Mary Chatanda: Freeman Mbowe amekosa shukrani kwa Rais Samia pamoja na kumtoa gerezani. Huenda ameathirika kisaikolojia

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao

"...anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."

Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.

Chanzo: Jambo TV
 
Ana akili fupi sana, pili mahakama ilimkuta Mbowe hana hatia na sio Samia kumto, atuachie upuuzi

Pia, mtu kukufanyia jema haimaanishi akifanya ujinga ushindwe mwambia

Hapa ndipo nazidi kujenga picha ya viongozi wetu, mtu akiwa kiongozi hawezi kemea uovu kisa hataonekana mwenye shukran ya uteuzi, hapa kweli tutegemee kutoboa kama taifa kweli?

Tujifunzeni Malaysia , CCM NA JUMUIYA ZAKE NI SHIT
 
Yaani ukimsikiliza vzr yule mama unaona kbs kichwani ni mweupe mnoo...inafikia unajiuliza kuwa ccm huchagua majinga kukiongoza chama??? Kwamba hakuna wamama ndani ya chama mpk wakampa mtu mjinga kama yule??? Eti mbowe alifungwa na hayati magufuri , kweli?? .. badala ya kujibu hoja yy analeta ngojera za kubumba bumba... kifupi ccm imekosa watu wa kuiongoza
 
View attachment 2690531

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao

"...anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."

Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.

Chanzo: Jambo TV

Huyo angeelezasera zake na si kupoteza muda kujadili viongozi wa vyama wanaowatetea wananchi.
Bosi wake wa chama ajatoka kutejitetea kama kweli kaingia mkataba mbovu au la.
 
View attachment 2690531

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) Taifa Mary Chatanda amemshukia vikali Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa Freeman Mbowe kwa kile alichokieleza kuwa amekosa shukrani kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye alimtoa gerezani alikokaa kwa muda mrefu tangu kipindi cha utawala wa serikali ya awamu ya Tano iliyokuwa ikiongozwa na Hayati Dkt.John Pombe Magufuli

Akizungumza kwenye Mkutano wa hadhara Mkoani Lindi, ikiwa ni muendelezo wa ziara zake kwenye mikoa ya Kusini mwa Tanzania Chatanda ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM amesema, hivi karibuni Mwenyekiti huyo wa CHADEMA amekuwa akimtukana Rais Samia kwa kueleza kuwa ameuza nchi jambo ambalo halina usahihi na linachonganisha Wananchi, hivyo kutoa wito kwa Wananchi hao kuwapuuza na kutowasikiliza pale watakapoitisha mikutano yao

"...anazungumza, anamtukata, anasema ameuza nchi, kwani sisi tumeuzwa hapa tulipokaa?, Kuna mtu anayesema kuwa nimeshawanunua ninyi ni watu wangu?, Wakija msiwasikilize.., anasema anaenda kujiandaa mikutano 70..."

Ameendelea kueleza kuwa kinachotokea kwa Mbowe sasa inawezekana ameathirika kisaikolojia baada ya kuwa jela kwa muda mrefu hivyo alipaswa kutulia kwakuwa jela kuna mambo mengi.

Chanzo: Jambo TV
Mbowe hawezi kukubali nchi iuzwe kisa alitolewa gerezani/alifutiwa mashtaka ya mchongo. Hawa watu bwana! Hizi ni akili za kuvua kufuli kwaajili ya vyeo.
 
Back
Top Bottom