Mary Chatanda: Shukrani zetu kwa Rais Dkt. Samia zimejikita kwenye dhamira yake ya kuliunganisha taifa

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
666
835
SHUKRANI ZETU KWA RAIS DKT. SAMIA ZIMEJIKITA KWENYE DHAMIRA YAKE YA KULIUNGANISHA TAIFA - MARY CHATANDA (MCC)

"Shukrani zetu Wanawake kwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, zimejikita kwenye dhamira yake ya dhati ya kuliunganisha Taifa kuwa kitu kimoja ambapo niwakumbushe tu kipindi ametoka kuapishwa na kuwa Rais aliwahi kusema...Nanukuu "...Huu si wakati wa kutazamayaliyopita ni wakati wa kutazama mbele na kuzika yaliyopita na kuacha tofauti zetu...huu si wakati wa kunyoosheana vidole bali ni wakati wa kuwa pamoja na kusonga mbele pamoja..."

"Tunamahukuru Rais Samia kwa kanuni yake ya uongozi ya 4R na kuunda kikosi kazi cha kukusanya maoni ya wananchi katika masuala mbalimbali ya sheria...tunampongeza kwa kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa kwakuwa imekuwa sehemu ya kuweka usawa wa kufanya shughuli za kisiasa kwa vyama vyote Nchini na kupelekea fursa ya kila chama kujipambanua kwa kunadi sera zao"

"Wanawake wote kwa pamoja tunampongeza Rais Dkt. Samia kwa ustahimiliu wake kwa kuacha uhuru wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ijapouwa wengine wamekuwa wakiitumia vibaya kwa kumsema vibaya na kuongea uongo dhidi yake...hakika ameonesha ukomavu mkubwa kama Mama mlezi wa Taifa hili"

Ndugu. Mary Chatanda (MCC)
Mwenyekiti wa UWT Taifa
IMG-20240327-WA0091(1).jpg
IMG-20240327-WA0104.jpg
IMG-20240327-WA0105.jpg

Akizungumza kwenye Kongamano la kumshukuru Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani katika kipindi cha miaka 3 ya uongozi wake.
 
UWT WATOA HATI YA SHUKRANI WA MWENYEKITI WA CCM NA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndugu. Mary Chatanda (MCC) wametoa Hati ya shukrani kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020 - 2025 katika kipindi cha miaka 3 ya Uongozi wake tangua mwaka 2021 - 2024.

Hati hii wamemkabidhi Ndugu. Issa Gavu - Katibu wa NEC, Idara ya Oganaizesheni CCM Taifa ambaye ni Mgeni rasmi katika Kongamano la Kumshukuru Rais Samia akimwakilisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu. Dkt. Emmanuel Nchimbi
IMG-20240327-WA0029.jpg
IMG-20240327-WA0028.jpg

🗓️ 26 Machi, 2024
 
Back
Top Bottom