Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,094
- 34,233
- Thread starter
-
- #2,681
🙏🙏🙏🙏Ndugu zangu waislamu naomba tuulizane hapa,hivi kuna Allah wa ramadhani na Allah wa nje ya Ramadhani?
Kama wapo tofauti ni sahihi sana kufuata maamrisho na makatazo ya huyu wa ramadhani ambaye tuna muheshimu sana
Ila kama Allah ni mmoja sasa inakuwaje hofu yetu na utii wetu ni kipindi cha ramadhani tu?
Je siku nyingine Allah hulala na kujisahau kutufuatilia ndio maana huwa hatumuogopi?
Ndugu zangu maisha ya dunia mwenye dunia yake anasema "maisha ya dunia ni starehe ya mda mfupi sana lkn maisha ya akhera ni yenye kuendelea na ya milele"
Inakuwaje haya maisha ya miaka 60 mpaka 7o tena hapa kwa walio jaaliwa maana si wote ni wenye kufika huko,tunayaona bora kuliko maisha ya milele,ambayo ni starehe kwa watendao mema na mateso kwa watendao maovu na wasio fuata amri ya Allah
Haya maisha ya hapa duniani mfano wake ni kama msafiri ambaye anasafiri kwenda sehemu fulani,akiwa njiani anakuta mti wenye kivuli na anaamua kumpumzika hapo kidogo kisha huyo huendelea na safar yake
Hapa duniani ni kama tupo kivulini tu kwa mda mchache kisha hao tunaelekea kwa Allah,je iweje kivuli cha mda mfupi tu kitusahau lishe safari yetu?
Huu uzima wetu na kuwa kwetu hai tusione tuna miaka mingi sana ya kuishi,hakika kifo ni fumbo kubwa sana,kwani hatujui siku wala saa,juzi tu ijumaa kabla ya swala ya ijumaa tulimswalia jirani yetu na kumkimbiza haraka makaburini kumzika ili tuwahi kuswali swala ya ijumaa
Tukiwa makaburini nikawa natafakari hapa huyu marehemu kitacho msaidia ni amali zake njema/vitendo vyake vyema,sijui alijiandaaje katika uhai wake?
Wakati tunaondoka nikawaza hapa sasa anatusikia tukiondoka na kumwacha peke yake na wakati huo malaika wawili mda si mrefu watamtembelea na kumuhoji maswala mbali mbali,je ana yapi ya kuwaeleza? Maana majibu yake yatategemeana na jinsi gani aliishi hapa duniani
Nilikuwa mnyonge sana,nikasema ipo siku moja watu watasema katika kaburi langu "leta dongo,lete majani na kuanza kufukia kaburi langu na hao wataondoka zao nibaki na malaika wawili,je nitasema nini ikiwa maisha yangu hayakuwa ya ucha mungu?
Allah atunusuru
Tumche Allah ukweli wa kumcha
Mtazamo wa mwezi tarehe 30 March au 31 Eid inaweza kuwa tarehe 31 March au 1 AprilMajirani eti Sikukuu ya Idd inaweza kuwa lini nipange ratiba zangu...
Tunakuombea kwa Mungu akuongozeAllah ni tapeli kama Mwamposa tu.
Tunakuombea kwa Mungu akuongoze
Kama hutojali naomba utuachie hili jukwaa letu kwa amani kabisa
Asante
Asante...Mtazamo wa mwezi tarehe 30 March au 31 Eid inaweza kuwa tarehe 31 March au 1 April
Nilitaka tuu kujua exactly day au siku inayoweza kuangukia nipange ratiba jirani jamani...Mbona bado sana jirani,kuna siku 15 au 14 mbele
Rabbana la tuzigh quloobana baAAda ith hadaytana wahab lana min ladunka rahmatan innaka anta alwahhabuAmiin amiin amiin ukhty,wallah kwa jinsi ambavyo nakuona imani yako waeza sema utadhani ulizaliwa ndani ya uislamu,kumbe ulikuwa upande wa pili na Allah akakuongoza katika nuru yake
Allah azidi kukuzidishia imani pamoja na kizazi chako pia
Nakupenda kwa ajili Allah
Allah atujalie tupate kivuli chake siku hii ya hesabu na zaidi atujalie tuwe miongoni mwa watakaopita bila ya hesabuNaam tuendelee katika moja wapo ya kipengele cha imani
Kuamini SIKU YA MWISHO,,muumini wa kweli basi ni lazima aamini kwamba kuna siku ya mwisho au siku ya kisimamo ambacho hapo matendo ya waja yata angaliwa na kila mtu kulipwa haki yake
Aliofanya uovu atalipwa kwa uovu wake na kwa aliefanya wema atalipwa pia kwa wema wake
Inasemwa kisimamo kitakuwa na urefu wa miaka 50,000 naam miaka 50,000,hapo kila mwanadamu atahojiwa na Allah
Ndio hapo mwanadamu atasema nilitoa sadaka na kuswali kwa ajili yako,ataambiwa hapana ulitoa sadaka ili watu wakuone kwamba wewe ni mtoaji mzuri wa sadaka,atasema niliswali kwa ajili yako,ataambiwa na Allah hapana uliswali ili uonekane mbele za watu kwamba unaswali lkn hukuswali kwa ajili yangu
Ndio maana huwa tunakumbushana kwa lolote unalofanya lenye kheri basi fanya kwa kutaka radhi za Allah
Lakini kuna watu wema watasimama kisimamo cha mda mchache kama mtu anayeswali rakaa mbili tu za sunna,yaani kuna watu kisimamo kitakuwa kifupi mno kutokana na matendo yao
Jua litashushwa na kuna watu kutokana na matendo yao majasho yao yatakuwa katika visigino vyao,wengine magotini na wengine karibia na midomo yao
Kuna watu ambao watapata kivuli kutokana na matendo yao,kwahiyo hiyo siku siyo nyepesi kama tunavyodhani bali hakika ni nzito mno,katika suratul fatiha Allah anasema yeye ni mfalme wa siku ya malipo
Kwahiyo kama Allah amasema yeye ni mfalme wa siku hiyo basi jua hiyo ni siku kubwa mno
Je kama kweli unaamini kuna Siku ya Mwisho je umejiandaa vipi ikiwa wewe ni mtu mwenye imani?
Tumche Allah ukweli wa kumcha
Allah akulipe ramadhani hii sikua na mpango kabisa wa kuingia jf lkn baada ya kufungua siku moja nikakuta notification yako ktk uzi huu kila baada ya ftari nalazimika kupita ktk uzi huu kupata darsa, allah akuhifadhi kakaIli mtu awe na imani lazima amuamini Allah ukweli wa kumuamini,kwamba hakuna yeyote anayepaswa kuabudiwa kwa haki au kususudiwa kwa lolote isipokuwa Allah,na kwamba wala hana mshirika katika ufalme wake na uumbaji
Haifai kwa mtu yoyote kufanya ibada kinyume na kumuabudu Allah,haifai kuombwa na kutakwa msaada kwa yeyote isipokuwa Allah
Kufanya ibada na kukusudiwa kiumbe kingine tofauti na Allah,hio ni shiriki au ushirikina ambao ni dhambi kubwa sana mbele ya Allah,na lau mtu akafa na itikadi hii basi huyo ni wa motoni Milele
Lakini kwa masikitiko makubwa kuna waislamu ambao ama kwa kujua au kutokujua wanaingia katika mkumbo wa kushawishiwa na marafiki na majirani zao kwenda kuombewa na hawa manabii na mitume wenye majina yao hapa mjini,pasina kujua kwamba wanamshirikisha Allah
Kule wanaombewa kwa kuegemeza nguvu zao kwa kiumbe ambacho kimeumbwa na Allah,yaani kiumbe cha Allah kimepewa sifa ya uungu ambacho hakina
Katika qur'an inaelezwa siku ya kiama,Issa bin Mariam ataulizwa,je uliwaambiwa watu wakuabudu wewe na mama yako?
Mja huyu wa Allah atasema "hakika haipaswi kwa mimi kusema maneno hayo,hakika ulikuwa na mimi nilipokuwa nao,na hao ni viumbe wako,ama ukiamua utawahukumu au utawasamehe"
Hayo ni maneno ya mja wa Allah,hakika aliondoka duniani na itikadi moja tu kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah,na hii ilikuwa ndio desturi ya mitume wote wa Allah
Changamoto zako za maisha zisikufanye ukafanya shiriki na baadae ukaja kuangamia
Ntakuja kuendelea na kipengele kingine inshallah
Tumche Allah ukweli wa kumcha
Hii siku ya malipo jaman Allah atupe tu pepo yake kwa rehema zake, nimejikuta nawaza ktk surah al haqqa kuanzia pale anaposema faama man uutiya kitabahu pindi mja atakapopewa kitabua chake huwa naweka hisia kabisa sijui nitapewa kwa mkono wa kulia ama laa subhanallah kisha kitabu kimehifadhi dogo na kubwa tena hakuna kitakachokuokoa isipokua matendo yako. Cheo na mali hazitatufaa kisha pasemwe mshikeni mfunge pingu kisha atupwe motoni la ilaha illa lah, naona bila rehema za Allah kutoboa ngumu lkn najipa moyo kuwa kuna njia mbili either kushukuru ama kukufuru na Allah atatufanyia wepesi ktk njia tutayoichagua, ya rabb tujalie mwisho uliokuwa mwema na usituache tukapotea baada ya kuaminiNaam tuendelee katika moja wapo ya kipengele cha imani
Kuamini SIKU YA MWISHO,,muumini wa kweli basi ni lazima aamini kwamba kuna siku ya mwisho au siku ya kisimamo ambacho hapo matendo ya waja yata angaliwa na kila mtu kulipwa haki yake
Aliofanya uovu atalipwa kwa uovu wake na kwa aliefanya wema atalipwa pia kwa wema wake
Inasemwa kisimamo kitakuwa na urefu wa miaka 50,000 naam miaka 50,000,hapo kila mwanadamu atahojiwa na Allah
Ndio hapo mwanadamu atasema nilitoa sadaka na kuswali kwa ajili yako,ataambiwa hapana ulitoa sadaka ili watu wakuone kwamba wewe ni mtoaji mzuri wa sadaka,atasema niliswali kwa ajili yako,ataambiwa na Allah hapana uliswali ili uonekane mbele za watu kwamba unaswali lkn hukuswali kwa ajili yangu
Ndio maana huwa tunakumbushana kwa lolote unalofanya lenye kheri basi fanya kwa kutaka radhi za Allah
Lakini kuna watu wema watasimama kisimamo cha mda mchache kama mtu anayeswali rakaa mbili tu za sunna,yaani kuna watu kisimamo kitakuwa kifupi mno kutokana na matendo yao
Jua litashushwa na kuna watu kutokana na matendo yao majasho yao yatakuwa katika visigino vyao,wengine magotini na wengine karibia na midomo yao
Kuna watu ambao watapata kivuli kutokana na matendo yao,kwahiyo hiyo siku siyo nyepesi kama tunavyodhani bali hakika ni nzito mno,katika suratul fatiha Allah anasema yeye ni mfalme wa siku ya malipo
Kwahiyo kama Allah amasema yeye ni mfalme wa siku hiyo basi jua hiyo ni siku kubwa mno
Je kama kweli unaamini kuna Siku ya Mwisho je umejiandaa vipi ikiwa wewe ni mtu mwenye imani?
Tumche Allah ukweli wa kumcha
Amiini,naam ni kweli kabisa hakuna kiumbe ambacho kitaingia peponi kwa amali zake bali kwa rehma ya Allah tu kwani hakika mkamilifu ni Allah pekeeHii siku ya malipo jaman Allah atupe tu pepo yake kwa rehema zake, nimejikuta nawaza ktk surah al haqqa kuanzia pale anaposema faama man uutiya kitabahu pindi mja atakapopewa kitabua chake huwa naweka hisia kabisa sijui nitapewa kwa mkono wa kulia ama laa subhanallah kisha kitabu kimehifadhi dogo na kubwa tena hakuna kitakachokuokoa isipokua matendo yako. Cheo na mali hazitatufaa kisha pasemwe mshikeni mfunge pingu kisha atupwe motoni la ilaha illa lah, naona bila rehema za Allah kutoboa ngumu lkn najipa moyo kuwa kuna njia mbili either kushukuru ama kukufuru na Allah atatufanyia wepesi ktk njia tutayoichagua, ya rabb tujalie mwisho uliokuwa mwema na usituache tukapotea baada ya kuamini
Mashaallah nafurahi kusikia hivyo,Allah atufanyie wepesi soteAllah akulipe ramadhani hii sikua na mpango kabisa wa kuingia jf lkn baada ya kufungua siku moja nikakuta notification yako ktk uzi huu kila baada ya ftari nalazimika kupita ktk uzi huu kupata darsa, allah akuhifadhi kaka
Hapa ilimaanisha kwamba hao waja wema watakaa kisimamo cha mda mchache kama kitambo cha mtu kuswali rakaa mbili za suna,yani watachukua mda mdogo sana kuhojiwa wastani kuswali rakaa mbili hazizidi dakika tanoAllah atujalie tupate kivuli chake siku hii ya hesabu na zaidi atujalie tuwe miongoni mwa watakaopita bila ya hesabu
(Naomba kujua hizi rakaa mbili za sunna ni zipi? Dhuha?, baadia na kablia ama zipi?
Nilisoma vibaya nimerejea nimeeelewa shukran, nilidhani kuna fursa ya sunna ya rakaa mbili kwa ajili ya wepesi wa siku hiiHapa ilimaanisha kwamba hao waja wema watakaa kisimamo cha mda mchache kama kitambo cha mtu kuswali rakaa mbili za suna,yani watachukua mda mdogo sana kuhojiwa wastani kuswali rakaa mbili hazizidi dakika tano