Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Mkuu simba heshima yako, sisi wengine tunakufatilia japo kimyakimya. hongera kwa kushea nasi haya mambo mazito kabisa.

Una pumzi ya uandishi! naungana na wakuu wanaoshauri kuyaweka haya kwenye kitabu chako.

Naomba uzoefu wako kwa mambo haya;

(1) je kuna faida/hasara zipi za mtu kuishi/kuchangamana au kuwa karibu na majini?

(2) pia umesema unaweza kuminya pete na usionekane kwa wengine. je hapo unakuwa katika hali gani? je unakuwa bado na mwili wa kibinadamu/mzimu au? mathalani je unaweza kuingia kwenye daladala au chombo cha usafiri bila kuhitaji mahali pa kuketi au kusimama?

(3) sala na utoaji sadaka vina nafasi gani katika kumlinda mtu dhidi ya uovu wa dunia
 
Mkuu hutaniwi?
Haya mkuu yaishe, nisijepiga samasoti bure'
Hata hivyo nimemjibu km mimi mambio sio Simba wala Arsis.
Uzi wenyewe ni 'vionjo vya Arsis'
Kwahiyo kuweka vionjo sio mbaya sana.
Nakubaliana,vionjo muhimu sana, viwe vyako lakini, sio ya kutaja jina la mwengine mpaka uwe na uhakika kweli kayasema yeye.
Simba.
 
Hajui.
Simba.
sawa, Kuna comment ulisema majani ya mkokamanga ni dawa ya hasadi ukiyachoma ukajifukiza je unajifukiza mabichi au unayakausha ? na vipi ukiyachemsha ukajifukiza mvuke wake?
 
Kuna jambo hapa ningependa niliongelee kidogo kutokana na mshiriki mmoja kusema kuwa haamini mungu anaweza kumchoma moto aliyemuumba

Je hayo yanayotokea duniani mfano palestina na israel,mauaji ya wazee,wanawake na watoto wasio na hatia,je mungu hayaoni?

Hayo yanayotokea huko kongo machafuko na watu kuuwawa je mungu hayaoni?

Hayo yaliyo tokea ruwanda, watusi na wahutu na watu karibia milioni moja kuuwawa,je mungu hakuyaona?

Ukimchukulia mungu kuwa kama wewe kwakuwa una huruma na hisia utaona kuwa mungu hawezi kumchoma mtu,tambua mungu amekamilika kwa kila sifa na hafanani na mtu yeyote yule,kwahiyo anafanya lolote apendalo

Lakini pili je hao ambao wanaua wenzao,kunyanyasa wenzao na wanafanya dhuluma kila kukicha je hawastahili adhabu?


Je wanao fanya shiriki na madhambi makubwa makubwa je hawastahili adhabu?

Vipi kuhusu hao ambao wanakana kuwepo kwa mungu ambaye amewaumba wao,je unafikiri hawastahili adhabu?

Kifupi ni hivi mungu hufanya atakalo bila kujali matokeo yake na hana sifa kama za binadamu,yeye ni wapekee na mambo yake ya kipekee kabisa
Sorry mkuu ni Mungu si mungu
 
Hawa hawakaidi maagizo ya Mola wao,ni watiifu sana na ndio maana wakawa wasaidizi wa Mungu.
Hapa naona umeteleza kidogo, Malaika sio wasaidizi wa Mungu, labda kama ni Mungu ambae si Allaah azza wajal.

Kwani kajielezea katika Surat Ikhlas ingawa sitaiandika hapa (Na nime-refer kwenye Quran kwasabab we ni Muislam tutaelewana).

Mwenyezi Mungu, ni mmoja na ni yeye pekee hana mshirika au washirika wala wasaidizi na hakuzaa wala hakuzaliwa na ni vyake vyote katika mbingu na ardhi aliyeumba ulimwengu na vilivyomo, tunavyovijua na tusivyovijua.

Sisi viumbe wote nchi kavu na nje ya nchi kavu, duniani na huko akhera. Watu, wanyama, majini kwa malaika ni waja wake na watumwa wake wala sio wasaidizi wake na hakuna kiumbe yoyote au popote pale mwenye sifa hiyo ya usaidizi. Mola wetu mlezi ametakasika kwa utukufu wake.

Nirejee tena kusema ametakasika kwa utukufu wake, anaendesha kila jambo namna apendavyo.

Hapa kuna hadithi pia sitaisema kama ilivyo ila nitaidodosa, katika zile hadith qudus (tukufu).

Mola wetu akisema lau kama viumbe wote tukiungana kufanya kinyume na amri yake hatutapunguza chochote katika ufalme wala utukufu wake. Vile vile anasema hata kama viumbe wote tukiungana kufanya kila alichokiamuru hatutaongeza chochote katika ufalme na utukufu wake. Ni sisi ndio tunamhitaji yeye ila sio yeye kutuhutaji sisi.

Sisi viumbe wooote (Binadam kwa malaika) kwake ni waja na watumwa wala sio Wasaidizi.

I know may be huenda hukumaanisha, but utanisamehe kidogo kuna kauli hua nikiziona nashindwa kujizuia kuzungumza. Kauli zenye sura hiyo.

Again huenda pia ikawa ni lugha gongana, lakini msaidizi ni yule anayekupa msaada kutekeleza majukum ambayo wewe hujaweza kutekeleza lel say mkeo ndani ya familia yako. Then kuna "mtumwa" ambae anafanya majukum ambayo wewe unayaweza kuyafanya but ukampa ayafanye.

Sasa viumbe wote kwa Allaah ni "watumwa" hatuna sifa ya kua wasaidizi kwake hakuna ambacho haezi kufanya ili ahitaji msaidizi au wasaidizi.
 
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 11.

Nikpigiga juisi ya maji ya miwa, nikaenda kuali nilipotoka, pale pale Masjid nje nikapata Kibajaji kikanipeleka kituo cha Kojani, nikamlipa kabisa mwenye Kibajaji nikiwa ndani ya Bajaji kabla hatujafika. Lengo likiwa nikishuka tu nijifiche, nisionekane.

Kufika tu nikaiminya pete kabla sijashuka, nikawa najisemea mwenye Kibajaji akigeuka kuatazama akiona hakuna mtu kazi kwake.

Niliposhuka nikamuona Jini 1 kwenye kona karibu na kiduka cha pale kivukoni, akaja, akanambia haya Sima tuwahi, umefanya vyema kabisa, mimi ningekua sina pete zetu hizi tusingeonana.

Tukavuka bila mimi kuonekana, Jini 1 pale hakijificha, alikua anaonekana yeye tu, maana yeye ndio alilipa alilipa pesa zaidi akamwambia Mwenye ngarawa, hizo zako, weka tu. Alikua hajui analipwa na nauli yuangu.

Tyulipofika viwanja vya chano, watu wanacheza, kama kawaida wakubwa wapo ndani, watu wamejaa vumbi, nikashangaa, nikaona leo walijipaka rangi nyeupe usoni, wengine zina mistari mekundu, wengine zina mistari meusi, wengine nyeupe tupu. Kufika meza kuu nikaona Bakora yupo pale na pembeni yake kuna nafasi ya kukaa, akanisharia nikakae pale. Nikamuona yule Mzee alioaibishwa na Bakora kwa kunyamazishwa na kukalishwa chini kiajabu yupo pale lakini alikuwa kawaida tu hana ile muonekano wa kugtamba tena, kanywea.

Watu wakaanza keleke tunachelewa tunachelewa. Mzee Ali akasimama akayamaZisha kila kitu, ngoma ile ya pale ndani ikasimama, nje uwanjani huko kulikua na ngpma zaidi ya moja, kama vikundi vikundi hivi hivi.

Mzee Ali; Endeleeni kushereheka, tunangoja wakuu waturiuhusu tuanze kumalizia ngwe ya mwisho ya shughuli yetu, anaeona anachelewa aondoke.

Bakora akaninong'oneza jifichue tu, na yeye akajifichua. Mzee Ali inageuka tu kuongea kutazama akae, akatuona, akashikwa na butaa, akatuuliza, tuendelee na shughuli wakuu au kuna maagizo yoyote. Nikaona hata meza kuu wote wameshangaa kutuona tumekaa pale.

Bakora: Endelea tu.

Mzee Ali; Akasimamisha tena ngoma kwa ishara tu, watu wakawa kimya; Shughuli yetu inaanza kama kawaida vyano vitapita nje hapo kama ada, na wakishapita watu wa chano wote ndipo sisi tutawafata nyuma. haya twendeni nje tukawapokee.

Mzee; Ali; Wakuu naomba twendeni, hapo mez kuu yote wameanza kushuka kuwahi nje.

Bakora: Nendeni, lakini msikipeleke chano mpaka sisi tufike, tangulieni, sisi tutakuja mwisho. Akshuka Mzee Ali akatoka nje ukumbi ukawa mytupi.

Bakora: Sikiliza, Simba, sisi tunakwenda kabla yao wakati wao wanapokea wenye kuleta Chano hapo nje, tutaingia kwenye maji ya tumbo, trunajificha kuanzai sasa wasituone, wakifika huko, tutajifichua kwenye maji watatuona sisi tunatokea baharini. Tukajificha tukaondoka.

Nje pale ndio nikaona kumbe zile rangi na walizojipaka na bendera zake na mwari wao aliebeba chano na kundi lao la ngoma. Ndio nikajoionea wapo watu wa kila aina hapo, taani waarabu, wazungum wahindi, na wakojani ndio wengi. Kila mmoja na kundi lake, wemye kucheza, wenye kulia, wenye kutingisha vichwa, yaani zaidi ya nusu waliokuepo pale nje wamepandisha mashetani.

Tukaingia kwenye maji kama Bakora alivinambia, hivyo hivyo na nguo zetu.

Nikaona wanakuja, Mzee Ali akaongea kitu na mbeba chano kikubwa. Lilikua sinia kubwa kweli, nikaona wamesimama ufukweni, yule binyti kasimama na chano Arsis akanambiajifichue tutoke. Nikasikia watu wanguna, haiwahi kuwatokea watu kutokea ghafla bahatini. Mzee Akawa anakodoa tu macho na wenzake wa meza kuu. Tukatoka tukasimasima pembeni kidogo, wakati tunatoka Bakora akamwambia endeleea na shughuli yenu. Maee Ali akaanza kupaza sauti...

Mzee Ali; Maini na mizimu ya pemba, na majini wote kutoka nchi na sehemu mbali mbali mliohudhuria, sasa kama ada ya hapa, kitatangulia chano kikubwa kupelekwa wengine wote mtabaki na vyano vyenu mpaka atoke mjumbe wa kupeleka chano. Aliebeba chano Kikubwa akaanza kuingia kwenye maji taratibu, huku Chano kipo kichwani.

Alipokua anaingia, wenye kushangulia wana shangilia, wenye kulia wanaliza, eengine wanapiga kelele za kufuru " mzimu mkuu wa kojani, gtutalie shida setu" mwengine nitatuiea shida zangu, yaani kila namna ya maombi anaombwa shetani. Mie nikawa naomba toba tu kimoyomoyo. Na hapo ndio nikajua kua yule mwari alikua akfungwa kanga tu kiustadi zilikuasio nguo zile, maana khanaga zilipoanza kuingia maji zikawa zinapanda, akaingia akatembea baharini mpaka maji takamfunika kabisa ikawa kanyua mikono kulibeba lile sinia, akaendelea kidogo mpaka likabaki sinia tu juu ya maji, naona akaliahcia lkakini ikawa kama analisuma kwa chini kuelkea baharini, yeye haonekani linaonekana sinia tu linakwenda, kufika sehemu, nikaona aja kutokea maji amabayo imetokeza shingo, na sinia lianenda zakw lenyewe.

Mie nikawa na shangaa na sinia linazidi kwenda tu lenyewe.

Bakora mchezo wa kuigiza tu huo, mazingaombwe tu hayo atakufahamisha Jini 1 baaadae.

Yule mnbeba chano aktoka moka nje Khanga zimerowa zimemnganda mwilini, ni binti kashibew wa haja kweli kweli, alipotoka tu.

Mzee Sli haya mpeni khanga zake mpya hizi hazirudiwi tena.

Kuna kina mama wakamletea kumfunga kanga mpoya wakafanya kama pazia hivi na khanga, walipotoa pazia ikawa yupo fresha na khanga zake kavu zimefungwa kiustadi kabisa.

Mzee Ali; Chanoi kikubwa kishapokelewa, haya sasa nyie pelekeni kwa mstari. Asiwafate asie na chano, kabisa tena, madhara yake makubwa.

Mabinti wakaanza kuelekea kama alivyofanya yule lakini hawa ikawa kila wakifika maji ya kiuno mooja anaenda kushoto mmoja kulia, yaana wanapanua wigo mpaka walipokaa mstari kwa baharini, wakaanza kuingia kama mpoka maji ya kunyatu mikono, kama alivonya yuule wa mwanzo mcheo ukawa huo wakaanza kutoka, sasa kila anaetoka kikundi chake akishatoika nje ndio kinafanya pazia anavikwa khanga mpya. Dah, hawa wabeba nikajua wanachaguliwa kweli kweli, yaani ni ushetani. Hakuna mwanamme rijali ataevumilia kuwamezea mate. Vile wanavyotoka zile khanga zingine zimepanda juu na zilivyogana mwilini show zote nje, si nyuma si mbele. Naona wanavotabasamu ni kama wamefundishwa kwa kina, waumize mioyo ya marijali.

Walipokwisha toka wote;

Mzee Ali; haya jamani, chano chote kimepokelewa, sasa kama kawaida yake mwenye lake aseme, mwenye chochote cha kupeleka baharini apeleka, na nawashauri sote tyujiyie kwenye maji japo mwili mzima upate maji, kila mtu kwa raha zake. Tukitoka hapa, karamu yetu kama kawaida kiwanjani, wale wapishi na wandalizi wawahi kutoka majini.

Bakotra; Haya simba wakati wanaingia bahatrini, jifiche tuondoke zetu.

Mzee Ali ndio alikua kaoingoiza msafara akaanzq yeye ne meza kubwa yote kuingia baharini, wakaftatia watu wote, wkubwa, wadogo, wazee, vijana, wanaume kwa wanawake. Mimi na bakora tukatazama kidogo oirika zao, wenye kwenda maji ya kina huko wenye kuongelea, waliobaki maji ya mwanzo mwanzo wanajizamisha haya.

Tukaondoka na Bakora akanambia, shughuli yao ndio imeisha, sasa wanapoakuliwa pilau, tukapita pale, hakuna watu uwanjani ndio nikaona masufuria makiubwa zaidi ya 20.

Bakora: Utangoja kula Simba?
Mimi; nani ale nyamafu hizo zilizochinjwa kwa ajili ya kafara za majini, twende etu bwana. Nimeshajionea shughuli zote za kishirikina za Kojani, inatosha. Bakora, haya twende, mengine atakuja Jini 1 kukueleza ukihitaji.

Bakora; Tulivofika karibu ya nbandari ya ngarawa akanambia jifichue tu. Tukapanda ngarawa na Bakora, upande wa pili tukakuta vibajaji kibao, tukaagana na bakora, nikapanda kimoja nikamuelekeza tukaondoka zetu.

Hoiteli, nikauliza resepshen kama Dokta amaesharudi, nikaambiwa bado. Nikapanda kwangfu nikakoga vizuei, nikasali. Nikakaa kuwasubiria, Niakapiga simu nyumbani kwa mama, baada ya kusalimian...

Mama; habari zote nazipata hapa, mkeo na mapoicha ananitumia. wanaonesha wamepapenda mkoani vijini huko.

Tukaagana nikapiga simu kwa wife. baada ya kusalimiana.

Wife; Nimekupigia sana simu inaita tu, umeshaoa Pemba mume wangu, hatiuambizani?
Mimi; Niliizima sauti msikitini nikasahau kuiongeza z)sauti. Vipi huko?
Wife; Ndio nilitaka kukuuliza muda mrefu, hapa madaktari wa Kipemba mashiga zake Dokta wa metuzuwia mpaka tule chakula cha usiku, sasa mume wangu, tutachelewa kurudi, si unajua vyakula na maongezi, tukichelewa usiwe na wasiwasi kama kuna choxxhote tutakujiulihsa. Hiwa wasi youer dayt?

Mimi; Siku nzuri nimetembea tembea nimeend mabli kidogo, nimerusi si muda mrefu. Vipi Dokta? Wife yupo, nimemwacha anaingea na wenzake, mimi nimetoka kidogo kuongea na wewe na simu. Njoo basi D. nikamwabia aah poa nyie endeleeni, sitaki kuwekwa mtu kati na wanawake watupu huko.

Wife; Unajifanya umesahau, ungesema hayo siku zile?
Mimi; Mke wangu tuombe tba tu, wala tusiyakubuke ya ushetani wa zamani, tulikua kizani.
Wife; Amiin, mimi naomba usku na mchana mume wangu kila nikisali, naomba sana Mwenyezi Mungu atutoie kabisa kizani.

Wife alikua kama mimi, haongei kabisa na simu zake mbele za watu, au kukaa, kua bize na meseji wakati anaongea na watu. Naona hio tabia, wote nyumbani tunayo.

Mzee anasema simu na wakati wake, nyinyi mushukuru sasa hivi tunapiga na lupokea simu wakati wowote. Zamani sisi ilkua hakuna hayo. Kupiga simu mpaka mtu aende posta ndio akapige. Nyinyi jopangieni, wakati wa simu n zisiwapotezee muda wenu, sana sana zinazidisha umbea tu. Tukawa tunamuelewa sana.

Nikawa sina budi, ni kuwasubiri tu.

...
Vionjo vya Arsis - Majini ya Kojani- Pemba 12.
Mpaka muda wangu wa kiulala usiku hawajarudi. Nimella usiku kama sita hivi, nikagongewa, nafungua naona wife ndio karudi.

Mu wangu, umelala mpaka umenitia wasiwsi nilikuja kwaanza kama saa tano hivi, nimegonga hujaamka.

Tumerudi na mgeni wa Dokta, toto la Kipemba Daktari la mkoani hilo, si mchezo. katuleta tumemzuia alale hapahapa. ngoja nikawaage, nakuja sasa hivi.
Hajachukua hata dakika tano akarudi.

Wife; Tungejua hata sokoni tusingeagiza ndizi, huyu Dokta anasema ndio kazi za kwao huko, kwa baba zake, wana mashamba ya mikarafuu na ndizi tu. Tumekubaliana nae watatufungia vizuri na watatupakilia, hukohuko mkoani kwenye meli ya kwenda Dar. Na vile vitu tulivyonunua hapa vyote tumpe aende navyo atasafirisha pamoja. Anasema ndio kazi ya kakake hio, anasafirisha ndizi mpaka Ulaya.

Tukalala, alfajiri nikawahi kwenda masjid, ipo jirani tu hapo. Nilipomaliza kusali nikaenda kutembea kidogo kama one hpur hivi kurudi nikakutana nao nje ya hoteli wote watatu.

Wife: Na sisis tumeoka kutembea, tumeona utafaidi peke yako hewa ya alfajiri ya karafuu, inagtia njaa, sasa ntakula vizuri. haya jamani gtukajitayarishe tukutane kwenye Brakfast. Dokta Moza, huyu ndio Simba, mume wangu.
Moza; Nimesikia sana jana habari zako kwa Dokgta zaidi, nikawa na hamu ya kukuona. Nimefurahi tumejuana.
Mimi: na mimi nimefurahi kupata mwenyeji Mkoani.
Moza; Karibu sana tena mume wangu anarudi kesho, kaenda Unguja kwa kazi zake, Dokta anamjua, partner wake.

Tukapanda juu, Madaktari wawwili wakenda kujitayarisha chumbani kwao mimi na wife tukaenda chumbani kwetu, kama nusu saa tu tukawa tumetoka tukakutana kwenye rakfast.

Wife; Sasa Simba, leo program yetu inabidi na wewe uwepo. Haina kukwepa wala ujanja hii.
Mimi: Sasa si nakua mateka wenu?
Moza; Ndio ushatekwa hivoo, inabidi ukubali matokeo tu.

Nikaona aah kumbe Dokta Moza ni muongeaji.

Wife; Simba, Dokta ana kazi hospitali ya Wete huko na waekubalina na Moza atampeleka na gari lake na yeye kaona aende, maana progtram hyao moja. Kwa hio wao wakiwa bize masaa mawili hospitali huko, mimi tabaki [eke yangu.
Moza; Tumemwabia aende awe na sisis hpospita;li, hataki, kazi zenyewe sio za kutazama wagonjwa ni za ofisini tu, kukusnya data tu za Dokta hapa.

Moza; nyie tuacheni hospitali mkazunguke na gari Wete yote, baada ya masaa mawili mtaturudia, halafu mimi nitawatembeza, naijua Pemba yote hii, hakuna kijiji sijafika kwa kazi zetu. mchoke nyinyi tu. Haya jitayarisheni tuwahi.

Tukaenda juu gtukajitayarisha, unajua kina mama ytena, wife akabeba begi , mwenyewe anakwambia lina nguo za kubadilisha ikibidi, tukatoka tukaanza safari ya Wete.

Njia ni ileile ya kwenda kojani kufika kona ya Kojani.

Moza; Dokta, kwenu huko, tukupeleke ukatembee?
Dokta; haloo sitaki hata kupaona wala kusikia, tena kanyaga mafuta tupite haraka hapa.

Tukaenda mpaka hospitali ya Wete, njiani nikaona raha, yunaelekezwa kila mahali, kila kitu a Moza. Kufika tu, tukashuka wote.
Moza; Funguo hii hapa nani ataendesha, nikamwambia Nisha ataendesha, mimi nataka kuenjoy view.

Nisha; leta funguo, mimi dereva wa kimataifa.

Tukaanza kupiga raundi Wete, barabra kubwa mpoja tu. tukaenda mpaka mwisho majumba yanaishia, tukarudi, tukaanza kuingia kila tunapopona njia ya ndani, ukiingia huendi sana, unakuta tena huko mbele mpaka uwe na mwenyeji. kwa ufupi tukazzunguka, masaa mawili kasorobo tukawa tusharudi.

Hatujakaa hata dakika tano madaktari wakaja.

Dokta tulikua tunachungulia mara kwa matra kama mmerudi, tunaona hapa zinapoegeshwa gari, kazi tumemaliza muda tu.

Moza; Mmeshakua wenyeji Wete?
Wife sana tena,mitaa yote ukiniuliza naijua.

Akaingia Moza akaaza kuendesha, akatupeleka bandari ya Wete, katupitisha tu njia kama inazunguka inatokea barabara ile kubwa lakini kwa mbele hivi. Kutoka akasimamisha gari barabfa ku wa kuna vigorofa viwili vitatu na maduka duka, aksema hapa ndio Doen Town Wrete, twendeni tukachukue zawadi za wete, tukaingi kimtaa kimoja, nyuma tukakuta sehemu kama watu wanakunywa kahawa na mbele kuna msikiti, kabla ya kufika tukaingia kushoto, nnikaona tumezunguka tu, tumetokea nyumba oile ile wanaokunywa kahawa kwa nyuma, kuna mlango akabisha hodi tukaingia.

Moza; Nikija Weyte lazima nije haa kununua kshata, ile kukaa tu kwenye benchi, yupo mama anamjua Dokta Moza.
Kashata: Dokta Moza leo umenisurprise na wageni?
Moza; Nimewaleta wanunua kshata, huyu anapajua hapa aliwahi kufika. hawa ndio mara ya kwanza. Tukaletewa kshata bado zinajotojoto, hizi za kuonja jamani kuleni, ngoja niwaletee na kahawa. akatuachia kisinia yeye akaenda kuchukua kahawa, tukapoiga pale, kashata za nazi, nzuri kweli kweli.

Moza; Mimi nifunhgie za efu tano.
Dokta: Mimi nifungie hoizo hizo zq elfu tano mra mbili lakini weka tifauti tofauti.
Woife; Mimi nifungie mara tano z elfu tano tani, zawadi ya wete hii Dar huko.

Tukachukua kashata zetu, tukaondoka.

Tukaenda kama tunarudi Chake lakini njiani huko Dokta akaingia kushoto, tukafika kimji fulani hivi, mwendo lakini aksema hii ndio mkisikia micheweni, tunapoita tu hapa. Tukaendelea tukapoita msiti mmpoja mnene mbele huko, aksema hii hifadhi ya misitu, hapakai mtu wanasema mpaka chuoi wa kipemba wapo humu.

Tukaendelea mpaka tukatokea beach hotel ya kigtalii, safi sana, tukaona na mxungu mwenye mali, tkaongea ingea nao, akasema sasa hivi wnaanza project mpya, ndio wanajitayarisha wanataa kuanz katikati ya bahari, wataweka vyumba vya watu kulala huku wanaona samaki baharini, akatuonesha onesha picha za dizaini kwennye simu yake.

Wife; Hamnilazi hapo hata mkinilipa mimi wacha mimi kulipia. Tukacheka. Tukatembezwa hoteli, tukanywa frdha juice tukaondoka, tukarudi Chake jioni kabisa. Moza hajataka kukaa tena.
Moza; Hii rukhswa yenyewe ya leo nimeipayta kwa mbinde. Tukawaambia hoteli vitu vyetu vya maboksi wavitoie wabitie kwenye gari, ytukampa na zoile kashata zote tukabakisha mfuko mmoja wa kula wenyewe, Tukamwabia dokta na hizi mtazifunga kwenye mizigi ya Dar.

Dokta: Mingine mizigo utaipata kedshi kama tulivyoongea, yote ya Dar. Hiyo.

Tukaagana.

Siku zilizobaki ikawa dikta anaeaenda kwenye program ya kazi zake, kisha tunaenda kuzurura tu matra beach hii mara hoteli hii, marfa sijui kijiji gani mpaka tunaondoka, wife kapoiga mapicha kama milioni.

Tukarudi Dar salama salmini. Vionjo vya Kojani Vikaishia hapo.

Tukirudi ni vionjo vya Comoros.
End of Kojani Episode.
Simba.
 
Hapa naona umeteleza kidogo, Malaika sio wasaidizi wa Mungu, labda kama ni Mungu ambae si Allaah azza wajal.

Kwani kajielezea katika Surat Ikhlas ingawa sitaiandika hapa (Na nime-refer kwenye Quran kwasabab we ni Muislam tutaelewana).

Mwenyezi Mungu, ni mmoja na ni yeye pekee hana mshirika au washirika wala wasaidizi na hakuzaa wala hakuzaliwa na ni vyake vyote katika mbingu na ardhi aliyeumba ulimwengu na vilivyomo, tunavyovijua na tusivyovijua.

Sisi viumbe wote nchi kavu na nje ya nchi kavu, duniani na huko akhera. Watu, wanyama, majini kwa malaika ni waja wake na watumwa wake wala sio wasaidizi wake na hakuna kiumbe yoyote au popote pale mwenye sifa hiyo ya usaidizi. Mola wetu mlezi ametakasika kwa utukufu wake.

Nirejee tena kusema ametakasika kwa utukufu wake, anaendesha kila jambo namna apendavyo.

Hapa kuna hadithi pia sitaisema kama ilivyo ila nitaidodosa, katika zile hadith qudus (tukufu).

Mola wetu akisema lau kama viumbe wote tukiungana kufanya kinyume na amri yake hatutapunguza chochote katika ufalme wala utukufu wake. Vile vile anasema hata kama viumbe wote tukiungana kufanya kila alichokiamuru hatutaongeza chochote katika ufalme na utukufu wake. Ni sisi ndio tunamhitaji yeye ila sio yeye kutuhutaji sisi.

Sisi viumbe wooote (Binadam kwa malaika) kwake ni waja na watumwa wala sio Wasaidizi.

I know may be huenda hukumaanisha, but utanisamehe kidogo kuna kauli hua nikiziona nashindwa kujizuia kuzungumza. Kauli zenye sura hiyo.

Again huenda pia ikawa ni lugha gongana, lakini msaidizi ni yule anayekupa msaada kutekeleza majukum ambayo wewe hujaweza kutekeleza lel say mkeo ndani ya familia yako. Then kuna "mtumwa" ambae anafanya majukum ambayo wewe unayaweza kuyafanya but ukampa ayafanye.

Sasa viumbe wote kwa Allaah ni "watumwa" hatuna sifa ya kua wasaidizi kwake hakuna ambacho haezi kufanya ili ahitaji msaidizi au wasaidizi.
Nawashauri nyote mkifatilie vizuri kisa cha Adam, ambacho In shaa Allah tutakianza tena leo hii. Kuna mafundisho mazuri sana ya viumbe wote, Malaika wakiwemo.
Simba.
 
Mkuu Arsis shikamoo nina shida nimekuwa ninashida ya usikivu tangu utoto ilinitokea nikiwa na miaka 8...sijui nimerogwa ila inawezekana, kadri siku, mwezi na miaka inavyosonga ndio nakuwa sisikii kiasi kwamba sahivi mpaka niangalie mdomo wa mtu ndio nielewe japo kwa shida sana je kuna tiba mkuu? msaada tafadhali mkuu wangu

Shida nyingine ni nina severe curve scoliosis(uti wa mgongo kupinda) siwezi kutembea niko kitandani mwaka wa nne sasa..pia vidole vya mguuni vinauma sana ata ukivishika tu kingine nimekonda sana ata nile vipi sinenepi pia mishipa ya mwili imesinyaa nakuwa sina nguvu kabisa

Naomba msaada wako mkuu ninataka kupona tena mkuu mana tiba nyingi zimeshindikana from hospitalini to ugangani mpaka sina hamu ya kuishi na haya mateso nayopitia lakini nimepata tumaini naweza kupata msaada


Mwambie Arsis I want to be his friend just like you.....I really do
Dah pole ndugu,Mungu atakusaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom