Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

hizo aya u;izoweka soijaona hapo Injil iko wai na kapewa nani?

Injil ipi unayoisoma wewe? Iko wapi? Na sisi tufaidike nayo.
Simba.
Inachekesha kidogo, ila so mbaya.

Hapo nimezungumzia aya juu ya vitab wala sikuwajibika kusema aya yenye neno injili ndani yake ila kama unataka list ya aya ambazo zinazungumzia Injili utazipata tu.

Moja nainukuu zingine nitazitaja uende ukazisome kwa mda wako.

Al Baqarah 2:241
Al Imran 3:3 (Hii ndio nitainukuu)
1000099138.jpg

Baada ya hapo endelea na huku
Al Imran 3:48, 65, 184
Al Maidah 5:46, 47, 66, 68, 110,
Ar Araf 7:157
At Taubah 9:111
An Anbiyaah 21:24
Fatir 35:25
As Saffat 37:168
Al Fath 48:29
Al Hadid 57:27 (Hii nayo nitainukuu)
1000099139.jpg

Bila kusahau As Saf 61:6

Ukimaliza pote huko utapata majibu iko wapi na kuhusu kapewa nani hapo kwenye Al Hadidi 57:27 ndio iko waaazi kabisa.

Lingine kwamba wapi inapatikana, Jibu ni sehem nyingi tu na moja wapo nyepesi na ya Haraka ni ndani ya Quran tukufu.
 
Teh sijajua kwako hili neno "kuelewa" lina maana gani. So huenda ninacho kimaanisha labda kikawa ni tofauti na kile wewe unacho kimaanisha.

Hayo niliyoyasema ni maana nazozijua ama kufahamishwa kuhusu Arsh ila haina maana ya kua ninazisadiki, kwamba ndivyo zinazotakiwa ziwe. Hapa sijui umenielewa ninacho jarib kukimaanisha?

Kusema "sielewi" ikiwa na maana ya kutowahi kusikia habari zake sio sahihi. Naelewa maana ila sijasadiki maana kwani kwangu katika hizo maana naziona kama zina ukakasi.

Kuhusu kuedelea kufatilia kisa, mie nipo Open Minded sana, sijajifunga kwa aina flan ya uelewa. Nimejiweka huru kujifunza kila aina ya elim mwisho kuchukua lile nalo liona lina faida na mimi.
Ukisadikia au usisadiki ni haki yako. Mimi nimetaka kujua unaelewa maana ya neno Arsh? Jibu jepesi tu, unaelewa au hulewi.

Kusadiki au kutokusadiki haisumbui wala sipo hapa kutaka kukusadikisha au kutokusadikisha kitu.
Simba.
 
Inachekesha kidogo, ila so mbaya.

Hapo nimezungumzia aya juu ya vitab wala sikuwajibika kusema aya yenye neno injili ndani yake ila kama unataka list ya aya ambazo zinazungumzia Injili utazipata tu.

Moja nainukuu zingine nitazitaja uende ukazisome kwa mda wako.

Al Baqarah 2:241
Al Imran 3:3 (Hii ndio nitainukuu)
View attachment 3099157
Hio list yako haimaanishi chochote.

Kucheka pasipo kichekesho ni dalili ya kisaikolojia ya kutojiamini.

Hio aya ulioinukuu ni tofauti na hizo tafsiri ulizoweka, Ndio maana nikakwambia usifate maneno ya Maulamaa fata maneno ya Allah. Jifune kufanya tafsil badala ya tafsiri. Ukishasema ni "tafsiri" hayo yanakua maneno ya mtu, au mwengine au wewe mwenyewe, kwa uelewa wake au wako.

Limeachwa hapo neno "baina ya mikono yake".
Umeliona hapo kwenye Kiarabu au hujaliona?

Kutajwa injili haimaanishi unaisoma injili, kwa hio listi yako haisaidii kitu, neno "injili" sio kitabu ni neno. Hata mimi ninapolitamka hapa neno 'injill" haimaanishi unaisoma injili. Nimetaja neno "injili" mara ngapi hapa?

Nimekuuliza juu huko hio injili unayoisoma wewe iko wapi?

Sasa nimeanza kuelewa kwanini husadiki, jibu ni jepesi sana, kwa sababu huelewi unachokisoma. Kwa maana hio nakuunga mkono ukweli wako wa kutokusadiki, utasadiki vipi kitu ambacho hukielewi?

Naona maswali myepesi unayajengea hoja ndefu mpaka unasahhau ulichoulizwa. Unakumbuka maswali niliokuuliza?

Mwaga elimu.
Simba.
 
Natamani hii thread iendeshwe kwa mfumo wa kimahakama ! Tuteue mawakili wetu hapa, mawakili watokane na uhodari wao wa majibizano kwa kuzingatia uchangiaji wao wa nyuma pamoja na jaji. Then mnyukano uanze hapa ! Otherwise hii elimu tutapewa kwa kusimangwa kama watoto waliofukuzwa Ada shuleni.
😎

Itabidi uteuliwe wewe hapo mleta wazo ha ha.
 
Kama hazina sawa, Mimi nishakupa zenye kisa cha adamu.
Muite Arsis ajibu maswali yamekuwa mengi
Nimerudi mahsusi kwa kisa cha Adam. Mengine In shaa Allah nitayajibu maswali yote ila kwa sas napitia maswala na majibu kuhusu Adam ili kila swali lijibiwe na kila mmoja wetu arisdhike na jibu. Ndio elimu. Kielimu hatuendi "kama hazina sawa" hio inaitwa "hanging" kielimu, yaani jibu linaloning'inia. Elimu inatakiwa iwe na majibu yenye ushahidi kamili. Ukiacha e;limu inaning'inia ina maana haijaeleweka.

Uuri wa elimu ya Allah, kipo kitabu chake, ndio rejea ya kwanza na ya mwisho. kama rejea ya hadithi basi ziwe rejea za haditthi ya Qur'an kama yenyewe inavyosema;

Q 45:6. Hizi Aya za Mwenyezi Mungu tunakusomea kwa haki; basi hadithi gani watakayo iamini baada ya Mwenyezi Mungu na Aya zake? 6
 
Natamani hii thread iendeshwe kwa mfumo wa kimahakama ! Tuteue mawakili wetu hapa, mawakili watokane na uhodari wao wa majibizano kwa kuzingatia uchangiaji wao wa nyuma pamoja na jaji. Then mnyukano uanze hapa ! Otherwise hii elimu tutapewa kwa kusimangwa kama watoto waliofukuzwa Ada shuleni.
Hakimu iwe rejea ya mwisho isio shaka, Qur'an kwa wanaoiamini, kwa wasioiamini watasema wao kitabu kipi ndio rejea ya mwisho.

Binafsi rejea yangu ya mwisho ni Qur'an.
Simba.
 
Mkuu simba heshima yako, sisi wengine tunakufatilia japo kimyakimya. hongera kwa kushea nasi haya mambo mazito kabisa.

Una pumzi ya uandishi! naungana na wakuu wanaoshauri kuyaweka haya kwenye kitabu chako.

Naomba uzoefu wako kwa mambo haya;

(1) je kuna faida/hasara zipi za mtu kuishi/kuchangamana au kuwa karibu na majini?

(2) pia umesema unaweza kuminya pete na usionekane kwa wengine. je hapo unakuwa katika hali gani? je unakuwa bado na mwili wa kibinadamu/mzimu au? mathalani je unaweza kuingia kwenye daladala au chombo cha usafiri bila kuhitaji mahali pa kuketi au kusimama?

(3) sala na utoaji sadaka vina nafasi gani katika kumlinda mtu dhidi ya uovu wa dunia

Ahsante kwa maswali yako mazuri sana.

1) Qur'an inatutaka tusiwaambu wala tusiwaamini majini. Nakushauri isome suratul Jinn nadani ya Qur'an imeelezea vizuri sana.

2) Hilo la pete inavyofanya kazi kunificha nililiuliza sana kwa alienipa hio pete, nimelielewa hivi; Pete nikiiminya kwa kuificha ni mawasiliano tu na Arsis ambae anaweka teknolojia ya kuwekewa kama pazia la kunificha nisionekane. Nabaki kuwa mimi mwenyewe na unaweza kunigusa au kunishika ukahisi lakini hunioni, ndio maana nakwepa sana kugusana na mtu nikifanya hivyo. Nilivypelewa mimi ni teknolojia tu au nsiseme mazingaombwe tu hakuna zaidi.

3) hayo ya sala na sadaka ni mambo makubwa sana kupita maelezo, Qur'an imeyasisitiza sana na ipo wazi kuhusu hayo. Ni kinga ya kila kitu. Mwenyezi Mungu wetu ni kila kitu. Maana mojawapo ya neno "sadaka" no urafiki, unapotoa sadaka unafanya urafiki na Muumba wako, kuna lipi lenye ubora zaidi ya kua rafiki wa muumba wetu?

Sadaka pia ina maana nyingine lakini zinaelekea hukohuko kwenye mema.
Simba.
 
Naomba no ya brother wako anipe elimu huyu arsis hamna kitu sio msaada kabisa
Msaada upi uliuhitaji kwangu?

Maisha yangu yote nimejitoa kutumikia watu wanaohitaji msaada, kadiri ya uwezo wangu na majaaliwa ya Muumba wetu.
Simba.
 
Mjadala unabaki Je ni sahihi mwanadamu na majini kushirikiana katika wema mfano
Kati ya shirikiano au kushirikiana... na ile ya Binadam kutaka msaada kwa kiumbe kingine. Ni kitu kimoja au vitu viwili tofauti???? Em nifahamishe hili.
 
Hapa mimi nina swali kwenye hoja ya kwanza ya Jini.

Kama jini ni kiumbe cha Allah wameumbwa ili wamuabudu Allah, je majini wanatumia kitabu gani?

Je majini ni dini gani?

Je majini wanaswali wapi?

Je kuna ukweli wowote kwamba kuna binadamu wanatengeneza majini na kuyafuga na kuyatuma?

Naomba na Arsis atie neno kwenye haya maswali yangu yanayonitatiza.

Asante.
Siingilii swali lako kwa ndugu yangu hapo ila hapa nafaham kua kuna utofauti wa kuabudu na kusali... Ibada na Sala.

Ndani ya Ibada kuna sala, Sala ni sehem ya Ibada. Kwamba Ibada ni "General", Sala ni "Specific".

Sijajua wengine mnalielewa vipi hili.
 
Mkuu huu uzi umenitisha na kunifundisha mengi sana ambayo mwanzo niliyajua kwa uchache.
Umenisaidia kuachana kabisa na habari za wanawake pia kuwa makini sana na watu tunaokutana nao.
Bila ibada hawa viumbe wanatuchezea km mpira.
Natamani Kiranga apite huku ila nna wasiwasi atatuharibia uzi.
Kuna simulizi inaendelea RADIO FREE AFRICA kwenye kipindi cha SITOSAHAU Juma pili saa 4:00 asubuhi .Kuna jamaa naye anasimulia jinsi gani alivyokutana na kuoa jini mpaka kuishi kwao baharini na vitu vingi vya kutisha Tufatilie huko kwa wanaopenda simulizi.
 
Kati ya shirikiano au kushirikiana... na ile ya Binadam kutaka msaada kwa kiumbe kingine. Ni kitu kimoja au vitu viwili tofauti???? Em nifahamishe hili.
Kama nitakuwa nimekuelewa una maanisha utofautti kati ya mwanadamu kushirikiana na majini na mwanadamu kutaka msaada kwa kiumbe kingine si ndio?
Kama ndivyo naweza kujibu hivi, Mwanadamu anaweza kushirikiana na kiumbe mwingine katika mambo yake hata maisha yetu ya kila siku tunashirikiana na viumbe vingine tunashirikiana na wanyama katika kazi mbalimbali ngo'mbe si huwa wanalima ndugu alafu mtu anashika lile jembe nyuma anyway, najua una maanisha ushirikiano kati ya mwanadamu na jini kama ni katika wema hamna shida ila mwanadamu kutaka msaada wa kiumbe kingine mfano kwenda kuomba mizimu ikusaidie upate mtoto au mali hiyo ni kufru ndugu hairuhusiwi.
Utofauti ni mdogo sana kushirikiana na jini katika wema maana yake wewe na jini wote mnamtegemea Mungu, Kinyume chake ni kuwa kuomba jini maana yake wewe unamtegemea jini na jini aliyekubali kuombwa maana yake anafanya shirki kwahiyo wewe unafanya shirki na jini anafanya shirki.
 
Maana yangu ni kwamba hizi dini kila mtu anamchukulia mwenzie kapotoka na upande alio yeye ndio upo sahihi!
Teh upo sahihi,

Binafsi naona ufaham ama uelewa na Iman ni kama vitu ambavyo kwa walio wengi vinaenda sambamba. Wengi utaona wana ule uelewa/ufaham wa kuamini sio wa kushuhudia.

Ukweli ama Uongo unageuka kua kama dhana ambayo ili ikubalike inaambatana na sababu nyingi nyingi.

Upendo huzaa imani juu ya kitu, mtu au lel say kitabu. Lolote lisemwalo basi mwenye upendo juu yake huliamini hata kama ni la uongo na kuliona kama "Kweli ya haki". Wivu nao huzaa chuki, Chuki huondoa imani, Na imani ikipotea basi lolote lile lisemwalo hata kama ni la haki ama kweli basi halitokubalika.

Kuna tofauti kubwa sana iliyopo sasa, kuanzia tofauti za kidini hadi kwenye tofauti za madhehebu. Kote kote katika hizi dini mbili kubwa Uislam na Ukristo.

Pale kwenye upendo na mahabba ndipo kunakopatikana mwanya wa kudanganyana, na pale kwenye chuki ndipo kunapatikana nafasi ya kupingana hata kwenye jambo la ukweli. Dini X inawachukia Dini V and viceversa is true. So lolote lisemwalo toka pande hizo mbili hawakubaliani kamwe hata kama ni la kweli. Walio dini X ama V wao kwa wao wanapendana, wanaaminiana na hata wakidanganyana huona wapo sawa na wapo katika njia iliyo sawa.

Itoshe tu kusema Elimu bila Maarifa ni mzigo kama mizigo mengine. Imani inayojengwa kwa msingi wa elim na Maarifa ni bora zaidi na ina manufaa. Lakini Elim inayojengwa kwa msingi wa Iman, yani Just kuamini tu kisa flan kasema ni mzigo pia kama mizigo mingine anayohitaji mtu kuitua ili awe huru.
 
Kama nitakuwa nimekuelewa una maanisha utofautti kati ya mwanadamu kushirikiana na majini na mwanadamu kutaka msaada kwa kiumbe kingine si ndio?
Yah ndio nilicho kimaanisha na naona umenijibu vizuri nimeridhika.
najua una maanisha ushirikiano kati ya mwanadamu na jini
🤣

Hapana usipige "ramli" ha ha just kidding, Sikumaanisha ushirikiano wa kijini pekee. Nilitaka kuongelea viumbe kwa ujumla wake. Umenijibu vizuri nimekuelewa.
 
Hayo mengine uwezi ukasemq Yesu ni Mungu kama Hauongozwi na Roho mtakatifu kukiri icho
Huyu Roho Mtakatifu ni nani, Em tupe elim tupate kumfaham. Itakua vyema zaidi kwenye maelezo au majibu yako ukianza na maana ya neno "Roho"
 
Wote wapo.

Pyramids zile za Misri zimejengwa na Wamisri wa zamani.

Zipo nyingi zaidi Sudan na nchi nyingi duniani, zinatofautiana kimo na style za ujenzi tu.
Simba.
Kuna zingine zimegunduliwa huko kwenye bara la Antarctica. Zinafanana na yasemekana ni kubwa zaidi ya hizi zilizopo Misri.

Nani alizijenga ilhali kule wanaishi Penguins 🐧 inabaki kua fumbo.
 
Yah ndio nilicho kimaanisha na naona umenijibu vizuri nimeridhika.

🤣

Hapana usipige "ramli" ha ha just kidding, Sikumaanisha ushirikiano wa kijini pekee. Nilitaka kuongelea viumbe kwa ujumla wake. Umenijibu vizuri nimekuelewa.
ha ha ha kama umeelewa ni vizuri, Karibu
 
Mathayo 4:10
"Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake."
Hapo alipomwambia nenda zako, walikua wana onana ana kwa ana au ilikua kiroho? Nawish kulijua hilo kama hutojali, vile vile na hapo kwenye "Msujudie Bwana Mungu wako, Umwabudu yeye peke yake", Vipi hua unafanya hivyo? Hua unamsujudia Mola wako? Bwana Mungu wako? Mmh? Na kama ni yeye peke yake hao watatu hua wanatoka wapi sasa. Tuelimishe na sie tusio jua tujue.
 
Imani ndio itamuokoa mtu na sio dini.
Huh hivi kwani dini ni nini? Iman ni nini? Ningependa kujua mtazamo au ufaham wako kuhusu hili.

Navyojua mie Dini ni mfumo na mwenendo wa Maisha. Kuanzia unakula vipi, unazungumza vipi, unatembea vipi, malezi kwa ujumla, utafutaji rizki na so sooo... kwamba mfumo mzima wa maisha ndio dini yenyewe. Na pale inaposemwa kuna dini nyingi duniani upande wangu naelewa kuna mifumo mingi ya maisha duniani. Kuna mifumo ya kiislam (Unyeyekevu), kuna mifumo ya kikristo, kipagani n.k

Then, Imani... Kwa ufaham wangu mimi ni kusadiki au kua na hakika ya mambo yanayoonekana na yasioonekana. Vile katika hili kuna Imani tofauti tofauti sana. Nitolee mfano Aina za Imani zinazofanana na tunacho kiongelea hapa. Imani ya Kiislam na Imani ya Kikristo.

Hua nshangazwa mtu anaposema toa mambo ya kidini hapa? How akati dini ni mfumo na mwenendo wa Maisha. Kwanini mtu huyo asiseme toa mambo yako ya kiimani hapa. Au kwanini isiwe mfia Imani iwe mfia dini? Kwani kiini cha mtifuano kipo kwenye Imani sio kwenye mienendo ya Maisha na kama ipo basi ni michache.

Nimesema haya kwasababu naona kama ni vitu viwili ambavyo vinatumika isivyo sawa kimazoea. Hivi viwili vinaweza kua pamoja au visiwe pamoja.

Kuna watu hawana Imani, yaani hawaamini katika yasio onekana ila wanaendesha maisha yao kwa kufata moja ya mifumo ya miasha iliyopo either ya Kiislam, Kikristo au mengineyo.

Kuna watu wana Iman ya Kiislam ila wanaishi kwa kufata mfumo wa Kikristo na kuna watu pia wana Iman ya Kikristo ila wanaishi kwa kufata mfumo wa maisha ya kiislam. Au pia unakuta wana imani za kiislam au kikristo ila wanaishi kipagani.

Kuna mda naonelea kutoelewa maana ya halisi ya vile tunavyozungumza inatosha kuchochea huu mkanganyiko uliopo... Na mkanganyiko uliopo hauwezi kutoka kamwe kama mtu hayupo radhi kujifunza kitu kipya hata kama kikiwa tofauti na kile ambacho tayari keshajifunza.

Hivi kuna mtu alishawah waza kwa nafasi yake vipi kama kila kitu unachofaham hadi leo hii ni Uongo na hakipo?
 
Hapo alipomwambia nenda zako, walikua wana onana ana kwa ana au ilikua kiroho? Nawish kulijua hilo kama hutojali, vile vile na hapo kwenye "Msujudie Bwana Mungu wako, Umwabudu yeye peke yake", Vipi hua unafanya hivyo? Hua unamsujudia Mola wako? Bwana Mungu wako? Mmh? Na kama ni yeye peke yake hao watatu hua wanatoka wapi sasa. Tuelimishe na sie tusio jua tujue.
Kuhusu kuonana nae au kiroho pitia hilo andiko then tubadilishane uelewa.. ilikua ana kwa ana au kiroho?

La pili lipo ndani ya uwezo wangu. ni kweli namwabudu Mungu mmoja asiye na dini wala imani. lugha wala kabila. nchi wala nyumba. Na naamini yuko peke yake...

labda unioneshe nilipoorodhesha watatu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom