Mwana JF aaga dunia!

Status
Not open for further replies.

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,076
7,857
Heshima zenu wana JF. Nasikitika kuwafahamisha kuwa mwana JF ambaye alitangazwa hapa na Maxence Melo kuwa anaumwa sana na kuomba tumwombee amefariki dunia.

Mwana JF huyu ambaye ni mke wa mwana JF mwingine ameaga dunia usiku wa kuamkia leo.

Kwa walio Dar es Salaam wasiliana na Maxence kwa maelezo zaidi.

Kwa niaba ya uongozi wa JF, napenda kutoa salaam za rambirambi kwa familia ya marehemu na kumwomba Mungu awape nguvu katika wakati huu.

Yote ni mapenzi ya Mungu.

Amen.
 
Bwana ailaze roho yake mahali pema peponi. Nimesikitishwa sana mmoja wa makamanda wa JF katutoka.
 
Mwenyezi Mungu amlaze mahala pema peponi. Familia ya mme Poleni sana, aidha tupo pamoja nanyi katika wakati huu mgumu.
 
Familia ya mme Mungu na awatie nguvu kipoindi hiki kigumu na ingekuwa vizuri kama tukielezwa msiba utakuwa wapi kwas ujumla wake ili kila mmoja aweze kushiriki kwa nafasi yake bila kutuma private sms kwa mjumbe mmoja kwani naamini hatakuwa na nafasi ya kujibu haswa ikizingatiwa yupo kwenye pilika za msiba .
 
Poleni sana wanafamilia ya marehemu!MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi!
"kwa maana tu mavumbi nasi mavumbini tutarudi"MWANZO 3:19.
Amen!
 
Namwomba Mwenyezi Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Pahali Pema Peponi. Amina.

Ninamasikitiko Makubwa Kusikia Habari Hizi.

Mme ambaye ni mwana JF na Familia Zote, Marafiki na Jamaa Wote Nawapa Pole.

SteveD.
 
Mbinguni Kuna Makao Mazuri Sana Kwa Mpiganaji Kama Yeye,aliyechukia Ufisadi Na Kupenda Haki Tulikupenda Lakini Mungu Alikupepa Upeo,wanafamilia Poleni Sana.
 
Inna lillahi wa Inna Illaihi Rajiuun.

Sisi sote ni wa Kwake Allah na Kwake Yeye Tutarejea!

Nawapa pole ndungu jamaa na marafiki wa marehemu.
 
'Uliumbwa kwa mavumbi na Mavumbini utarudi'. It is hard time for relatives and friends of the late FD, We wanaJF, we would like to remind you that stay cool, show your solidarity, comforting each other this is how God directs us to do when faced difficult situation.
 
INNA LILLAHI WA INA ILAHI RAJIUUN, Napenda kutoa pole zangu za dhati wa wanafamilia, Mungu amlaze marehemu mahala pema Amina.
 
Mungu akupe moyo wa kulikabili hili mme uliyefiwa. ni mapenzi yake. Apumzike kwa amani.
 
Malaika na wampokee mwenzetu uko mbinguni ,akapate kupumnzika kwa amani ,Amina

Pole sana mme uliyefiwa, Familia yote iliyokuwa karibu na marehemu ,pamoja na wanachama wote wa Jf,tulimpenda mwenzetu ila mungu kampenda zaidi na tuendelee kumuombea na kuiombea Familia yake katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
 
Poleni wote wanafamilia kwa msiba wa mpendwa wenu. Mungu aiweke Roho ya marehemu mahala pema na pa juu na please ukimuona fisadi yeyote huko afu akakuomba umpige tafu kwa walau tone la mate kupunguza ukali wa moto, geuka nenda zako!
Amina.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom