10102ac521314716b0cdeb7f1e57ec04.jpg


Wanajukwaa poleni na misukosuko ya kujibadili kutoka kuwa walaji wa Mwisho kuelekea nchi ya Viwanda.

Uwanja huu ni maalumu kama ule wa Safari za nje za Jakaya kikwete ila huu ni mahususi kukusanya mambo mazuri ya Awamu ya tano chini ya Rais Magufuli juu ya maendeleo yetu hasahasa kauli yake kuu Juu ya Nchi ya Viwanda na Elimu Bure nk.

Unaruhusiwa kugusia miundo mbinu, Afya, Usafiri, Maendeleo ya Majeshi Yetu, Uvuvi,Michezo, Habari, Siasa, Viwanda,Teknolojia, Pato la Taifa nk.
Ila tu iwe kwa tulipotoka na Alipofanikiwa na nini tufanye kumsaidia kujiongeza zaidi.

Mpaka sasa kafanya haya;

Hostel za Chuo cha UDSM.
Hostel za Askari Magereza.
Ununuzi wa Ndege 2 (Nyingine 3 ziko mbioni kuja).
Ujenzi wa Flyover Tazara na Ubungo
Upanuzi wa Airport Mwanza
Upanuzi barabara ya Moroco Dsm
Upanuzi wa Kisasa Airport Dar
Kukomesha Rushwa
Kurejesha nidhamu Makazini.
------------

Na haya ameanza tarehe 12/4/2017;

Uzinduzi ujenzi wa reli kwa ajili ya treni ya Umeme.
Ujenzi wa barabara ya Mtwara-Tandahimba

Kukomesha Watumishi Wenye Feki hivyo kuokoa Mabilioni ya Fedha.

Barabara ya kuunganisha Wilaya za Kibondo kigoma Kaliua huko Tabora.

Miradi Mikubwa ya Maji :

Uwezeshaji Ujenzi Bomba la Mafuta kutoka Hoima mpaka Tanga

1. Upanuzi wa Airport Mwanza-Kikwete
2. Upanizi wa Airport Dar-Kikwete
3. Rushwa ipo sana tu na leo nimetoa
4. Kazini hakuna nizamu kuna uoga wakutumbuliwa labda kama uoga na nizamu ni kitu komoja
5. Hostel za chuo alianzisha kikwete yoyote ambaye angekuja madarakani zingefanyika
6.Upanuzi wa barabara iyo ipo kwa Tanroads miaka zaidi ya 10 kwenye plan yao yoyote anayeengia alikuwa anafanya
6. ununuzibwa ndege kavunja sheria za ununuzi alitakiwa ashitakiwe
 
1. Upanuzi wa Airport Mwanza-Kikwete
2. Upanizi wa Airport Dar-Kikwete
3. Rushwa ipo sana tu na leo nimetoa
4. Kazini hakuna nizamu kuna uoga wakutumbuliwa labda kama uoga na nizamu ni kitu komoja
5. Hostel za chuo alianzisha kikwete yoyote ambaye angekuja madarakani zingefanyika
6.Upanuzi wa barabara iyo ipo kwa Tanroads miaka zaidi ya 10 kwenye plan yao yoyote anayeengia alikuwa anafanya
6. ununuzibwa ndege kavunja sheria za ununuzi alitakiwa ashitakiwe
Gharama ya kuwa mjinga ni ndogo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
uongozi aliyoanza nayo.

Lakini kadiri muda unavyoenda ndivyo umaarufu wake unazidi kushuka na kukosa uungwaji mkono wa watanzania, wengi wameanza kumuona kama mbabaishaji asiye jali maisha ya watanzania wakiwemo hao anawaita wanyonge, yapo mambo amefanya vizuri kama watumishi hewa na vyeti lakini mengi kaharibu, mambo yaliyosababisha umaarufu wake kushuka ni pamoja na, uchumi mbaya unawakumba watanzania wengi kwa sasa hali iliyopelekea kuongezeka kwa umasikini miongoni mwa jamii, ukosefu wa ajira, ukosefu wa mikopo kwa watoto wa maskini, imagine serikali imetangaza kuwa itatoa mikopo kwa vijana 30000 tu ili hali wenye uhitaji ni zaidi ya 90000, uminyaji wa demokrasia na unyanyasaji wa viongozi wa upinzani, kauli mbaya za rais zinatokana na hulka na tabia yake.

Kwa hakika endapo uchaguzi ukifanyika leo ukiwa huru na haki rais atashindwa vibaya sana.

Shukrani za pekee ziwaendee kitengo cha propaganda cha ccm ambacho kinatumia nguvu kubwa kuwaaminisha watu kuwa rais anakubalika lakini hali iliyopo mtaani amepoteza umaarufu kwa kiwango kikubwa sana.
 
Mbona hizi thread za kumsifia jamaa na kutaja aliyofanya leo zimepamba sana moto, kuna mtu amenotice hili? Naona jana Lumumba homework ilikuwa hii. Leo nadhani watakuwa wameahidiwa buku ten badala ya buku saba
 
Ukweli Kila ajaye husoge hili kutoka point aliyoikuta kuenda point nyingine katika tofauti. Baadhi yake atarudisha nyuma na nyingine mbele.
Safari ya taifa letu ni ya kudumu hakuna wa kulisogeza Hadi mwisho. Tusijaze masifa. Kuzi ya kiongozi ni kusema HARAAAMBEE na wananchi huitika na kuinua na kusukuma mbele. Hakuna kiongozi ambaye alikabidhiwa nchi asifanye hayo.
Wengine wamejikalia kimya kumshangilia kiongozi kwa kumjaza misifa eti yeye tu ndo anasukuma wanasahau kuwa sisi ndio wasukumaji na lazima wote tushibe kwana na tuhamasishwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Each President has done his part during his time. Among the achievements of President Magufuli are setting priorities right. One of these is Railways. Presently the best way to reduce transportation cost is railways. Secondly, recognition that scarce mineral resources that are available to us much more easily due to our being located in the confluence of the Great Rift Valley need to be exploited such that we Tanzanians need to be the primary beneficiaries; not by way of trickle down effect of exploits of the multinationals but by constructive participation in win-win situation. Constructing good hostels at the universities is a step in the direction of self reliance in the knowledge and technology sector which certainly needs big boost as with the ongoing help of IT multinationals as Microsoft. Use of IT in schools, hospitals, government institutions, businesses, outreach to rural areas and particularly the farmer; this is the way forward that is indeed apparently happening. Knowledgeable farmer is less likely to be exploited and therefore better off than the one who is not able to go beyond subsistence. Easy connectivity and mobility for all, when that is happening, that apparently is the right direction.
 
Kama kawaida, siku zote changamoto ndio mwanzo wa mafanikio, kiukweli hivi karibuni kumezuka mengi sana na kila mtu anaongea lake, wapo wanamlaumu Rais Magufuli na pia wapo wanao laumu upinzani kwa kile kinachoitwa kutoa siri za taifa, uchochezi na kadhalika.

Binafsi mimi naona hizi ni changamoto kwa Rais wetu na anapaswa kuzipokea kwa mikono miwili, muhemiwa rais anapaswa kuyafanyia kazi kwa busara na hekima matatizo yanayojitokeza na sio kuziba ufa kwa matope anaekwambia umekosea huyo ujue anakupenda.

Kadhalika kwa upande wa upinzani mimi naona ni bora kutumia busara na hekima zaidi ya nguvu kwani haiwezekani umtukane dereva au umchome mkuki dereva wakati wewe ni abiria.

Tanzania ni yetu. Tuunganekuijenga Tanzania Tusitafute umaarafu ubabe, ushabiki na chuki tuziweke pembeni Tujenge taifa.
 
TANZANIA NI YETU.TUUNGANE KUIJENGA TANZANIA TUSITAFUTE UMAARUFU..ubabe, ushabiki na chuki tuziweke pembeni. TUJENGE TAIF
Tatizo hakuna hata pande moja iliyo na nia dhabiti ya kuijenga nchi. Mfano mzuri ni humu jukwaani ni vijembe na matusi tu baina ya hizo pande mbili vilivyo tawala.
 
hahahahaha akili hizi wangekuwa nayo wahusika afadhali bila aibu wanasema kukamatwa kule ni kwa kutengenezwa akili zao bhana hahaha
 
Kama kawaida, siku zote changamoto ndio mwanzo wa mafanikio, Kiukweli hivi karibuni kumezuka mengi sana na kila mtu anaongea lake, wapo wanamlaumu rais magufuli na pia wapo wanao laumu upinzani kwa kile kinachoitwa kutoa siri za taifa,uchochezi na kadhaalika.
Binafsi mimi naona hizi n changamoto kwa rais wetu na anapaswa kuzipokea kwa mikono miwili , muhemiwa rais anapaswa kuyafanyia kazi kwa busara na hekima matatizo yanayojitokeza na sio kuziba ufa kwa matope.anaekwambia umekosea huyo ujue anakupenda. Kadhaalika kwa upande wa upinzani mimi naona ni bora kutumia busara na hikema zaid ya nguvu kwani haiwezekani umtukane dereva au umchome mkuki dereva wakati wewe ni abiria.
TANZANIA NI YETU.TUUNGANE KUIJENGA TANZANIA TUSITAFUTE UMAARUFU..ubabe, ushabiki na chuki tuziweke pembeni. TUJENGE TAIFA
Ukimwambia ukweli kuwa mkuu nguo uliyovaa imetoboka anachukia, yeye anataka umsifie tu kuwa nguo uliyovaa imekupendeza sana kama malaika hapo atacheka mpaka kile kicheko chake cha kolomije
 
Saa nyingine kwenye hilo lori kuna abiria wanaojua kuendesha vizuri zaidi so huyo dereva akubali kuelekezwa. Sio macho yote mbele mda nwingine ni vigumu kuona mashimo
 
Back
Top Bottom