PostGE2025 Msigwa: Uhakiki wa video za CNN unaendelea, serikali inatoa wito wa CNN kufuata weledi na maadili ya uandishi
Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Kuhusu serikali kufanya uhakiki wa ripoti ya CNN, Msigwa amesema:

Uhakiki wa makala unaendelea, lakini hawajafuata weledi na uadilifu kwenye uandishi wa habari.

Si kweli CNN ilishindwa kupata upande wa serikali, akisema inashangaza chombo kama CNN kufanya makosa ya kiweledi kama hayo.

Serikali inatoa wito kwa CNN kuzingatia maadili na weledi na kujiepusha kuchapisha habari bila kufuata vyanzo halali na rasmi, kupotosha na kuzua taharuki.

Ntakuwa wa mwisho kuamini jamaa hawa kuchukua Initiatives yoyote kwenye kupata mrejesho toka kwenye uongozi husika kabla na baada ya report yao. Ngoja tuone Larry atajibu nini mana baada ya huu mrejesho
 
Kuhusu serikali kutoa ufafanuzi juu ya ripoto ya CNN, msigwa amesema:

Uhakiki wa makala unaendelea, lakini hawajafuata weledi na uadilifu kwenye uandishi wa habari.

Si kweli CNN ilishingwa kupata upande wa serikali, akisema inashangaza chombo kama Cnn kufanya makosa ya kiweledi kama haya

Serikali inatoa wito kwa cnn kuzingatia maadili na weledi na kujiepusha kuchapisha habari bila kufuata vyanzo halali.
Vyanzo halali ndio vilivyofanya mauaji, sasa wanajiandaa kutoa habsri ya uongo. CNN wameshatupa ripoti ya kweli.
 
Ili kuja na "detailed" verification njia ni ile ile:​
-Geolocated video analysis​
-Forensic analysis​
-First hand account from witnesses and victims​
-Victims document​
-Satellite images analysis​
-Drone video analysis​
Ukweli haupambwi, kama kuna maslahi binafsi ni hakika yatajidhihirisha yenyewe.​
Maarifa ya "remote sensing and imagery" ni muhimu sana katika zama hizi.​
 
Kuhusu serikali kutoa ufafanuzi juu ya ripoto ya CNN, msigwa amesema:

Uhakiki wa makala unaendelea, lakini hawajafuata weledi na uadilifu kwenye uandishi wa habari.

Si kweli CNN ilishingwa kupata upande wa serikali, akisema inashangaza chombo kama Cnn kufanya makosa ya kiweledi kama haya

Serikali inatoa wito kwa cnn kuzingatia maadili na weledi na kujiepusha kuchapisha habari bila kufuata vyanzo halali.
Tatizo la kuwa muongo unadhani unaweza kudanganya kila kitu na kila mtu..
 
Uhakiki wenyewe ndio huu waliosema hii ni CCTV footage ya gari lililomteka Mo Dewji?
20251122_045519.jpg
 
Back
Top Bottom