Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani lasimika askofu wa kwanza anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
Inavunja moyo na kuumiza kusikia na kuona Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani (Evangelical Lutheran Church of America) limemsimika rasmi Askofu wa kwanza anayejihusisha hadharani na mapenzi ya jinsia moja (shoga). Si mwingine ni Askofu Megan Rohrer.

Askofu huyu anayejihusisha na mapenzi ya jinsia moja alivalia vest maalumu ya kuzua risasi (bullet proof) ndani ya joho lake wakati wa sherehe za kusimikwa kwa HOFU ya kushambuliwa kwa risasi na watu wanaopinga vitendo vya ushoga kubarikiwa ndani ya Kanisa.

Katika ibada hiyo ya kusimikwa Askofu huyo, baadhi ya Maaskofu na Wachungaji na hata waumini walionekana kuvalia ribbon, cola, na vitambaa vyenye rangi ya bendera inayotumika kutambulisha wapenzi wa jinsia moja (mashoga, wasagaji miongoni mwa wengine) tazama picha.

Askofu huyo katika hotuba yake baada ya kusimikwa aliwashukuru wote waliompigia Kura wakiwemo Wachungaji wanaounga mkono vitendo vya mapenzi ya jinsia moja akisema "tunataka kuionesha dunia kuwa watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wanaweza kuhubiri Injili na kwamba ni watu wazuri na waaminifu kwa Mungu.

Rohrer anakuwa mmoja kati ya Wachungaji 7 wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ) waliokubalika na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani mwaka 2010 baada ya Kanisa hilo kuruhusu kubariki Wachungaji wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja wakiwe wakiwemo mashoga na wasagaji. Licha ya Rohrer kuwa shoga lakini ameoa na ana mke na watoto wawili.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Marekani ni moja ya Kanisa kubwa nchini humo ambapo lina wafuasi wanaopindukia milioni 3.3.

Wimbi la Wachungaji na Maaskofu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja lilianza kwa kasi ndani ya Kanisa la Anglican huko Uingereza ambapo upepo huo sasa umeenea katika makanisa mengi barani Ulaya, America hususani Marekani na hata Afrika. Je hili linamaanisha nini kwa Kanisa?

Je ni mwanzo mwingine wa kuilekea Sodoma na Gomorrah?

Je umewahi kuwaza utajisikiaje siku unamuona Mchungaji au Askofu shoga anakuongoza misa na sala?

Nini maoni yako?
IMG-20210916-WA0001.jpg
 
Tutahamia kwa Mwamposa tuachane nao

Tatizo makanisa ya sasa yamekuwa kama majumba ya ukumbusho na kusali kumekuwa kama utamaduni,ndio maana watu wanaingia kanisani na kutoka na matatizo yao

Kama kanisa linamhubiri Kristo kweli na moto wa roho mtakatifu unashuka huyo pepo wa Ushoga anapenyaje yani?
 
wakristo ndo mambo yao
Usiuhusishe ukristo na usheratani wao. Wao wanachofanya nikuingiza maovu yao kwa kivuli cha ukristu lakin ukiwauliza ni wap kwenye biblia kumeruhusiwa kufanya hvyo hawato kuonesha. Ndio maana ata kwenye biblia wakristu wameaswa wazijaribu kila roho zinazokuja kwa jina lake maana alijua sio ajiitaye mkristu ni wa kristu
 
Back
Top Bottom