Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Niliyoyashuhudia nilipofunguliwa macho

Arsis alishawambia Wao wengi wanatumia Ukristo kujifundishia Uislam. Yani kama Bongo walimu wanavyotumia Kiswahili kufundishia Kiingereza. Matokeo tunayo..!!
Mfano mzuri sana huo, nimemuelewa sana Arsis, Waislam imewaingia sana hiyo.

Nawashauri Waislam wenzangu tuanze kutumia Qur'an kufundisha Uislam.

Qur'an haina shaka ndani yake.
 
Tukija Kwa Suala la Adam kuwa wa kwanza au la.. Bado kuna utata kwa upande wangu kwa Mujibu wa Bible hiyohiyo.

Rejea.
"Mwanzo 26 mpaka 30: "

26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.

27 Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanamume na mwanamke aliwaumba.

28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.

29 Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu;

30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.

-Kwa hapo unaona waliumbwa watu wawili na wakapewa maagizo kwa pamoja mpaka ya kuzaliana.

-Ukirudi kwenye Habari za Adamu sasa utakuta maagizo ya Kuzaa ni kama laana kwa mwanamke (Hawa) au adhabu ya kosa walilolifanya na kula kwa jasho ikawa adabu ya Mwanaume. (Adamu)

-Bado maandiko yanasema Mungu alimuona Adamu ni mpweke. Je si kwasababu alikua anajua palikua na pea ya Binadamu wa kiume na kike kama alivyowaumba ila sasa kabaki Adam peke ake ndio kumtia usingiz ili huyu mwanamke wa sasa Atokane na yeye mwenyewe na si kumuumbia mwingine tena.

-Kwaniwazavyo mimi, kama Adamu ndie Mtu wa kwanza kuumbwa basi hakuumbwa peke ake au tayari walihaumbwa watu wengine kabla yake.

-Na kama ni yeye, basi inabidi tumfahamu aliyeumbwa nae ni nani na akaenda wapi hadi Adam akabaki mpweke?. Na Je mwanamke huyo sio ndio Shetani aliyemdanganya Hawa? Na kama ndiye je Sio ndio haya Majini tunayopata story zakua na uwezo wakua chochote kile?

Huu Uzi unaniconnectisha Dot Dot nyingi sana ambazo nabahatikaga kukutana nazo katika maandishi na story mbao mbali za kiroho na kimwili plus na tafakari za uhuru wa fikra zangu.
Adam na mke wake wa kwanza Lilith waliumbwa kwa udongo Lilith akawa tatizo she was powerful, Hawa ni mke wa pili wa Adam hakuumbwa kwa udongo.

Tafuta reference kwenye Apocrypha books na wanazuoni wa kale wa Kiebrania.

Ukiganda kwenye Biblia hii tu ya vitabu 66 kuna vitu vingi vitakutatiza lakini ukweli unajurikana kwa wenye bidii ya kusoma na kudadisi.
 
Ndugu Simba, Hatuwezi acha kuelezea tofauti za maulamaa kama kuna ikhtilaf ni jambo la msingi sana katika kujifunza.
Hii ni kutokaana na ukweli kwamba kila mtu ana angalia jambo kwa uelewaa tofauti hivyo kuna jambo ulamaa fulani anaweza kulitizama kwa udogo asione baadhi ya mambo na mwingine akaliangali kwa ukubwa akaona baadhi ya mambo ambayo mwenzake hajaona sasa wewe uki ignore kuwasoma hawa maulamaa huoni kuna mambo utashindwa kuyang'amua kwani huenda na wewe usione baadhi ya mambo.
Binafsi napenda kufuatialia tofauti za maulamaa kisha naangali hoja za nani zina nguvu nachanganya na uelewa wangu ndio napata hitimisho nibaki na msimamo upi.
Kikubwa zaidi ni kuwa maulamaa hawa reference kubwa yao ni Quran na hadithi utofauti utakuja katika uelewa tu kwenye baadhi ya mambo.
Sijakataa hitilafu zipo, ninachosema tunaposema Maulaamaa wamehitilafiana tiseme ni Qur'an wamehitilafiana tafsiri au wamehitilafiana Hadithi au wamehitilafiana yao wenye we tu.

Mfano kufunga mikono au kungua mikono Maulamaa wamehitilafiana, au sio?
Hapo wamehitilafiana Aya za Qu'an? Au hadithi? Au siasa zao tu?
Simba.
 
Nimesoma mpaka mstari wa 10 Yesu alipomfukuza Ibilisi.. haya nipe mfano halisi wa mtu aliyewahi kulifukuza jini lililomkumba
nahisi ukisoma vionjo vya Arsis yapo hayo. Kama bado hajafika yapo siku za usoni.

Labda wamejifunza kwa Yesu, haiwezekani?
Simba.
 
Adam na mke wake wa kwanza Lilith waliumbwa kwa udongo Lilith akawa tatizo she was powerful, Hawa ni mke wa pili wa Adam hakuumbwa kwa udongo.

Tafuta reference kwenye Apocrypha books na wanazuoni wa kale wa Kiebrania.

Ukiganda kwenye Biblia hii tu ya vitabu 66 kuna vitu vingi vitakutatiza lakini ukweli unajurikana kwa wenye bidii ya kusoma na kudadisi.
nakushauri usome na kisa cha Adam cha Qur'an na kinavochambuliwa na Arsis.
Simba.
 
Uzi naenda nao tangu mwanzo... ninacho
nahisi ukisoma vionjo vya Arsis yapo hayo. Kama bado hajafika yapo siku za usoni.

Labda wamejifunza kwa Yesu, haiwezekani?
Simba.
pinga ni kama yale unayoyakataa watu kutumia tafsiri zao na kulazimisha ndivyo ilivyo kwa ushahidi wa Vitabu.

Mfano Hai ni wewe Simba je unavyomuwakilisha Asis hapa jukwaani je Amekumba au upo na fahamu zako wewe kama wewe na Arsis mnawasiliana kama wewe na mimi tunavyowasiliana hapa kwa njia ya maandishi.?

Nnachopinga na sikiamini ni Mtu aliyekumbwa na Jini halafu alitoe yeye mwenyewe bila msaada wa kutoka nje ya yeye. Je hilo linawezekanaje?
 
Nimekuelewa sana, nawawachia wajuzi walioleta hizo aya za biblia waje kutufafanulia, Sisi tunapata elimu ya ziada.

Naona kama walikuja malaika kumsidia, niliposoma mimi aya ya 1 mpaka 14. Mimi ni mgumu sana wa kuandika nisiloweza kulitetea.
Simba.
 
Nimekuelewa sana, nawawachia wajuzi walioleta hizo aya za biblia waje kutufafanulia, Sisi tunapata elimu ya ziada.

Mimi ni mgumu sana wa kuandika nisiloweza kulitetea.
Simba.
Simba swalamaa!
Nafatilia kwenye post.. Azazel unamzungumziaje?
 
Adam na mke wake wa kwanza Lilith waliumbwa kwa udongo Lilith akawa tatizo she was powerful, Hawa ni mke wa pili wa Adam hakuumbwa kwa udongo.

Tafuta reference kwenye Apocrypha books na wanazuoni wa kale wa Kiebrania.

Ukiganda kwenye Biblia hii tu ya vitabu 66 kuna vitu vingi vitakutatiza lakini ukweli unajurikana kwa wenye bidii ya kusoma na kudadisi.
Tupo pamoja kabisa.. hata ukinisoma nimeichahngamsha hoja tuu... ili tupanue fikra zaidi hadi nje ya hiv vitabu vya kiimani.

Habar za Lilith nimezisoma pia.
 
Nimekuelewa sana, nawawachia wajuzi walioleta hizo aya za biblia waje kutufafanulia, Sisi tunapata elimu ya ziada.

Naona kama walikuja malaika kumsidia, niliposma mimi aya ya 1 mpaka 14. Mimi ni mgumu sana wa kuandika nisiloweza kulitetea.
Simba.
Malaika walikuja baada ya Ibilisi kufukuzwa na kuondoka. na walikuja kumpa Big up na kumsujudia.

Swali: mbali na Mungu je Malaika wanaweza kumsujudia Mwanadamu.? Mathayo 4 mstari wa 11. au ni kweli Yesu ni Mungu?
 
FaizaFoxy umetuwekea namba tu za aya, tuwekee mistari uje kujibu maswali wewe mwenyewewe na sisi tiufaidike.

Hilo la kusujudia, naweza kulijibu ki lugha. Kusujudu ni neno amblo Kiswahili imelitoa kwenye kiarabu, inategemea na lilipotumika ndio utapata maana yake szaidi. Mfano hata Msikiti Kiarabu ni Masjid, lakini mtu unaweza kusujudu popote hata kama sio msikitini,

Kusujudu kwa Kiarabu pia haimaanishi kwenda mpaka paji la uso liwe ardhini, unaweza kusjudu hata kwa ishara tu, ukiwa umekaa au umelala. Unaweza pia kusujudu kiheshima kwa kuinamisha kichwa kidogo kuonyesha unyeyekevu lakini haimaanishi kusujudua ya kwenye ibada tu. Ipo ya Kiheshima kwa Kiarabu inategemea na sentensi ilivyoandikwa.

Hio ya Biblia sijaisoma n au uifanyia kazi kwa kina aya hizo. Kigiriki limetumika neno lipi? si unajua Biblia Kiswahili ni tafsiri au tarjama tu? Na tafasiri inategemea alietafsiri aliamua kutumia neno lipi, ndio utatata tunaoupata hata Waislam kwenye tafsiri au tarjama za lugha nyingine.

Wacha aliezileta aya hizo kuashiria kua Yesu alikumbwa na spepo sijui hetani au jini aje kutufafanulia, akishindwa tutaingia kufanya tafiti ya kuchambua watafsiri tofauti, na kigiriki zote zipo hizo. Au unasemaje?
Simba.
 
ASILI YA MAJINI -- 1
Katika mada hii tutaanza kuangalia asili ya hawa viumbe kwa mujibu wa Quran na hadithi.
Majini ni Viumbe walioumbwa na ALLAH, Viumbe hivyo vimeumbwa kwa mwale wa moto kama quran inavyosema katika Sura Al-Hijr (15:27)

وَالْجَانَّ خَلَقْنَاهُ مِن قَبْلُ مِن نَّارِ السَّمُومِ - "And the jinn we created before from smokeless fire"
Tafsiri '' Na majini tuliwaumba kabla kutokana na moto''
Aya hii inaonesha kuwa majini wameumbwa kutokana na moto na hapa nikuelezee kidogo ikiwa majini wameumbwa kutokana na moto na tunajua kuwa moto unatoa joto ambalo ni form of energy ukirudi katika sayansi utaona kuwa Energy can be transform from one form to another kama ilivyo katika law of conversation of energy ilivyo elezwa na Robert mayor mwaka 1842 hivyo basi ikiwa jini kaumbwa na moto na moto unatupa form of energy ambayo ni Thermal energy na energy hii inaweza kubadilika kutoka form moja kwenda nyingine ndio maana Majini wanaweza kubadilika katika namna tofauti.
Lakini pia aya hii inatupa jibu kuwa ndio maana hatuwezi kuwaona majini katika umbo lao kwani wakiwa katika umbo lao wanakuwa kama form of energy ambao huwezi kuwagusa au kuwaona bali unaweza kuhisi uwepo wao kama vile ambavyo huwezi kuligusa joto ila unaweza kujua hapa kuna joto kupitia ngozi yako either utaungua au jasho litakutoka au mfano mwingine huwezi kugusa mwanga ambao tunasema ni light energy ila unaweza kuhisi mwanga kwa giza kuondoka au mwangaza kuongezeka.
Sasa swali linakuja ikiwa hatuwezi kuwagusa au kuwaona vipi baadhi ya watu wanasema mameona majini au wametokew na majini? Hapa jibu ni kuwa wamewaona katika umbo ambalo sio asili yao yaani jini amekuja katika form ya mwanadamu au mnyama au akajidhihisha kwa sauti tu.
Tuje katika hadithi Je hadithi za bwana mtume zinasemaje juu ya asili ya viumbe hivi. Nitarudi kuhusu hadithi za mtume
ASILI YA MAJINI --2
Baada ya kuona kuwa majini wameubwa kwa moto kwa mujibu wa quran nije katika hadithi za bwana mtume muhammad swalalah alaiy wasalam.
Aisha (RA) alieleza kwamba Mtume Muhammad (SAW) alisema: "Malaika waliumbwa kutokana na nuru, majini waliumbwa kutokana na moto na Adamu aliumbwa kutokana na kile kilichoelezwa kwenu."
عن عائشة رضي الله عنه قالت: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «خُلقت الملائكة من نور، وخُلق الجَانُّ من مَارِجٍ من نار، وخُلق آدم مما وُصِفَ لكم».
[صحيح] - [رواه مسلم]
Hadthi hii ni sahihi na imepokewa na muslim, Katika hadithi hii tumeona kuwa Malaika wameumbwa kutokana na nuru , majini kutokana na moto na wanadamu kutokana na kile tulichoelezwa kwa maana hapa mtume alisha waeleza kuwa mwanadamu kaumbwa kutokana na udongo.
Hivyo hakuna shaka kuwa asili ya majini ni mwale wa moto. Tuje katika melengo yao kwanini majini wameumbwa?

LENGO LA KUUMBWA MAJINI.
Imetajwa katika Quran kuwa lengo la wanadamu na majini kuumbwa ni kumuabudu Allah. Kama ilivyokuja katika quran (Adh-Dhariyat 51:56)
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ -- sikuumba majini na watu ila waniabudu.

Hapa tunaona kuwa lengo kuu la kuumbwa majini na sisi wanadamu ni kumuadu Allah, swali linakuja ikiwa ilo ndio lengo la kuumba mbona majini na wanadamu tunafanya mambo ya kumkufuru mungu nadhani umesoma katika kisa cha bwana simba mabalaa ya majini jinsi wanavyokata majii(kunywa pombe), wanavyofanya uchawi na mabalaa mengine, Kuhusu wanadamu apo bwana Battor unajua mabalaa ya mwanadamu uzinzi, wizi, rushwa, chuki, uongo, dhulma, zinaa, mauaji, kukata undugu, kusengenya, ushoga, utapeli n.k kwanini yote haya na Allah anasema lengo ni kumuabudu yeye?
Quran inajibu kwa kusema katika surah Al-Insan (76:3) ''Hakika Sisi tumemwongoza katika njia. Ikiwa atashukuru au akufuru."
إِنَّا هَدَيْنَاهُ السَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرًا وَإِمَّا كَفُورًا
Hapo wamezungumzwa wanadamu kuwa muongozo upo na njia ni mbili tu ushukuru au kukufuru na majini pia imeelezwa katika surat jinn kuwa kuna kundi la majini lilisikia quran nalikakiri kuwaa ni ya ajabu na inaongoza katika haki na hawatamshikisha mola wao.
"قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا * يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَنْ نُشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا"
Lakini pia katika aya ya 11 ya surat jiinn inasema

''وَأَنَّا مِنَّا ٱلصَّـٰلِحُونَ وَمِنَّا دُونَ ذَٰلِكَۖ كُنَّا طَرَآئِقَ قِدَدٗا'' -- Na hakika miongoni mwetu wapo walio wema, na miongoni mwetu wapo kinyume na hivyo; tulikuwa njia mbalimbali.
Hapa utaona kuwa majini wenyewe wanasema kuna wema na wabaya hivyo suala linabaki kwa mwanadamu au jinn kuchagua njia ya kufuata na watakao mtwii Allah malipo yao ni pepo na watakao kufuru na kumuasi ALLAH ni motoni kama ilivyo katika quran
"قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ فِي النَّارِ"
(Allaah) Atasema: Ingieni motoni pamoja na ummah zilizokwishapita kabla yenu miongoni mwa majini na wana Aadam”. [Al-A’araaf: 38]

Toka nimeanza kuelezea mpaka hapa kuna mambo utagundua kuwa kwa mujibu wa uislamu:-
  • Malaika wameumbwa kwa nuru, Majini kwa moto na wanadamu kwa udongo
  • Lengo la majini na wanadamu ni kumuabudu Allah.
  • Watako fanya kinyume na kumuabudu Allah malipo yao ni Moto.
Hivyo basi, Ushirikiano wowote wa mwanadamu na majini katika kumuasi Allah ni makosa na imekatazwa katika uislamu hilo halina mjadala, ni KUFRU.
Mjadala unabaki Je ni sahihi mwanadamu na majini kushirikiana katika wema mfano bwana Arsis alivyoshirikiana na Simba katika kumuokoa msukule huko unguja na mifano kama hiyo Je yafaa?
Inshaalah, Nitalieleza pia kwa kadri ninavyoelewa, Hapa hapataki muhemko maana pana mambo mtu anaweza ona yafaa kumbe haifai na mengine kuona hayafai kumbe yafaa.
Nitarudi kuelezea maisha ya majini, kuzaana kwao, tabia zao, na kubwa zaidi kwanii wanasumbua wanadamu.
 
Sijakataa hitilafu zipo, ninachosema tunaposema Maulaamaa wamehitilafiana tiseme ni Qur'an wamehitilafiana tafsiri au wamehitilafiana Hadithi au wamehitilafiana yao wenye we tu.

Mfano kufunga mikono au kungua mikono Maulamaa wamehitilafiana, au sio?
Hapo wamehitilafiana Aya za Qu'an? Au hadithi? Au siasa zao tu?
Simba.
Quran itaitalifiana vipi wakati ni moja ?
Kwani unaposikia maulamaa wameitalifiana unaelewa nini?
Mbona sentensi injieleza hiyo maulamaa ndio wameitalifina sio quran, wameilafiana katika kufasiri quran, Ndio maana kuna tafsiri za quran kwa mujibu wa fulani na nyingine kwa mujibu wa fulani.
Point yangu ni kuwa katika hizo itilafu zao ni muhumu kuzisoma katika kutafuta elimu ni sawa na wewe unataka kufanya Scientifi Research ya kitu fulani ni lazima upitie nakala mbalmbali za waliotangulia kufanya research ya jambo ilo au linalofanana na hilo inaitwa "To conduct a Literature Review"
 
Sio Qur'an inahitilafiana, wanahitilafiana maulamaa na tafsiri.

kama mada ya Adam inaoendelea humu, wapo wanasema Adam ni mtu wa kwanza na mmoja tu, wapo maulamaa hilo hawalikubali, sasa tuisome Qur'an mwenye ushahidi wa Qur'an ndio mshindi au sio?

Si uliona Arsis kapandisha video clip ya Alim mkubwa sana anasema Adam wapo wengi ttena aliisitiza kwa Kiarabu :kathiiiir".

Na wewe si ulikua unahitilafiana na hilo au sasa umeshakubali kua Adam hatajwa kua ni mtu wa kwanza kuumbwa ndani ya Qur'an?
Simba.
 
Quran itaitalifiana vipi wakati ni moja ?
Kwani unaposikia maulamaa wameitalifiana unaelewa nini?
Mbona sentensi injieleza hiyo maulamaa ndio wameitalifina sio quran, wameilafiana katika kufasiri quran, Ndio maana kuna tafsiri za quran kwa mujibu wa fulani na nyingine kwa mujibu wa fulani.
Point yangu ni kuwa katika hizo itilafu zao ni muhumu kuzisoma katika kutafuta elimu ni sawa na wewe unataka kufanya Scientifi Research ya kitu fulani ni lazima upitie nakala mbalmbali za waliotangulia kufanya research ya jambo ilo au linalofanana na hilo inaitwa "To conduct a Literature Review"
Kuna kitu sielewi, tunaambiwa waislamu wanahifadhi Quran vifuani mwao, sasa hii tafsiri ya maulamaa ni ya kazi gani? Au waislamu hawaelewi wanachokariri kama mimi shuleni nilivyokuwa nakariri somo la physics bila kuelewa?
 
Hata swala Adam kuwa binadamu wa kwanza lipo kwenye Biblia, waandishi wa Quran walisahau kucopy.
alafu huyu Arsis huko post za nyuma alisema biblia ni kitabu cha wagiriki..nyie kama wakristo mnasemaje kuhusu hilo embu mbane Arsis atupe majibu kuhusu biblia ni kitabu cha wagiriki kivp yaan?
 
Kuna kitu sielewi, tunaambiwa waislamu wanahifadhi Quran vifuani mwao, sasa hii tafsiri ya maulamaa ni ya kazi gani? Au waislamu hawaelewi wanachokariri kama mimi shuleni nilivyokuwa nakariri somo la physics bila kuelewa?
Swali zuri sana hilo. Lakini ukweli ni kua wengi kwanza tunafundishwa Qur'an kuisoma, halafu baadae ndio tunafundishwa masomo mengiune baada ya kujua kuisoma, sasa wengi wetu wakishajua kuisoma hawaendelei tena utawasikia "nimehitu".

Wale wanaoendelea kuisoma na mafundisha yake wengine hawabebi tafsiri ya mtu, tena wanahitilafiana na tafsiri za watu wengine.
Simba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom