hii analogy ya muungano na ndoa sijui inatoka wapi!, iwapo muungano kati ya tanganyika na zanzibar ni kama ndoa,basi ni nani dume na ni nani jike?.
 
Muungano ni kama ndoa..na kama ikishindikana kuishi pamoja basi tupeane talak kila mmoja atazame ustaarabu wake.

Muungano haukuwepo na unaweza usiwepo.Kwa wazanzibari wengi wao be it CUF au CCM deep down wanaamini kuwa muungano hauna faida kwao, na zaidi ule mkutano wa Butiama ambao CCM ZNZ walimtisha JK kuwa kama anataka kuwasikiliza hao CUF basi na wao watarudi ZNZ kivyao.Na hapo bado hatujazungumzia 60/40

Bara nao wanaona kuwa watu wa ZNZ wanaishi kwa income support ya kodi wa watu wa Bara sasa je mnasemaje wana JF tuuvunje huu muungano?

Maoni yenu Tafadhali

JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY

Bora uvunjike kama unavyosema ni kweli kwa maana hao CUF na wapemba kila siku imekuwa kimeo. Wewe GT unasemaje? Maana Zanzibar na Pemba population ni kama 1 million wakati bara ni kama 37 million. Sasa CUF mlioko UK sijui mko wangapi?
 
KaNchi kadogo kapewe mshiko wa kupigishwa kura ya Maoni kama kinataka kihendelee na linchi likubwa katika Muungano.
Ila lihatari kama hili linchi likubwa litatumia mamluki kuitawala kanchi kadogo kale.
 
hii analogy ya muungano na ndoa sijui inatoka wapi!, iwapo muungano kati ya tanganyika na zanzibar ni kama ndoa,basi ni nani dume na ni nani jike?.

Zanzibar ndo dume ndo maana, kila kitu wanataka wapendelewe si unajua mfumo dume ulivyo, zanzibar wanapenda sana kulalama, mara tunanyonywa, hoo tunataka umeme bure, hoo mifereji bure, hoo mitihani ya shule hiwe tofauti, you can see na serikali ya muungano wanawakubalia, kila kitu hewala bwana.
 
Actually Bara ndio wanaongangania Muungano..wenyewe kule visiwani hawautaki na walimwambia JK juzi kule butiama

Watu wengi wabara wanaamini wananchi wa kule wanaishi kwa INCOME SUPPORT au wana wa SUBSIDIES za wabara..hivi kama mngesikia maneno waliyokuwa wakitamka wajumbe wa CCM ZNZ kule Butiama ndio mtaamini kuwa bara kwenye hili ni ma SIMPS
 
kwanza hatuwezi kuufananisha muungano na ndoa.
ndoa kuvunjwa mungu hapendi, lakini mungu hajasema anachukia kuvunja muungana wa tanganyika na zanzibar.

muungano una dis-advantages nyingi kwa bara kama ilivyo kwa visiwani.

watu wa visiwani wengi kwa kweli muungano hawautaki, kwa vile wanaona hawawezi kuamua kitu chao mpaka kipitishwe na bara.

watu wa bara cha kwanza wamekosa identity yao. mtanganyika sasa hayupo tena, wakati mzanzibari japo ndani ya tanzania tu anatambulika.

muungano kama hauwezi kutatuliwa kirahisi, basi kusipotezwa pesa nyingi na energy nyingi kutafuta ufumbuzi, na uvunjwe.
 
sasa kama muungano wenyewe ndo huu tulio nao,mimi sioni faida yake, na hata tukiuvunja leo sioni hasara.Sababu zilizotufanya tuungane zilikuwa dhaifu sana na ndio maana mpaka asubuhi hii jamaa wanatutisha kana kwamba sisi sio nchi kamili.Leo wanakwambia magari yaliyosajiliwa bara yakienda Unguja inabidi yasajiliwe upya and viceversa,labda mimi sijui sisi Watanganyika tunapata nini toka Unguja,kama ni heshima ya kisiasa sawa.
 
Solution ndogo tu,

Referendum on both sides, simple majority on both sides wins.

No takes precedent over yes.If Zanzibar says No to the union by 51% and the mainland votes yes 80% then the union is off, for the union to continue it needs to have more than 51% on both sides.
 
kwanza hatuwezi kuufananisha muungano na ndoa.
ndoa kuvunjwa mungu hapendi, lakini mungu hajasema anachukia kuvunja muungana wa tanganyika na zanzibar.

muungano una dis-advantages nyingi kwa bara kama ilivyo kwa visiwani.

watu wa visiwani wengi kwa kweli muungano hawautaki, kwa vile wanaona hawawezi kuamua kitu chao mpaka kipitishwe na bara.

watu wa bara cha kwanza wamekosa identity yao. mtanganyika sasa hayupo tena, wakati mzanzibari japo ndani ya tanzania tu anatambulika.

muungano kama hauwezi kutatuliwa kirahisi, basi kusipotezwa pesa nyingi na energy nyingi kutafuta ufumbuzi, na uvunjwe.

Huyo mungu unamwamini wewe tuu wengine hawamwamini sasa hebu ondoa hii analogy ya mungu kwenye serikali ambayo ni secular.

Nakubaliana na wewe if it doesnt work lets break it..kama Kosovo, Eritrea etc
 
Solution ndogo tu,

Referendum on both sides, simple majority on both sides wins.

No takes precedent over yes.If Zanzibar says No to the union by 51% and the mainland votes yes 80% then the union is off, for the union to continue it needs to have more than 51% on both sides.

Hii referendum both sides wakati tunajua wa Bara ndio wanaon ungangania unategemea mimi yaani 40 million vs 1 million?
 
Hii referendum both sides wakati tunajua wa Bara ndio wanaon ungangania unategemea mimi yaani 40 million vs 1 million?

..kama unafuatilia vizuri maongezi ya watu siku hizi,utabaini kuwa hata watu wa bara hawautaki huo muungano.

..wanaotaka muungano ni tabaka tawala! watu wa kawaida wanaona hauna faida.
 
Muungano si vizuri kuuvunja ila tunahitaji kurekebisha katiba na muundo wa muungano ili uendane na hali ya sasa ya siasa. Tutahitaji seikali tatu na hilo liko wazi na nilazima litakuja kuwa ila kwa sasa tunaliahirisha tu.

HAPANA, TUWE NA SERIKALI MOJA TU AU TUSIWE NA MUUNGANO KABISA
 
Actually Bara ndio wanaongangania Muungano..wenyewe kule visiwani hawautaki na walimwambia JK juzi kule butiama

Watu wengi wabara wanaamini wananchi wa kule wanaishi kwa INCOME SUPPORT au wana wa SUBSIDIES za wabara..hivi kama mngesikia maneno waliyokuwa wakitamka wajumbe wa CCM ZNZ kule Butiama ndio mtaamini kuwa bara kwenye hili ni ma SIMPS

Hapana hawa walikuwa wameshatumwa na kufundishwa cha kuzungumza,unajua kuwepo kwa CCM zanzibar katika bunge ndiko kunakoifanya CCM ibakie hai,kumbuka tu watu hawa kutoka Zanzibar hawana faida ya maslahi kwa Taifa ni kama wapiga debe wa viongozi wa juu wa serikali.,
 
There is a completly diferent MIND SET in Zbr and Tnky. If we are big enough and bold enough to accept facts/reality ,you will not have any problem knowing the reason for the Union.It was formed out of a neccessity that was obvious to Mwalimu but not so obvious to the common man on both sides.(The threat of aligning to the Commuinist block;that it is now history.)Today, Zbr would be much better off on its own,economically.Aid will pour in from the Islamic states,and the Western Block.It could well become another Singapore,if it were to break away.
 
Wenye uwezo wa kufanya hili ni serekali ya CCM iliyopo madarakani and we all know what they will say, we have heard it before- 'tupate ridhaa ya wananchi!' as if wakati wa kuunda huo muungano kulikuwa na kitu kama hicho.

Umenipa pakuanzia!

Ni kweli kama mtoa hoja alivyosema kuwa wazanzibari deep down their heart hawaupendi muungano. Hawaupendi muungano kwakuwa wanaona hawafaidiki nao. Kisiasa mtaona wanafaidika lakini ukiangalia kwa makini utaona wana point.

Rais wa zanzibar hana tofauti na Mhe Kandoro yule mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Zamani Rais wa zanzibar alikuwa makamu wa rais siku hizi hakuna hilo! mnajua kwa nini? Hii ni choyo ya CCM wanajua kuwa hawashindi ZNZ ikija tokea CUF wakiwazidi maarifa wakashindwa "kuchukua kuweka waa" Seif au mwingine yeyote wa CUF awe Rais wa ZNZ then awe makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano! hilo haliwezekani kwani wao CCM tu ndio wamezaliwa katika dunia hii watawale!

Wenyewe wazanzibari wana ZNZ yaani Zanzibar Nzuri Zamani

Wa bara wanaosema Zanzibar wananyonya mapato ya Tanzania bara au uchumi wake unategemea Bara si kweli ila naamni kama Bara inafaidika sana na Muungano kuliko Zanzibar na nina hoja. Misaada yote inayoipata Tanzania inakuja kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania yaani Zanzibar ikiwamo maana haiji kwa serikali ya Tanganyika. Kwa taarifa yenu misaada hii haifiki hata Chumbe! inaishia Dar es Salaam!

Ukiangalia hati ya muungano kuna yale mambo 11 ya awali katika yale mambo suala la mgawanyo wa pesa zipatikanazo mafuta na gesi ya asili halikuwepo limekuja kuongezewa tu baada ya kungundulika zanzibar ina neema hiyo! ndio rafiki zangu wazanzibari wanahoji mbona madini hawakuyaweka tugawane mapato pia?

Zanzibar ni nchi ikiyokuwa imepiga hatua kubwa sana wakati inaingia katika muungano.

Msiojua Zanzibari ni nchi ya kwanza kuwa na taa za bara barani barani afrika, ya kwanza kuwa na television ya rangi barani afrika.

Kwa maana hiyo Muungano umeirudisha Zanziba kimaendeleo pengine bila la Muungano Zanzibar ingekuwa Brunei

Kareme baba aliwahi kusema "muungano ni kama koti ukiona linakubana livue" sasa ni hiari yao wabara na wazanzibari kulivua au kulifumua makwapani!

Naomba kuwakilisha hoja!
 
Back
Top Bottom