuu kwa hali yoyote.



Ni madhehebu ya Maalik – kama anavyojulikana - , Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Ibn Hazm. Kauli hii imepokelewa toka kwa Maswahaba wengi. [Al-Istidhkaar (1/308), Al-Mudawwanah (1/8-9), Al-Ummu (1/19), Al-Majmu’u (1/24), Al-Mughniy (1/178), Al-Insaaf (1/202), Al-Muhalla (1/235)].

Hoja yao ni:



(a) Hadiyth ya Bisarrah binti Swafwaan kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema:

من مس ذكره فليتوضأ

(( Mwenye kugusa dhakari yake, basi atawadhe)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abu Daawuud (181), An-Nasaaiy (1/100) na Ibn Hibaan (1112)].



(b) Hadiyth ya Ummu Habiybah kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

من مس فرجه فليتوضأ

((Mwenye kuugusa utupu wake, basi atawadhe)). [Ni Swahiyh kwa Hadiyth nyingine kama hii iliyopokelewa na Swahaba mwingine. Imefanyiwa “ikhraaj” na Ibn Maajah (481), Abu Ya-’alaa (7144) na Al-Bayhaqiy (1/130). Angalia Al-Irwaa (117)].



Mfano wa Hadiyth hizi mbili umepokelewa katika Hadiyth ya Abuu Hurayra iliyohadithiwa na Binti Unays, ‘Aaishah, Jaabir, Zayd bin Khaalid na ‘Abdullahi bin ‘Amri.

Wamesema: Hadiyth ya Bisarrah inatiliwa nguvu kuliko Hadiyth ya Twaliq. Hii ni kwa sababu zifuatazo:



(a) Kwamba Hadiyth ya Twaliq ina kasoro. Imekosolewa na Abu Zar-’a, na Abu Hatim. Na An-Nawawiy katika Majmu’u (2/42), amezungumza sana akieleza kuwa wahafidhi wamekubaliana kuifanya Hadiyth hii dhwa’iyf!!



(b) Ingelikuwa ni Swahiyh, basi Hadiyth ya Abuu Hurayrah yenye maana sawa na Hadiyth ya Bisarrah, ingelitangulizwa, kwa vile Twaliq alikuja Madiynah wakati wanaujenga Msikiti nailhali Abu Hurayrah alisilimu mwaka wa Khaybar baada ya hilo kwa miaka sita. Na kwa ajili hiyo, Hadiyth yake itaondosha hukmu ya Hadiyth ya Twaliq. [Na kati ya waliosema kuwa hukmu yake imeondoshwa (naskh) ni: At-Twabaraaniy katika Al-Kabiyr (8/402), Ibn Hibaan (3/405), Ibn Hazm katika Al-Muhalla (1/239), Al-Haazimiy katika Al-I’itibaar (77), Ibn Al-‘Arabiy katika Al-‘Aaridhwa (1/117) na Al-Bayhaqiy katika Al-Khilaafiyyaat (2/289)].



(c) Kwamba Hadiyth ya Twaliq inaubakisha uasili, lakini Hadiyth ya Bisarrah ni yenye kunukuu. Nayo hutangulizwa kwa vile hukmu za kisharia ni zenye kunukuu yale waliyokuwa wakiyafanya.



(d) Kwamba wapokezi wa kutenguka wudhuu kwa kugusa ni wengi na Hadiyth zake ni mashuhuri zaidi.



(e) Ni kauli ya Maswahaba wengi.



(f) Kwamba Hadiyth ya Twaliq imechukuliwa kuwa yeye alijikuna paja akaigusa dhakari yake juu ya nguo kama inavyoonyesha riwaya kuwa yeye alikuwa katika Swalaah.





Kauli ya tatu:



Wudhuu unatenguka ikiwa mtu kagusa dhakari yake kwa matamanio, na kama si kwa matamanio, basi hautenguki.



Hii ni riwaya toka kwa Maalik, na ni kauli iliyochaguliwa na Al-‘Allaamah Al-Albaaniy. [Angalia vitabu rejea vilivyotangulia vya madhehebu ya Maalik na kitabu cha Tamaam Al-Minna (uk 103). Hapo ameinasibisha kauli hii kwamba ni chaguo la Ibn Taymiyah. Amesema: “Ninavyokumbuka”. Ninasema: “Bali ni madhehebu ya nne ya Ibn Taymiyyah kama utakavyokuja kuona. Ametukuka Allaah Asiyesahau”].



Wenye kusema hivi, wameichukulia Hadiyth ya Bisarrah juu ya kama itakuwa ni kwa matamanio, na Hadiyth ya Twaliq juu ya kama si kwa matamanio. Wamesema kuwa kiashirio cha hilo ni neno lake:



((Hiyo ni sehemu ya mwili wako)).



Kwa hiyo kama ataugusa utupu wake bila ya matamanio, basi anakuwa ni kama aliyegusa kiungo chake kingine chochote.





Kauli ya nne:



Kutawadha kwa sababu ya kugusa dhakari kumesuniwa kwa hali yoyote na wala si wajibu.

Ni madhehebu ya Ahmad katika moja ya riwaya zake mbili na Shaykh wa Uislamu Ibn Taymiyah. Ni kauli ambayo Al-‘Allaamah Ibn ‘Uthaymiyn - Allaah Amrehemu – anaonekana kuwa ameipondokea zaidi, isipokuwa amelijaalia hilo kuwa ni Sunnah endapo kama ataigusa dhakari bila matamanio, na akatilia nguvu kuwa ni wajibu kama ni kwa matamanio kwa njia ya tahadhari. [Majmu’u Al-Fataawaa (21/241) na Ash-Sharhu Al-Mumti’i (1/233)]. Kwa hivyo wameichukulia Hadiyth ya Bisarrah kuwa ni Sunnah na Hadiyth ya Twaliq kuwa maswali yaliyoulizwa yalikuwa ni kwa upande wa wajibu.



Kauli mbili za mwisho zinazosimamia juu ya mkondo wa kukusanya zinatolewa dalili kwa haya yafuatayo:



(a) Ni kwamba dai la kuwepo “naskh” kwa vile Twaliq alitangulia kusilimu kabla ya Bisarrah, ni lazima liangaliwe. Kwa kuwa dai hilo si dalili ya kuwepo “naskh” kwa upande wa wahakiki waliobobea katika fani ya taaluma ya “Uswuul”, kwa sababu aliyetangulia kusilimu anaweza kuwa alihadithia akiwa amenukulu toka kwa mwingine.



(b) Katika maelezo ya Twaliq, kuna sababu ambayo haiwezi kuondoka, nayo ni kuwa dhakari ni sehemu ya mwili wake. Na kama hukmu itafungamanika na sababu isiyoweza kuondoka, basi hukmu haiondoki. Kwa hiyo “naskh” haiwezekani kuwepo.



(c) Kisha ni kuwa suala halipelekwi katika “naskh” ila baada ya kushindikana kukusanya na hasahasa tukizingatia kuwa haifai kufanya “naskh” kama ilivyotangulia.



Ninasema: "Kauli ya mwisho ndiyo yenye nguvu kwa mujibu wa hali. Lakini endapo kama Hadiyth ya Twaliq bin ‘Aliy itakuwa ni Swahiyh - na hili liko mbali bali kauli ya kuifanya Dhwa’iyf ndiyo yenye mwelekeo zaidi - , basi kauli itakayokuwa na uzito ni ile isemayo kuwa kugusa uume kunatengua wudhuu kwa hali yoyote, ni sawasawa ikiwa ni kwa matamanio au bila ya matamanio, kwa vile matamanio hayana mpaka na wala hakuna dalili ya kipimo chake. Na Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.



Faida Kuhusu Yaliyotangulia



(a) Mwanamke akigusa utupu wake atatawadha:

Ni kwa Hadiyth ya ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake aliyenukuu toka kwa babu yake, amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((من مس ذكره فليتوضأ، وأيما امرأة مست فرجها فلتتوضأ))

((Mwenye kuigusa dhakari yake atawadhe, na mwanamke yeyote aliyeugusa utupu wake, basi atawadhe)). [Swahiyh kwa nyingine: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ahmad (2/223) na Al-Bayhaqiy (1/132)].



Hadiyth hii inatiliwa nguvu na kauli ya ‘Aaishah Allaah Amridhie isemayo:



“Mwanamke akiugusa utupu wake, atawadhe”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ash-Shaafi’iy katika “Musnadi yake” (90) na Al-Bayhaqiy (1/133). Al-Haakim amesema ni Swahiyh (1/138)].



Na asili ni kwamba wanawake ni washiriki wa wanaume katika hukmu. Na haya ndiyo madhehebu ya Ash-Shaafi’iy na Ahmad kinyume na Abu Haniyfah na Maalik!!



(b) Kugusa utupu wa mwingine:



Ikiwa mwanamume ataugusa utupu wa mkewe, au mkewe akaigusa dhakari yake, basi hakuna dalili ya kutenguka wudhuu wa yeyote kati yao isipokuwa tu kama madhii au manii yatatoka. Hapo wudhuu utatenguka kwa kutokwa na maji hayo na si kwa kuguswa. Lakini Maalik na Ash-Shaafi’iy wamesema kuwa ni lazima kutawadha kwa kujengea juu ya madhehebu yao kuwa wudhuu unatenguka kwa kumgusa mwanamke. Baadaye tutakuja kuona kwamba kauli yenye nguvu ni kinyume cha hivyo. [Mawaahib Al-Jaliyl (1/296) na Al-Ummu (1/20)].



Aidha, wudhuu hautenguki ikiwa mwanamke au mwanamume ataugusa utupu wa mtoto. Maalik amekubaliana na hili. Nayo pia ni kauli ya Az-Zuhriy na Al-Awzaa’iy. [Al-Kaafiy cha Ibn ‘Abdu Al-Barri (1/149) na Al-Awsatw (1/210)].





(c) Yote ni sawasawa kuugusa utupu kwa makosa au kwa kukusudia [Al-Muhalla (1/241) na Al-Awsatw (1/205-207)].



Ni madhehebu ya Al-Awzaa’iy, Ash-Shaafi’iy, Is-Haaq na Ahmad.



Na kundi la Maulamaa linaona kuwa lenye kutengua wudhuu ni kukusudia kuugusa. Kati yao ni Mak-huul, Jaabir bin Zayd na Sa’iyd bin Jubayr. Pia ni madhehebu ya Ibn Hazm aliyetolea dalili kwa Neno Lake Subhaanah:



((وَلَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ فِيمَا أَخْطَأْتُمْ بِهِ وَلَٰكِنْ مَا تَعَمَّدَتْ قُلُوبُكُمْ ۚ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا))

((Wala si lawama juu yenu kwa mlivyokosea, lakini zipo lawama katika yale ziliyofanya nyoyo zenu kwa makusudi)). [Al Ahzaab (33:6)]



Yenye nguvu zaidi ni kauli ya kwanza. Ibn Al-Mundhir amesema: “Inampasa aliyekufanya kuugusa utupu kwa maana ya hadathi yenye kuwajibisha kutawadha, akufanye kukusudia kwake au kutokusudia kuwa ni sawa kama ilivyo kwa hadathi nyinginezo”.



Ninasema: “Kukosea na kusahau kwa yanayohusiana na masharti na nguzo, kunasamehewa lakini hakuondoshi hukmu. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi".





(d) Kugusa juu ya nguo hakutengui:



Kwa vile hili haliitwi kugusa kama inavyoonekana. Hili linatiliwa nguvu na Hadiyth ya Abu Hurayrah ambayo ni marfu’u:



إذا أفضى أحدكم بيده إلى ذكره ليس بينهما شيئ فليتوضأ

((Akipeleka mmoja wenu mkono wake katika dhakari yake bila kuwepo kizuizi kati yao, basi atawadhe)). [Hadiyth Hasan: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-Daara Qutwniy (1/147) na Al-Bayhaqiy (1/133). Na tizama pia katika Asw-Swahiyhah (1235)].





(e) Kugusa tundu ya nyuma hakutengui [Al-Muhallaa (1/238) na Al-Awsatw (1/212)].



Ni kwa vile tundu ya nyuma haiitwi utupu. Na si sahihi kuwekwa mizani moja na dhakari kwa kutokuwepo sababu jumuishi kati ya kugusa tundu ya nyuma na dhakari. Na kama mtu atasema kuwa sehemu zote mbili ni mapitio ya najsi, basi atajibiwa kuwa hiyo siyo sababu ya kutenguka wudhuu kutokana na kugusa. Halafu ikiwa kugusa najsi hakutengui wudhuu, basi vipi utenguke kwa kugusa mapitio yake?!! Hii ni kauli ya Maalik, Ath-Thawriy na Abuu Haniyfah na wenzake kinyume na Ash-Shaafi’iy.





6- Kati ya yanayotengua wudhuu ni kula nyama ya ngamia:



Aliyekula nyama ya ngamia sawasawa ikiwa mbichi, iliyopikwa au ya kuchoma, ni lazima atawadhe. Hii ni kwa Hadiyth ya Jaabir bin Samrah anayesema kwamba mtu mmoja alimuuliza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): “Je, tutawadhe kwa kula nyama ya kondoo au mbuzi?” Akamjibu:

((إن شئت توضأ، وإن شئت فلا تتوضأ))

((Ukitaka tawadha, ukitaka usitawadhe)).

Akamuuliza: “Je, tutawadhe kwa kula nyama ya ngamia?” Akasema:

((نعم، توضأ من لحوم الابل))

((Ndiyo, tawadha ukila nyama ya ngamia)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (360) na Ibn Maajah (495)].



Na imepokelewa toka kwa Al-Barraa bin ‘Aazib kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

توضأوا من لحوم الابل، ولا توضأوا من لحوم الغنم

((Tawadheni kwa kula nyama ya ngamia, na msitawadhe kwa kula nyama ya kondoo na mbuzi)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (184), At-Tirmidhiy (81) na Ibn Maajah (494)].



Na haya ni madhehebu ya Ahmad, Is-haaq, Abu Khaythamah, Ibn Al-Mundhir na Ibn Hazm. Pia ni moja kati ya kauli mbili za Ash-Shaafi’iy na ni chaguo la Shaykh wa Uislamu. Aidha, ni kauli iliyopokelewa toka kwa Ibn ‘Umar na Jaabir bin Samrah.



Lakini Jamhuri ya Maulamaa kama Abu Haniyfah, Maalik, Ash-Shaafi’iy, Ath-Thawriy na kundi la watangu wema, hawa wanaona kwamba si lazima kutawadha kwa kula nyama ya ngamia bali ni Sunnah. [Al-Mabsuwtw (1/80), Mawaahib Al-Jaliyl (1/320), Al-Majmuu (1/57), Al-Mughniy (1/138), Al-Muhalla (1/241) na Al-Awsatw (1/138)].





Na hii ni kutokana na Hadiyth ya Jaabir aliyesema: “Amri mbili za mwisho toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kutotawadha kwa kula kilichoivishwa kwa moto”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (192), Attirmidhiy (8) na An-Nasaaiy (1/108)].



Wakiizungumzia kauli hii wamesema: “Neno lake “kile kilichoivishwa kwa moto” linakusanya nyama ya ngamia vilevile, nayo imethibiti kunasikhiwa”.

Hili linajibiwa kwa mambo mawili: [Al-Muhallaa (1/244) na Al-Mumti’i (1/249)].





La kwanza:



Ni kwamba Hadiyth ya Jaabir ni jumuishi, na yale yaliyopokelewa katika kutenguka wudhuu kwa kula nyama ya ngamia ni hali maalumu. Na jambo jumuishi hutangulizwa kabla ya jambo maalumu, na hapo hutoka lile ambalo umaalumu wake umeainishwa na dalili. Na hapa naskhi haizungumziwi kwa vile inawezekana kukusanya.



La pili:



Amri iliyokuja kuamuru kutawadha kwa kula nyama ya ngamia, ni hukmu inayohusiana na iliyoivishwa kwa moto au mbichi. Kwa hiyo kuivishwa kwa moto hakuwajibishi kutawadha, na kwa hivyo hukmu yake inakuwa nje ya habari zilizokuja kuhusu kutawadha kwa kula kilichopikwa na kwa kunaskh wudhuu.



Baadhi yao wanasema kwamba makusudio ya wudhuu katika Hadiyth ni kuosha mkono!! [Majmu’u Al-Fataawaa (21/260 na baada yake)].



Hili ni batili kwani hakuna wudhuu mwingine uliokuja kupitia maneno ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zaidi ya wudhuu wa Swalaah. Kisha, katika Hadiyth ya Jaabir bin Samrah iliyopokelewa na Muslim, amri ya kutawadha kwa sababu ya kula nyama ya ngamia, imefungamanishwa na kuswali katika sehemu ya malalio yao kwa kutofautisha kati ya hilo na kuswali katika mapumzikio ya mbuzi. Hivi ndivyo unavyojulikana wudhuu wa Swalaah bila mjadala.



Lenye Nguvu:



Ni kuwa ni lazima kutawadha kwa kula nyama ya ngamia kwa hali yoyote ile. Na kwa ajili hiyo, An-Nawawiy katika kitabu cha “Sharh Al-Muslim” (1/328) anasema: Madhehebu haya yana nguvu zaidi ingawa Jamhuri ya Maulamaa wako kinyume nayo.



Tanbihi:



Ya kwanza:



Katika “Sharh Al-Muslim” (1/328), An-Nawawiy ameinasibisha kauli ya kutolazimu kutawadha kwa kula nyama ya ngamia kwa Makhalifa Wanne Waongofu!! Madai haya hayana dalili yoyote wala haijulikani Sanad yoyote kwao inayohusiana na hilo. Ibn Taymiyah Allaah Amrehemu ametanabahisha kuhusu madai haya akisema: “Ama yule aliyenukulu toka kwa Makhalifa Waongofu au Jamhuri ya Maswahaba kwamba wao walikuwa hawatawadhi kwa kula nyama ya ngamia, basi amewatendea kosa. Hilo anakuwa ameliwazia na kulidhania tu kutokana na yale yaliyonukuliwa kuhusu wao ya kuwa walikuwa hawatawadhi kwa kula kilichoivishwa kwa moto…”. [Al-Qawaaid An-Nuwraaniya (uk.9) ikinukulu toka kwa Tamaam Al-Minnah (uk.105)].





Ya pili:

Kisa Mashuhuri Cha Uzushi [Tizama Adh-Dhwa’iyfah ya Al-Albaaniy (1132) na Qaswasun Laa Tathbut cha Mash-huur Hasan (uk.59)].



Kimetangaa baina ya watu wa kawaida kisa wanachokihadithia mara kwa mara. Kisa hiki wamekisikia toka kwa wanafunzi wanaoeleza kwamba ni lazima kutawadha kwa kula nyama ya ngamia. Kisa hiki kinaeleza kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa katika kundi la Maswahaba wake, akasikia harufu ya ushuzi kwa mmoja wao. Swahaba huyo akaona haya kunyanyuka kati ya watu, naye alikuwa amekula nyama ya ngamia. Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

((من أكل لحم جزور فليتوضأ))

((Aliyekula nyama ya ngamia basi akatawadhe)).

Hapo wote waliokuwa wamekula ngamia wakanyanyuka wakaenda kutawadha!!

Kisa hiki ni Dhwa’iyf kwa upande wa Sanad na Munkari kwa upande wa Matni.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



032-Mambo Yasiyotengua Wudhuu



Alhidaaya.com





Mambo haya Maulamaa wamehitilafiana juu ya kutengua kwake wudhuu. Na kwa kuyatafiti kwa kina, itabainika kwamba hayatengui. Kati ya mambo hayo ni:



1- Mwanaume kumgusa mwanamke bila ya kizuizi



Suala hili lina kauli tatu za Maulamaa:



Kauli ya kwanza:

Mwanamume kumgusa mwanamke kunatengua wudhuu kwa hali yoyote. Haya ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy. Ibn Hazm amemuunga mkono. Ibn Mas’uud na Ibn ‘Umar wamesema hivyo hivyo. [Al-Ummu (1/15), Al-Majmu’u (2/23 na baada yake) na Al-Muhalla (1/244)].



Kauli ya pili:

Hakutengui kwa hali yoyote. Ni madhehebu ya Abu Haniyfah na Muhammad ibn Al-Hasan Ash-Shaybaaniy. Pia ni kauli ya Abbaas, Twaawus, Al-Hasan na ‘Atwaa. Kauli hii pia imeungwa mkono na Shaykh wa Uislamu Ibn Taymiyah, nayo ndio kauli yenye nguvu. [Al-Mabsuwtw (1/68), Al-Badaai-’i (1/30), Al-Awsatw (1/126) na Majmu’u’ Al-Fataawaa (21/410)].



Kauli ya tatu:

Kugusa kunatengua kama ni kwa matamanio. Haya ni madhehebu ya Maalik na Ahmad kama ilivyo mashuhuri kwake. [Al-Mudawwanah (1/13), Haashiyat Ad-Dusuwqiy (1/119), Al-Mughniy (1/192) na Kash-Shaaf Al-Qinaa’i (1/145)].



Ninasema (Abu Maalik): "Kigezo cha kimsingi walichokitolea dalili waliosema kwamba wudhuu unatenguka kwa kumgusa mwanamke, ni kauli Yake Allaah Mtukufu:



(( أوْ لامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا))

((..au mmewagusa wanawake, na hamkupata maji, basi tayammum..)). [Al-Maaidah (5: 6)]



Imepokelewa kwa njia sahihi toka kwa Ibn Mas-’oud na Ibn ‘Umar wakisema: “Kugusa ni chini ya daraja ya kuingilia”. [Kauli Swahiyh: Tafsiyr At-Twabariy (1/502) kwa Sanad tofauti Swahiyh].



Lakini Mwanachuoni Mweledi wa umma Ibn ‘Abbaas amehitilafiana nao akisema: “Kugusa na “mubaasharah”, kunamaanisha kuingilia, lakini Allaah Hukifanyia kinaya Akitakacho kwa Akitakacho”. [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Twabariy (9581) na Ibn Abu Shaybah (1/166)].



Na hakuna shaka kwamba tafsiyr yake inapewa kipaumbele kuliko ya wengineo. Halafu, ndani ya Aayah yenyewe, kuna dalili juu yake. Neno Lake Allaah Mtukufu:



(( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا))

((Enyi mlioamini! Mnaposimama kwa ajili ya Swalaah, basi osheni…)).[Al-Maaidah (5: 6)]



Hii ni twahara ya hadathi ndogo kwa kutumia maji. Kisha Akasema:



(( وَإِنْ كُنْتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا ۚ ))

((..na mkiwa na janaba, basi ogeni..))



Hii ni twahara ya hadathi kubwa kwa kutumia maji. Kisha Akasema:



(( وَإِنْ كُنْتُمْ مَرْضَىٰ أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ فَلَمْ تَجِدُوا مَاءً فَتَيَمَّمُوا))

(( Na mkiwa wagonjwa au mmo safarini, au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake na hamkupata maji, basi tayamamuni..))



Na Neno Lake:

(( فَتَيَمَّمُوا))

((Basi tayamamuni)).



Hii ni badali ya twahara mbili. Kwa hiyo Neno Lake:

(( أَوْ جَاءَ أَحَدٌ مِنْكُمْ مِنَ الْغَائِطِ ))

((..au mmoja wenu ametoka chooni… ))



…ni ubainisho wa sababu ndogo. Na Neno Lake:

(( أَوْ لَامَسْتُمُ النِّسَاءَ ))

((Au mmewagusa wanawake..))

..ni ubainisho wa sababu kubwa. [Ash-Sharh Al-Mumti’i (1/239) na mfanowe katika Al-Awsatw (1/128)].



Ijulikane kwamba taawili ya Ash-Shaafi’iy mwenyewe ya maana ya Aayah Tukufu, haikuwa kwa njia ya kukata moja kwa moja, bali inavyoonekana kutokana na maelezo yake ni kuwa yeye amelielezea hilo kwa aina fulani ya tahadhari. [Ameyaelezea haya Shaykh Al-Mash-huwr (Allaah Amhifadhi) katika uhakiki wake wa “Masuala Yenye Mivutano” (2/217)].



Ninasema: "Na kati ya yanayotilia nguvu kwamba kumgusa mwanamke hakutengui wudhuu ni haya yafuatayo:



(a) Hadiyth ya ‘Aaishah aliyesema: “Nilimkosa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) usiku kitandani. Nikapapasa kumtafuta na mkono wangu ukagusa tumbo la nyayo zake mbili zikiwa zimesimamishwa na yeye yuko katika sijdah. Alikuwa akisema:



((اللهم إني أعوذ برضاك من سخطك))

((Ee Mola! Hakika mimi najilinda kwa radhi Zako kutokana na hasira Zako)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (222), Abuu Daawuud (865) na At-Tirmidhiy (3819)].



(b) Na imepokelewa vile vile kutoka kwa ‘Aaishah akisema: “Nilikuwa nikilala mbele ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hali ya kuwa miguu yangu iko sehemu yake ya Qibla. Anaposujudu, alikuwa akinibonyeza na mimi huikunja miguu, na anaposimama nainyoosha”. Anaongeza akisema: “Na nyumba nyakati hizo zilikuwa hazina taa”.[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (382), Muslim (272) na wengineo].



Na katika tamko jingine: “Hata anapotaka kuswali witri, alikuwa akinigusa kwa mguu wake”.[Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na An-Nasaaiy (1/101)].



(c) Waislamu wamekuwa siku zote wakiwagusa wake zao. Na hakuna yeyote aliyenukulu toka kwake (Rasuli) kuwa alikuwa akiwaamuru Waislamu kutawadha kwa kufanya hilo. Na wala haikunukuliwa toka kwa Maswahaba wakieleza kwamba alitawadha kutokana na hilo katika maisha yake. Na wala haikunukuliwa kutoka kwake kwamba alitawadha kwa sababu ya hilo, bali lililonukuliwa kutoka kwake katika As-Sunan, ni kuwa alikuwa akiwapiga busu baadhi ya wakeze na wala hatawadhi. [Maimamu wameitia doa: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (178) na An-Nasaaiy (1/104). Na waliotangulia wameitia ila. Tazama Sunan Ad-Daar Qutwniy (1/135-142)].



Kuwa Hadiyth hii ni Swahiyh kuna hitilafu. Lakini hata hivyo, hakuna hitilafu kuhusu kwamba haikunukuliwa kuwa yeye alitawadha kwa sababu ya kumgusa (mwanamke). [Majmu’u Al-Fataawaa (21/410, 20/222) na sehemu nyinginezo].



Ama kauli ya kutenguka wudhuu kwa kugusa kwa matamanio au kutotenguka kwa kugusa bila matamanio, kauli hii haina hoja. Lakini hata hivyo inaweza kusemwa: “Ikiwa atatawadha kwa sababu amemgusa mwanamke kwa matamanio lakini bila ya kumwingilia, basi itakuwa ni vizuri kwa ajili ya kuzima matamanio kama ilivyokuwa imesuniwa kutawadha kwa sababu ya hasira ili kuzituliza. Ama kulazimu kutawadha, hilo haliko. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi".





2- Kutoka damu sehemu isiyo ya kawaida sawasawa ikiwa ni kwa jeraha au kuumikwa, au ikiwa ni nyingi au kidogo



Hili halitengui kwa mujibu wa kauli mbili sahihi za Maulamaa. Ni madhehebu ya Ash-Shaafi'iy na Maalik. Lakini Abuu Haniyfah anasema kwamba hili linatengua. Na wafuasi wa Hanbali wanasema kuwa wudhuu hutenguka kama damu ni nyingi. [Al-Ummu (1/180), Al-Majmu’u (2/55), Al-Istidhkaar (2/269), Al-Mabsuwtw (1/74) na Al-Mughniy (1/184)].



Kauli ya kwanza ndio yenye nguvu zaidi kutokana na mambo yafuatayo:



(a) Hadiyth zinazowajibisha kutawadha kutokana na kutokwa damu si Swahiyh.



(b) Ni kwamba asili (ya mambo) ni uhalali. Kwa hiyo anayetawadha wudhuu sahihi, wudhuu huu hautenguki ila kwa matni au Ijma’a.



(c) Ni Hadiyth ya Jaabir bin ‘Abdillah katika kisa cha vita vya Dhaat Ar-Riqaa’i. Anasema: “Swahaba Muhaajir alilala, na mwenzake Mwansari alisimama kuswali. (Akiendelea kuswali) mtu mmoja alimlenga mshale. Akauchomoa akauweka mpaka ikafikia mishale mitatu. Kisha alirukuu na kusujudu na mwenzake (aliyelala) akagutuka. Na alipojua (mlenga mshale) kuwa wao wataweza kumkamata, alikimbia. Na mara Swahaba Muhaajir alipoziona damu zikimchuruzika Mwansari alisema: “ Subhaana Llaah. Kwa nini usingenigutusha mara tu alipokulenga? Akasema: “Nilikuwa nikiisoma Surah na sikupenda kuikatisha”. [Isnadi yake ni Dhwa’iyf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy kama ni Hadiyth Mu’allaq (1/280), Ahmad ameitoa kama ni Hadiyth Mawswuwl (195), Ahmad (3/343), Ibn Hibaan (1096), Al-Haakim (1/156) na Ad-Daara Qutwniy (1/223) na Sanad yake ni Dhwa’iyf kwa sababu ya ‘Uqayl bin Jaabir. Katika Swahiyh Abiy Daawuud (193), Al-Albaaniy ameiona ni Swahiyh!!].



Inavyojulikana ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alilijua hilo na wala hakumkatalia kuendelea na Swalaah baada ya kutokwa na damu. Na lau kama damu ingelikuwa inatengua wudhuu, basi Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) angelimbainishia hilo na wengineo wote waliokuwepo katika vita hivyo. Haijuzu kuchelewesha kulibainisha jambo wakati inapohitajika kufanya hivyo. [As-Sayl Al-Jarraar (1/99)].



(d) Imethibiti kuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab alipochomwa kisu, aliswali na hali jeraha lake linafuka damu.



(e) Habari zimetangaa kutoka zama hadi zama kwamba askari waliokuwa wakipigana Jihadi, walikuwa wakipata maumivu ya majeraha. Hakuna anayeweza kupinga kwamba majeraha haya hayakuwa yakitoka damu na nguo zao kutapakaa damu. Pamoja na haya, walikuwa wakiswali hivyo hivyo. Na hakuna yeyote aliyenukulu toka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba aliwaamuru watoke kwenye Swalaah au wasiswali. Na kwa ajili hiyo, Al-Hasan Al- Baswriy anasema: “Waislamu wangali wanaswali na majeraha yao”. [Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy kama ni Hadiyth Mu’allaq (1/280). Na Ibn Abi Shaybah ameifanya kuwa Hadiyth Mawswuul kwa Sanad Swahiyh kama ilivyo katika Al-Fat-h (1/281)].



3- Kutapika na mfano wake



Madhehebu ya Maulamaa katika suala hili, yako vilevile kama yalivyo katika suala la kutokwa damu. Na lililo sahihi ni kuwa kutapika hakutengui wudhuu kwa vile hoja zinazowajibisha kutawadha hazina usahihi wowote na kwamba asili ya mambo ni uhalali.



Ama Hadiyth ya Mi’idaan bin Twalha aliyenukuu toka kwa Abi Ddardaai kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitapika, akafungua kisha akatawadha, hakuna shaka kwamba Hadiyth hii haimaanishi kuwa ni lazima kutawadha kama mtu ametapika, kwani hicho ni kitendo tu. Na lengo la kitendo hicho ni kuonyesha kuwa ni vizuri (mustahabbu) kufanya hivyo. Na Allaah Ndiye Ajuaye Zaidi. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (87) na Abu Daawuud (2381). Tazama Al-Irwaa (111)].



4- Kucheka ndani ya Swalaah au nje yake



Maulamaa kwa sauti moja wamekubaliana kwamba kucheka nje ya Swalaah hakutengui twahara wala hakuwajibishi kutawadha, na kwamba kucheka ndani ya Swalaah huibatilisha. Lakini Maulamaa hao wamehitalifiana katika kutenguka wudhuu kwa kucheka ndani ya Swalaah. Abu Haniyfah na wenzake, Ath-Thawriy, Al-Hasan na An-Nakh’iy wanaona kwamba hilo linatengua wudhuu. Wao wameitolea hoja Hadiyth Munqati’i isiyozingatiwa, nayo ni Hadiyth ya Abu Al-‘Aaaliyah isemayo: “Mtu mmoja kipofu alikuja hali ya kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anaswalisha watu. Mtu yule aliporomoka katika shimo ndani ya Msikiti na baadhi ya watu wakacheka. Hapo Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwamuru kila aliyecheka atawadhe na aswali upya”.[Isnadi yake ni dhwa’iyf sana: Imefanyiwa “ikhraaj” na Ad-Daara Qutwniy (1/162) na Ibn ‘Uday (2/716)].



Hadiyth iliyothibiti ni ya Jaabir, nayo ni Mawquuf isemayo: “Ni kwamba (Rasuli) aliulizwa kuhusu mtu anayecheka ndani ya Swalaah”. Naye akajibu:



((يعيد الصلاة ولا يعيد الوضوء))

((Atarudia tena Swalaah yake, lakini hatotawadha upya)). [Hadiyth Swahiyh Mawquwf: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy ikiwa Mu’allaq (1/280), Al-Bayhaqiy kama Hadiyth Mawswuwl (1/144) na Ad-Daara Qutwniy (1/172)].



Hadiyth hii ndio Swahiyh. Ni madhehebu ya Ash-Shaafi'iy, Maalik, Ahmad, Is-Haaq na Abu Thawr. [Al-Majmu’u (2/61), Al-Kaafiy (1/151), Al-Mughniy (1/117) na Al-Awsatw (1/227)].





5- Kuosha maiti na kuibeba



Mwenye kuosha maiti au kumbeba, basi wudhuu wake hautenguki kwa mujibu wa kauli yenye nguvu. Lakini baadhi ya Maulamaa wanaona ni vizuri kuoga kwa aliyemwosha maiti, na kutawadha kwa aliyembeba. Hii ni kwa Hadiyth ya Abu Hurayrah anayesema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:



((من غسل ميتا فليغتسل، ومن حمله فليتوضأ))

((Mwenye kumwosha maiti aoge, na mwenye kumbeba atawadhe)). [Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (3162), At-Tirmidhiy (993), Ibn Maajah (1463) na Ahmad (2/433). At-Tirmidhiy, Ibn Hajar na Al-Albaaniy wameifanya Hadiyth Hasan katika Al-Irwaa (1/174). Lakini linaloonekana ni kuwa inahitaji kuchunguzwa zaidi, kwani imekosolewa!!]

Lakini ikiwa Hadiyth hii ni Swahiyh.





6- Mwenye wudhuu kufanya shaka ya kutenguka wudhuu wake



Mwenye kutawadha wudhuu sahihi, kisha akafanya shaka kama wudhuu umemtenguka au la, basi atabakia juu ya uasili wa kile alichokiyakinisha katika utwahara mpaka atakapopata uhakika kwamba wudhuu wake umetenguka. Na ikiwa atafanya shaka nailhali yuko ndani ya Swalaah, basi hatoivunja mpaka ayakinishe kutenguka wudhuu. Hii ni kwa Hadiyth ya ‘Abdullah bin Zayd aliyesema: “Rasuli alishtakiwa kuhusu mtu anayekuwa na wasiwasi katika Swalaah”. Rasuli akasema:

((لا ينصرف حتى يسمع صوتا أو يجد ريحا))

((Haivunji mpaka asikie sauti au anuse harufu)). [Hadiyth Swahiyh: Imetangulia kuelezwa hivi karibuni].



Al-Baghawiy katika Sharhus Sunnah (1/353) amesema: “Maana yake: Mpaka apate uhakika wa hadathi, kwa vile kusikia sauti au kuwepo harufu ni sharti”.
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



033-Wudhuu Unapasa Kwa Ajili Ya Swalaah Tu Na Si Vinginevyo



Alhidaaya.com







Wudhuu unapasa kwa yule anayetaka kuswali – kama hana wudhuu – sawasawa ikiwa Swalaah ni ya Faradhi, Sunnah au Maiti. Hii ni kwa Neno Lake Subhaana:



((يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُواا))

(( Enyi mlioamini! Mnaposimama kuswali, basi osheni…..)). [Al Maaidah (5:6)]





Na kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((لايقبل الله صلاة بغير طهور))

((Allaah Haikubali Swalaah bila ya wudhuu)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (224) na wengineo].



Haipasi kutawadha kwa jambo jinginelo lisilokuwa Swalaah, na wala haikatazwi kwa asiyekuwa na wudhuu kufanya jambo jingine lolote isipokuwa Swalaah. Lakini wudhuu umesuniwa katika mambo yafuatayo:





Kutufu Al-Ka’abah



“Hatujagundua au kuipata dalili yoyote sahihi na ya wazi yenye kuwajibisha kutawadha kwa wenye kutufu. Maelfu kwa maelfu ya Maswahaba ambao idadi yao hakuna aijuaye ila Allaah, walikuwa wakitufu katika enzi ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Na sisi hatujapata habari yoyote inayoeleza kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwamrisha yeyote kati yao kutawadha kwa ajili ya kutufu pamoja na kuwepo uwezekano wa kutenguka wudhuu kwa wengi kati yao wakati wa kutufu, na kuingia wengi wao katika ‘ibaadah hiyo bila ya wudhuu na hususan katika siku hizo ambapo msongamano ulikuwa mkubwa kama katika twawaf za “Quduwm” na “Ifaadhwah”.



Na kwa vile hakuna dalili yoyote iliyopokewa juu ya kupasa kutawadha kwa ajili ya twawaf, na wala hakuna Ijma’a ya Maulamaa juu ya kupasa hilo pamoja na kuhitajika, basi inabainika kwamba si lazima”. [Jaami'u Ahkaamin Nisaai cha Shaykh wetu Allaah Amhifadhi (2/515)].



Maulamaa wameitolea dalili Hadiyth Marfu’u ya Ibn 'Abbaas juu ya ulazima wa kutufu isemayo:

((الطواف بالبيت صلاة إلا أن الله أباح فيه الكلام))

"Kutufu Nyumba ni Swalaah, isipokuwa Allaah Ameruhusu kuzungumza ndani yake". [Hadiyth Mawquwf: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Al-Haakim na wengineo.



Na haifai kuwa ni Hadiyth Marfu’u, bali lililo sawa ni kuwa ni Hadiyth Mawquwf kama alivyobainisha Shaykh wetu Allaah Amnyanyulie cheo chake katika kitabu cha Jaami'u Ahkaamin Nisaai (2/515-521) kinyume na Mwanachuoni Mkubwa Al-Albaaniy (Allaah Amrehemu) aliyesema kuwa ni Swahiyh katika kitabu cha Al-Irwaa'i (1/156)].



Wamesema: "Ikiwa twawaf ni Swalaah, basi inapasa kutawadha kama ilivyo katika Swalaah". Lakini kauli yao hii inakataliwa kwa mambo mawili:





Kwanza: Si sahihi kwamba Hadiyth hii ni Marfu’u. Lililo sawa ni kuwa ni Hadiyth Mawquuf kutokana na maneno ya Ibn 'Abbaas. Aidha, hili limetiliwa nguvu na At-Tirmidhiy, Al-Bayhaqiy, Ibn Taymiyah, Ibn Hajar na wengineo.





Pili: Na kama tukijaalia kuwa ni Hadiyth Swahiyh, basi haimaanishi kuwa twawaf ni kama Swalaah katika kila kitu mpaka ishurutishiwe masharti yanayohusiana na Swalaah. [Tazama katika Majmu'u Al-Fataawaa (26/198) na Jaami'u Ahkaamin Nisaai (2/522). Ndani yake kuna tofauti 11 kati ya Swalaah na twawaf].



Si hivyo tu, bali Swalaah ya kisharia ambayo sharti yake ni utwahara na mfano wake, ni ile inayofunguliwa kwa takbiyr na kumalizwa kwa tasliym.



Na kwa ajili hiyo, Shaykh wa Uislamu amesema: " Imenidhihirikia kwamba kujitwaharisha na hadathi, - bila shaka yoyote - hakushurutishwi katika twawaf na wala si wajibu. Lakini twahara ndogo (wudhuu) imesuniwa katika twawaf, kwani dalili za kisharia zinaonyesha kuwa si wajibu, na hakuna katika sharia lenye kuthibitisha wajibu wa kutawadha katika twawaf." [Majmu'u Al-Fataawaa (26/298)].



Abu Muhammad Ibn Hazm amekubaliana na hili. [Al-Muhalla (7/179)].







Kugusa Mswahafu:



Maalik, Ash-Shaafiiy, Ahmad na Jamhuri ya Maulamaa, wanaona kwamba haijuzu kwa mwenye hadathi kugusa Mswahafu. [Al-Majmu'u (1/17), Al-Istidhkaar (8/10), Al-Mughniy (1/147) na Al-Awsatw (2/102)].



Kigezo cha ushahidi wao ni mambo mawili:



1- Neno Lake Allaah Mtukufu:

((لَا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ))



(( Hapana akigusaye ila waliotakaswa)). [Al-Waaqi'ah (56: 79)].



2- Hadiyth ya Amri bin Hazm kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaandikia watu wa Yemen barua. Kati ya yaliyoandikwa ni:

((لا يمس القرآن إلا طاهر))

((Asiiguse Qur-aan isipokuwa aliye twahara)). [Hadiyth Dhwaíyf: Ina Sanad Dhwa’iyf na baadhi yake ni karatasi tu zisizo na Sanad yoyote. Maulamaa wametofautiana katika kuipandisha ifikie ngazi ya Hadiyth Hasan. Lakini Al-Albaaniy amesema kuwa ni Swahiyh katika kitabu cha Al-Irwaa (1/158). Lililo wazi zaidi ni kuwa Hadiyth hii haipandi. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi].



Ninasema: "Waliyoyatolea ushahidi yanajibiwa kwa yafuatayo:



1- Haiwezekani kuitolea dalili Aayah hiyo Tukufu isipokuwa kama kiwakilishi kilichopo katika (يمسه) kitarejeshwa kwa Qur-aan. Na kauli dhahiri iliyoshikiliwa na wafasiri wengi ni kuwa kiwakilishi hicho kinarejea kwa Kitabu kilichohifadhiwa huko mbinguni; nacho ni "Al-Lawh Al-Mahfuwdh". Na waliotwaharika ni Malaika. Na hili linaonyeshwa kutokana na muundo wa Aayah Tukufu:





إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾

Hakika hii bila shaka ni Qur-aan tukufu.



فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾

Katika Kitabu kilichohifadhiwa.



لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ ﴿٧٩﴾

Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa. [Al-Waaqi'ah (56: 77-79)].





Na hili linatiliwa nguvu na Neno Lake Subhaanah:



فِي صُحُفٍ مُّكَرَّمَةٍ ﴿١٣﴾

Katika Sahifa zenye kuadhimishwa.



مَّرْفُوعَةٍ مُّطَهَّرَةٍ ﴿١٤﴾

Zimetukuzwa na zimetakaswa.



بِأَيْدِي سَفَرَةٍ ﴿١٥﴾

Katika mikono ya Malaika waandishi.



كِرَامٍ بَرَرَةٍ ﴿١٦﴾

Watukufu, watiifu. ['Abasa (80 : 13-16)].





2- Ama Hadiyth, basi ni Dhwa’iyf na haifai kutolewa dalili, kwa vile imetokana na nyaraka zisizosikika mbali na kuwepo mvutano mkali kuhusu wapokezi wake.

Ama kama tukijaalia kuwa Hadiyth hii ni Swahiyh na kwamba kiwakilishi kinarejea kwa Qur-aan, basi tunasema:



"Kilichotwahara" ni katika visawe vya kilafudhi. Inaweza kuwa kwa maana ya Muumini, au kwa maana ya mtu aliyejitwaharisha na hadathi kubwa, au kwa maana ya mtu aliyejitwaharisha na hadathi ndogo, au kwa maana ya mtu ambaye hana najsi katika mwili wake. Hivyo suala inabidi lirejeshwe katika taaluma ya fani ya "Uswuul" isemayo:



"Mwenye kujuzisha kukichukulia kisawe cha kilafudhi kwa maana zake zote, basi maana hizo atazichukulia hapa. Lakini kwa vile haijuzu kutumia jina la najsi kwa Muumini asiye na wudhuu au mwenye janaba sawasawa ikiwa ni kweli anayo najsi hiyo, au kimajazi, au kilugha kwa kauli ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((المؤمن لا ينجس))

((Muumini hawi najsi)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (279) na Muslim (371)]…….mbali na kuthibiti kuwa Muumini daima ni twahara, basi haiwezekani Aayah au Hadiyth kuitumia maana hiyo. Hivyo basi, inalazimu kulichukulia tamshi kwa asiye mushriki kama Alivyosema Allaah Mtukufu:

((إنَّمَا الْمُشْرِكُونَ نَجَس))

((Hakika washirikina ni najsi)). [At-Tawbah (9 : 28)].



Na kwa Hadiyth iliyokataza kusafiri na Qur-aan kwenda nayo katika nchi ya adui.

Na mwenye kusema kuwa kisawe tamshi kimekusanya maana zote, kwa hivyo hakiwezi kutumiwa mpaka ibainishwe, atajibiwa kuwa hakuna hoja katika Aayah wala Hadiyth na hata kama jina la "aliyetwaharika" litakuwa na maana ya mtu asiye na hadathi ndogo au kubwa. [Limezungumziwa katika Nayl Al- Awtwaar (1/260)].



Kwa hivyo, imejulikana kuwa hakuna dalili yoyote inayoashiria kuwa ni lazima kutawadha kwa ajili ya kugusa Msahafu. Na haya ni madhehebu ya Abu Haniyfah, Daawuud na Ibn Hazm. Na ndivyo hivyo hivyo alivyosema Ibn 'Abbaas na kikundi cha watangu wema. Pia Ibn Al-Mundhir yupo katika mkondo huo huo. [Al-Badaai-'i (1/33), Haashiyat Ibn 'Aaabidiyn (1/173), Al-Muhalla (1/81) na Al-Awsatw (2/103)].



Faida



Hakuna ubaya kusoma Qur-aan kwa mwenye hadathi ndogo au hadathi kubwa bila kugusa Msahafu kwa mujibu wa kauli za Maulamaa zenye nguvu. Suala la kusoma Qur-aan ni jepesi zaidi hapa kuliko suala la kugusa Msahafu kwa mambo yafuatayo:



1- Hakuna Hadiyth yoyote Marfu’u ya Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inayokataza kusoma. Kila Hadiyth iliyopokelewa ni dhwa’iyf na haina hoja yoyote. Ni kama Hadiyth Marfu’u ya ‘Abdullah bin 'Amr:

((لا يقرأ الجنب ولا الحائض شيئا من القرآن))

((Mwenye janaba au hedhi asisome chochote katika Qur-aan)).



Na Hadiyth ya Ibn Rawaaha:



((Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza yeyote kati yetu kusoma Qur-aan akiwa na janaba)).



Na Hadiyth ya ‘Abdullahi bin Maalik:



((إذا توضأت وأنا جنب أكلت وشربت، ولا أصلي ولا أقرأ حتى أغتسل))

"Ninapotawadha nami nina janaba, ninakula na kunywa, lakini siswali wala sisomi mpaka nioge".



Hadiyth zote hizi si Swahiyh. [Zitazame katika Al-Irwaa (192, 485) cha Mwanachuoni Mkubwa Al-Albaaniy na maelezo ya Shaykh Mash-huwr katika Al-Khilaafiyyaat cha Al-Bayhaqiy (2/11). Basi ni vizuri yapitiwe].





2- Imethibiti kutoka kwa 'Aaishah kuwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimdhukuru Allaah Mtukufu katika nyakati zake zote. [Hadiyth Swahiyh Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (373), na imetolewa maelezo na Al-Bukhaariy kabla ya Hadiyth ya (608)].





3- Ni kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamuru wanawake wenye hedhi kutoka siku ya ‘Iyd waketi nyuma ya watu na wafuatilize takbiri zao na du’aa zao. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (971) na Muslim (890)].





Kwa hiyo, hii inaonyesha kuwa mwenye hedhi hupiga takbiyr na humdhukuru Allaah Mtukufu.



4- Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia 'Aaishah wakati alipokuwa na hedhi:

((إفعلي ما يفعل الحاج غير أن لا تطوفي بالبيت))

((Fanya yote ayafanyayo mwenye kuhiji isipokuwa tu usizunguke Ka’abah)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1650)].



Inajulikana kwamba mwenye kuhiji humdhukuru Allaah na husoma Qur-aan.

Na kwa vielelezo hivi, inafahamika kuwa mwenye hadathi hazuiliwi kusoma Qur-aan. Shaykh wa Uislamu anasema: "Haya ndiyo madhehebu ya Abu Haniyfah na ndio madhehebu mashuhuri ya Ash-Shaafi'iy na Ahmad". [Majmuu Al-Fataawaa (21/459) na Al-Awsatw (2/97)].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



34-Mambo Ambayo Mtu Akiyafanya Imesuniwa Awe Na Wudhuu





1- Wakati wa kumdhukuru Allaah Mtukufu



Hapa unaingia uradi wowote, kusoma Qur-aan, kutufu Al Ka’abah na mengineyo.

Wudhuu umesuniwa kwa hayo kutokana na Hadiyth ya Al-Muhaajir bin Qunfudh kwamba yeye alimsalimia Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa anatawadha, naye hakumjibu mpaka alipomaliza. Kisha akamwambia:

((إنه لم يمنعني أن أرد عليك إلا أني كرهت أن أذكر الله إلا على طهارة))

((Hakika hakuna kilichonizuilia kukujibu isipokuwa tu niliona uzito kumdhukuru Allaah mpaka niwe katika twahara)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Abuu Daawuud (17), An-Nasaaiy (1/16), Ibn Maajah (350), Ad-daaramiy (2/287) na Ahmad (5/80). Ni Hadiyth Swahiyh kama ilivyo katika As-Silsilat As-Swahiyhah (834)].



Lakini, Hadiyth hii haiambatani na Hadiyth ya 'Aaishah iliyosajiliwa na Muslim (4/68) isemayo:

Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akimtaja Allaah katika nyakati zake zote.



2- Wakati wa kulala



Imepokelewa toka kwa Al-Barraa bin 'Aazib Allaah Amridhie, amesema: " Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

((إذا أتيت مضجعك فتوضأ وضوئك للصلاة، ثم اضطجع على شقك الأيمن، ثم قل: اللهم أسلمت نفسي إليك...))

((Unapotaka kulala, basi tawadha wudhuu wako wa Swalaah, kisha lala kwa ubavu wako wa kulia, halafu sema: Ee Allaah! Nimeisalimisha nafsi yangu Kwako)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (247), Muslim (2710) na wengineo].



3- Kwa mwenye janaba kama akitaka kula, au kunywa, au kulala, au kumwingilia tena mkewe



Imepokelewa toka kwa 'Aaishah Allaah Amridhie, amesema: "Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapokuwa na janaba na akataka kula au kulala, alikuwa akitawadha wudhuu wa Swalaah". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (288), Muslim (305) na tamko ni lake, Abuu Daawuud (222), At-Tirmidhiy (118), An-Nasaaiy (1/138) na wengineo].



Na imepokelewa na Abuu Sa'iyd Allaah Amridhie toka kwa Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((إذا أتى أحدكم أهله ثم أراد أن يعود فليتوضأ))

((Anapomwingilia mmoja wenu mkewe kisha akataka kurejea tena, basi atawadhe)).[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (3/217), Abu Daawuud (217), At-Tirmidhiy (141) na An-Nasaaiy (1/42)].



4- Kabla ya kuoga



Imepokelewa na 'Aaishah Allaah Amridhie, amesema: "Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipokuwa akioga janaba, huanza kwa kuosha mikono yake, kisha humimina maji katika mkono wake wa kushoto kwa kutumia mkono wa kulia na kuosha utupu wake, kisha hutawadha wudhuu wake wa Swalaah".[Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (248), Muslim (316) na wengineo].



5- Baada ya kula kilichopikwa kwa moto



Ni kwa neno lake Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((توضأوا مما مست النار))

((Tawadheni kwa (kula) kilichopikwa kwa moto)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (351), Abuu Daawuud (192), At-Tirmidhiy (79), An-Nasaaiy (1/105) na Ibn Maajah (485)].



Amri hapa ni ya kupendezeshea kutokana na Hadiyth ya 'Amri bin Umayyah Adh-Dhamriy aliyesema: "Nilimwona Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akilikata bega la kondoo, akala sehemu, kisha akaitwa kwenda kuswali, akasimama, akakitupa kisu, akaswali na wala hakutawadha". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (1/50), Muslim (4/45 An-Nawawiy) na Ibn Maajah (490)].



6- Kujadidisha wudhuu kwa kila Swalaah



Ni kwa Hadiyth ya Buraydah Allaah Amridhie, amesema: "Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akitawadha wakati wa kila Swalaah. Na ilipokuwa siku ya Al Fat-h, alitawadha, akapukusa juu ya khufu zake, akaswali Swalaah nyingi kwa wudhuu mmoja.." Hadiyth. [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Muslim (277), Abuu Daawuud (171), At-Tirmidhiy (61), An-Nasaaiy (1/89) na Ibn Maajah (510)].



7- Kila pale wudhuu unapotenguka



Ni kutokana na Hadiyth ya Bilal iliyotajwa nyumba ya kwamba Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisikia mchakato wa viatu vyake mbele yake peponi. Akamwambia:

((بم سبقتني إليها))

((Ni kwa jambo gani umenitangulia kuelekea huko))?

Akasema: "Ee Rasuli wa Allaah! Kamwe sikuadhini ila niliswali rakaa mbili, na wala kamwe sikupata hadathi ila nilitawadha".

Na Rasuli (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

((لهذا))

((Ni kwa hili)). [Isnadi yake ni Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy alipotaja wudhuu wakati wa hadathi (3689), Abuu Daawuud (3055), Ahmad (21962) na tamko ni lake. Asili yake ni katika Swahiyh Mbili bila ya sehemu ya ushahidi].



8- Kwa kutapika



Ni kwa Hadiyth ya Mu'daan bin ‘Abi Twalha toka kwa Abu Ad-Dardaai kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitapika, akafungua, kisha akatawadha. Kisha alikutana na Thawbaan katika Msikiti wa Damascus akalitaja hilo kwake na Thawbaan akamwambia: "Amesema kweli, na mimi ndiye niliyemmiminia maji yake ya kutawadhia". [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na At-Tirmidhiy (87) na Abuu Daawuud (2381) kwa Sanad Swahiyh].
 
Swahiyh Fiqh As-Sunnah



Mlango Wa Twahara



036- Hukmu Ya Kupukusa Juu Ya Khufu Mbili



Alhidaaya.com





Kupukusa juu ya khufu mbili kunajuzu, lakini kuosha miguu ni bora zaidi kwa mujibu wa Jamhuri ya Wanazuoni. Mahanbali wanaona kwamba kupukusa juu ya khufu mbili ni bora zaidi kwa ajili ya kuitumia ruksa. [Fat-h Al-Qadiyr (1/126), Ash-Sharh Asw-Swaghiyr (1/227), Al-Majmu’u (1/502) na Muntahaa Al-Iraadaat (1/23)].



La sawa ni kuwa lililo bora kwa kila mtu ni kwa mujibu wa hali yake ya uvaaji. Kwa aliyezivaa, basi apukuse juu yake na wala asizivue kwa ajili ya kumfuata Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake. Ama kwa asiyezivaa, basi aoshe miguu na wala asifanye uchu wa kuzivaa ili tu apukuse. [Hili ni chaguo la Shaykh wa Uislamu kama ilivyo katika Al-Ikhtiyaaraat (uk.13)].



Pia, asipapie kuzivua ndani ya muda wake ili tu apate kuosha miguu. Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi.
 
Back
Top Bottom