Mzee Kikwete ameongea jambo la busara sanaaa, japo Kwa uzoefu wangu, viongozi walio wengi wakisema "kuchanganya dini na siasa" Huwa wanawalenga wanaowakosoa tu, wakisifiwa msikitini au kanisani huwezi kusikia kamwe wakikemea...

Ukiachilia mbali maoni yake juu ya kuchanganya dini na siasa, atwambie pia kama MKATABA huh anauona kuwa sawa au lah... Samia ametuangusha mno kwenye hili jambo, anafanya watanzania wengi kumkumbuka Magufuli wao!
 
JAKAYA UMECHELEWA SANA .DINI NA SIASA

Wassalamu Aliukhum Mabibi na Mabwana.

Kwanza nianze kwa kumshukuru Mola wetu kwa yote mema, aliotujaalia.

Naitwa Abubakari Mtanzania toka hapa tanganyika

Kubwa lililonisukuma kuandika majibu ya hoja ya dini kwa Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,

(1)ni kauli yake ya udini & siasa kuchanganywa
(2)Kwanini Leo jumapili
(3)anajua kilichotufikisha hapa au hakijui?

Mzee kikwete Kwanza heshima yako Baba yangu na nikupongeze Sana kwa hotuba nzuri ulipotoka Leo hii jumapili siku maalumi kwa ndugu zetu wakristo wanayokutana na kufanya Ibada kwa Mola .

~FIKRA ZANGU HURU~

Nilijiuliza Sana kwanini Mzee wangu aka wa msoga ameamua kuleta taharuki kwa kauli yake ya dini na siasa?

Na ikifuatana na Ile ya ndugu Camilius wambura inayohusu kupinduliwa kwa serikali

Naomba NImkumbushe ndugu Jakaya haya yafuatayo

(1)anafahamu taasisi za dini kuwa zinatambulika kisheria ?

(2)katika tawala zetu zote kila zinapoanza kazi pale ikulu sio lazima ila mara nyingi wamekuwa wakiwaita viongozi wa dini na kutambua uwepo wao na hiii ni kutokana na majukumu ynayofanya na dini zetu katika jamii zetu hasa kimwili na kiroho pia

Lakini pia serikali inapotaka kufanya kampeni za Amani,ama maendeleo hutumia majukwaa haya ya kidini kutimiza malengo Yao na kutaka kuungwa mkono na waamini

Sasa dini na siasa ni mambo ya ayokwenda pamoja maana hata mzungu na mwarabu walikuwa na malengo nyuma ya dini hizi walizotuletea

Ambayo kimsingi hayana tofauti na siasa na ajenda hiyo ni moja tu kukuwekea mfumo wezeshi wa kukutawala wewe kikwete na Mimi Abubakar,Peter na John

Wakishindwa kuwagawa katika siasa watawagawa kupitia dini zenu

Mzee kikwete unakumbuka kuwaona DPW wakipita misikitini na kutoa misaada hapa tanzania

Na nikajiuliza kwanini hawajaenda makanisani

Lakini kwanini wapite kutoa misaada nyakati hizi ambazo sio rafiki kwao wala kwetu tena tukiwa tunajadili mikataba ilioletwa na wao na serikali yetu?

Na walipomaliza Hilo tuliona waislam wenzetu wakitoka na kupambana na watanzania wengi wanaojitokeza kupinga issue ya mkataba wa bandari

Mzee kikwete hukusema neno ulikaa kimya Mzee wangu, watanzania pia walipiga kelele kwa serikali iwazuie DP world kupitia misikitini na kuwanunua viongozi wa dini hizi kwa hongo ndogo ndogo huku wakiwa na lengo la viongozi hao wa dini watetee Jambo ambalo ni kharam kwa mujibu wa quran tukufu..

Sasa Mzee kikwete nini kimekusibu Leo ikiwa siku ya ndugu zetu wakiristu kuabudu ndio ukaja na tamko hili kwanini usingoje?

Lakini swala la kuichanganya dini na siasa Sisi raia tumejifunza toka kwenu ninyi watawala hasa serikali yetu hii sasa kama kuanza dhambi hii basi serikali ndio imeanza na Sisi tunamalizia

Mzee kikwete nadhani kingine umeshau ni kujiuliza nini kimetufikisha hapa . Naamini unakifahamu na kama ukifahamu nikumbushe

Mzee kikwete shida ni mkataba wa hovyo ulioingiwa na serikali ya tanzania na Dubai port would (DPW) tuliousoma mkataba huu tumegindua Una shida nyingi Sana ambazo kama taifa hatupaswi kufikiria hata kidogo kuingia mkataba wa aina hii

Huku majukwaani genge lako la wanasiasa wanakuja kutudanganya na wanatulazimisha tukubaliane na uongo wao

Mzee kikwete si wewe uliondoa dubwasha la Richmond?Mzee lowasa alipokuandikia anataka kujiuzuru ukabariki sio

Sasa ni sawia na hili watanzania huku mtaani tumeusoma mkataba na HATUUTAKI

Matarajio yetu mengi yalikuwa ni kukuona wewe kikwete uje hapa na ueleze msimamo wako kwenye Hilo Sakata la bandari na sio kukaa kimya ama kujificha kwenye mgongo wa dini la hasha haitotusaidia

Tumewaona baadhi ya wataafute wenye heshima kubwa katika taifa hili wakitoa maoni Yao juu ya hili la bandari ila wewe umekaa kimya

Sasa Baba yangu kikwete nikumbushe tatua tatizo lililotufanya tujikwae na usije ukatatua tatizo la hapa tulipoangukia

Lakini mwisho nikutoe hofu Mzee wangu wa msoga NI,huku mtaani sote tunaongea lugha moja tu nayo ni KATAA MKATABA WA DUBAI PORT WORLD (DPW)

kwa swala la udini hatuna shida kabisa na Moshi uliomwaga na hawa wakiristu Leo ni Sisi pamoja na Mimi Abubakar ndio hasa tunachokitaka kifanyike na sio vinginevyo

Hawa viongozi wetu wa dini hizi tunawajua baadhi Yao wakipewa makobazi, tende ,na mafuta ya Kula huku wakinogeshwa na nyama ya ngamia basi wanatusaliti

Tunawajua vyema sauti yeti Sisi watanzania hatutaki uwekezaji kharam usio na manufaa na taifa hili

Sasa Mzee kikwete njoo tusikie maoni yako ili tuokoe lasilimali za wajukuu wa Ridhiwani,na Mimi Abubakar wakati ninyi mkiwa mmeshatuacha katika dunia hii

Asante Baba wako mwananchi
Abubakar zuberi Mlangumbulu
Tanzania
 
Kwanza atwambie kwa nini anachukua 9% kila mwezi toka mapato ya bandarini. Familia ya wezi na wasioridhika na pesa kana kwamba hawatakufa! Hana audacity yoyote ya kuongea hapa!
 
Mzee Kikwete ameongea jambo la busara sanaaa, japo Kwa uzoefu wangu, viongozi walio wengi wakisema "kuchanganya dini na siasa" Huwa wanawalenga wanaowakosoa tu, wakisifiwa msikitini au kanisani huwezi kusikia kamwe wakikemea...

Ukiachilia mbali maoni yake juu ya kuchanganya dini na siasa, atwambie pia kama MKATABA huh anauona kuwa sawa au lah... Samia ametuangusha mno kwenye hili jambo, anafanya watanzania wengi kumkumbuka Magufuli wao!
Elimu dunia tu ndo inayowasumbua!
 
Wakati wahadhiri wa kiislamu wanaunga mkono kuuzwa bandari ulikuwa kimya ukifurahia ,Wala hukuona ubaya wake,
Kuuzwa bandari ni sera ya ccm, wahadhiri wa kiislamu waliunga mkono sera ya Chama ,hapo hawakuchamganya dini na siasa? Bali wanaopinga ndiyo wanachanganya dini na siasa! Mstaafu utakuwa wa ajabu kidogo.
Wewe umekuwa , kamanda wa jeshi, unajua kabisa kama kamanda ,maamuzi mabaya yatawagawa wafuasi, ili kurejesha mshikamano wa wafuasi wako lazima kuondoka au kuacha utekelezaji wa maamuzi mabaya iwe ni Kwa wazi au kimya kimya.
Umekuwa kiongozi tena wa nagazi ya juu kabisa katika nchi yetu. Unajua vema maamuzi mabaya yanagawa watu. Ukweli ni kwamba Kwa maamuzi haya mabovu ya ccm watanzania wamegawika SI kidini bali kimsimamo kutokana na maamuzi mabaya.
Wakati mtoto mdogo anawatukana wazee waliolitumiakia Taifa hili Kwa heshima, wengine wakiwa walimu wake , kuwa ni wapumbavu! Ulikaa kimya unaona ni sawa tu.
 
Nchi yetu imekua na Viongozi taburarasa Sana.. Viongozi wetu siku zote huwa wanajiona wako sahihi. Katika hili swala. Wakisifiwa na dini sawa ila wakikosolewa wanatoka mashimon kama panya waliovamiwa na paka
20230820_194933.jpg
 
JAKAYA UMECHELEWA SANA .DINI NA SIASA

Wassalamu Aliukhum Mabibi na Mabwana.

Kwanza nianze kwa kumshukuru Mola wetu kwa yote mema, aliotujaalia.

Naitwa Abubakari Mtanzania toka hapa tanganyika

Kubwa lililonisukuma kuandika majibu ya hoja ya dini kwa Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,

(1)ni kauli yake ya udini & siasa kuchanganywa
(2)Kwanini Leo jumapili
(3)anajua kilichotufikisha hapa au hakijui?

Mzee kikwete Kwanza heshima yako Baba yangu na nikupongeze Sana kwa hotuba nzuri ulipotoka Leo hii jumapili siku maalumi kwa ndugu zetu wakristo wanayokutana na kufanya Ibada kwa Mola .

~FIKRA ZANGU HURU~

Nilijiuliza Sana kwanini Mzee wangu aka wa msoga ameamua kuleta taharuki kwa kauli yake ya dini na siasa?

Na ikifuatana na Ile ya ndugu Camilius wambura inayohusu kupinduliwa kwa serikali

Naomba NImkumbushe ndugu Jakaya haya yafuatayo

(1)anafahamu taasisi za dini kuwa zinatambulika kisheria ?

(2)katika tawala zetu zote kila zinapoanza kazi pale ikulu sio lazima ila mara nyingi wamekuwa wakiwaita viongozi wa dini na kutambua uwepo wao na hiii ni kutokana na majukumu ynayofanya na dini zetu katika jamii zetu hasa kimwili na kiroho pia

Lakini pia serikali inapotaka kufanya kampeni za Amani,ama maendeleo hutumia majukwaa haya ya kidini kutimiza malengo Yao na kutaka kuungwa mkono na waamini

Sasa dini na siasa ni mambo ya ayokwenda pamoja maana hata mzungu na mwarabu walikuwa na malengo nyuma ya dini hizi walizotuletea

Ambayo kimsingi hayana tofauti na siasa na ajenda hiyo ni moja tu kukuwekea mfumo wezeshi wa kukutawala wewe kikwete na Mimi Abubakar,Peter na John

Wakishindwa kuwagawa katika siasa watawagawa kupitia dini zenu

Mzee kikwete unakumbuka kuwaona DPW wakipita misikitini na kutoa misaada hapa tanzania

Na nikajiuliza kwanini hawajaenda makanisani

Lakini kwanini wapite kutoa misaada nyakati hizi ambazo sio rafiki kwao wala kwetu tena tukiwa tunajadili mikataba ilioletwa na wao na serikali yetu?

Na walipomaliza Hilo tuliona waislam wenzetu wakitoka na kupambana na watanzania wengi wanaojitokeza kupinga issue ya mkataba wa bandari

Mzee kikwete hukusema neno ulikaa kimya Mzee wangu, watanzania pia walipiga kelele kwa serikali iwazuie DP world kupitia misikitini na kuwanunua viongozi wa dini hizi kwa hongo ndogo ndogo huku wakiwa na lengo la viongozi hao wa dini watetee Jambo ambalo ni kharam kwa mujibu wa quran tukufu..

Sasa Mzee kikwete nini kimekusibu Leo ikiwa siku ya ndugu zetu wakiristu kuabudu ndio ukaja na tamko hili kwanini usingoje?

Lakini swala la kuichanganya dini na siasa Sisi raia tumejifunza toka kwenu ninyi watawala hasa serikali yetu hii sasa kama kuanza dhambi hii basi serikali ndio imeanza na Sisi tunamalizia

Mzee kikwete nadhani kingine umeshau ni kujiuliza nini kimetufikisha hapa . Naamini unakifahamu na kama ukifahamu nikumbushe

Mzee kikwete shida ni mkataba wa hovyo ulioingiwa na serikali ya tanzania na Dubai port would (DPW) tuliousoma mkataba huu tumegindua Una shida nyingi Sana ambazo kama taifa hatupaswi kufikiria hata kidogo kuingia mkataba wa aina hii

Huku majukwaani genge lako la wanasiasa wanakuja kutudanganya na wanatulazimisha tukubaliane na uongo wao

Mzee kikwete si wewe uliondoa dubwasha la Richmond?Mzee lowasa alipokuandikia anataka kujiuzuru ukabariki sio

Sasa ni sawia na hili watanzania huku mtaani tumeusoma mkataba na HATUUTAKI

Matarajio yetu mengi yalikuwa ni kukuona wewe kikwete uje hapa na ueleze msimamo wako kwenye Hilo Sakata la bandari na sio kukaa kimya ama kujificha kwenye mgongo wa dini la hasha haitotusaidia

Tumewaona baadhi ya wataafute wenye heshima kubwa katika taifa hili wakitoa maoni Yao juu ya hili la bandari ila wewe umekaa kimya

Sasa Baba yangu kikwete nikumbushe tatua tatizo lililotufanya tujikwae na usije ukatatua tatizo la hapa tulipoangukia

Lakini mwisho nikutoe hofu Mzee wangu wa msoga NI,huku mtaani sote tunaongea lugha moja tu nayo ni KATAA MKATABA WA DUBAI PORT WORLD (DPW)

kwa swala la udini hatuna shida kabisa na Moshi uliomwaga na hawa wakiristu Leo ni Sisi pamoja na Mimi Abubakar ndio hasa tunachokitaka kifanyike na sio vinginevyo

Hawa viongozi wetu wa dini hizi tunawajua baadhi Yao wakipewa makobazi, tende ,na mafuta ya Kula huku wakinogeshwa na nyama ya ngamia basi wanatusaliti

Tunawajua vyema sauti yeti Sisi watanzania hatutaki uwekezaji kharam usio na manufaa na taifa hili

Sasa Mzee kikwete njoo tusikie maoni yako ili tuokoe lasilimali za wajukuu wa Ridhiwani,na Mimi Abubakar wakati ninyi mkiwa mmeshatuacha katika dunia hii

Asante Baba wako mwananchi
Abubakar zuberi Mlangumbulu
Tanzania
Kikwete unajua vizuuri sana kwamba siasa ipo ndani ya dini , umesoma habari za Mohamed I mtume wa Mungu, utawala wake chanzo chake ni dini, habari za utawala wa Roma huwezi kutenganisha na dini, dini ni maisha ya watu na waasisi wa siasa lengo ni maisha ya watu. Viongozi wa dini wamefanya jukumu lao. Kuwa mkweli itakusaidia.
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.

"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.

"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.

"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."

Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Mstaafu huyu ana 'moral authority' ipi kuanza kukemea viongzoi wa dini wanaotoa maoni kinzani dhidi ya uamuzi wa serikali kuhusu rasilimali za umma lakini anashindwa kukemea wanaosifia kila kitu kuhusu mkataba wa bandari wenye vifungu tata?
Maadamu yeye mwenyewe ametamka kwamba walipojitokeza kundi la wasabato masalia anajua namna alivyomalizana nao!!! Sasa swali ni kwamba aliwapeleka wapi hao waumini wa kanisa la wasabato malia 51 ambao aliamuru wapigwe picha na askari wa uwanja wa ndege tarehe 3 Septemba na tarehe 4 Septemba 2008?
"......KUNDI la waumini wa Dhehebu la Waadventista Wasabato Masalia, kwa mara
ya tatu limesambaratishwa na askari wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere, baada ya kurudi tena uwanjani hapo huku wakiwa
wameongezeka idadi yao kutoka 17 hadi kufikia 51.............
Baada ya kujibiwa hivyo, askari hao waliamua kuorodhesha majina ya
waumini hao na kuchukua jukumu la kuwapiga picha mmoja mmoja na
kuwaamuru watoweke katika viwanja hivyo.............
Waumini hao wakati wakiondoka kwa maandamano, walisindikizwa na kundi
la askari wa uwanja wa ndege, ambao walipofika barabara ya Nyerere,
askari hao walizuia magari kwa muda wa sekunde kadhaa ili kundi hilo la
waumini liweze kuvuka.........."

Kwa hiyo yeye ndio rais kwa sasa na anataka amalizane na TEC kwa mtindo upi?
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.

"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.

"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.

"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."

Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Kumbe alikuwa mwenyewe kwenye hadhira ya dini, akasahau yeye ni mwanasiasa. Huwezi kutenganisha dini na siasa. Dini na siasa ni maisha ya mwanadamu. Hakuna mwenye hati miliki ya kingine! Kama vile ambavyo Kikwete amezungumzia masuala ya dini ndivyo ambavyo Kiongozi wa Dini anaweza kuzungumzia masuala ya siasa. Ukienda kwenye nyumba za Ibada utawakuta wanasiasa kadhalika ukienda kwenye mikutano ya siasa utawakuta viongozi wa dini. Askofu Gwajima na viongozi wengine wa dini walipitishwa na viongozi wa kisiasa. Kikwete, mwanasiasa, asisahau alimteua Mchungaji Lwakatare, kiongozi wa kidini, kuwa mbunge.

Tungejibu hoja zilizotolewa naTEC kuhusu mkataba badala ya hoja za dini na siasa. Ikumbukwe kuwa bandari ni yetu sote; maaskofu wa Tanzania na wengine. Baraza lina haki ya kuhoji juu ya rasilimali zetu.
 
Waislam kwa miaka mingi sana tumejazwa ujinga kwa makusudi kabisa kuaminishwa kuwa ni mwiko kuchanganya siasa na dini.

Huo ni uongo na tumekuwa tukijazwa ujinga "brainwashed" kuamini hilo.
Umeongea ukweli mtup kikwete asitutoe kwenye reli
 
Back
Top Bottom