Tuvunje mwungano.

Wakati huo huo tukijiandaa kupeleka majeshi ya kulinda amani Pemba na Unguja.
 
Mpaka sasa sijapata wazo lolote la maana kuhusu kuudumisha Muungano. kwanza sababu za kuwepo huu muungano kwa sasa hazina maana tena. Kwani marehemu Mzee Karume baada ya kufanya mapinduzi ya kumuondoa Shamte na utawala wake baada ya uhuru wa Zanzibar mwaka 1963(ambao ccm na waunga mkono mapinduzi hawautambui)ila historia inatuambia hivyo. sasa Mzee Karume alihofia kwamba baada ya kuuondoa utawala halali kwa mapanga basi na yeye ipo siku watamuondoa hivyo njia kepee aliyoiona ni muungano na kupata ulinzi wa bara. sijui kama hali hii ya kuhitaji ulinzi bado ipo kwa wazenji.
 
TIt was formed out of a neccessity that was obvious to Mwalimu but not so obvious to the common man on both sides.(The threat of aligning to the Commuinist block;that it is now history.)
You are right on this shouldn't we follow what happened to the former Czechoslovakia? Formed under the same premisses , they decided to go apart peacefully to form Czech and Slovakia. As of today there is no hard feeling to the extent they have formed a joint intervention unit for participation in International peace keeping. Do we have the will and wisdom to do it neatly, look at how we have handled the EAC in 1977.

Today, Zbr would be much better off on its own,economically.Aid will pour in from the Islamic states,and the Western Block.It could well become another Singapore,if it were to break away.
I wonder if the so called aid from the Islamic block will be realised.They have done that now when there is an opportunity for donor agency to offer direct support to areas of interest, As for the Singapore analogy, it had already been tried but on wrong premisses of Tanzania being one country, hence no borders between Tanganyika and Zanzibar, no extra dutiee should be charged on imports thru Zanzibar transited to Tanganyika. We saw the effect, it was only a few traders who benefitted. The business dried up when the importers had to pay the tariff diference for goods transited to Tanganyika. The traders abandoned Zanzibar for Dar es Salaam. So all in all these matters are not as simple as we presume. Uganda is a member of OIC but we don't see the said flow of aid, what has Zanzibar to offer to create the flow?
 
HATMA ya mpasuko wa kisiasa visiwani Zanzibar, kati ya Chama cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM), imezidi kugubikwa na giza, baada ya vyama hivyo, kuanzisha mchezo wa kutegana katika kulipatia ufumbuzi wa kudumu suala hilo.


Mchezo huo, umedhihirika baada ya kila upande kueleza kwamba, unasubiri majibu kutoka kwa mwingine ya barua walizoandikiana kuhusu hatma ya mwafaka wa suala hilo.


Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba aliliambia gazeti hili jana kuwa wanasubiri majibu kutoka CUF kuhusu suala hilo na kwamba, haoni sababu ya kujibu barua aliyoandikiwa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad ya kukataa kuendeleza mazungumzo yaliyoitishwa upya na CCM.


"Tulitoka Butiama, tukawaandikia barua kuwaomba turejee katika mazungumzo. Wao wakatuandikia kuwa hawataki. Sasa unataka niwajibu nini? Mimi ndiye nangoja majibu kutoka kwao," alisema Makamba kwa njia ya simu jana.


Kauli hiyo ya Makamba, ilitolewa saa chache jana baada ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF Taifa ambaye pia ni Mbunge wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed, kuliambia gazeti hili kuwa, yapata wiki sasa CCM hawajajibu barua yao.


"Tuliwaandikia barua, wiki nzima sasa hawajajibu," alisema Hamad ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.


Katika barua hiyo yenye Kumbumbuku namba CUF/AKM/CCM.II/2008/007 ya Aprili 14, 2008 iliyosambazwa kupitia mtandao wa intaneti, Maalim Seif alisema CUF haiko tayari kushirikiana na CCM kuwahadaa Watanzania kwa kuendeleza mazungumzo yasiyo na mwisho na yaliyokosa nia njema.


Nakala ya barua hiyo ya Maalim Seif, ilipelekwa pia kwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume na Mwenyekiti wa CUF Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba.


Wengine, ni Mwenyekiti Mwenza wa Mazungumzo ya Mwafaka kutoka CUF, Hamad Rashid Mohamed na Mwenyekiti Mwenza wa Mazungumzo hayo kutoka CCM, Kingunge Ngombale-Mwiru.


Maalim Seif alisema pendekezo la kufanya kura ya maoni aliyoiita kuwa ni kiini macho chenye lengo la kuchelewesha utiaji saini na utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa, hakikubaliki kwa CUF.

Source: Gazeti Mwananchi
 
Zee la shamba,


Fikiri kabla haujanena muungwana. kauli yako imekwenda kushoto,hebu uko tanzania au?
Wewe wajua kuwa CCM wanaiweka nchi rehani, wanatanguliza masilahi yao mbele bila kujali yajayo, hii ni hatari sana ktk taifa letu changa.Lakini pia tusiitupie lawama CCM, lABDA TUSEME NI VIONGOZI WACHACHE NDANI YA CHAMA CHETU.
 
na Mwanne Mashugu, Zanzibar



SIKU moja baada ya kupita kwa sherehe za miaka 44 ya Muungano, wanafunzi kadhaa wa vyuo vikuu visiwani hapa, wamesema mabadiliko kuhusu hadhi ya Rais wa Zanzibar katika Serikali ya Muungano, ni kasoro kubwa inayopaswa kurekebishwa haraka.

Kutokana na kasoro hiyo, wanafunzi hao walishauri Serikali ya Muungano kurejesha haraka utaratibu wa Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Walisema marekebisho ya sheria yaliyomuondolea hadhi Rais wa Zanzibar kushika wadhifa huo, umeishushia hadhi yake Zanzibar katika nyanya ya kimataifa.

Wanafunzi hao walisema hayo walipokuwa katika kongamano kuadhimisha miaka 44 ya Muungano wa Tanzania.

Hadhi ya Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano iliondolewa kupitia mabadiliko ya 11 ya Katiba ya Muungano.

“Rais wa Zanzibar mamlaka yake yameondoka katika nyanja za kimataifa na uraia wetu umepotea kwa vile hata misaada inaishia Tanzania Bara,” alisema Khamis Issa Mohammed wa Chuo cha Elimu Chukwani.

Katika kongamano hilo lililoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar Tunguu, Haji Habib Kombo alisema kwamba hivi sasa Rais wa Zanzibar analazimika kuingia katika Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano kama waziri asiyekuwa na wizara maalum, jambo ambalo halileti picha nzuri.

Aidha, mwanafunzi huyo alibainisha kuwa hata mfumo uliopo, hauonyeshi kinagaubaga mamlaka aliyonayo makamu wa rais.

Akifafanua, alisema kuwa licha ya taratibu kueleza vinginevyo, lakini hali halisi inaonyesha kuwa mamlaka ya utendaji ya Waziri Mkuu ni makubwa kuliko ya Makamu wa Rais, suala ambalo linahitaji kuangaliwa upya, ili kurejesha hadhi ya Makamu wa Rais.

“Bila ya Zanzibar hakuna Tanzania, na bila ya Afro Shiraz Party hakuna CCM… marekebisho ya katiba yafanyike kumpa hadhi Rais wa Zanzibar,” alisisitiza.

Alieleza kuwa mfumo huo mbaya wa Muungano, hauathiri katika masuala ya utawala pekee, bali pia katika nyanja nyingine.

Alisema kuwa kutokana na mfumo huo, Zanzibar imekuwa ikiathirika kiuchumi na kutoa mfano kuwa pamoja na elimu ya juu kuwa suala la Muungano, hakuna chuo kikuu hata kimoja kilichojengwa na Serikali ya Muungano visiwani Zanzibar.

Kombo alisema kwamba Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kinapaswa kupokea ruzuku kutoka Serikali ya Muungano, badala ya kuendeshwa kwa gharama za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar peke yake kama ilivyo sasa.

Issa Kheri wa Chuo cha Elimu Chukwani alisema kwamba kero za Muungano zinachelewa kupatiwa ufumbuzi kutokana na viongozi kutozipa umuhimu.

Alisema kwamba zipo ripoti nyingi zilizokusanywa juu ya Muungano, ikiwemo ile ya Tume ya Jaji Robert Kisanga, lakini inashangaza kuwa hadi sasa mapendekezo yake hayajatekelezwa.

Alisema kwamba iwapo ripoti ya Jaji Kisanga na Francis Nyalali zingefanyiwa kazi, hivi sasa kero nyingi za Muungano zingekuwa zimeshamalizwa.

Alieleza kuwa badala ya kutekeleaa mapendekezo ya Tume ya Jaji Kisanga, Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, alitumia muda mwingi kumshambulia jaji huyo, kwa kutoa ripoti hiyo ambayo kimsingi ilikuwa inawakilisha maoni ya wananchi.

“Tume nyingi zimeundwa ikiwemo ile ya Jaji Kisanga, ikafanya kazi nzuri tu, lakini Rais mstaafu Mkapa akamshambulia kutokana na maoni yaliyopendekezwa na wananchi,” alisema.

Alieleza kwamba hakuna njia itakayosaidia kuwa na Muungano bora zaidi ya wananchi kushirikishwa na kuamua kwa kupitia utaratibu wa kura ya maoni.

Alisema kwamba hivi sasa historia ya Tanganyika ipo hatarini kupotea, kwa vile baadhi ya Watanzania wanaoishi Zanzibar wanapoambiwa wanatoka Tanganyika, wanahisi kama wanatukanwa.

Naye Omar Suleiman, alisema kwamba kero za Muungano haziwezi kutatuliwa kwa makongamano, bali kwa wananchi wa Zanzibar kujenga umoja, ili kuhakikisha matatizo yote ya Muungano yanatatuliwa kwa muda muafaka.

Alisema kwamba Zanzibar inashindwa kusonga mbele kutokana na tabia iliyojitokeza ya majungu na kuendeleza tofauti za Unguja na Pemba na hivyo kuzorotesha maendeleo ya wananchi.

“Jambo la msingi sisi Wazanzibari tuwe na msimamo, tuache tabia ya fitina na ubaguzi kwa misingi ya Upemba na Uunguja, ili tuweze kusonga mbele kutatua matatizo ya Muungano,” alisema.

Alisema Zanzibar hivi sasa ni nchi kamili yenye utawala wake, lakini rais wake hana nguvu nje ya Zanzibar.

Akifungua kongamano hilo, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Said Mzee, alisema kwamba Zanzibar inarudi nyuma kutokana na wasomi wake kuwa waoga na kushindwa kujitokeza kudai mambo ya msingi ya nchi yao.

Alisema kwamba njia nyingi za kiuchumi Zanzibar zimevurugwa na mfumo mbaya wa Muungano, lakini wasomi wengi wamekaa kimya licha ya wao na jamii kuguswa na masuala hayo.

Makamu mwenyekiti huyo alisema vikao vya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi havitasaida kutatua kero za Muungano. Alishauri kuwa watu wengi zaidi washirikishwe katika kujadili masuala ya Muungano, kwa vile mambo hayo yanagusa taifa na si CCM au serikali pekee.

Aidha, alisema kuwa udhaifu wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika utekelezaji majukumu yao, umechangia Zanzibar kukabiliwa na matatizo mengi ya kiuchumi yakiwemo yaliyo nje ya Muungano.

“Wawakilishi wetu hawana elimu ya kutosha katika kujadili mipango ya maendeleo na kiuchumi, ndiyo maana Baraza la Wawakilishi limedorora, hawa ni wazee wetu tunawaheshimu, lakini ukweli wanaburuzwa na serikali,” alisema.

Alieleza kwamba umefika wakati wajumbe wa baraza hilo kufuata nyayo za Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zito Kabwe, aliyekubali kujitolea kutetea maslahi ya wananchi na taifa.
 
Asha ni kweli bado kuna kasoro zinazojitokeza ktk muungano, ila kwa kuwa tunaye Rais (Kikwete)anayetusikiliza hakika haya yatakwisha siku moja, usiwe na shaka.
Pia usisahau tuko ktk kipindi cha mpito kwa sasa, kwani wewe ni shahidi wa haya yanayotokea, hivyo tuwe na subira ili ilo la muungamo litekelezeke
 
Hao wapelekewe kura ya maoni kama wanautaka muungano au hawautaki ,huu si wakat wa kubebeshana lawama huyo raisi wao ni lake mwenyewe kama anataka kujulikana kimataifa na kuwa na hadhi ya Kimataifa uamuzi ni wake ila kama ameridhika na hapo alipo basi makelele ya nini,yeye kama Raisi wa Zanzibar na anaamini wananchi wamemchagua sio angojee baraka za Bunge ,kwa ufupi asitishe kuhudhuria vikao ambavyo anahudhuria kama waziri asie kuwa na wizara maalum ,ijulikane rasmi kuwa sababu kuu ni hiyo ,yaani hakubaliani ,lakini hatujamuona kususa kama Mkapa !!! Inaonyesha hajiamini kama yeye ni Raisi ila Seif alisema kwenye mkutano wa juzi kuwa yeye ndie raisi halali wa Zanzibar hatujaona kushitakiwa wala kutaka atoe maelezo kutokanana na kauli hiyo naweza kusema seifu alitangaza rasmi kuwa yeye ndie Raisi ila hakufahamika na kama amefahamika na watu wamesikia na wameshindwa kumfanya chochote basi kweli Sefu ndie Raisi.
 
UAMUZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kugoma kusaini makubaliano ya mwafaka wa kisiasa ili iundwe serikali ya mseto visiwani Zanzibar, umeibua mapya, baada ya Chama cha Wananchi (CUF), kuanzisha rasmi kampeni ya kulirudisha suala hilo kwa wananchi ili waamue kuchukua hatua watayakayoiona inafaa.


Kampeni hiyo ilitangazwa rasmi na Naibu Katibu Mkuu wa CUF visiwani humo, Juma Duni Haji, alipohutubia wafuasi wa chama hicho, katika Ukumbi wa Hoteli ya Kauleti, Vingunguti, jijini Dar es Salaam jana.


Kampeni hiyo ambayo imepangwa kufanyika nchini kote, ilianzishwa rasmi na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Shariff Hamad mwanzoni mwa mwezi huu, Unguja na Pemba.


Duni alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, CCM na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), hawataki mgogoro wa kisiasa visiwani humo uishe.



Akifafanua, alisema sababu kubwa inayoifanya CCM na viongozi wa serikali zake zote, kukataa mgogoro huo kuisha, inatokana na kuhofu kushindwa uchaguzi Zanzibar, hali ambayo inaweza kuwasibu pia Tanzania Bara.


Alimshutumu Rais Kikwete kwa kumwita "mnafiki" kwa madai ya kuonyesha 'undumilakuwili' katika kuwakabili wanaokwamisha mwafaka huo, hali ambayo alisema inamtofautisha na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa na msimamo katika jambo analoliamini.


"JK ya Kikwete ni tofauti kabisa na JK ya Mwalimu Nyerere. JK ya Mwalimu Nyerere alipokuwa akisema hili liwe, basi ndilo linalokuwa. Lakini JK ya Kikwete anazomewa na wajumbe wa NEC?," alihoji Duni.


Alisema kutopatikana ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar kumesababisha hali mbaya ya uchumi, ukosefu wa ajira kwa vijana na kudumisha ubaguzi na upendeleo katika mgao wa madaraka kati ya Wa-Unguja na Wapemba.


"Katika nafasi 192 za uongozi serikalini na kwenye vyombo vya dola, Wapemba ni 26 tu. Je, hakuna aliyesoma kutoka Pemba," alihoji Duni na kuongeza: "Hayo ndiyo tunayosema tumegombana, tusikilizane".


Hata hivyo, alisema uwapo wa matatizo hayo, unatokana na wananchi wenyewe kuridhika na hali hiyo tofauti na msimamo alionao yeye (Duni).


"Mimi nilifungwa jela miaka mitatu. Nilipotoka, nilisimama kwenye maandamano kwa sababu nafsi yangu imesema 'no'. CCM jeuri wanaipata kwa sababu watendwa bado tunashiriki. Zanzibar waliwahi kususia biashara ya Sheha pale walipoamua. Hivyo, ndioa tumeamua kulirudisha suala hili kwa wananchi. Habari ndio hii," alisema Duni.


Naye Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Ilala, Waziri Doni, aliliambia gazeti baada ya mkutano huo kuwa wamepokea kwa mikono miwili maelekezo yao na kwamba, watachukua hatua pindi wakati mwafaka utakapofika.


Hatua hiyo ya CUF, inakwenda sambamba na uamuzi wa chama hicho wa kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza CCM kusaini makubaliano hayo.


Maandamano hayo yalishafanyika Unguja na Dar es Salaam kwa nyakati tofauti, mwanzoni na katikati ya mwezi huu.


CCM wanagoma kusaini makubaliano hayo, badala yake wanataka suala hilo likaamuliwe na wananchi Zanzibar kwa njia ya kura ya maoni, jambo linalopingwa vikali na CUF ambao wanauita uamuzi huo kuwa, ni "Usanii wa kisiasa wa CCM".
Source: Gazeti mwananchi
 
Kaazi kweli kweli.

CUF wakishauriwa na CCM wawaachie wananchi waamue juu ya serikali ya mseto hawataki, badala yake CUF inawaachia wananchi waamue juu ya utulivu. Sijapata kuona chama kibovu kama CUF.
 
Back
Top Bottom