Na Shilatu E.J
1. Amesimamia vyema utolewaji wa ELIMU BURE kuanzia shule ya msingi hadi sekondari kwa wanyonge.
2. Amesimamia vyema mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi nchini.
3. Amesimamia vyema kulinda maisha na kuhakikisha rasilimali za nchi ni mali ya Watanzania wote.
4. Amesimamia vyema nidhamu, uwajibika na uadilifu kwa Watumishi wa umma
5. Amefufua shirika la ndege la ATCL kutoka kutokuwa na ndege hadi kuwa na ndege mpya 6 za kisasa zinazopasua anga za kitaifa na kimataifa.
6. Amesimamia Tanzania kufika uchumi wa kati unaokuwa kwa asilimia 7.1% kupitia mafanikio ya sera ya Tanzania ya viwanda zaidi ya 3000 vilivyojengwa.
7. Amesimamia vyema Serikali kuhamia Dodoma ikiwa ni ndoto aliyoiacha Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
8. Amejenga reli ya kisasa yenye kasi inayotumia umeme (SGR) na kufufua reli ya Dar - Tanga - Moshi Kilimanjaro.
9. Ameongeza makusanyo ya mapato ya ndani na kusimamia nidhamu ya matumizi ya pesa.
10. Amesimamia ujenzi wa mradi wa umeme Mto Rufiji wa Stiglers gogle utakaozalisha megawatts 2115.
11. Amesimamia ujenzi miundombinu ya kisasa ya mitandao ya barabara, flyover na madaraja.
12. Amekomesha biashara ya ujangiri na madawa ya kulevya nchini.
13. Ameleta maboresho ya afya nchini kwa kujenga hospital zaidi ya 57, vituo vya afya zaidi ya 350, ununuzi wa madawa na vifaa tiba hospitalini.
14. Ameisimamia vyema katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kulinda amani na usalama nchini hali inayofanya Watanzania tuendelee kujivunia uhuru wetu na kuvutia Watalii nchini.
15. Amejenga umoja, mshikamano wa kitaifa nchini.
*Rais Magufuli ameyafanya yote haya, Mimi ni nani haswa nisimchague tena 2020*
