ASILI YA MAJINI --2
Baada ya kuona kuwa majini wameubwa kwa moto kwa mujibu wa quran nije katika hadithi za bwana mtume muhammad swalalah alaiy wasalam.
Aisha (RA) alieleza kwamba Mtume Muhammad (SAW) alisema: "Malaika waliumbwa kutokana na nuru, majini waliumbwa kutokana na moto na Adamu aliumbwa kutokana na kile kilichoelezwa kwenu."
عن عائشة رضي الله عنه قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «خُلقت الملائكة من نور، وخُلق الجَانُّ من مَارِجٍ من نار، وخُلق آدم مما وُصِفَ لكم».
[صحيح] - [رواه مسلم]
Hadthi hii ni sahihi na imepokewa na muslim, Katika hadithi hii tumeona kuwa Malaika wameumbwa kutokana na nuru , majini kutokana na moto na wanadamu kutokana na kile tulichoelezwa kwa maana hapa mtume alisha waeleza kuwa mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo.
Hivyo hakuna shaka kuwa asili ya majini ni mwale wa moto. Tuje katika melengo yao kwanini majini wameumbwa?
LENGO LA KUUMBWA MAJINI.
Imetajwa katika Quran kuwa lengo la wanadamu na majini kuumbwa ni kumuabudu Allah. Kama ilivyokuja katika quran (Adh-Dhariyat 51:56)
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ -- sikuumba majini na watu ila waniabudu.
Hapa tunaona kuwa lengo kuu la kuumbwa majini na sisi wanadamu ni kumuadu Allah, swali linakuja ikiwa ilo ndio lengo la kuumba mbona majini na wanadamu tunafanya mambo ya kumkufuru mungu nadhani umesoma katika kisa cha bwana simba mabalaa ya majini jinsi wanavyokata majii(kunywa pombe), wanavyofanya uchawi na mabalaa mengine, Kuhusu wanadamu apo bwana
Battor unajua mabalaa ya mwanadamu uzinzi, wizi, rushwa, chuki, uongo, dhulma, zinaa, mauaji, kukata undugu, kusengenya, ushoga, utapeli n.k kwanini yote haya na Allah anasema lengo ni kumuabudu yeye?
Quran inajibu kwa kusema katika surah Al-Insan (76:3) ''Hakika Sisi tumemwongoza katika njia. Ikiwa atashukuru au akufuru."
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
Hapo wamezungumzwa wanadamu kuwa muongozo upo na njia ni mbili tu ushukuru au kukufuru na majini pia imeelezwa katika surat jinn kuwa kuna kundi la majini lilisikia quran nalikakiri kuwaa ni ya ajabu na inaongoza katika haki na hawatamshikisha mola wao.
"قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا"
Lakini pia katika aya ya 11 ya surat jiinn inasema
''وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا'' -- Na hakika miongoni mwetu wapo walio wema, na miongoni mwetu wapo kinyume na hivyo; tulikuwa njia mbalimbali.
Hapa utaona kuwa majini wenyewe wanasema kuna wema na wabaya hivyo suala linabaki kwa mwanadamu au jinn kuchagua njia ya kufuata na watakao mtwii Allah malipo yao ni pepo na watakao kufuru na kumuasi ALLAH ni motoni kama ilivyo katika quran
"قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ"
(Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wana Aadam”. [Al-A’araaf: 38]
Toka nimeanza kuelezea mpaka hapa kuna mambo utagundua kuwa kwa mujibu wa uislamu:-
- Malaika wameumbwa kwa nuru, Majini kwa moto na wanadamu kwa udongo
- Lengo la majini na wanadamu ni kumuabudu Allah.
- Watako fanya kinyume na kumuabudu Allah malipo yao ni Moto.
Hivyo basi, Ushirikiano wowote wa mwanadamu na majini katika kumuasi Allah ni makosa na imekatazwa katika uislamu hilo halina mjadala, ni KUFRU.
Mjadala unabaki Je ni sahihi mwanadamu na majini kushirikiana katika wema mfano bwana Arsis alivyoshirikiana na Simba katika kumuokoa msukule huko unguja na mifano kama hiyo Je yafaa?
Inshaalah, Nitalieleza pia kwa kadri ninavyoelewa, Hapa hapataki muhemko maana pana mambo mtu anaweza ona yafaa kumbe haifai na mengine kuona hayafai kumbe yafaa.
Nitarudi kuelezea maisha ya majini, kuzaana kwao, tabia zao, na kubwa zaidi kwanii wanasumbua wanadamu.