TANZIA Mwenyekiti wa CCM Tabora Hassan Wakasuvi afariki dunia akiwa ofisini

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,815
4,565
1708615792622.png

Hassan Wakasuvi enzi za uhai wake

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Hassan Wakasuvi kilichotokea Leo tarehe 22 Februari, 2024 Mkoani Tabora.

Chama Cha Mapinduzi kitamkumbuka Ndugu Hassan Wakasuvi kwa utii, uaminifu na uzalendo wake katika kukitumikia Chama na Taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan anatoa salamu za pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki, wanachama wa CCM na Watanzania wote walioguswa na msiba huu.

Aidha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Dkt. Samia Suluhu Hassan anawaomba wafiwa wote waendelee kuwa na subra na uvumilivu katika kipindi hichi kigumu cha majonzi ya kumpoteza mpendwa wao.


1708615598046.png


---

Chanzo cha mwenyekiti CCM Tabora kufariki akiwa ofisini​

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora, Hassan Wakasuvi amefariki dunia ghafla akiwa ofisini kwake mkoani humo.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo Alhamisi Februari 22,2024, kwa njia ya simu, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Tabora, Iddy Mambo amethibitisha kifo cha kiongozi huyo wa chama na kusema mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitete mkoani humo.

Mambo amesema mwenyekiti huyo amefariki akiwa ofisini kwake wakati akisuburia ugeni wa Mwenyekiti wa Jumuiya Wazazi CCM Taifa, Fadhil Maganya, aliyetarajiwa kuanza ziara yake ya chama mkoani humo.

“Ni kweli kabisa Mzee wetu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tabora na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM ametutoka, muda kama saa 8:30 mchana, ameamka leo akawa anadai kwamba hajisikii vizuri, lakini akaja ofisini kwa maana tulikuwa na shughuli ya kumpokea mwenyekiti wa wazee Taifa ambaye alikuwa na ziara ya siku nne katika mkoa wetu.


“Wakati tunasubiria pale basi akasema alikuwa ana changamoto anasikia jasho linamtoka kwa wingi na hajisikii, kwa hiyo akabaki ofisini kwa ajili ya kutusubiria. Sisi tulivyokwenda kumpokea mwenyekiti wa wazazi Taifa, nikapigiwa simu kwamba mzee wetu anaumwa kwa hiyo nilivyoenda kumchukua kwa ajili ya kumpeleka hospitalini tukiwa njiani bahati mbaya kumbe alikuwa ameaga dunia,” amesema Mambo.


Mwenezi huyo amesema Wakasuvi ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM mkoa mwenye umri mkubwa, atakumbukwa kwa uzalendo ndani ya chama, uwezo wa kusimamia na kutopenda uonevu jambo linalotajwa kumfanya adumu kwenye siasa za chama hicho.

“Nadhani ziara haitokuwepo kwa mujibu wa itifaki za chama chetu, kwa sababu watu wote tuko kwenye majonzi, tunaratibu shughuli za mazishi ya mpendwa na kiongozi wetu. Alikuwa ni mtu mwema sana kwa sababu amekisaidia chama kwa muda mrefu,” amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Louis Bura akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Dk Batilda Buriani, amesema uongozi wa mkoa huo umeitisha kikao cha dharura na familia ili kupanga taratibu za mazishi yanayotarajiwa kufanyika nyumbani kwake eneo la Mabama wilayani Uyui mkoani humo.

“Niliposikia taarifa za kifo chake nilienda hospitalini kujiridhisha nikakuta ni kweli ni yeye amefariki na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Kitete. Tutatoa taarifa za mazishi kadri tunavyojaaliwa,” amesema Bura.

Naye, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora ya Kitete, Mark Waziri, amekiri kumpokea mwenyekiti huyo na kusema baada ya vipimo kufanyika ilibainika alikuwa ameshafariki kabla ya kufikishwa hospitalini hapo.

“Kutokana na historia yake inaonekana alikuwa na shinikizo la damu la kupanda ambalo ndilo linadhaniwa kusababisha kifo cha mwenyekiti huyo. Mwili wameuhifadhi vizuri ukisubiria maziko,” amesema Dk Waziri.

Mkazi wa Uyui mkoani humo, Hassan Ahmed ameeleza kusikitishwa na kifo cha kiongozi huyo, huku akidai alikuwa aliamini kuwa nguvu kazi ya taifa ni vijana hivyo chama hicho tawala kiwekeze nguvu kwa vijana ili kuwa na taifa imara.

Mwananchi
 
View attachment 2912394
Hassan Wakasuvi enzi za uhai wake

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimepokea kwa masikitiko na huzuni kubwa taarifa ya kifo cha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Hassan Wakasuvi kilichotokea Leo tarehe 22 Februari, 2024 Mkoani Tabora.
vyo chama hicho tawala kiwekeze nguvu kwa vijana ili kuwa na taifa imara.

Mwananchi
Akalipwe sawasawa na aliyowatendea Wapinzani[CHADEMA]!
 
Nimepokea taarifa za kifo cha Mwenyekiti wetu wa CCM Mkoa wa Tabora, na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, babu yangu Mzee Hassan Mohammed Wakasuvi, kwa mshtuko mkubwa sana.

Ni wiki iliyopita tu niliongea naye na tukapanga ziara ya kwenda eneo la Matanda ya Nzega, Kijiji cha Malilita kilichopo kata ya Wela, kuzungumza na wananchi walio na mashaka juu ya ujio wa mradi mkubwa wa umwagiliaji bonde la Manonga na kwamba watanyang’anywa mashamba yao.

Tulizungumza mengi ikiwemo mradi wake wa kuku unavyoendelea vizuri.

Mzee Hassan Wakasuvi, leo akiwa kikaoni kumpokea Makamu Mwenyekiti wa Wazazie Taifa ghafla akajisikia vibaya na kupoteza uhai wake. Kwa hakika kifo ni fumbo kubwa sana.

Pamoja na mshtuko mkubwa niliopata, napata faraja kwamba nilipata nafasi ya kufanya kazi na wewe kwa ukaribu na kuchota hekima, busara na maarifa mengi kutoka kwako. Utumishi wako wa chama na serikali wa zaidi ya miaka 50 ilikuwa encyclopedia kwetu tuliochipukia kwenye siasa miaka ya hivi karibuni, na kwa kuwa haukuwa na choyo wala roho mbaya, hukusita kutumwagia maarifa yako.

Pumzika kwa amani babu yangu.

Inna lillah wa inna ilayhir rajiuun. #HK
20240222_214501.jpg
 
Back
Top Bottom