Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Je huu uumbaji wa kwanza wa mwanzo 1:27 inawezekana hawa watu walioumbwa kwanza mke/mume ndio majini?
Hapana, hapo Mungu aliumba mtu kwa sura na mfanano wake kisha akamuweka katika mwili.

Asili ya mwili ni ardhi/udongo na asili ya mtu ni Mungu, kwaiyo tunaona chanzo ndo kinabeba nguvu ya kitu. Mwili unahitaji chakula kinachotokana na ardhi ili upate afya na mtu anahitaji chakula(kuwa karibu na chanzo chake ili awe na nguvu), hii siri hata mashetani wanaitambua kuwa mtu ndo kiongozi na wao hawana mamlaka juu yake ndo maana wanajaribu kumuweka mbali na chanzo chake(kumdhoofisha).
 
Kingine ni kuwa, Ili kuelewa zaidi juu ya swali lako ni vema kuanza kujifunza kuwa kwa mujibu wa quran majini ni viumbe gani na kwanini wameumbwa? Ukishayajua haya kwa mujibu wa quran ni rahisi kuelewa majibu nitakayokupa ila bila kuelewa haya ata nikikuambbia ndio inafaa nitakuacha na maswali zaidi au nikikuambia haifai bado utabaki na maswali mengi zaidi au nikikuambia maulamaa wametofautiana hapo ndio nitakuchanganya zaidi.
Sasa bwana Battor Tutaanza na Majini ni viumbe gani kwa mujibu wa quran na kwanini wameumbwa.
Nitakuwa na kuelezea kidogokidogo kwa kuendeleza mada katika hii reply na katika kila muendelezo nita kutag ili uone kwa urahisi. Natumai uta enjoy majibu ya Quran na hadithi za bwana Mtume muhammad (swalallah alaiy wasalam), Kuna mambo mengi sana utajifunza, This is more than interesting !, KARIBU.
Shusha vitu mkuu mimi naamini quran ni kitabu cha mwenyezi Mungu pia.
 
Ninaposema kiini namaanisha yeye aanze kutoa hoja mbadala mfano anasema adamu sio binadamu wa kwanza, Hoja mbadala hapa zinaweza kuwa adamu sio wa kwanza wa kwanza ni nani ?
Kwanini ulazimishe kitu ambacho Allah kaamua asikitaje kwenye Qur'an? Allah hakusenma kwenye Qur'an ni mtu yupi wa kwanza kumuumba. Wewe unatakiwa usiongeze lako kwa kujifanya unajua zaidi ya Allah. nani anakupa ubavu huo, wa kulazimisha Allah aandike kwa fikra zako wewe? kama dalil yako ni biblia sema ukweli tu, hiyo nimeisoma kwanye biblia, sema tu.

Dinosaurs hawakutajwa kwenye Qur'an haina maana kua hawapo ilhali wanasayansi wanachimbua mifupa yao ardhini.
Kingine ni kuwa, Ili kuelewa zaidi juu ya swali lako ni vema kuanza kujifunza kuwa kwa mujibu wa quran majini ni viumbe gani na kwanini wameumbwa? Ukishayajua haya kwa mujibu wa quran ni rahisi kuelewa majibu nitakayokupa ila bila kuelewa haya ata nikikuambbia ndio inafaa nitakuacha na maswali zaidi au nikikuambia haifai bado utabaki na maswali mengi zaidi au nikikuambia maulamaa wametofautiana hapo ndio nitakuchanganya zaidi.
Sasa bwana Battor Tutaanza na Majini ni viumbe gani kwa mujibu wa quran na kwanini wameumbwa.
Nitakuwa na kuelezea kidogokidogo kwa kuendeleza mada katika hii reply na katika kila muendelezo nita kutag ili uone kwa urahisi. Natumai uta enjoy majibu ya Quran na hadithi za bwana Mtume muhammad (swalallah alaiy wasalam), Kuna mambo mengi sana utajifunza, This is more than interesting !, KARIBU.
Hao unaosema "Maulamaa wamehitilaiana" kwenye Qur'an? Tafsiri Ya Qur'an au kwenye Hadith? Au mitazamo yao bifsi tu?

Wewe mjibu kwa mujibu wa unavyoelewa wewe. Sio "ulamaa". Kama huelewi sema "sielewi".
Simba.
 
Natamani hii thread iendeshwe kwa mfumo wa kimahakama ! Tuteue mawakili wetu hapa, mawakili watokane na uhodari wao wa majibizano kwa kuzingatia uchangiaji wao wa nyuma pamoja na jaji. Then mnyukano uanze hapa ! Otherwise hii elimu tutapewa kwa kusimangwa kama watoto waliofukuzwa Ada shuleni.
 
Wengi watachomoka, ambao hawajajaaliwa kupata elimu inayotolewa hapa. Elimu ni majaaliwa.
Simba.
 
Kwanini ulazimishe kitu ambacho Allah kaamua asikitaje kwenye Qur'an? Allah hakusenma kwenye Qur'an ni mtu yupi wa kwanza kumuumba. Wewe unatakiwa usiongeze lako kwa kujifanya unajua zaidi ya Allah. nani anakupa ubavu huo, wa kulazimisha Allah aandike kwa fikra zako wewe? kama dalil yako ni biblia sema ukweli tu, hiyo nimeisoma kwanye biblia, sema tu.

Dinosaurs hawakutajwa kwenye Qur'an haina maana kua hawapo ilhali wanasayansi wanachimbua mifupa yao ardhini.

Hao unaosema "Maulamaa wamehitilaiana" kwenye Qur'an? Tafsiri Ya Qur'an au kwenye Hadith? Au mitazamo yao bifsi tu?

Wewe mjibu kwa mujibu wa unavyoelewa wewe. Sio "ulamaa". Kama huelewi sema "sielewi".
Simba.
Nomba unijibu ili swali mkuu ushawahi kufanya salat janaizer maarufu kama kumsalia maiti?
 
Nomba unijibu ili swali mkuu ushawahi kufanya salat janaizer maarufu kama kumsalia maiti?
Sijawahi "kufanya", mimi nafata imam tu kwenye sala hio, nimeshaisali sana kama maamuma..
Simba.
 
Inatokea post namba 114.

Ile kuingia jiji la gharama Dar, ndio nikajuwa kweli macho yamefunguka. Njiani nilikua natafakari sana kilichotokea Chalinze na nini kiliendelea baada ya sisi kuondoka, sijapata jibu la haraka. Nikadhamiria, tukifika nyumbani nimuite Arsis anieleze.

Kufika Kariakoo Dar, ikanijia sauti ya Arsis, ikinieleza "kua makini sana, sasa huku ndio kuna mengi sana utayaeshuhudia, kitu kilichokuponza pale Chalinze ni wale wanga walikua na uwezo wa kuiona pete yako. Kuanzia sasa tunaiwekea pazia, na wewe ukiingia sehemu ukiona watu sio wa kawaida igeuze pete, kwenye hicho kito chake kiwe ndani ya kiganja. Itasaidia, kutotambulika haraka kama una uwezo wa kuwaona. Lakini chunga sana utavyo "behave" ukiona chochote ambacho sio cha kawaida (alisema "behave" hivyo hivyo kwa Kingereza). Nikawa namjibu bila kutoa sauti kua nimeelewa.

Tukaingia Kariakoo, mitaa ya kati kabisa, mtaa wa Tandamti nadhani na Nyamwezi ile, nyuma ya kituo cha polisi ya Msimbazi. Mzee akatushusha, mama akasema nipeleke, tukiwa tayari sisi tutaende na traxi nyumbani. Tukaagana na mzee na Sister wangu wao wakaendelea na safari, mimi na mama tukashuka. Ile tunatembea njiani nikaanza kuona maajabu.

Nikaanza kuona watu wapo uchi kabisa, nikaanza kuona viumbe vya kiajabu ajabu, ambavyo sio binadam kabisa, lakini nikajua hata mama yangu havioni, kwani tulipishana navyo vyenyewe ndio vinatukweppa sisis alakini sisi tukawa tunatembe kama hakuna kitu, Kidogo nianz kuwakwepa lakini sauti ikanijia ikanambaia usiwakwepoe, huwei kugongana nao hao. Ukiwakwepa wataju unawaona wataanisha ugomvi.

Muhimu ilikua ni maajabu tu kwangu, mama akaingia maduka anayoyuataka pale mtaa wa lsikukuu na Tandamyti, kuna maduka makiubwa mawili matatu ya vyakula, alienda kununua avitakavyo mimi nikamwambia nakungija kwa pembeni hapa. Basi niloyashuhudia, kama mtu una roho ndogo unaweza ukatoka mbio. Kuna wateja waliokuja pale sio binadam kabisa na wao walikua wanaagiza vitu, lakini nina uhakika waliokua wanwahudumia na wateja wengine waliwaona kama binadam, mimi nilikua pete yangu nimeigeuza na kiganja nimekifunga isionekane kabisa.

Mama alipomaliza pale, tukaenda mbele kidogo kuna maduka ya vufungashio, mwenye mama alikua na biasshra zake na kina mama wengine. Akanunua anavyovitaka, tukaenda kiyuo cha taxi hapo hapo karibu tu, mwenye duka la vifungashiuo anaonesha anafahamiana sana na mama, akamwabia usijali mama vitakufata vitu vyako mpaka nyumbani, ukichelewa utavikuta vimeshafika. Huyo kijana ndio yule simba wako? Mama akamwabia umemsahau, jamaa wa dukani akasema amkua sasa anatisha, ulikua ukija ne hapa bado kabisa. Alikua wapi siku nyingi sijamuona? Mama akasema yupo, si unajua wakikua hawa hawataki kutoka na mama zao. Yule jamama akasema "wajinga hawa, hawajui maana ya soko na biashra". Mama akacheka, aksema huyo mtu wa spana na baba yake, yeye garo lako likiwa na shida mtafute. Jamaa akasema, tena itakua vizuri, mana mafundi wasumbufu sana. Mama akamwabia yupo na baba'ke gereji, babake anamsisitiz hataki mteja wake apewe usumbufu. Jamaa wa dukani, tutembelee simba, nipe zako, gari likikorofisha nikupigie. Nikampa namba tukaondoka zetu.

Tukapanda taci akamwambia mwenye taxi, nipitishe kw Issa hapo nichukue vitu vyangu. Huyu Issa ni maariufu sana duka lake la vyakula pale Kariakoo, ndipo nilipoona wateja wengine sio binaadam wanenda kununua vitu. Ka ufupi Kariakoo nzima ilijaa mambo ya ajabu ajabu, kuna watu wako uchi, kuna watu unawaona vilema kumbe sio watu. Kuna watu huoni kabisa sura zao, Kuna watu wamebeba watu wengine kama wanawatembeza lakini wengine hawawaoni. Yaani pale ni vurugu tupu, Kuna watu niwashuhudia wapo nje madukani, wakiwa uchi kabisa na wamekaa juu ya viti, tena maduka mengi tu. Nikaona watu wanauza bidhaa mtaani uchi kabisa. Kama wale kina mama wa Chalinze, tena wanawake kwa wanaume. Nikaona wanawake wanauza bidhaa uchi lakini ukiwatazama viuri unaona ni kama wanaume aliovaa kimjini wanafanya biashara. Mjjini wansema ni vurugi mechi.

Tulipoondoika kuelekea Ilala ndio nikaufaidi mtaa wa uhuru, kuanzia ile raundi abauti ya Uhuru mpaka tunaelekea Ilala ni vituko vitupu, watu wapo uchi kwa makundi, kuna watu wamekaa pale raundi abauti uchi wa nyama, hawana hata habari ya dunia, wenye juruka, wenye kutua. Niliona kitu kimoja cha ajabu mpaka nikata kustuka, ndani ya taxi. Niliona kuna watu wawili warefu wamevaa nguo sio za kaiwa kama sare fulani, lakini walikua wanatembea kiukakamavu huku wanakagua kila kitu wanachokiona, wakatazama sana taxi tulioipanda nikaona kama wamnesemezana kitu wakawa wanaifata taxi kama wameona kitu kisicho cha kawaida, pale pale ikaja sauiti ya Arsis ikanambia, usiogope hawawezi kuwafikia kabisa, wataishia kuwatazama tu. Nitakueleza zaidi kuuus hao unaowana baadae. Basi taxi yetu kila inapokwenda na wao wako pembeni wanatembea nyuma yake lakini hawaifikii, mwisho wake wakageuza wakarudi walipotoka, kama wamaumua hawawezi kuifikia.

Tukafika nyumbaniu salama salmini, mimi nikiwa hoi kwa mawazo. Nikaingia chumbani kwangu moja kwa moja, sikungoja kitu nikaingia kukoga, nikaslai. Ndio nikatoka nje nikachukua nanasi moja kubwa nikalimenya nikawa nalila peke yangu, likiua tamu kweli. Nikasema leo sili kitu, hili hili linatosha kabisa, nilipomaliza nikanawa nikaingia chumbani kujipumzisha kidigi nilikua nimechika zaidi kiakili kuliko kimwili.

Itaendelea.
kambi
 
hahaha ! Wakati unaswali kama maamuma ulikuwa unaushahidi gani unafanya jambo sahihi na limeelezwa kwenye quran?
Nimekuta wazazi wangu wanafanya. Sijaisoma kwenye Qur'an. nimesoma baadhi ya muhadithin wakieleza hilo.

Una badili mada?Mada ya Adam kua hajatajwa kua ni mtu wa kwanza kuumbwa kwenye Qur'an. Na Hawa mmemtoa wapi? Imekua ngumu kwako?

Jibu maswali twende taratibu hapa najua uwezi toka, Ulianza kuswalia maiti baada ya kuwasoma baadhi ya mhadithin au kabla ?
 
Jibu maswali twende taratibu hapa najua uwezi toka, Ulianza kuswalia maiti baada ya kuwasoma baadhi ya mhadithin au kabla ?
kabla.

Swali li[pi sijakujibu? Mimi sichei na elimu kwa kupindisha pindisha maneno. Sijafundishwa hilo kwenye elimu, au najua au sijui. Arsis anasema "Evidence based knowledge is either black or white, no gray shades".

Adam hajatajwa kua ni mtu wa kwanza kuumbwa ndani ya Qur'an, unakubaliana na hili au hukubaliani?

Hawa umemtoa wapi?
Simba.
 
Nimekuta wazazi wangu wanafanya. Sijaisoma kwenye Qur'an. nimesoma baadhi ya muhadithin wakieleza hilo.

Una badili mada?Mada ya Adam kua hajatajwa kua ni mtu wa kwanza kuumbwa kwenye Qur'an. Na Hawa mmemtoa wapi? Imekua ngumu kwako?
Simba.
Alafu sijabadili mada nipo kwa Adamu bado ila kwakuwa wewe unaubishi usio na hoja ngoja nikufundishe kwa mifano rahisi. Mbona Arsis kaanza kutuelezea mfano wa mbu nahatujamwambia ana badili mada? Tunajua kuna hoja anayo kupitia mfano huo na mimi kupitia swali hilo nina hoja wewe jibu utaelewa tu. Uzuri nishajua ni kwanini huelewi kwahiyo nimebadili njia ya kukufundisha hii njia itendana na ubishi wako swali lingine umesema umekuta wazazi wako wanafanya Je uliwauliza wanafanya hivyo kwa nini? na wametolea wapi?
 
kabla.

Swali li[pi sijakujibu? Mimi sichei na elimu kwa kupindisha pindisha maneno. Sijafundishwa hilo kwenye elimu, au najua au sijui. Arsis anasema "Evidence based knowledge is either black or white, no gray shades".

Adam hajatajwa kua ni mtu wa kwanza kuumbwa ndani ya Qur'an, unakubaliana na hili au hukubaliani?

Hawa umemtoa wapi?
Simba.
Safii !!! kama ni kabla ulifanya kwa ushahidi gani na umesema hujaisoma kwenye quran na ulikuwa hujawasoma muhadithin?
 
Hivi mkuu kwa mujibu wa Quran inaruhusiwa mashirikiano kati ya mtu na jini?
Elimu niliopewa mimi ni kua chochote kama hakijakatazwa kwenye Qur'an na serikali ya unapoishi unaruhusiwa kukifanya.

Kuhusu majini imekatazwa kuwaabudu kwenye Qur'an.

Kumbuka pia majini kwenye Qur'an wametajwa kama kikundi cha watu ambao kwa sasa tunawaita "wasioonekana", ki lugha Jini ni neno linalotokana na Jan au kutokuonekana (wasioonekana). Nimetoa mfano mara kadhaa huko nyuma, "ki lugha" hata sisi hapa JF ni majini kwa kutokuonekana kwetu.

Soma hizi aya mbili za Qur'an, tarajama ya Ali Muhsin Barwani, nadhani zipo wazi kabisa, zipo kwenye Sabaa Q34; 40-41.

40.
Na siku atakayo wakusanya wote, kisha atawaambia Malaika: Je!Hawa walikuwa wakikuabuduni?40
41. Waseme: Subhanak, Umetakasika. Wewe ndiye kipenzi chetu si hao.Bali wao walikuwa wakiwaabudu majini; wengi wao wakiwaamini hao.41
Simba.
 
Safii !!! kama ni kabla ulifanya kwa ushahidi gani na umesema hujaisoma kwenye quran na ulikuwa hujawasoma muhadithin?
Si kila ninachokifanya kipo kwenye Qur'an, ambacho hakipo ni hakipo tu, silazimishi kiwepo.
Najitahidi sana kutofanya yote ambayo yamekatazwa na Qur'an, sijaona kama sala ya kusalia maiti imekatazwa au wewe umeona imekatazwa kwenye Qur'an?

Unayo aya ya au aya za Qur'an zinazosema Adam ni mtu wa kwanza kuumbwa au hauna?

Ewaaaa! sasa unaanza kuelewa haya niambie wapi pameandikwa adamu si binadamu wa kwanza?
 
Bwana Arsis kuna kitu nimekiona kwako ambacho si kizuri katika kutafuta elimu,,unaleta ubishi badala ya kusikiliza na kisha upime kile unachoambiwa

Bwana Lidafo alikuwa anakuuliza kuhusu kuswali swala ya jeneza / Maiti,msingi wa hoja yake,je kwenye qur'an limeelezwa hilo? Jibu ni hapana je kwanini watu wanaswalia maiti wametoa wapi hayo?

Unaanza kukimbia kwa kujua kwamba tutakuja kule kule kwenye hoja yetu ya msingi,kuswali maiti kumeelezwa na Mtume,kwahiyo hata adam kuwa mwanadamu wa kwanza qur'an haijaweka wazi lkn kupitia ulimi wa Mtume Muhammad (s.a.w) ametufahamisha hivyo

Sasa kama kila kitu ambacho hakipo katika qur'an hukikubali,je hizo swala tano unaswali za nini wakati qur'an haijaelekeza namna ya kuziswali? Je unaswali swala ya jeneza ya nini wakati qur'an haijaeleza na listi itakuwa nyingi hapo

Yeyote mwenye akili huru na timamu atakubaliana na hoja zetu juu ya kuwa adam ni mwanadamu wa kwanza.

Nimechangia hili kwasababu naona unakwepa hoja za Lidafo kitoto kabisa

Mwambie Arsis aendelee na mada yake
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom