Ndugu zangu waislamu naomba tuulizane hapa,hivi kuna Allah wa ramadhani na Allah wa nje ya Ramadhani?
Kama wapo tofauti ni sahihi sana kufuata maamrisho na makatazo ya huyu wa ramadhani ambaye tuna muheshimu sana
Ila kama Allah ni mmoja sasa inakuwaje hofu yetu na utii wetu ni kipindi cha ramadhani tu?
Je siku nyingine Allah hulala na kujisahau kutufuatilia ndio maana huwa hatumuogopi?
Ndugu zangu maisha ya dunia mwenye dunia yake anasema "maisha ya dunia ni starehe ya mda mfupi sana lkn maisha ya akhera ni yenye kuendelea na ya milele"
Inakuwaje haya maisha ya miaka 60 mpaka 7o tena hapa kwa walio jaaliwa maana si wote ni wenye kufika huko,tunayaona bora kuliko maisha ya milele,ambayo ni starehe kwa watendao mema na mateso kwa watendao maovu na wasio fuata amri ya Allah
Haya maisha ya hapa duniani mfano wake ni kama msafiri ambaye anasafiri kwenda sehemu fulani,akiwa njiani anakuta mti wenye kivuli na anaamua kumpumzika hapo kidogo kisha huyo huendelea na safar yake
Hapa duniani ni kama tupo kivulini tu kwa mda mchache kisha hao tunaelekea kwa Allah,je iweje kivuli cha mda mfupi tu kitusahau lishe safari yetu?
Huu uzima wetu na kuwa kwetu hai tusione tuna miaka mingi sana ya kuishi,hakika kifo ni fumbo kubwa sana,kwani hatujui siku wala saa,juzi tu ijumaa kabla ya swala ya ijumaa tulimswalia jirani yetu na kumkimbiza haraka makaburini kumzika ili tuwahi kuswali swala ya ijumaa
Tukiwa makaburini nikawa natafakari hapa huyu marehemu kitacho msaidia ni amali zake njema/vitendo vyake vyema,sijui alijiandaaje katika uhai wake?
Wakati tunaondoka nikawaza hapa sasa anatusikia tukiondoka na kumwacha peke yake na wakati huo malaika wawili mda si mrefu watamtembelea na kumuhoji maswala mbali mbali,je ana yapi ya kuwaeleza? Maana majibu yake yatategemeana na jinsi gani aliishi hapa duniani
Nilikuwa mnyonge sana,nikasema ipo siku moja watu watasema katika kaburi langu "leta dongo,lete majani na kuanza kufukia kaburi langu na hao wataondoka zao nibaki na malaika wawili,je nitasema nini ikiwa maisha yangu hayakuwa ya ucha mungu?
Allah atunusuru
Tumche Allah ukweli wa kumcha