Mwana JF aaga dunia!

Status
Not open for further replies.
Bwana ametoa bwana ametwaa, nimwanajashi tuliempenda sana hapa JF , lakini mungu kampenda zaidi yetu.

mapenzi ya bwana jatimizwe

Emen
 
Hili ni pengo kwa wana JF, lakini mapenzi ya Mungu yatimizwe! Mme mfiwa ambaye ni mwana JF, tukopamoja nawe katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Mungu akutie nguvu!
 
Pole mme kwa kupoteza mwenza - Mungu akupe nguvu kukabiliana na haya,
Poleni ndugu wa marehemu,
Pole Maxe - marehemu alikua zaidi ya mwana JF kwako, alikugusa moja moja,
Poleni wana JF wote, sehemu yetu imepungua na tuna maumivu.
MUNGU AMWANGAZIE MAREHEMU MWANGA WA MILELE AMEN.
 
Pole zimfikie mwana JF mwanzetu mme....bwana alitoa na bwana ametwaa...
Kazi yake haina makosa...My her soul rest in internal peace.
Amina.
 
Dah....Mkuu wangu mwanaume uliyefiwa pole sana, pole pia kwa familia

Tuko pamoja Mkuu na Mola akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu

Tunamuombea marehemu roho yake ilale pahala pema peponi, Amina.

Pole sana!
 
Mwanaume uliyefiwa pamoja na familia yako nzima, ndugu jamaa na marafiki pamoja na jumuia nzima ya JF, naomba nitoe pole nyingi sana kwa msiba huu uliotokea...... Bwana alitoa, naye ndiye aliyetwaa.... Jina la Bwana Lihimidiwe!!!
 
This is unbelievable...R.I.P....The work of the lord is done
and one blessed soldier heads home to prepare a place for
the rest of us.
Mungu ni Mkuu!​
 
mungu akupe moyo wenye subira na uvumilivu na wenye kushukuru.

na zaidi uombe sana na kusema mola asikufitinishe baada yake.

na hii ina maana usije ukawaza kuwa mola amekuonea au hakufanya kile ulichotaka wewe

maamuzi ya bwana ni yenye hekima kuliko maono yetu

kubwa zaidi nnamuomba jaala ampuzishe pahala pema huko kwenye mabustani ya milele na maisha ya milele
 
Masikitiko makubwa japo sote njia yetu ndo hiyo hiyo, ila kutangulia kunauma

Poleni sana familia ya mme pamoja na wanandugu wote na wana JF wote

Aluta continua
 
Poleni wafiwa kwa msiba huu mzito wa mwanaharakati mwenzetu.

Mungu aiweke mahali pema peponi roho yake.
 
Pole Maxe - marehemu alikua zaidi ya mwana JF kwako, alikugusa moja moja,
Kweli kabisa mkuu Roya,

Huyu kwangu alikuwa zaidi ya mwana JF. Alikuwa sehemu ya familia kwangu. Mme wake kwangu ni kama kaka, yeye kwangu badala ya shemeji nilimwona dada kwani alikuwa ni mtu wa kunipa ushauri kila nilipouhitaji.

Sijaenda kazini, nipo njiani kuelekea msibani. Nasikitika nikiwa huko sintokuwa online.

Mungu ndiye mpangaji, alimleta duniani na amemchukua mwenyewe kwa mapenzi yake. Mapenzi yetu yalikuwa ni kuendelea kuwa naye lakini yeye (Mungu) kampenda zaidi.

Jina lake na lihimidiwe!
 
Shocking news!
Soldier in the army of JF has completed her race on earth, Let her have a rest from illness troubles. Pole mme and family
r.i.p madam
 
Pole sana mwenzetu kwa kuondokewa na mwenzi wa maisha, ni msiba mzito. Mwenyezi Mungu akupe nguvu za kukabiliana na hali hii, na akujaalie moyo wa subira na wa kuyakubali yote yatokayo kwake, kwa maana yeye ndiye ajuaye wakati wa kuvuna shambani mwake. Mshukuru Mungu kwa maisha aliyomjalia marehemu hadi kipindi hiki alipoamua kumtwaa.

Bwana ampokee pumzikoni milele
Aone mwanga wa milele
Apumzike kwa amani
Amina.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom