kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Mazishi ya shoga wa nchini Uganda David Kato ambaye alikuwa mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga wenzake nchini humo, yalikumbwa na balaa baada ya mchungaji kuwaambia waombelezaji wa msiba kuwa ushoga ni dhambi na wanaume waache kujigeuza wanawake.

Hasira zilitanda miongoni mwa mashoga na wasagaji wa nchini Uganda ambao walihudhuria mazishi ya David Kato, shoga mwanaharakati wa kutetea haki za mashoga nchini Uganda ambaye aliuliwa nyumbani kwa kushushiwa kipigo cha nguvu na watu wasiojulikana.

Wakati misa ya mazishi ikiendelea, mchungaji aliyekuwa akiendesha misa hiyo aliwageukia waombelezaji na kuwaambia kuwa ushoga na usagaji ni dhambi na hivyo watu wanaofanya vitendo hivyo watubu na kumrudia Mungu au la watakumbana na adhabu kali za Mungu.

Mchungaji Thomas Musoke akimalizia misa ya David Kato aliyeuliwa siku ya jumatano nyumbani kwake kwa kusema "Dunia inaelekea kubaya, watu wanayapa mgongo maandiko, wanalazimika kuacha mchezo wanaoufanya na kumrudia Mungu, huwezi kumtamani mwanaume mwenzako".

Ghafla mmoja wa mashoga alinyanyuka na kumfokea Mchungaji Musoke, "Hatujaja hapa kupigana", alisema huku mwanamke mmoja msagaji akiibuka na kusema "Wewe sio mtu wa kutujaji sisi, Kato ameenda kwa Mungu wake aliyemuumba Sisi ni nani mpaka tumhukumu Kato?".

Mchungaji Musoke alinyang'anywa mikrofoni na kuanza kusukumwa sukumwa na kuwafanya polisi waliokuwepo kwenye mazishi hayo waingilie kati na kumuondosha eneo hilo.

Kifo cha Kato kimekuwa gumzo kwenye vyombo vya habari vya magharibi ambapo taasisi za kutetea mashoga na wasagaji zimekuwa zikilaani kuuliwa kwake. Hata hivyo nchini Uganda habari za kuuliwa kwake hazijapewa kipaumbele.

Kato alikutwa ameuliwa ndani ya nyumba yake mjini Kampala baada ya kushushiwa kipigo cha nguvu na watu wasiojulikana.

Kato alijipatia umaarufu nchini Uganda baada ya kulifikisha mahakamani gazeti la Rolling Stone kwa kuitoa picha yake kwenye gazeti na kumtangaza kuwa ni shoga.

Taarifa za awali zimesema kwamba watu ambao hawajajulikana walivamia nyumba yake na kumshushia kipigo kizito kilichopelekea kufariki kwake.

Polisi wamemkamata mshukiwa mmoja. Hata hivyo mshukiwa mkuu ambaye alikuwa ni mwanaume aliyekuwa akiishi nyumba moja na Kato bado anatafutwa na polisi baada ya kukimbia.
 
Mmmmmmmhhhhh....eti ww ni nani kutujaji sis? Mchungaji alikuwa anasoma maandiko Matakatifu kuwa ushoga ni dhambi, sasa hawa mashoga wanapinga nini? By the way, ilikuwaje huyu shoga kato azikwe na mchungaji? Mi nadhani kwa kutetea ushoga hadharani tayar alitangaza kujitenga na kanisa hvyo asingepaswa kuzikwa na pastor.
 
kwani mashoga hawamwamini mungu?

Mmmmmmmhhhhh....eti ww ni nani kutujaji sis? Mchungaji alikuwa anasoma maandiko Matakatifu kuwa ushoga ni dhambi, sasa hawa mashoga wanapinga nini? By the way, ilikuwaje huyu shoga kato azikwe na mchungaji? Mi nadhani kwa kutetea ushoga hadharani tayar alitangaza kujitenga na kanisa hvyo asingepaswa kuzikwa na pastor.
 
mwache apate haki yake tangu lini shoga akaombewa misa ya nini??amevuna alichopanda

wewe si ni wale wapendwa???hamfundishwi upendo kwa binadamu wengine??na kutokuwa judgemental since mungu mwenyewe ndio mwenye kuhukumu???hauoni kabisaa kuwa huyo mchungaji kakosea?...haya bwana...:coffee::twitch:
 
wewe si ni wale wapendwa???hamfundishwi upendo kwa binadamu wengine??na kutokuwa judgemental since mungu mwenyewe ndio mwenye kuhukumu???hauoni kabisaa kuwa huyo mchungaji kakosea?...haya bwana...:coffee::twitch:

mashoga ndo walioiangamiza dunia ya sodoma na gomorah.....na wapo hapa kuangamiza hii pia...
 
YAAH ni kweli hivi kwanini marekani imeruhusu watu hawa?na baadhi ya dini zimeruhusu uwepo wa watu hawa huku zikijua fika sodoma na gomola iliteketea kutokana na tabia hizo
mashoga ndo walioiangamiza dunia ya sodoma na gomorah.....na wapo hapa kuangamiza hii pia...
 
Moja ya makundi yaliyo mpa kura kwa wingi Obama ni hao mashoga.... Mchungaji alifuata nini huko???
 
hata Yesu alikulana wenye dhambi. Mchungaji alienda pale kuwaambia ukweli na ujumbe ukawaingia barabara ndio maana wakamjia juu.jamani hii laana kabisa tena zaidi ya sodoma na gomora.nashangaa viongozi nakataa kumwogopa Mungu na kuwatii zaidi binadamu huu ni upupu kabisa.
 
So sad to hear that some people hate their fellow man without any apparent reason and, i am appalled this is like saying born with dark skin or blue eyes is wrong, so sad,

people actually hate and even kill homosexuaals becase of what who they are! This is shame and unfair, being a guy or lesbian is not against human nature therefore guys must be treated in the same way that others who are not guys do! It is better to know that being guy is a matter of choice, rather is inborn,,, so they can't change who they are!

If homosexuality is against nature why some animal,, (about 450 species) who are well reserched are practicing homosexuality and u have to understand that technically we are all mammals,,, so we have nothing to do with who we are!
Better leave guys alone as long as their happiness never makes you sad!
 
So sad to hear that some people hate their fellow man without any apparent reason and, i am appalled this is like saying born with dark skin or blue eyes is wrong, so sad,,,people actually hate and even kill homosexuaals becase of what who they are! This is shame and unfair, being a guy or lesbian is not against human nature therefore guys must be treated in the same way that others who are not guys do! It is better to know that being guy is a matter of choice, rather is inborn,,, so they can't change who they are!
If homosexuality is against nature why some animal,, (about 450 species) who are well reserched are practicing homosexuality and u have to understand that technically we are all mammals,,, so we have nothing to do with who we are!
Better leave guys alone as long as their happiness never makes you sad!

guys are good we just hate gays.....anyway sucks to be you
 
Binafsi siwezi kumhukumu mtu kwa matendo yake, Mungu ndio kazi yake, na pia katika Biblia nadhani imeandikwa katika agano la kale ya kuwa watu hao wauwawe kwa kupigwa mawe, mbona hilo halifanyiki kama watu wanafuata vitabu vya Mungu? wakati umebadilika, na maandiko nayo yanaenda na wakati...
 
Ninyi mnasema nini!

hapa USA kuna Kesi ya nguvu ilifunguliwa dhidi ya Mapadre wa RC kuwala witi Vijana wadogo wa miaka 10 mpka 17.

Hukumu ilitolewa na Kanisa Katoliki kutozwa mamilioni ya Dola.

Trip nyingi za papa hapa Marekani ni kuilanisha migogoro ya kula witi na ile ya Mapadre wa USA kutaka kuasi na kuoa.

Askofu/mchungaji Eddy Long kanisa moja la uamsho hapa Marekani Maarufu kwa kutoa misaada nchini Kenya anakabiriwa na Tuhuma za kuwala witi vijana kadhaa ambao ni sehemu ya kondoo wa zizi lake.

images


images



images



Wanakemea Dhambi kisha wanarudi kuzitenda mafichoni hawa si wachungaji wa kondoo wa Bwana ni Mbweha wabaya na Hatari kwa kondoo wa Bwana waliopotea.
 
Back
Top Bottom